Kama ni mgeni hapa namshauri kwamba kama ana mawazo kuwa JF ni club ya elites basi atakuwa amekosea njia. hapa ni mahala pa wote, wapo waliokwenda shule na wasiokwenda shule lakini wengi kama si wote ni WATANZANIA, hapa wapo wajenga hoja na pia wapo wapinga hoja lakini wengi kama si Wote ni WATANZANIA, wapo wanaofurahisha na wapo wanaokera, kwako wewe itategemea ni wepi hao si lazima wawe sawa na wa kwangu mimi lakini bottom line ni kwamba Wengi kama si wote Wote ni WATANZANIA. kiufupi hapa ni reflection ya jamii ndo maana pakaitwa jamiiforums, siyo club ya waliosoma peke yao, kwa hiyo ukiwa hapa dr itabidi ucheze namba zote, yaani ureflect jamii yetu, lakini kwa lengo la kuisukuma mbele
dr habari ndo hiyo!