Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
CCM, kiasili ni chama cha waovu, hata kwa mtu binafsi ni vigumu sana, kuiacha asili yake. Hivyo tusitegemee ni rahisi CCM kuuacha uovu.
Ukisikia mafisadi, wapo CCM: Uthibitisho: marehemu Magufuli aliwahi kutamka kwa uwazi kuwa majizi na magisadi yapo CCM.
Ukisikia waabudu ushirikina, wapo CCM:
Uthibitisho: kuna mchawi/mganga wa kienyeji mmoja kule Kigoma alikuwa anatamba, tena mpaka kutaja majina ya viongozi wa CCM ambao huwa wanaenda kwake wakati wa uchaguzi ili waweze kupata madaraka.
Ukisikia wevi waliobobea katika wizi wa kura wapo CCM:
Uthibitisho: Nape aliwahi kutamba kwamba wakishindwa kupata kura, watafunga kwa goli la mkono, na Samia aliwahi kunena kuwa hata wananchi wakiwapigia wagombea wa upinzani, kura zao zitahesabiwa CCM. Bashiru naye alinena kwa uwazi kuwa CCM itatumia dola kubakia madarakani. Mara kadhaa mabox ya kura fake yamekamatwa wakati wa uchaguzi yakiwa na kura fake za wagombea wa CCM.
Ukiwatafuta wauaji kwaajili ya kutetea madaraka yao, wapo CCM:
Uthibitisho: Rais mstaafu Kikwete aliwahi kunena kuwa CCM hawaachiani hata glass ya maji mezani kwa kuogopa kuuana. Mtuhumiwa mkubwa wa shambulio la kukusudia kumwua Lisu, ni kiongozi wa CCM. Aliyepigwa marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani kwa sababu ni muuaji, ni kiongozi wa CCM.
Hivi chama kilichojijenga kwenye uovu wa kiasi hiki, tunatarajia kitabadilika mara moja na kuanza kuuchukia uovu na kupenda matendo mema?
Siku za karibuni, baadhi ya viongozi wakuu wa CCM, Mwenyekiti wa CCM na Makamu Mwenyekiti, wametoa kauli ambazo zinaonekana siyo halisia, ukiangalia na uhalisia katika matendo. Rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, amekuwa akisistiza haki. Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, amesikika akisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu na wa mwakani, utakuwa huru na wa haki. Cha ajabu, kwenye uchaguzi mdogo kule Zanzibar, CCM waliiba kura za mgombea wa ACT. Na ilipodhihirika, katika kujikosha, sijui kama ni kwa maamuzi binafsi ya mgombea au kwa kulazimishwa, ikabidi mgombea wa CCM aliyepewa ushindi kupitia wizi, ajiuzulu. Leo tena tunapata taarifa toka Mtwara kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo amekutwa na kura fake za mgombea wa CCM, na wananchi walipochachamaa, polisi wameamua kumlinda msimamizi huyo, na kiongozi wa ACT alipojaribu kuwahoji polisi sababu za kumlinda mhalifu, ameishia kukamatwa na polisi.
Je, matendo haya, yanatoa picha gani kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani? Hivi kweli tunaweza kujipumbaza na kuamini kutakuwa na uchaguzi, katika maana halisi ya uchaguzi?
Fikiria chama ambacho wazazi walikuwa wevi wa kura. Wakawaingiza watoto wao kupitia chipukizi na UVCCM, na huko kote ama wameshiriki au wamekuwa wakifundishwa namna ya kuiba kura, sahizi ndiyo viongozi, na kila waliposhinda uchaguzi walitegemea kura za wizi, unadhani ni rahisi leo hii watu hao katika kutaka kuupata uongozi, watakubali wategemee kura halali za wananchi?