Fortilo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 5,614
- 16,959
Wakuu salam.
Kwa wafuatiliaji wa siasa za Tanzania toka zilivyoanza kuchangamka 1995 mtakubaliana na mimi kuwa Dr. Slaa ni mmoja wa wanasiasa "Contraversial" na mwenye ushawishi kwa muda mrefu, takribani Miongo mitatu sasa.
Ni Dr. Slaa huyu huyu aliewahi kuhoji na kufanya Jack Zoka Naibu Mkuu wa Usalama wa taifa kutoka hadharani kukanusha shutuma mbalimbali ikiwemo ya kutaka kuwadhuru wakosoaji wa kisiasa awamu hiyo mwaka 2012.
Soma pia: Majibu ya Jack Zoka yana utata!
Hivi Jana Dr. Slaa kanukuliwa kwamba amepewa habari na watu wanaompenda na waliopo "Usalama wa Taifa" kwamba Freeman Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA amepewa rushwa kubwa na Rais ili kuhonga wajumbe wampigie kura.
Hakuishia hapo, akasema amepewa hadi maafisa wa vyombo vya dolla kuimarisha ulinzi na kuhakikisha anashinda katika uchaguzi huo...
Sina tatizo kama tuhuma hizi ni za kweli, lakini kitu cha muhimu sana hapa ni kuwa na uhakika na taarifa ambazo mara nyingi huwa anazitoa kwa maslahi yake binafsi.
Mara nyingi ukimsikiliza akitaka kumchafua mtu anatumia kuwa kapewa "Data" na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwanini yeye mara nyingi apewe data za kuchafua wenzake, na hii imekuwa style yake ya uongozi toka anaanza harakati za Ubunge Karatu mwaka 1995 mpaka leo hii.
Hao wana usalama wanaompa Dr. Slaa Data kwa miaka zaidi ya 30 sasa ni kina nani? hasa katika harakati za kuwaharibia wenzake reputation na kukuza jina lake...
Uzalendo ni pale tu anapotaka kuharibu majina ya wengine? Tuhuma anazotoa nani anaweza kuzithibitisha pasi na shaka?