Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Jamani jamani.mbona mnapost uongo? Docta slaa hajamkataza kagame kukutana na waasi. Docta kamwambia kikwete unawezaje kwenda kusema nchi nyingine udhaifu wa mwingine badala ya kwenda kumshauri live? Nimesoma hilo gazeti docta kamwambia kikwete, badala ya kulumbana hadharani ni vema wakakutana wao wenyew kwanza kumalza ugomvi wao ndipo wakakutane na waasi.huwez kukutana na mgomvi wako live bila kupatanishwa na wengine wa nje.
 
MziziMkavu naona umehamua kujichanganya kabisa yani title na habari ni kusi na kasi.

dr slaa amepinga mazungumzo na waasi maana ana wachukulia wauaji alaf wewe unaandika amewa kingia kifua. naona unaona ni bora kupotosha na huu ni zaidi ya ujinga wa kijinga.

Binafsi sioni ubaya wa ushauri wa jk na si kubaliani na matusi ya kagame dhidi ya jk na huyu kagame ni mjinga sana na hakukuwa na sababu za kujibiwa ni mtu aliyepaswa kupuuzwa.

nakushauri uache uzushi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita, huo ushauri umefika katika wakati muawafaka, Rwanda ni moja ya mataifa ambayo wapinzani wanaendesha harakati zao wakiwa nje ya nchi. Kila anaemkosoa Kagame asipokimbia nchi ataishia kuawa au kufungwa, dunia nzima imeshajua upuuzi unaoendelea Kigali. Nakumbuka mwaka 2000 spika wa bunge la rwanda Joseph Sebarenzi Kabuye aliwatahadhakisha akina Kagame na Bizimungu kuhusiana na genoside kutumika vibaya. Baada ya kutoa ushauri kama huo ilibidi ajiuzuru na uspikana akimbie nchi kuokoa maisha yake.

sASA ndugu Morinyo kama unafahamu kuwa wapinzani wote wa Kagame wako nje ya nchi, na hao FDLR wako misituni sasa Kikwete anawezaje kumshauri Kagame akazungumze nao? kundi la FDLR limeshatajwa kuwa ni kundi la kigaidi na ndivyo dunia inavyolitambua, sasa Kikwete anaanzaje kumshauri Kagame aafanye mazungumzo na magaidi? mbona asiishauri marekani kuingia kwenye meza ya mazungumzo na al qaeda? au ameshindwa nini kumshauri Kenyata aondoe majeshi yake somalia na kukaa na al shabab katika meza ya mazungumzo? Ushauri mwingine kabla hujaautoa ni vizuri ukajipima kwanza kama ungekuwa wewe ungeuchukuliaje.
 
Hao uliowapendekeza hawajui hata maana ya diplomasia, ni nani asiejua kuwa Dr Slaa ni mwanasiasa mbabe na jeuri?, ukimkabidhi hili sakata kikubwa atakacho fanya ni kuitisha vita tu kumbe room ya mazungumzo ipo wazi.

Kwakuwa Kikwete anaijua diplomasia ameshindwa nini kuzungumza na wananchi wa Mtwara na badala yake amewatumia batallion ya JWTZ inayowateka, kuwatesa, na kuwabaka wananchi wanaohoji juu ya rasilimali za gesi? hiyo diplomasia yenu ina makengeza?
 
===>> As of this moment, day... NAMTOA KABISA . SLAA ktk viongozi wenye uelewa na weledi na uzalendo wa nchi yangu....

===He can't differentiate among many things.... he is attacking JK personally na kuchanganya vitu hovyo hovyo.... he is poor analyst...

... hajui siasa za CHAMA NA CHAMA...NCHI YAKE NA NCHI ZA NJE... he is mixed up himself...with cdm politics (internal) na external politics hajui asumame wapi..... SLAA CHOCHOTE JK ASEME YEYE KUPINGA TU.... HATA RAIS ATUKANWE NA KUTISHIWA MAISHA...SLAA KAZI KUMPINGA JK TU....NA HATA KAFIKIA HATUA YA KUSEMA JK AOMBE MSAMAHA HUMU JF.....poor Slaa.... Josephine kakuharibu kwa tabia na umekuwa little minded... u can*t compete with anybody.... na usijaribu eti kuutaka Urais wa nchi yangu.... poor leader....

=== Sikujua utasema uongo hivyo eti JK hajawahi kukutana na wapinzani kuongea nanyi....

=== NIKUANIKE WW SLAA UNAZEEKA VIBAYA....WW NDIO ULIKUWA HUTAKI KATA KATA KUONANA NA JK.... nakumbuka hata siku ya KUAPISHWA JK UWANJA WA TAIFA ULISUSA....that time sijakuelewa...kumbe ww una uchu sana wa madaraka hadi umeusahau UZALENDO WA TANZANIA.....

===>> I declare HUFAI HATA KIDOGO WW....hv ulikuwaje padri na roho ya hivyo....

== Mungu wa ajabu kweli....HIVI WW NA JK nani aombe msamaha...¡¿¿¿ NILIFIKIRI UNGESEMA UMEKOSEA.....na kuomba radhi.... instead... ur useless kabisa....

====>> JK made a right decision..... go ahead achanana haka kazee .... Slaa ur brain is desintegrating rapidly.... take action...

===> Na koma kutufanya wapuuzi ukifikiri kila usemacho uko sahihi.... hufai -100%

Naungana na ww mkuu!!Katika majanga slaa nae ni janga lingine!
 
Kosa kubwa la Rais Kikwete ni kutamka maneno hayo hadharani angeweza kumwita kagame wakaongea naye badala ya kukimbilia kutoa matamko hadharani ni kama anamwona kagame hana akili

sure..
and from that point namuunga mkono dr slaa
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE
Kama DR. Kasema hivi basi mbombo jilipo na yeye sio kichwa tena kama tunavyodhani. No doubt his integrity should be in question, Kagame kasimamia miradi mikubwa ya Rehabilitation na kumaliza chuki miongoni mwa wahanga wa kimbari pamoja na kusamehena miongoni mwa wanyarwanda vipi yeye awezi zungumza nao wakati alishawishi wananchi kusamehe waliowaulia ndugu zao na kuganga yajayo.


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Jamani jamani.mbona mnapost uongo? Docta slaa hajamkataza kagame kukutana na waasi. Docta kamwambia kikwete unawezaje kwenda kusema nchi nyingine udhaifu wa mwingine badala ya kwenda kumshauri live? Nimesoma hilo gazeti docta kamwambia kikwete, badala ya kulumbana hadharani ni vema wakakutana wao wenyew kwanza kumalza ugomvi wao ndipo wakakutane na waasi.huwez kukutana na mgomvi wako live bila kupatanishwa na wengine wa nje.
Did you mean na yeye amalize kwanza na wachumba zake kabla ya kutatua matatizo ya watz. Jamani ndio tumefika hapa usirushe jiwe mpaka uwe msafi badi hatutakuwa na viongozi kamwe.


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.

STRATEGY FAILURE!
(We've just lost a Queen for our opponent's Pawn!)

Kweli kabisa tunawezavuna kura za watutsi, lakini tusishangae kupoteza kura nyingi zaidi za wanaokerwa na hila za watutsi,ambao ni wengi, kwenye mikoa ya maziwa makuu na kwingineko nchini! Mbinu ya 'ENEMY'S ENEMY IS A FRIEND' ina madhara yake, na hapa kwakweli Dr. Slaa katupaka matope!
Uongozi wa chama chetu uweke uzalendo mbele, kura zitafuata!
DAIMA, KWENYE 'SENSITIVE ISSUES' TAIFA LETU LIBAKI MOJA!
 
Hivi huyu Slaa ndo tunategemea aje eti ashike urais??? CDM kwa usawa huu watasubiri 50 years..this guy is not a presidential material...hii alioongea ni pumba at a higher level...CDM itabidi wajipange upya huyu hata udiwani hapati maana ni dhaifu kuliko udhaifu wenyewe...
 
Huwezi kutenganisha HELLEN KIJO BISIMBA na RWANDA na Vile vile huwezi kutenganisha huyu mama na SLAA , kwa hiyo siwezi kushangaa anamkosoa JK

Ndugu yangu usisukumwe na hisia kutoa maamuzi.
Ukisema Dr Hellen Kijo-Bisimba ni Mnyarwanda kwa kua tu anakosoa serikali unakuwa unasukumwa na hisia zaidi ya kufikiri.
Helleni Kijo ni Mtz kama alivyo Mtanz mwingine na wote wana haki ya kuikosoa Serikali wanapoona makosa, Hellen Kijo kukosoa Serikali hakumfanyi awe Mnywaranda, acha fikra potofu.
Dr Slaa kakosoa njia aloitumia Dr Kikwete kuishauri Rwanda na waasi lakini pia katoa ushauri, kuwa Dr Kikwete angemuita Kagame na Waasi alafu awapatanishe.

Sasa mara Hellen Kijo Bisimba na Dr Slaa mara na Rwanda yametoka wapi haya???

Dr Kikwete alitumia njia isiyo nzuri kutoa ushauri wake, japo Kagame hakutumia njia sahihi kumjibu pia Kikwete.
 
Jamani jamani.mbona mnapost uongo? Docta slaa hajamkataza kagame kukutana na waasi. Docta kamwambia kikwete unawezaje kwenda kusema nchi nyingine udhaifu wa mwingine badala ya kwenda kumshauri live? Nimesoma hilo gazeti docta kamwambia kikwete, badala ya kulumbana hadharani ni vema wakakutana wao wenyew kwanza kumalza ugomvi wao ndipo wakakutane na waasi.huwez kukutana na mgomvi wako live bila kupatanishwa na wengine wa nje.
Slaa ni mbea na mnafiki jk aliongea kwenye kikao halali na alitoa ushauri huo live sasa wewe unaongea utumbo gani.
 
Hili swala ni dogo sana, lakini kwa jinsi linavyomtikisa huyu Mheshimiwa Rais, kwa kweli nashindwa kuelewa! Kulikuwa hakuna sababu yeyote ya kujieleza kiasi hicho mbele ya taifa as if unajipendekeza kwa Kagame. Inasikitisha sana. Kagame is in frustration, wao na M7 wanakimbiakimbia tu hovyohovyo maporini huko, sasa hivi wamempata Uhuru wakumvuta masikio basi, wamepata jeuri ya kutishia watu. Yeye Kagame kam anauwezo adhubutu basi tumwone.

Rais alitakiwa amwite tu Kagame, akigoma, tuma watu wakazungumze basi! Rwanda hawana ujanja wowote kivita au kiintelligenisia kupambana na watanzania. Yaani we have so many options kuwa maliza bila hata kushika mtutu!!


Tatizo letu watz ni ccm basi!!

Na hii ndiyo LOGIC YA DR W.P. SLAA mkuu iwapo umemsoma kwa kina!..Tatizo ni moja tu kwa wana CCM wanaojipambanua kwa michango yao humu jamvini, ni kwa sababu tu hayo yamesemwa na Dr Slaa ambao kwao ni adui yao mkuu na kikwazo kikubwa kwao!!

Alichokifanya JK ni kosa tu la kiufundi kwani inawezekana nia yake ni njema (mimi sina hakika) hata kama ni kiongozi wa AU au SADC au EAC. Kamwe hawezi kuongea jambo lolote linalohusu Rwanda na Wanyarwanda na Kagame Rais wao kana kwamba anaongea na mkuu wake wa mkoa wa KIGOMA. Rwanda ni nchi huru ni lazima iheshimiwe hata kama ina matatizo yake kama hayo.Na wale wanaosema kuwa wanaweza kuipiga Rwanda kama upigavyo mwanao wa miaka mi5 ni KUJILISHA UPEPO TU kwani ukubwa wa pua si uwingi wa kamasi.....Hatujui wanawaunga mkono Rwanda ni kina nani.Na je, sisi tunawajua marafiki na maadui zetu??...JK kama kaamua kuwa mpatanishi,basi afanye hivyo kwa uwazi na kuyaheshimu makundi yote!!
 
Ndugu yangu usisukumwe na hisia kutoa maamuzi.
Ukisema Dr Hellen Kijo-Bisimba ni Mnyarwanda kwa kua tu anakosoa serikali unakuwa unasukumwa na hisia zaidi ya kufikiri.
Helleni Kijo ni Mtz kama alivyo Mtanz mwingine na wote wana haki ya kuikosoa Serikali wanapoona makosa, Hellen Kijo kukosoa Serikali hakumfanyi awe Mnywaranda, acha fikra potofu.
Dr Slaa kakosoa njia aloitumia Dr Kikwete kuishauri Rwanda na waasi lakini pia katoa ushauri, kuwa Dr Kikwete angemuita Kagame na Waasi alafu awapatanishe.

Sasa mara Hellen Kijo Bisimba na Dr Slaa mara na Rwanda yametoka wapi haya???

Dr Kikwete alitumia njia isiyo nzuri kutoa ushauri wake, japo Kagame hakutumia njia sahihi kumjibu pia Kikwete.
Mkuu huna akili ili rais aweze kuwaita viongozi wa nchi nyingine mpaka awe ameteuliwa kuwa mpatanishi wa kimataifa wa hilo swala vinginevyo awaite kirafiki,

kumbuka kile kilikuwa ni kiakao halali na ule mgogoro ilikuwa ni sehemu ya maswala yaliyokuwa mezani kwa maana ya mada mojawapo kwa nini useme kuwa jk alitoa ushauri mahala ambapo siyo sahihi,

halafu swala la helen kijo bisimba yule ni mburundi siyo mrwanda na anatumika hovyo na wanasiasa kwa kufanya anayofanya,huyu mama sijawahi kumsikia akitetea watu waliopatwa matatizo mpanga wawe ni wapinzani wa serikali.
 
Slaa yupo sahihi. Chadema mkuwaua kwa mabomu bunge linaendelea halafu leo mnawataka waoneshe utaifa¡ huo ni ujinga. Taifa limegawanyika kwa uovu wa ccm. Hongera slaa
 
Back
Top Bottom