Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Nikiwa napitapita humu jamvini nimemuona Dr.Slaa akiwa anaendelea kusoma najua atakuwa mchangiaji muhimu sana kwetu .
Karibu Dr Slaa.
 
think BIG

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
236
30
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!

Makamba anatumia kweli internet?
wanaomjua na waseme
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,666
65,356
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!

Kwi kwi kwi, hata hoja zao zina fanana sana, ah! yote heri, kama kweli Doctor yupo jamvini basi naanza kuuona mwanga kwa mbaaali.
Karibu sana Kamanda, vita ndio imepamba moto.
 
Mgagagigikoko

JF-Expert Member
Jul 1, 2007
474
0
Nikiwa napitapita humu jamvini nimemuona Dr.Slaa akiwa anaendelea kusoma najua atakuwa mchangiaji muhimu sana kwetu .
Karibu Dr Slaa.[/QUOTE

Kwanini leo? waliopo hapa kumponda Wangwe ameona hawatoshi? inaonekana Wangwe alikuwa tishio sana mmemtoa huko kwa matusi kwenye vyombo vyote vya habari mnaona bado hadi JF.
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
885
Lakini si inawezekana kuwa ni guest siyo registered member? Anakuja huku kuongeza data na kupata maoni ya netizens wa Bongo!
Think Big: hii imenichekesha sana maana sipati picha... Makamba typing away furiously on the computer....kwikwikwi
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!
Kumbe ndo maana anapost propaganda zake alafu anaishia!
Dr Slaa karibu as guest or as registred member!
 
lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
574
nashukuru Wana Jf. Nchi Ni Yetu Tushirikiane Kuijenga.

Kalibu Mpiganaji Na Tutakupa Nondo Kibao. Hii Ndio Chemchem Ya Kila Kitu. Tunafikiri Utakuwa Mdomo Wetu Wa Kuwapasha Mafisadi. Kalibu Sana Shujaa
 
Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
50
Sijui niseme jina langu?Shida hamta niamini.Ila naunga mkono siku moja tuseme majina yetu mtashtuka.Wengine mtapata heart attack.
 
Dr Willibrod Slaa

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
675
1,522
Nawashukuru kwa sasa najiandaa kwenda Bungeni. Nondo ziwe na ukweli tena ukweli mtupu ili tuweze kuwanusuru vijana hadi vitukuu vyetu.
 
Mnyoofu

Senior Member
Feb 24, 2008
153
49
Mh Daktari

Nakupa changamoto...ukiwa kule seminari lazima ulipitia msemo huu wa kilatini: Vita vivenda non vitanda est! Haya ndio maisha aliyokuchagulia Mungu kuishi kwa wakati huu..watumikie wananchi wote bila woga, tuko pamoja, ukiwa na jambo unataka tukufanyie research tutakupa the whole of our dedication mpaka kieleweke! Its in our hands!

Karibu sana!
 
Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,019
9,220
Kama ni mgeni hapa namshauri kwamba kama ana mawazo kuwa JF ni club ya elites basi atakuwa amekosea njia. hapa ni mahala pa wote, wapo waliokwenda shule na wasiokwenda shule lakini wengi kama si wote ni WATANZANIA, hapa wapo wajenga hoja na pia wapo wapinga hoja lakini wengi kama si Wote ni WATANZANIA, wapo wanaofurahisha na wapo wanaokera, kwako wewe itategemea ni wepi hao si lazima wawe sawa na wa kwangu mimi lakini bottom line ni kwamba Wengi kama si wote Wote ni WATANZANIA. kiufupi hapa ni reflection ya jamii ndo maana pakaitwa jamiiforums, siyo club ya waliosoma peke yao, kwa hiyo ukiwa hapa dr itabidi ucheze namba zote, yaani ureflect jamii yetu, lakini kwa lengo la kuisukuma mbele

dr habari ndo hiyo!
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom