Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,373
- 217,433
Wilbroad Slaa ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Chadema kabla ya kurejea CCM, ameisifu hotuba ya Tundu Lissu aliyoitoa Temeke huku akidai kwamba imegusa penyewe hasa.
Amedai kwamba kitendo cha Lissu kuzungumzia ugumu wa maisha na kupanda kwa bei za vyakula kwa kiwango cha kutisha kama bei za sasa ni jambo la muhimu sana , ambalo linagusa jamii yote ya Kitanzania wakiwemo Polisi , ambao amesema hawana masoko binafsi ya kununua mahitaji yao ya vyakula , bei ikipanda hata polisi wanasota , amesema kwamba bila wananchi kushiba huwezi kuwaeleza kuhusu SGR wala Madaraja maana hawatakuelewa .
Dr Slaa pia amesifu muunganiko wa Hotuba ya Lissu na Mbowe na hasa baada ya Mbowe kurudisha suala la Katiba kwa wananchi kwa kutaka wajiorodheshe kwa majina yao kwa kila mtaa .
Amesifu lugha iliyotumika kwenye Hotuba hiyo , akidai kwamba ni lugha ngumu ambayo ilibidi kutumika ili kufikisha ujumbe , japo amedai pamoja na ugumu wake hakuna maadili yaliyokiukwa
Kwa ujumla Dr Slaa ameona fyucha ya Chadema katika mtazamo Chanya , ambao anasema kuna dalili ya Chama hicho kutwaa madaraka 2025
TOA MAONI YAKO