- Alianza Mheshimiwa Nape kwa kusema kwamba Dr. Slaa anayo kadi ya CCM, Dr. Slaa akamjibu kwamba ni kweli anayo, and then Mh. Nape akaongeza tena kwamba DR. Slaa amekuwa akiilipia Kadi yake ya CCM kila Mwezi, akiwa na maana hata Mwezi uliopita ameilipia, na yupo tayari kuonyesha risiti za Dr. Slaa akilipia kadi yake hiyo ya CCM.
- Mpaka leo Dr. Slaa hajakanusha wala kukubali kwamba huwa anailipia kadi yake, huu ni wakati muafaka sasa Chadema na Dr. Slaa wakakanusha au kukubali, ama sivyo inaweka wingu kubwa sana kwenye Uongozi wao wa Taifa na Mamluki, hasa ukizingatia kwamba ni majzui tu Chadema wamefukuza the so called Mamluki, sasa kama kina Slaa wanaachiwa ina maana Chadema ikishika Taifa kutakuwa na Sheria mbili, moja ya Slaa na nyingine ya wananchi wa kawaida?
LE MUTUZ - THE KING OF ALL BONGO NETWORK SOCIAL MEDIA. at williammalecela.blogspot.com
Mtu mwelewa kuanza kuandika propaganda za namna hii wakati kuna vitu vingi sana vya kuvichallenge, Tunashangaa kuona hawa jamaa wanakomalia issue ya Kadi ya Dr Slaa kuliko Mabilioni yaliyofichwa Uswiss, kuliko Mradi wa Gesi unaotaka kumalizi gesi yote kwenye kugharimia Mradi, Kuliko Ufisadi unaofanywa secta ya Afya, Elimu na Bandari.
Sijawahi kuona huyu Bwana akizungumzia Wizi unaofanywa na CCM Pamoja na Makada wake zaidi kushadadia mambo ambayo hayawasaidii waTZ.
Kwa Mtanzania wa Kawaida Dr Slaa hata ungesema si Mtanzania bado watu watamwami kwa matendo yake na Uadilifu wake katika kutetea Maslahi ya Nchi hii na watu wake.
Na amekuwa hapepesi Macho linapokuja swala ufisadi na Uadilifu wa mtu, huwa hana Mzaha katik hilo na Amekuwa na Record hiyo tangu watu tumfahamu.
Si dhambi Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM, kwani Dr Slaa alishawahi kusema alilipia kwa muda mrefu tangu wakati huo.
Mnachokifanya nyinyi ni kutekeleza kazi ya Vuvuzela Nape, mjiandae 2015 Dr Slaa ndiyo Rais wa Nchi kwa hiyo mjiandae kujibu ufisadi mnaoufanya.
Tuna Records zinazoonyesha mnanufaika vp na Unyonyaji unaofanywa na CCM na mko radhi hata mtu afe kuliko hiyo mirija yenu ikatike.
Sijawahi kuona Vobaka wanawasifia polisi kwa hiyo sishangai, Mzee Mandela alifungwa kwa ajili ya kutetea haki, Nyerere alikufa kwa ajili ya kutetea Rasilimali za WaTZ sishangai kuona nyinyi mnafanya juu chini kupambana na Watu safi wenye nia njema na watanzania,
Ila ni vigumu sana kupambana na haki na ukweli maana sijawahi kuona watu wachache wachafu wakiwashinda walio wengi kwani mungu yupo pamoja na sisi tumeibiwa na wazee wenu, sasa mnataka kutuibia nyinyi watoto, watoto wenu watawaibia wajukuu ambao watasota kulipa madeni ambayo hayana msingi.
We are tired enough is enough.