Dr. Slaa: CCM imebanwa Igunga; yajipanga kuchakachua kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: CCM imebanwa Igunga; yajipanga kuchakachua kura

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by palalisote, Sep 27, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya wananchi wa Igunga kuamua nani atakuwa mbunge wao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amenasa siri nzito ya jinsi vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyojipanga kuiba kura.

  Dk. Slaa alisema kwa takriban wiki moja sasa, CCM imekuwa ikifanya mbinu mbalimbali na juzi na jana walikuwa na vikao vizito kupanga jinsi ya kuiba kura baada ya kubaini kuwa chama hicho hakiwezi kushinda. “Safari hii, CCM wamekabwa kwelikweli na ukiona mtu mzima (CCM), analalamika, ujue ameshikwa mabaya. Sasa kwa kujua hilo, wamepanga mikakati ya kuiba kura. Jana walikuwa na kikao cha siri kilichofanyika Peac Hotel na leo walikuwa na kikao kingine, mipango na kila walichojadili nimepata,” alisema Dk. Slaa.

  Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita na kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitaja mbinu nyingine ya CCM kuhakikisha inapata ushindi kuwa ni pamoja na kutengeneza kura hewa, kuchoma karatasi za kula kama walivyofanya Msalala, kununua shahada na kuwapiga wafuasi wa CHADEMA.

  “Kama mlivyosikia, tayari wameanza kuwapiga watu wetu, wameanza kuwapa vitisho, vijana wanakamatwa na kuwekwa ndani hovyo ili kuwatisha,“ alisema Dk. Slaa.

  Kiongozi huyo wa CHADEMA, pia alisema mbinu nyingine inayotumiwa na CCM ni kumwaga pesa na kutolea mfano wa kijiji cha Karenga ambacho kimepewa sh milioni 10 kwa kisingizio cha kutumika kwenye miradi ya maendeleo, jambo ambalo alisema sio kweli.
  “Katika baadhi ya vijiji jana nilishuhudia mwenyewe watu wa CCM wakigawa mahindi. Vijiji hivyo ni Mwamwapuli, Mwamwagogo na vingine ambavyo sivikumbuki kwa sasa, kote huko waligawa mahindi ili kuwarubuni wawapigie kura,” alisema Dk. Slaa.

  Hata hivyo pamoja na mbinu zote hizo za kuiba kura, Dk. Slaa alisema chama chake kimejipanga vizuri na kuwahakikisha wanachama wake kuwa hakuna kura itakayoibwa.

  “Nakuhakikishia, mbinu zote tunazijua, tumejipanga vizuri sana kuhakikisha hakuna hata kura moja itakayoibwa au kuchomwa moto. Tutapambana hadi tone la mwisho na tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura,” alitamba Dk. Slaa.

  Alilitahadharisha jeshi la polisi pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa makini siku hiyo, vinginevyo taifa linaweza kuingia katika matatizo mazito sababu ya kuibeba CCM ambayo alisema kwa sasa haibebeki.

  Malalamiko ya Dk. Slaa, yaliungwa mkono na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimedai kuwa CCM ina mpango wa kuiba kura na inacheza rafu kwa kuleta malori saba ya sukari, kugawa mahindi na kuingiza Janjawid ili kuwatisha wananchi wa Igunga siku ya kupiga kura.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, aliliambia gazeti hili kuwa malori hayo yako njiani kutoka Mara kuelekea Igunga kwa lengo la kugawa kwa wapigakura.

  “Kwa sababu vyombo vya dola ukiripoti havitachukua hatua kwa vile wanailinda CCM, tumejipanga vya kutosha kuyadhibiti malori hayo, tunazo taarifa za kutosha tunajua yamelala wapi juu wameweka nini, chini wameweka nini.

  “Tumewapanga vijana wetu na tutayakamata kwa nguvu zetu kisha tutawaonyesha waandishi wa habari na taifa lione, tunatoa tahadhari kwamba mbinu zao zimegundulika, makontena ya sukari yanaletwa Igunga ili kuigawa siku mbili kabla ya kupiga kura.

  “Hatutakubali haki za Watanzania kuchagua kiongozi bora ziondolewe kwa sababu ya kilo za sukari…tunalishughulikia hili,” alisisitiza kiongozi huyo wa timu ya kampeni za CUF Igunga.

  Aidha, ameionya CCM kuacha mpango wa kutaka kugawa mahindi Septemba 30 na Oktoba mosi kwa wakazi wa jimbo hili kwa kuwa hiyo ni rushwa wanayoitoa kwa mgongo wa njaa.

  CHANZO. GAZETI LA TANZANIA DAIMA
   
 2. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  mmeanza kuleta visingizio sasa.chadema inatoa vitisho kuwa itapambana mpaka tone la mwisho, kwani tuko vitani?,tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura,jamani hivi sinivitisho?.visingizio vya nini kama unauhakika wa kushinda?.nyie kila siku mnaibiwa na njia za wizi mnazifaham kwanini msizitumie kama mnazifaham sasa?.
   
 3. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Sambamba na mipango hiyo, habari iliyonifikia kutoka kwenye chanzo kinachofanya kazi ili kufanikisha mpango huo ni kwamba CCM wameamua kupeleka mamluki toka mikoa mingine hasa Dar. Chanzo hicho kinadokeza kuwa kuna vijana waliopelekwa Igunga kutokea Dar es salaam ili wakasaidie CCM.

  Miongoni mwa kazi wanazofanya ni

  (i) Kuhakikisha wanashangilia sana kwenye kampeni za CCM ili kuoesha kuwa chama hicho kinakubaliwa

  (ii) Kufanya fujo, kutisha na kupiga wananchi kwa kujifanya wao ni supporters wa vyama vya Upinzani.

  (iii) Kwa kutumia kadi na majina feki watatumiwa kupiga kura ili kukipatia ushindi CCM

  Wengi wa vijana hao ni wale wanao patikana kwenye vijiwe, na wengi wao ni madereva Bajaji, Madereva Pikipiki na wale wasio kuwa na kazi maana huko wanalipwa.

  Source ni muhusika anayehusika kufanya kazi hiyo huku akiamlishwa na walio juu yake. Anafanya hayo kulinda kitumbua chake ila hafurahishwi na mipango hiyo.

  Mpango wa CDM wa kulaza helkopita yao Nzega tena kwenye kituo cha polisi nao umeonesha kuharibu mipango ya CCM walio kuwa wameshapanga. Kitendo hicho kimeonesha kuwazidi kete maana walishapananga kuichoma moto, ila issue inabaki itachomwaje ikiwa polisi.

  My take CDM kuweni makini sana kwa kila hatua na mipango mnayo ipanga. Mnayo support toka kwa hao waliotumwa wengine, ingawa hawajioneshi ila mnatakiwa kuwa makini kwa kila movement mnayofanya.

  Imarisheni ulinzi wa kura. Hakikisheni vizuri majina ya wapiga kura na je anayepiga ndiye aliyeandikishwa! Hakuna kulala.
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nadhani kama wamegundua mbinu hizo kama alivoziainisha basi ni kudhibiti,kuanzia hayo malori ya sukari,mahindi na inshu ya kuchoma kura au kupandikiza zingine. mawakala wawekwe kuhakikisha hilo halitendeki. Otherwise itakuwa ni kuweweseka tu so far so good naombea upinzani CDM ama CUF washinde jimbo hilo kutoka kwa manyang'au ccm
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kuna hoja katika hayo yaliyosemwa na Dr. Slaa na siyo kuishia kusema tu kuwa kila siku nyie. Ni jambo lililo wazi kuwa kuna upendeleo wa hali juu kuanzia uripotiji wa habari hadi vyombo vya dola. Cha msingi narejea kauli fulani iliyowahi kutolewa na mwanasiasa mmoja kuwa "KUWA IKITAKA KUISHINDA CCM BASI ISHINDE KWA KURA NYINGI ILI HATA WAKITAKA KUIBA BASI WASHINDWE" Kauli hiyo inabidi kufanyiwa kazi kwa vitendo na watu kujitoa mhanga ili kuhakikisha haki yao haipotei.
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Kwa mtazamo wangu bila shaka pale Igunga hawa magamba wakitaka pachimbike wajaribu wanachotaka kufanya. Wao wana pesa,CDM wana MUNGU.
   
 7. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  CCM wana roho mbaya kama mashetani. Wanaoijua tabia ya shetani huwa hawapendi maendeleo mazuri ila wanaushawishi wa kuangamiza. Yaani waichome helkopta kwa ajili ya kumpeleka Kafumu bungeni, Kafumu mwenywe muongo kama nyoka alivyojichubua na kusema amejitoa gamba. Kumbafu kabisa.
   
 8. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #8
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  NATABIRI UCHAGUZI HAUTAFANYIKA J2 HII YA OCTOBEr 2
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wewe tahira wa wapi..hujui hata vita ni nini?
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwa madaraka uliyo nayo huko kwenye chanma chenu cha magamba hustahili kabisa kuzungumza manenno kama haya!!!!!!!!! bwahaha ahahah ahahaha ahahaha ahahahah!!!!
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Only I can push is for cdm to get tactical and protecting all the votes. Starting today, cdm should have plans to check all voting boxes before the votes and to protect all polling stations and vote counting. cdm must have a plan for responding to all voting criminality, even to remove this gov.

  cdm must make this clear, ccm are not supported by the people and full of arm gangs!

  ccm can only fool the foolishness!

   
 12. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mods isitoshe tu kuiondoa Post ya Omr isipokua mngempa Ban ya ukweli kwa sababu hawezi mtukana Dr Slaa ndio maana nilijaribu kureply nikaambiwa sina access hyo,kipi cha ajabu ambacho Dr Slaa kakosea juu ya hizo wakati inajulikana wazi kua CCM ni wezi wakubwa wa kura na wanajulikana na mbinu zao chafu za kuiba kura? Madai ya Dr Slaa yana ukweli kabisa sio kupuuza kama baadhi ya wana Magamba wanavyotaka kutuaminisha hapa.
   
 13. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  Ukiona mtu mzima tena ana PHD ya ucha mungu kutoka vatikan anadanganya ujue anazeeka vibaya na ndio matatizo ya kuanza mapenzi uzeeni haya.Kulalama kwa chadema na cuf ni alama tosha kuwa CCM imeisha shinda.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Niliisha wahi kuuliza swali humu ndani ya JF na hakuna hata mmoja aliyejibu. Na nauliza tena ' KURA ZINAIBIWAJE?'
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CDM bana mkipingwa kidogo kwa hoja zenu dhaifu mnazoleta ndani, mnaanza kuwatishia watu kuwa ban, sasa hapo watu wataacha kuamini vp kuwa JF ni jukwaa la CDM? ni ngumu kulibishia hili labda uwe zuzu
   
 16. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  hilo swali hata mimi linanisumbua sana.
   
 17. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata hapo juu kabisa imeelezwa.
  Kuchoma moto/kuharibu kwa makusudi kura za mpinzani wako, kurubuni mawakala wa mpinzani wako ili muhujumu, kushiriki katika kuelekeza wapiga kura kumpigia kura (ndani ya kituo cha kura) mgombea wako, kuchukua shahada za wapiga kura hasa wale ambao unaamini watampigia mpinzani wako, kutoa vitisho kwa wapiga kura ambao unaamini ni wa mpinzani wako, kuingiza kura hewa ndani ya ballot box........njia zipo nyingi sana zinazotumiika na magamba.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama tangu mfumo wa vyama vingi TZ uanze, kuna hata mara moja CCM waliwahi kushinda kihali!
   
 19. Mlamoto

  Mlamoto JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Twahil kwanini unafanya watu wote watoto? Unajua fika kinachoendelea na unajua wazi kuwa watu wote wanajua kuwa dola na ccm ni moja. Kesi ya ngedere kuamuliwa na nyani haki itapatikana? Tutaendeleza kesi zetu kwenye majukwaa kama haya ili tuweke wazi uozo wenu! Ipo siku kamba itakata jiwe!
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama ndivyo basi huwa mnashindwa kihalali . Mbinu mnazijua na mnasema mnazidhibiti halafu mnashindwa, hapo hakuna kuibiwa kura huwa mnashindwa kihalali.
   
Loading...