Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.


Hivi wale vijana viongozi wa CCM, akina Masha, Ngeleja, n.k., kwa nini wasijiunge hapa wakatetea chama na serikali yao? Wao si wamekuwa na kusoma kwa kutumia internet?

Mi nadhani kabla ya kuanza kutetea kitu ni lazima uwe na imani nacho tena imani ya kutosha. Hawa vijana wanajua kabisa hapa hakuna cha kutetea na wanakaa kimya kwa sababu hawapo katika siasa kwa maslahi ya mtu mwingine yeyote yule isipokuwa wao peke yao.
 
baada ya hapo itakuwa wabunge wote wajiandikishe humu, then wafanyakazi wote wa serikali, na mwisho wa siku sheria ya JF itabadilika na kuwa NI MARUFUKU KUTUMIA NICK NAME, kila member atumie jina lake halisi, namba na address! (just a day dream)

Mama,
sheria hiyo itakua haiwatendei haki Makamba types! Kwani hawajui kutumia kompyuta,hata TV zenyewe wanajua ku-switch On na Off tu.
 
Mheshimiwa Daktari Slaa... Kula Breki!!!

Pamoja na slur😀 zangu kule-Kula Breki!!!- Mapambano yanaendelea!

Karibu!
 
Dr. Slaa,

Karibu sana hapa jamvini.

Mkao wa hapa ni mkao wa Utaifa na Uzalendo wetu. Naamini utajisikia uko nyumbani na usiwe na hofu.

Kama Jmvi lnavyosema, leta ishu, kata ishu. Tumekaa na Zitto kwa miaka kadhaa, anatufahamu JF ni watu wa namna gani.

Nia yetu ni kuhakikisha kuwa Safari ya Mtanzania inapunguziwa vigingi na lile gurudumu la maendeleo linamaliza kupanda kilima na kuanza kuzunguka kwenye tambarare.

Jamvini tuna mitazamo tofauti, itikadi tofauti na mapenzi tofauti hasa katika siasa za Tanzania. Usihofu kero za Mchungaji kuhoji hoja na mwelekeo wa Chama chako, tupo hapa kujifunza na kujijenga.

Karibu tena, jisikie uko nyumbani. Nakuomba uwalete Jamvini wabunge wenzako wa pande zote, CCM, CUF, UDP na wanasiasa wote wengine.

Tupo hapa kulijenga na kulitetea Taifa na maslahi yake.
 
yokwenda.

Pamoja na kazi yote alifanya Mwalimu JK Nyerere, hawezi kabisa kukwepa lawana za kuwaacha kwa makusudi kabisa watanzania wengi wakiwa wajinga wasio na elimu wala uelewa wa jinsi nchi inavyoendeshwa. Lengo hasa lilikuwa ni kutoa mwanya wa kutawala kirahisi bila upinzani kutoka kwa watu wenye upeo. Tatizo hili limeendelea kutusumbua tangu uhuru na litaendelea kwa muda mrefu kuzingatiana na mazingira ya elimu nchini. This's probably the main drawback of Nyerere regime!

Pamoja na kwamba hatuzungumzii ujio wa Mwalimu kwenye Forum hii nimekereketwa kujibu hoja iliyotolewa kuhusu Mwalimu.
Hakuna drawback yoyote kwenye regime ya Mwalimu kuhusu elimu ya kujua nchi inavyoendeshwa. Tatizo halikuwa Mwalimu. Watu wenye upeo walikuwepo kutokana na kuelimishwa na Mwalimu huyohuyo. Tusisahau kwamba Mwalimu alikuwa akitimiza kwa dhati wajibu wake kwa wananchi aliokuwa akiwaongoza ndio maana baadhi yetu, ama babu zetu, kama sio baba zetu, shangazi zetu, wajomba zetu, kaka zetu, dada zetu, binamu, shemeji zetu n.k. walipewa elimu bure kabisaa. Bila shaka hawakuweza kuitumia elimu yao kudai haki ya kudai sababu waliridhika na jinsi Serikali ilivyowajali na kuwapatia elimu ya bure ambayo iliwanufaisha sana kimaisha. Kama hawakudai kupewa elimu ya kujua nchi inavyoendeshwa basi nahisi walifanya hivyo kama binadamu wenye shukrani walioridhika sana kwa waliyotendewa na Nyerere regime. Nadhani isingetolewa elimu ya bure iliyokuwa na manufaa wakati ule wengi wetu tusingelikuwemo kwenye mtandao huu! Tungelikuwa tukisaidiana na wananchi wenzetu ambao hawakubahatika kupata elimu wanaochunga ng'ombe na mbuzi ama kukwea minazi ama kutembeza mashati mitaani.
 
Dr. Slaa sina muda mrefu kwenye forum hii ingawa huko nyuma nilibahatika kuwa mwanachama wa forum kadha wa kadha ikiwemo Nyenzi.com

Kukukaribisha kwangu kuwakuwa ni kukupa changamoto wewe. chama chako na vyama vingine. Kwa mawazo yangu sidhani kwamba mnaweza kufua dafu mbele ya CCM katika chaguzi iwapo mtaendelea na mtindo wa kuibuibua issues tata kwenye vyombo vya habari mkitarajia kwamba wapiga kura wote watapata habari. Pia sidhani kwamba ikifika wakati wa chaguzi mtafanikiwa kuipiku CCM kwa kwenda kuwaambia wananchi kwamba tuliibua issue hii na hii wakati aidha mambo yatakuwa yameishapita ama CCM wameyazima kwa namna moja ama nyingine na kujikosha kwa wananchi kwa njia wanazozijua zitawalainisha wananchi.

Kwa hiyo basi, ili kuweza kupata utashi wa wananchi wapigakura ambao wengi wao wako vijijini na kama mna nia ya dhati kabisa ya kutaka kuikomboa nchi yetu kutokana na udhalimu wowote unaofanywa na CCM kama Serikali ama Chama Tawala yawapasa mkaze buti zenu. Unganeni na kuunganisha nguvu ili muweze kuwafikia wananchi na kuwaeleza kwamba mna nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo. Wananchi wanachotaka ni kuona hali zao zinakuwa nzuri siku hadi siku badala ya kurudi nyuma. Wananchi wanataka wapate matibabu wanayostahili kupata na si kusikia viongozi wao wanaenda kutibiwa nje kwa fedha za kodi zwanazotozwa wananchi wakati walipakodi wanakufa kila siku kwa maradhi ambayo yangeliweza kutibiwa iwapo Serikali ingelikuwa na mipango ya dhati inayojali maslahi ya wananchi.

Dr. Slaa, yapo mengi ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM kwa manufaa ya wachache badala ya wengi. Mkiwa 'vivuli' vya uongozi wa nchi hii jipangeni myashughulikie ipasavyo kama mnavyoyatamka kwa pamoja Bungeni mkiwa kambi ya upinzani bila kujali vyama mnavyotoka.

Naomba pia nijitambulishe kwamba mimi ni mkereketwa na mwenye imani kubwa na misingi aliyoiweka Baba wa Taifa katika kuitafutia maendeleo, amani na utulivu nchi yetu. Ukiwa unakubaliana na misingi hiyo hata kwa chembe tu na kuifanyia kazi ya ujenzi misingi hiyo utakuwa umelisaidia sana taifa letu.
 
Pamoja na kwamba hatuzungumzii ujio wa Mwalimu kwenye Forum hii nimekereketwa kujibu hoja iliyotolewa kuhusu Mwalimu.
Hakuna drawback yoyote kwenye regime ya Mwalimu kuhusu elimu ya kujua nchi inavyoendeshwa. Tatizo halikuwa Mwalimu. Watu wenye upeo walikuwepo kutokana na kuelimishwa na Mwalimu huyohuyo. Tusisahau kwamba Mwalimu alikuwa akitimiza kwa dhati wajibu wake kwa wananchi aliokuwa akiwaongoza ndio maana baadhi yetu, ama babu zetu, kama sio baba zetu, shangazi zetu, wajomba zetu, kaka zetu, dada zetu, binamu, shemeji zetu n.k. walipewa elimu bure kabisaa. Bila shaka hawakuweza kuitumia elimu yao kudai haki ya kudai sababu waliridhika na jinsi Serikali ilivyowajali na kuwapatia elimu ya bure ambayo iliwanufaisha sana kimaisha. Kama hawakudai kupewa elimu ya kujua nchi inavyoendeshwa basi nahisi walifanya hivyo kama binadamu wenye shukrani walioridhika sana kwa waliyotendewa na Nyerere regime. Nadhani isingetolewa elimu ya bure iliyokuwa na manufaa wakati ule wengi wetu tusingelikuwemo kwenye mtandao huu! Tungelikuwa tukisaidiana na wananchi wenzetu ambao hawakubahatika kupata elimu wanaochunga ng'ombe na mbuzi ama kukwea minazi ama kutembeza mashati mitaani.

Bibi Ntilie,

Wengi hawatambui sacrifice zilizofanywa kujenga Taifa hapa lilipo pamoja na Ulofa wake.

Kama isingekuwa hiyo elimu mbovu ya UPE na Watu wazima, Nusu ya Wachangiaji hapa tungekuwa vijijini tukiswaga Ng'ombe.

Ni elimu hiyo ya Bure kwa Taifa changa na masikini ndiyo iliyotupa Upevu na kuongezeka kwa Idadi wanaojua kusoma na kuandika nyakati hizo.

Kiwango chetu cha watu wasio wajinga kilikuwa ni kikubwa kuliko nchi tajiri au zile zilizokuwa huru kabla yetu.


Ndiyo tulilea umasikini kwa kutumia kila tulichopata ili watu wapate kujua kusoma na kuandika ili maarifa yalete juhudi kubwa.

Shukrani ya Punda ni mateke, Mwalimu alikubali hilo, kaondoka kwa Amani bado tunamsakama huku tunamiaka karibu kumitangu aondoke na sasa twaambiwa kuwa asilimia 31% ya Watanzania watu wazima wapiga kura hawajui Kusoma au Kuandika.

Je Miaka 10 baada ya Mwalimu Kufa bado ni kosa lake kuwa tumeendelea kuwa Wajinga?
 
Tunataraji mengi kutoka kwako kwani wewe ni mtu makini sana na zaidi ni miongoni mwa wazalendo wakubwa sana tulionao nchini. Tuko pamoja katika vita hivi dhidi ya ufisadi na mafisadi. Aluta continua
 
Nimefurahi kuwa Dr Slaa kujiunga JF, naona sasa tutapata first hand information
 
Tunawafahamu sana wanCCM humu. Wanaleta topic za kuchokonoa halafu wanakaa pembeni kuasikilizia.
 
Very true. In fact wanavuma, hasa kwa misimamo yao.

Kuna wana-CCM wengi sana humu wenye hoja zinazoenda pamoja na wapinzani kwa maslahi ya Taifa. Pia tupe tusio na vyama (Mushi tupo wote dogo). Tatizo la Tz ni kuamini kwamba bila CCM hatuwezi kufika ndiyo maana watu wengine ambao ni strong bado wanaendelea kuwa CCM ila wanamawazo ya kipinzani.

Kwa uhakika, wanaoichukia Serikali ya awamu ya nne si wapinzani peke yao wapo CCM wengi (hasa wasiounga mkono ufisadi).

Tupo wote, kisipendwe kitu (chama, nk) bali Tanzania.
 
Sidhani kama CCM bado wapo strong maana wameshamaliza sasa wameanza kulana wenyewe kwa wenyewe.
 
Nikiwa napitapita humu jamvini nimemuona Dr.Slaa akiwa anaendelea kusoma najua atakuwa mchangiaji muhimu sana kwetu .
Karibu Dr Slaa.

Lakini nani anaweza kuthibitisha kuwa huyo Dr. Wilbroad Slaa ndio yeye wa yule Dr. Slaa wa CHADEMA na Mbunge, Nahitaji mtu anisaidie kuhakikisha, asije akawa mtu amejipachika kam yule Bwana Mdogo alivyojipachikam kuwa yeye ndiye Invisible. Dr. Slaa anaweza akaja live KLH News na kuthibisha kuwa ndiye yeye hasa?
 
Sidhani kama CCM bado wapo strong maana wameshamaliza sasa wameanza kulana wenyewe kwa wenyewe.
Do. Kama CCM sio strong. Nani aliye strong. Nahakika CUF siyo kwani ni walegevu kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom