Mkuu
ZeMarcopolo,
All that said and done, suala la msingi hapa ni jinsi gani Dr. Slaa has stimulated my thinking; Swali linalofuatia kwako ni je:
· Kuna haja ya kuhalalisha gongo au hakuna haja?
Binafsi naamini kwamba kuna haja ya kuhalalisha gongo, na nikaenda mbali na kujadili kwanini nafikiri hivyo na nipo katika maandalizo ya sehemu ya pili ya mada yangu. Tumuache Dr. Slaa kwa sasa, badala yake, mimi na wewe tuingie katika mjadala ambao umekuja baada ya Dr. Slaa kusema neno moja tu la msingi kwamba kuna haja ya kuhalalisha gongo, hoja ambayo nimeiendeleza kama ulivyokwisha soma
#1 . Nadhani kwa mtindo huo, tutaacha kujadili personality (DR. Slaa) na kujadili ISSUE (whether to legalize or continue to ban Gongo).
Nimejadili kwamba ndio ipo haja, na kwa ufupi (rejea kwa kirefu bandiko namba moja), nimejikita zaidi katika kuchambua juu ya
umuhimu wa serikali kuhalalisha gongo kwa manufaa ya uchumi wa mtengenezaji, afya ya mnywaji, pamoja na multiplier effect ya kuhalalisha pombe za namna hii katika uchumi wa taifa, hasa katika nchi ambayo serikali yake inatambua vilezi vingine vya kienyeji kama kama vile mbege, chibuku, chimpumu, lakini vile vile vinywaji vya kigeni ambavyo ni moja ya vyanzo vikuu vya kodi ya serikali. Tanzania ingekuwa ni nchi ambayo imepiga marufuku vilevi vyote kwa mujibu wa sheria, hoja yangu na ile ya Dr. Slaa zingekosa mashiko.
What are your counter arguments katika hili? Kumbuka hata Serikali ya TANU chini ya Nyerere ilifikiria kuhalalisha pombe hii kwa hoja inayofanana sana na ya Dr. Slaa miaka 30 baadae; Kilichoikwamisha TANU ni gharama kwa mnywaji kutokana na regulation and licensing effects on the producer. Kwa vile suala hili ni more socio-economic, huku siasa ikiwa ni daraja tu la kuitekeleza au kutoitekeleza kupitia sera na udhibiti, political spinning haina nafasi hapa, tulijadili bila ya kujali itikadi za vyama.
Mkuu,
Kwenye kichwa cha habari yako unasema "Dr. Slaa na kuhalalisha gongo..". Unaosema hutaki kujadili alichosema Dr. Slaa badala yake twende moja kwa moja kwenye kile ulichoandika unakuwa unakimbia mjadala ambao umeuanzisha wewe mwenyewe.
Kwa vile umetaka twende kwenye kile ulichosema hapa na kuacha mjadala uliouanzisha, mimi pia nitakubaliana na wewe. Tujadili kuhalalishwa kwa gongo, bila kumhusisha Dr. Slaa or personalities.
Here I come,
Gongo maana yake ni pombe kali inayotengenezwa kiholela ambayo pamoja na vitu vingine huwa na sumu inayoathiri afya ya binaadamu.
Pombe hii ina madhara ya kibaiolojia, kisaikolojia, kiuchumi, na kijamii. Ili kufuisha urefu wa post hii nitagusa kila madhara kwa juu juu tu na nitakuwa nikiingia deeper kadri mjdala utakavyoendelea.
Madhara ya kibaiolojia: Yapo madhara ya muda mfupi na muda mrefu kwa afya ya binaadamu kama upofu, magonjwa ya ini, kudhoofisha kinga ya mwili, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kuunguza uwezo wa kuconcentrate.
Kisaikolojia: Matumizi ya gongo ya muda mrefu yanamjengea mtu hali ya kutokujiamini na hivyo kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi.
Kiuchumi: Ni dhahiri kwamba watu wanaokunywa gongo wanashiriki kidogo katika GDP kuliko wale wasiokunywa gongo.
Kijamii: Gongo imekuwa sababu ya mahusiano mabaya katika jamii. Wanandoa kuachana, vijana kujifunza tabia ya wizi.
Kwanini gongo haipaswi kuruhusiwa kisheria?
Pamoja na kwamba gongo ina madhara mengi, lakini sababu kuu ya gongo kutokuruhusiwa kisheria ni moja, ambayo ni kutokukidhi viwango vya ubora unaohakikisha usalama wa wanywaji wake.
Leo hii iwapo mpika gongo atahakikisha kuwa anachouza ni salama kwa matumizi ya binaadamu, basi hatakatazwa kukiuza. Taratibu za yeye kupewa kibali cha kutengeneza, kusambaza na kuuza pombe salama zipo.
Unaposema gongo iruhusiwe ni kwamba unasema pombe kali inayoweza kupofua watu macho iruhusiwe kuuzwa. This is exactly what you just said in your post.
Je, unadhani ni sahihi kurusu pombe inayopofua macho kuuzwa just because tunataka muuzaji apate kipato?