Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 79
Kuhani, inabidi ujifunze kidogo juu ya elimu ya mapadre wakatoliki. Kabla hawajapata Udaktari huwa wamepitia miaka karibu saba ya digrii za kwanza. Falsafa inachukua miaka 2, na Theolojia inachukua miaka 4 (wanapomaliza kutegemea na upadre wao wa jimbo au utawa) wanapata elimu ambayo ni sawa na shahada, baadhi ya Seminari siku hizi wanakupa shahada kabisa. Padre wakikatoliki anapotoka Seminari huwa na angalau shahada moja.
Nikuoneshe kitu kwenye CV ya Dr. Slaa:
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE (ni certificate gani inachukua miaka mitatu)
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
Utaona kaingia seminari baada ya kidato cha sita na kutumia kuanzia 1972-1977 (miaka mitano) kusomea certificate. Wakati ule (na sitoshangaa hata sasa) mapadre wengi wa jimbo wakihitimu hawapewi shahada bali vyeti tu. Siku hizi hasa US na nchi nyingine wamebadili kwamba ukimalizia mwaka wa Falsafa unapata BA in Philosophy na ukienda Theolojia unaweza ukamaliza na MA.
Ni kwa sababu hiyo basi alipomaliza Seminari ya Juu aliweza kuapply kwenye Chuo cha Kipapa cha St. Urban mojawapo ya vyuo vikuu vya zamani zaidi duniani (est 1627). Ingawa hili ni off topic ni kuwa mojawapo ya matatizo ya mapadre au vijana walioacha seminari baadaya theolojia tu walijikuta hawana vyeti vya kuonesha kuwa wana digrii isipokuwa stashahada tu na wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwa wao kupata kazi "uraiani". Ndio maana wale ambao walipata nafasi ya kujiendeleza kwenye Vyuo Vikuu kama Dr. Slaa hupata heshima ya pekee kwani kama ni elimu wameisotea sana.
Hivyo utaona kuwa kuanzia 1972-1981 Dr. Slaa alikuwa anakula kitabu cha nguvu.. so ile miaka ya mwisho ya udaktari make sense...
Natumaini nitakuwa nimesaidia kidogo hapo.
Ahsante.
Kwa hiyo chuo cha Kipapa hakusomea sheria.
Maana CV inasema ana PhD ya Law.
Bachelors na Masters ya Sheria alizipatia wapi? Sidhani kama ni kwenye seminary za mikoani, kabla ya kwenda chuo cha "Kipapa."
(I wish you knew what that word means ukiwa viwanja ninavyo penda kutembelea Buguruni Sisiemu. Ushafika Buguruni CCM wewe? Kuna gambling spot moja kama Las Vegas. Mambo yose mumo!)