Dr. Slaa awatembelea Majeruhi wa Kijeshi

Dr. Slaa awatembelea Majeruhi wa Kijeshi

Dr. Slaa kabla ya kutafuta kuonekana anajali mashujaa wa Marekani alipaswa kufanya yafuatayo:

1. Kuhudhuria sherehe za kumbukumbu za mashujaa wa nchi yetu.

2. Kuhudhuria sherehe za kumbukumbu ya Uhuru wa nchi yetu.

3. Kutokuikejeli serikali ya Mwalimu Nyerere jinsi ilivyoheshimu mashujaa wetu.

Maswali yako yamejibiwa na narudia

1:Kuhudhuria kumbukumbu ya Mashujaa bila kufikiria namna ya kuwasaidia Mashujaa walioko hai tena wakiwa na ulemavu inasaidia nini?Ndiyo akili kubwa hiyo?
Ziara ya Dr.Slaa Hospitalini hapo kwa nafasi yake kama Chairman wa CCRBT kweli huoni fursa?

Hii ndiyo tofauti kati ya CHADEMA na Watawala walioshindwa.

Wasanii ni wale wanaohudhuria kumbukumbu za mashujaa kupiga picha kinafiki huku mashujaa waliobaki hai wakiteseka bila msaada wa Afya na huduma nyingine.Wanafiki hao utawaona wakienda misibani na nyuso za kinafiki na kung'ang'ania kupiga picha.Ubinadamu sijui uko wapi hapo.Unahitaji roho ya kishetani pekee kuweza ku-fit katika mazingira hayo

2:Kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika hakuna maana ikiwa mkoloni Mweusi amechukua nafasi ya mkoloni mweupe.Tutapambana hadi tupate uhuru kamili.Ndoto za Mababu zetu waliopigania uhuru hazijatimia kwani walioingia madarakani wamewasaliti.Kuna haja gani ya kuwa sehemu ya usaliti huo?

3😀r.Slaa hajamkejeli Nyerere badala yake waliomkejeli ni wale wanaokumbatia rushwa,waliopalilia pengo kati ya maskini na matajiri,waliouza nchi na hasa zie raslimali alizoacha kwa vizazi vijavyo,waliotelekeza mashujaa wetu bila huduma bora,walioasi azimio la Arusha .

Dr.Slaa anamuenzi Mwl.Nyerere kwa vitendo katika kupambana na maadui watatu MARADHI,UJINGA,UMASKINI na adui Mwingine aliyeongezeka UFISADI.

Hata wewe utakombolewa maana adui UJINGA anakusumbua sana.
 
Naona askari majeruhi wa wafadhili ni bora kuliko askari majeruhi wa Kitanzania kwa Slaa. Hapo hujagusia, umejaribu kupindisha lakini uelewe unaemjibu ni FF, huwa sipigwi chenga na msukule.
Utaalamu wa kuwahudumia mashujaa hao wa Marekani ndio unaohitajika hapa nyumbani.

Halafu chunga sana kauli zako,usipende kutusi watu kama huwezi kukabiliana na hoja just sign out.Be warned!
 
2:Kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika hakuna maana ikiwa mkoloni Mweusi amechukua nafasi ya mkoloni mweupe.Tutapambana hadi tupate uhuru kamili.Ndoto za Mababu zetu waliopigania uhuru hazijatimia kwani walioingia madarakani wamewasaliti.Kuna haja gani ya kuwa sehemu ya usaliti huo?

Ben,
Wewe ni kijana mdogo lakini unakoelekea hakufai. Ninashangaa kuona na wewe unaanza kuwa na elements za kiextremist za kusema Uhuru uliopatikana mwaka 1961 hauna thamani.

Hivi Ben, unadhani nchi hii isingekuwa huru ungepata fursa ya elimu uliyoipata? Unaelewa maana ya ukoloni?

Hizi kauli za kiextremist zifikirieni kwa umakini.

Watu kama Mzee Mtei wanajulikana kwanini hawauthamini Uhuru, lakini kijana kama wewe kuingia kwenye mkondo huo ni kukosa heshima kwa wapigania Uhuru.
 
Asante kwa ufafanuzi Ritz

Mzee Mtei alikacha kupigania Uhuru ndio maana anasympathise na watu wasiothamini Uhuru. Na hata chama chake anachokimiliki cha Chadema kinasema Tanzania haijapata Uhuru bado. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Mzee Mtei, Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla HAWAUTAMBUI Uhuru uliopokelewa na Nyerere mwaka 1961...

Uhuru upi ikiwa siku hizi kama ilivyokua enzi za Chifu Mangungo wa Msovero na Carl Peters JK anakumbatiwa na Obama na kusifiwa jwa kuuza raslimali za nchi kwa mikataba ya siri?

Uhuru Upi ambao Watanzania wanaufurahia ikiwa akina mama wanajifungua sakafuni,Ikiwa watoto wanakaa na kusoma chini ya miti?Ikiwa ajira nzuri wamepewa wageni na vijana wa kitanzania wanapewa ajira mbaya na wengi wao ni jobless then you still have temerity to call it eti "SHEREHE ZA UHURU" .

That is only reserved for fools!
 
Padri slaa yupo picknikn anatumia pesa za ruzuku za Cdm na mke wa Mtu kisha mnamlaumu kikwete anasafiri sana
 
Uhuru upi ikiwa siku hizi kama ilivyokua enzi za Chifu Mangungo wa Msovero na Carl Peters JK anakumbatiwa na Obama na kusifiwa jwa kuuza raslimali za nchi kwa mikataba ya siri?

Uhuru Upi ambao Watanzania wanaufurahia ikiwa akina mama wanajifungua sakafuni,Ikiwa watoto wanakaa na kusoma chini ya miti?Ikiwa ajira nzuri wamepewa wageni na vijana wa kitanzania wanapewa ajira mbaya na wengi wao ni jobless then you still have temerity to call it eti "SHEREHE ZA UHURU" .

That is only reserved for fools!

Kwahiyo sherehe za Uhuru ni kwajili ya fools. Sasa iwapo ndoto za Alinacha za Josephine Mushumbusi zikitimia na Chadema ikashinda Urais kutakuwa hakuna maadhimisho ya siku ya uhuru wa 9 Desemba?

Extremism is on the rise among Bavicha members!!!

Inabidi mjifunze kukomaa kisiasa na kutambua kwamba the fact kwamba mnaweza kuota kushinda Uchaguzi Mkuu ni matunda ya Uhuru.
 
Ben,
Wewe ni kijana mdogo lakini unakoelekea hakufai. Ninashangaa kuona na wewe unaanza kuwa na elements za kiextremist za kusema Uhuru uliopatikana mwaka 1961 hauna thamani.

Hivi Ben, unadhani nchi hii isingekuwa huru ungepata fursa ya elimu uliyoipata? Unaelewa maana ya ukoloni?

Hizi kauli za kiextremist zifikirieni kwa umakini.

Watu kama Mzee Mtei wanajulikana kwanini hawauthamini Uhuru, lakini kijana kama wewe kuingia kwenye mkondo huo ni kukosa heshima kwa wapigania Uhuru.
Sina mgogoro na mashujaa wetu waliopigania uhuru kwa kuwa walikua na ambition,walikua na ndoto ya kulikomboa taifa letu.Mababu zetu akina Mkwawa,Isike,Mirambo,Dossa Aziz,Sykes,Bibi Titi,Nyerere,Kambona,Kombo,Babu na wengineo wamesalitiwa.Watawala wanamuenzi Chifu Mangungo wa Msovero kama ilivyotokea juzi kwa JK badala ya kuwaenzi mashujaa niliowataja.Chief Mangungo ninaweza kumsamehe kwa kuwa hakuwahi kwenda shule tofauti na hawa machifu wa sasa hivi ambao naona ni majina tu yamebadilika kama Rais,Waziri badala ya Chifu.

I'm reclaiming our forefather's dream that's Pride,dignity and intergrity as a sovereign state.Wakoloni weusi waliopo mamlakani wamekua wabaya kuliko wakoloni weupe.Ni brokers katika ku-mortgage raslimali zetu kwa wakoloni wale weupe waliofukuzwa na mababu na mashujaa zetu.Ni madalali wa maisha ya wananchi wake wa sasa na hata vizazi vijavyo.Unataka nisherekee uhuru upi?I must be out of my mind.

Wako kama Nguruwe wanaotafuna watoto wao.Ni canibals

Usiniambie kuhusu Elimu,Kama wakoloni weupe walitoa Elimu pamoja na kuwa ilikua kwa maslahi yao kuna tofauti gani na watawala hawa na hata mentality unayoonyesha hapa kwamba kama msomi ni lazima niipigie magoti serikali?

Elimu niliyopewa haiwezi kunipa pride ikiwa walionizunguka wamekosa elimu hiyo au wana-hustle katika mazingira magumu.Nitakua msaliti mkubwa kujivunia elimu hiyo na kuwasifu wakoloni hawa weusi kuwa eti walinipa elimu.Hiyo ilikua haki yangu kwa kuwa walikusanya kodi ya watanzania na bado wakaendelea kuwanyima fursa watoto wengine wa kitanzania.Siwezi kukubaliana na hili hata kidogo

Hii haikua ndoto ya mababu zetu,haikua ndoto ya mashujaa wetu waliokuja kusalitiwa na weusi wenzao.We are reclaiming the dream.Second Liberation.Kama hii ni extremism let me be an extrimist square!
 
Uhuru upi ikiwa siku hizi kama ilivyokua enzi za Chifu Mangungo wa Msovero na Carl Peters JK anakumbatiwa na Obama na kusifiwa jwa kuuza raslimali za nchi kwa mikataba ya siri?

Uhuru Upi ambao Watanzania wanaufurahia ikiwa akina mama wanajifungua sakafuni,Ikiwa watoto wanakaa na kusoma chini ya miti?Ikiwa ajira nzuri wamepewa wageni na vijana wa kitanzania wanapewa ajira mbaya na wengi wao ni jobless then you still have temerity to call it eti "SHEREHE ZA UHURU" .

That is only reserved for fools!

OMG
ndo mnataka nchi huku mnatuita watanzania tunaosherekea siku ya uhuru fools!!
 
Dr.W.Slaa,

Punguza usanii hata siku mmoja umeshindwa kuhudhuria kumbukumbu ya mashujaa nchini kwako leo hii unajifanya unawanyenyekea wanajeshi wa Marekani.
Mkuu sio vizuri kumuumbua mzee wa watu,

Ameonyesha ana uchungu zaidi na wamarekani kuliko watanzania.
 
Olesaidimu,
Tumia akili uliyopewa bure na Mwenyeezi Mungu. Sikuenda Water Reed kufariji. Kufariji ni sehemu ya lazima ya mawasiliano Kati ya binadamu na binadamu. Water Reed ndiyo Hospitali kubwa ya kijeshi kwa Marekani yote. Inatumia teknolojia ya kisasa katika kutoa huduma ya matibabu. Inaona jinsi wapiganaji wao, miguu yote imekatwa lakini wanatumia miguu bandia kana kwamba hakuna kilichotokea. Ni binadamu wa ajabu tu atawaza Kama unavyowaza badala ya kujifunza teknolojia hiyo iwasaidie wapiganaji wetu. Dr Slaa siyo wa aina unayofikiri. Nenda CCBRT hospitali ambayo Dr Slaa ni mwanzilishi na Mwenyekiti uone huduma wanayopewa watanzania wenzako. Fikiria kabla hujatamka daima. Kuna taifa kufanya utafiti kabla ya kutoa tamko lolote. Nina hakika kwa kutembelea Water Reed Hoospital, Taifa letu litanufaika kwa kiwango kikubwa. Taifa linajengwa na watu wenye positive thinking. Watu wanaotafuta kila sekunde solutions kwa mazingira magumu yanayotukumba. Watanzania tushikamane, Hali yetu ngumu haitokani na maamuzi ya Mungu Bali ugumu wa mioyo yetu, above wa mipango yetu, kukosa vipau mbele. Fikiria wazee wetu wamepigania kukomboa Taifa letu toka Nduli Amini, Leo hawana miguu, wengine mikono, lakini wameachwa na kutelekezwa na Taifa walilotetea hata kwa kupoteza maisha Yao. Ushabiki hautufikishi mahali watanzania. Tulipokosea tukubali na turekebishe.

Kuna siku nilikua namuona ndugu yangu alikua anatibiwa pale CCBRT na alifuatwa mkoani kuja Dar akagharamiwa kila kitu na akatibiwa tatizo lake mpaka kupona na kurudishwa mkoani...
Siku hiyo nilimuona Dr Slaa akiongozana na Anna Makinda nadhani kulikua na adhimisho fulani nilifurahi sana tena saana...na hivi majuzi tuu ndugu zangu wengine wawili wameanza matibabu yao kwa matatizo yaliyowasumbua kwa miaka zaidi ya umri wangu na wanaendelea kutibiwa vizuri... Sina cha kuwapa ila nawaombea kwa Mungu awape kila lililo la kheri...
I call u Papa!
 
Kwahiyo sherehe za Uhuru ni kwajili ya fools. Sasa iwapo ndoto za Alinacha za Josephine Mushumbusi zikitimia na Chadema ikashinda Urais kutakuwa hakuna maadhimisho ya siku ya uhuru wa 9 Desemba?

Extremism is on the rise among Bavicha members!!!

Inabidi mjifunze kukomaa kisiasa na kutambua kwamba the fact kwamba mnaweza kuota kushinda Uchaguzi Mkuu ni matunda ya Uhuru.

Ni kwa ajili ya Fools ikiwa UJINGA,MARADHI,UMASKINI na sasa UFISADI umeongezeka katika mapambano yetu ambayo kipimo cha uhuru ilikua ni kuyashinda hayo.Wewe unaonaje?

Kama huwezi kuyatawala mazingira kama kipimo cha kwanza kabisa kama mwanadamu unajionaje?

Falsafa ya kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu,Ardhi yenye rutuba na Siasa safi ambayo katika taaluma yangu ya uchumi nikienda deep kabisa naona hii ya Mwisho ni derivative quantity maana hivyo vya viwili vya kwanza ni nguzo muhimu maana tunavyo,na leo hii hatuwezi kukamilisha definition kifilosofia,kinadharia na hata kwa vitendo unaweza vipi kujenga dhana ya vitu hivi viwili "Kusherehekea" na msamiati wa neno "UHURU"?
 
OMG
ndo mnataka nchi huku mnatuita watanzania tunaosherekea siku ya uhuru fools!!

Majibu niliyompa ZeMarcopolo yanakufaa wewe pia.Yasome na ujichagulie kundi.Utaishia kubaki katika kundi hilo peke yako.Watchout!
 
Last edited by a moderator:
Ni kwa ajili ya Fools ikiwa UJINGA,MARADHI,UMASKINI na sasa UFISADI umeongezeka katika mapambano yetu ambayo kipimo cha uhuru ilikua ni kuyashinda hayo.Wewe unaonaje?

Kama huwezi kuyatawala mazingira kama kipimo cha kwanza kabisa kama mwanadamu unajionaje?

Falsafa ya kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu,Ardhi yenye rutuba na Siasa safi ambayo katika taaluma yangu ya uchumi nikienda deep kabisa naona hii ya Mwisho ni derivative quantity maana hivyo vya viwili vya kwanza ni nguzo muhimu maana tunavyo,na leo hii hatuwezi kukamilisha definition kifilosofia,kinadharia na hata kwa vitendo unaweza vipi kujenga dhana ya vitu hivi viwili "Kusherehekea" na msamiati wa neno "UHURU"?

Ben,

Nimekuelewa vizuri. Kwahiyo hata kuruhusiwa kuanzisha chama cha Chadema na kushiriki uchaguzi kwenu mnaona sio jambo la manufaa. Hii kauli inatolewa na wewe kijana ambaye hujui maana ya ukoloni. Ndio tatizo ya elimu ya nadharia, umesoma historia kinadharia lakini umeshondwa kuelewa maana ya ukoloni na madhara yake.

Maneno yako haya nayaweka kwenye kumbukumbu.
Ni sahihi mtu kama wewe kuwa kwenye chama kinachomilikiwa na Mzee Mtei ambaye haoni thamani ya Uhuru.
 
Kwanini aende ubalozi wa kenya hapa.Mtu kwenda kutoa pole ,sio lazima aende muda huo huo.Watu wana programme zao mpaka zikiisha akiwa free ndio anaweka mikakati mingine.Hunafikiri Dr slaa ni kama Vasco da gama wako akisikia mtu kafiwa huko tandale ndani ghafula vasco da gama twende huko.anawapa tabu sana maafisa wa usalama wa taifa.anajifanya ana upendo.huo nasema ni upendo wa mshumaa tu.husiende kwenye msiba kuonyesha upendo.angalia kwa nini huyu mtu alikufa ili tafuta solution wengine wasife.sio kwenda kuuza sura kwake huyo vasco da gama wako.aibu sana huyo mkuu wako.

Unasemaje? watu wasife! watu wanatoa sadaka, na kufanya mema mengi ili baba awapokee wakifa, sasa itakuwaje kama hawatokufa??????!
 
mi nilijua amewatembelea mashujaa wa vita ya Kagera?
 
Ben,

Nimekuelewa vizuri. Kwahiyo hata kuruhusiwa kuanzisha chama cha Chadema na kushiriki uchaguzi kwenu mnaona sio jambo la manufaa. Hii kauli inatolewa na wewe kijana ambaye hujui maana ya ukoloni. Ndio tatizo ya elimu ya nadharia, umesoma historia kinadharia lakini umeshondwa kuelewa maana ya ukoloni na madhara yake.

Maneno yako haya nayaweka kwenye kumbukumbu.
Ni sahihi mtu kama wewe kuwa kwenye chama kinachomilikiwa na Mzee Mtei ambaye haoni thamani ya Uhuru.
Hata wakoloni weupe waliruhusu kuanzisha vyama vya upinzani ndiyo maana babu zetu kupitia TANU waliongoza vuguvugu la ukombozi wa kwanza.So nothing special

CHADEMA tunaongoza mapambano ya uhuru wa pili.

Utaweka kwenye kumbukumbu?Weka na nitayarudia hadi tupate uhuru wa pili.

Ukoloni maana yake ni.kutawaliwa kiuchumi,kijamii na Kisiasa.Uhuru maana yake ni kujitawala kiuchumi,kijamii na kisiasa na hii ndiyo ilikia ndoto ya uhuru ya mababu zetu na indicators za uhuru ilikua kushinda UJINGA(Kama huu unaokusumbua),UMASKINI Wa Mali na KIFIKRA(Kama Huu unaokusumbua na wenzako) na MARADHI.Hadi muda huu indicators hizi hazionyeshi uhuru na badala yake Maadui hawa wamezaa mtoto mwingine katika ukoo wa maadui hao UFISADI chini ya malezi ya wakoloni hawa weusi na wasaliti wakubwa wa Taifa hili.
 
Sawa,

Vijana extremist wa Bavicha endeleeni kupigania Uhuru wa nchi yenu. Nchi yetu sisi ilipata Uhuru mwaka 1961 na sasa tuko katika hatua ya kuijenga nchi.
 
Sawa,

Vijana extremist wa Bavicha endeleeni kupigania Uhuru wa nchi yenu. Nchi yetu sisi ilipata Uhuru mwaka 1961 na sasa tuko katika hatua ya kuijenga nchi.

Duuh,
Hii ni hatari kama mtu anajenga nchi kwa kutumia msingi wa tope na wakati huo akitegemea kuishi humo kufichama dhoruba kuu la kimbunga,mvua,mafuriko,tetemeko na tufani nyingine nyingi zitokeazo ktk ulimwengu huu na akitegemea usalama wa maisha yake kudumu kwa muda mrefu!!! Kweli nimeamini kwa vyovyote vile the house built on that kind of foundation could only be the house for "fools" to stay as it has been cited by Ben.
Ben, keep giving them civic education even if they strongly remain adamant cause they'll only be judged for their own foolishness and not otherwise.
Well articulated,I subscribe to what Ben utters provided the ideas are of objective truth so far.
 
Utaalamu wa kuwahudumia mashujaa hao wa Marekani ndio unaohitajika hapa nyumbani.

Halafu chunga sana kauli zako,usipende kutusi watu kama huwezi kukabiliana na hoja just sign out.Be warned!
Mpelekee bosi wako huu ujumbe

Najiuliza lakini nashindwa kuelewa kwa mtu mwenye PhD kama Dr Slaa kuonyesha unafiki wa hali ya juu kwa kujipendekeza kwa wanajeshi wa Marekani wakati huku nyumbani kila kukicha yeye ana ugomvi na majeshi ya Tanzania?

Dr Slaa anawachukia sana jeshi la polisi Tanzania (tayari ameishajenga chuki kubwa dhidi ya jeshi la polisi)

Dr Slaa analichukia jeshi la wananchi Tanzania (hata siku moja hajawahi kuwatembelea majeruhi wa kijeshi wa Tanzania au kuhudhuria sherehe yeyote ya kijeshi iwe ya Uhuru au mashujaa)

Dr Slaa anajua kabisakuwa ukiwa Rais ndio unakuwa amiri jeshi mkuu lakini yeye kama mgombea urais wa kudumu kwa tkt ya Chadema hata siku moja hajawahi hata kuwatembelea askari magereza kuona ni jinsi gani wanavyofanya kazi kwa bidii kutunza wahalifu na badala yake anajenga mazingira watu wafiukiri kuwa chadema ikichukua nchi hakutakuwa na magereza.

Huu ni unafiki na usaliti wa hali ya juu kwa mtu anaeutaka uraisi kwa nguvu zote kudharau majeshi ya nchi yake halafu leo anakwenda kupiga picha na majeshi ya kimarekani. Hii ni dharau kubwa kwa majeshi yetu tunayoyategemea kutulindia nchi yetu

Mimi natoa ushauri kwa Dr Slaa, ukirudi Dar tafadhali nenda pale Lugalo kuna wanajeshi wengi tu walioumia wakiwa kwenye kazi huko Sudan na wengine Congo. Pia ukisikia kuna mwanajeshi kafariki vitani uwe unakwenda kutoa pole au kuhudhuria mazishi laa sivyo hata ukifanikiwa ndoto yako utaishia kuwa kama Morsi tu wa Egypt.

JITAMBUE!
 
Back
Top Bottom