Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Pepsin,kuna mwingine eti yuko busy kumpa promo Fisadi Lowassa halafu eti mbunge anapigia CCM wengine nimewaona hawana maana kabisa.

Hivi wanafikiri bila Dr.Slaa huyo mgonjwa wao angepata wapi pa kukimbilia?Tunachohitaji ni kupigania tupate wabunge wengi huyo mgonjwa wao tumuache wampigie debe wenyewe.
 
Yaani ni aibu mkuu. Kwa kweli nikupongeze Tetty kwa uelewa na msimamo
 
Kwa staili hii ya kusaliti wapambanaji wa kweli....vijana wenye moyo hawatojitokeza kwa mfano huu mbovu uliooneshwa na baadhi ya vijana wa Chadema..... siamini kama walitumia akili zao zaidi ya kutumwa tu....
 
Hao ccm wamewezaje kumtusi na kumsifu kwa wakati mmoja mkuu emu fafanua?

CCM waliokatwa, namaanisha waliokaribishwa juzi CHADEMA ndio wanaomtusi Dr Slaa kwa kuwa wanajua Dr Slaa hataruhusu wao kujiendea kiholela. Wao wanatamani Dr Slaa aondoke ili wajiendee. Wanaomsifu ni CCM wanaotamani CHADEMA kigawanyike na kisiingie kwenye uchaguzi kikiwa na umoja na mshikamano. Kwao wanafanya Divide and Rule.
 
Mungu akulinde sana .
 
Hili kundi ni la ajabu kweli linatukana kila kiongozi wa Chadema anaehoji au kupingana na misimamo yao.

Ni kundi lenye nguvu na ushawishi mkubwa sana, na Vijana wa Chadema bila kujijua wamesombwa na mafuriko ya kundi hili kiasi cha kukashifu viongozi wao waliokuwa pamoja kwenye jua na mvua usiku na mchana.

Ni kundi lisilo na uchungu na Chama, lenyewe linawaza madaraka tu, halijui miiko, misingi, itakadi wala taratibu za Chama.

Ni kundi linalowaza madaraka tu, lina uchu na tamaa ya madaraka bila kujali yatapatikana kwa njia gani au kwa kumwathiri nani.

Halina msimamo, wala halijali kitu asubuhi litakusifia jioni litakuponda halina uvumilivu wa kisiasa.

Limeua slogan zote za CHADEMA , sasa hivi huwezi kusikia nguvu ya uma, M4C wala kukemea ufisadi ...... Hili kundi limeua slogan ya Chadema safari ya uhakika, sasa hivi wote tunaimbishwa safari ya matumaini Na Lowassa tu.

Muda sio mrefu tutaona rangi halisi ya kundi hili, wale waliosombwa na mafuriko ya kundi hili watajikuta wako kondeni mithili ya takataka zilizosombwa na maji... na maji yamekauka.

Nawaasa Team Lowasa japo mmekaribishwa mpaka Chumbani muwe na nidhamu kwa wenyeji wenu.!
 
Yaani ni aibu mkuu. Kwa kweli nikupongeze Tetty kwa uelewa na msimamo

Nadhani uongozi
Tunachotakwa niAh! Rafiki msimamo wangu ni makali nadhani kuliko Dr.Slaa na Mnyika.NitakuPm.
 
We gamba vipi.....tulihitaji sana hili kundi lije tuungane nalo
 
Dr. Slaa hawezi kukereka kwa hoja za kikindagateni kama hizi. heey!. tafuta hoja za kuongea hizi zko outdated mno. magamba yamepaliwa na mafuriko.
 
Kwa taarifa yao huyo Slaa ndio muhimili wa kweli wa cdm na alichokisimamia ndio kilichotufanya mpaka leo tuwe cdm. Wajua baada ya uchaguzi mkuu 2010 ndiye aliyetembea nchi nzima kujenga chama mpaka leo EL akaona ndio panapofaa kuja. Kuna vyama vingi mbona EL hakwenda chausta au tadea? Team EL msione vyaelea.
 
Chadema ilijengwa na Zitto Kabwe. Slaa alikuwa anasafiria nyota ya Zitto Kabwe..
 
Back
Top Bottom