palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,455
ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya wananchi wa Igunga kuamua nani atakuwa mbunge wao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amenasa siri nzito ya jinsi vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyojipanga kuiba kura.
Dk. Slaa alisema kwa takriban wiki moja sasa, CCM imekuwa ikifanya mbinu mbalimbali na juzi na jana walikuwa na vikao vizito kupanga jinsi ya kuiba kura baada ya kubaini kuwa chama hicho hakiwezi kushinda. Safari hii, CCM wamekabwa kwelikweli na ukiona mtu mzima (CCM), analalamika, ujue ameshikwa mabaya. Sasa kwa kujua hilo, wamepanga mikakati ya kuiba kura. Jana walikuwa na kikao cha siri kilichofanyika Peac Hotel na leo walikuwa na kikao kingine, mipango na kila walichojadili nimepata, alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita na kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitaja mbinu nyingine ya CCM kuhakikisha inapata ushindi kuwa ni pamoja na kutengeneza kura hewa, kuchoma karatasi za kula kama walivyofanya Msalala, kununua shahada na kuwapiga wafuasi wa CHADEMA.
Kama mlivyosikia, tayari wameanza kuwapiga watu wetu, wameanza kuwapa vitisho, vijana wanakamatwa na kuwekwa ndani hovyo ili kuwatisha, alisema Dk. Slaa.
Kiongozi huyo wa CHADEMA, pia alisema mbinu nyingine inayotumiwa na CCM ni kumwaga pesa na kutolea mfano wa kijiji cha Karenga ambacho kimepewa sh milioni 10 kwa kisingizio cha kutumika kwenye miradi ya maendeleo, jambo ambalo alisema sio kweli.
Katika baadhi ya vijiji jana nilishuhudia mwenyewe watu wa CCM wakigawa mahindi. Vijiji hivyo ni Mwamwapuli, Mwamwagogo na vingine ambavyo sivikumbuki kwa sasa, kote huko waligawa mahindi ili kuwarubuni wawapigie kura, alisema Dk. Slaa.
Hata hivyo pamoja na mbinu zote hizo za kuiba kura, Dk. Slaa alisema chama chake kimejipanga vizuri na kuwahakikisha wanachama wake kuwa hakuna kura itakayoibwa.
Nakuhakikishia, mbinu zote tunazijua, tumejipanga vizuri sana kuhakikisha hakuna hata kura moja itakayoibwa au kuchomwa moto. Tutapambana hadi tone la mwisho na tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura, alitamba Dk. Slaa.
Alilitahadharisha jeshi la polisi pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa makini siku hiyo, vinginevyo taifa linaweza kuingia katika matatizo mazito sababu ya kuibeba CCM ambayo alisema kwa sasa haibebeki.
Malalamiko ya Dk. Slaa, yaliungwa mkono na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimedai kuwa CCM ina mpango wa kuiba kura na inacheza rafu kwa kuleta malori saba ya sukari, kugawa mahindi na kuingiza Janjawid ili kuwatisha wananchi wa Igunga siku ya kupiga kura.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, aliliambia gazeti hili kuwa malori hayo yako njiani kutoka Mara kuelekea Igunga kwa lengo la kugawa kwa wapigakura.
Kwa sababu vyombo vya dola ukiripoti havitachukua hatua kwa vile wanailinda CCM, tumejipanga vya kutosha kuyadhibiti malori hayo, tunazo taarifa za kutosha tunajua yamelala wapi juu wameweka nini, chini wameweka nini.
Tumewapanga vijana wetu na tutayakamata kwa nguvu zetu kisha tutawaonyesha waandishi wa habari na taifa lione, tunatoa tahadhari kwamba mbinu zao zimegundulika, makontena ya sukari yanaletwa Igunga ili kuigawa siku mbili kabla ya kupiga kura.
Hatutakubali haki za Watanzania kuchagua kiongozi bora ziondolewe kwa sababu ya kilo za sukari tunalishughulikia hili, alisisitiza kiongozi huyo wa timu ya kampeni za CUF Igunga.
Aidha, ameionya CCM kuacha mpango wa kutaka kugawa mahindi Septemba 30 na Oktoba mosi kwa wakazi wa jimbo hili kwa kuwa hiyo ni rushwa wanayoitoa kwa mgongo wa njaa.
CHANZO. GAZETI LA TANZANIA DAIMA