Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.
Sijui chadema ni ni hapa JF, kama vision na mission yetu ni kuokoa hii inchi kutokana na ufisadi Dr. Slaa amefanya mengi na makubwa kuliko yeyote. Only Nyerere ndo hajamzidi kutokana na viwango vyangu. Kama wewe unamtazamo tofauti better kukaa kimya kuliko kukurupuka. Huo ndo mchango wangu kwa Dr. Slaa. Mimi chama changu ni Mzalendo wa Tanzania. Chadema ndo nini kwanza? Nchi haijengwi na malaika, na nchi sio mawe. Kwani wanaomtukuza JK is people.

Naona una wivu. Dr. anaheshima ya kipekee katika jamii hii kama hutaki basi
 
Nipo na karibu na Dk Slaa hapa Bungeni, kwa kuwa amejiandikisha kwa jina lake halisi, sidhani kama anaweza kukataa akiulizwa iwapo amejiunga. Hivyo nitaenda akumuuliza na akionyesha hata mshangao mdogo, hata mimi nitaanza kuwa na mashaka iwapo kweli huyu ni Dr Slaa real

Facts are:

a. Jina la Dr Slaa Limesaliwa JF

b. Hakuna ushahidi wa kudhibitisha Kuwa Jina hilo na usajili huo kuwa umefanywa na Mwenye jina anayefahamika kama Mbunge wa Karatu.

c. Kwa hali ya "kawaida" hakuna namana ya "kujustfy" jina na mwenye jina.

Ok Na wewe Mpita njia, ukishamuuliza na kuongea naye ..na kupata conclusion utakayoipata etc..tutakuamini vipi kuwa umefanya hivyo?

Ushauri:

The best thing ni Kuwa Objective, kujali mada iliyopo na kuichangia honestly bila kujali jina la mtu.
 
Asante kwa mawazo yako yasiyojenga.Samahani kwa hili..Kwanini tumekuw awashabiki wa mambo??Hili ni tatizo kwa Watanzania na nahisi sasa kweli tumelogwa.

Mie nampa Hongera ila suala hili haliwezekani na namuomba Invisible aniunge Mkono katika hili.Wakati Mwamunyange alivyopandishwa Cheo kwa haraka watu walikuja juu hapa na mkapinga ila hili mnataka kulihalalisha?

Nyie ndiyo wa kwanza kupinga watu kupandishwa vyeo kwa suala la kujuana na umaarufu au Ukabila mlikuja juu ila hapa mnataka mtu apandishwe bila Vigezo vilivyoweka?

Kweli,Mpaka kieleweke mie nahisi ushabiki huu unaoufanya unasukumwa na kitu flani

Ngoja nidhibitishe kama Dr. Slaa
 
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!

Makamba anajua kweli mambo ya mtandao!!!!!!!HAHAHA
 
Huu ni UFISADI na USHAURI WA KIJINGA AMBAO SIJAWAHI KUUONA KATIKA KARNE HII.USHAURI WA KUWATUKUZA WATU..??na hii ndiyo sababu ya kuwa na mafisadi nchi hii.

Nyie ndiyo wa kwanza kupinga mambo kama haya leo mmeona kwa kuwa anatoka CHADEMA,apandishwe cheo.

Kitila,kuna maneno niliyaongea katika thread ya Wangwe...nadhani umeona ni watu wa namna gani niliokuwa nawazungumzia
 
Hata mzimu wa Mwalim Julius Kambarage Nyerere inasemekana upo ,na kinachochomshughulisha ni lini Watanzania kwa asilimia kubwa wataweza kuelimika kwa mtandao huu wa utandawazi. na hata ikiwezekana ziwepo sehemu huru ambazo zitamilikiwa na vyama vya upinzani kwa kila mkoa ili kuweza kuruhusu wananchi wa miji mikuu ya wilaya kuweza kupata na kujisomea moja kwa moja nakala zipatikanazo hapa JF.
Yaani kila wilaya iweze kutoa kituo kimoja cha kupata habari kupitia mitandao.Na hata kuruhusiwa kupata nakala za siri kwa kutoa ronyo ili waliko vijijini wapatiwe habari muhimu za yapitayo hapa Tanzania badala ya kungojea magazeti yenye habari za kufikirika.
 
Naomba niingili hapa mara moja.

a. Hakuna mwanachama ambaye atavushwa hapa kwa kuangalia jina lake au mchango wake mahali kwingine. Akija Kikwete, Salim, hata mmojawapo wa wa mitume watapanda daraja taratibu kama wengine walivyofanya. Hivyo hilo wazo la kurusha watu madaraja sidhani kama lina nafasi katika JF. Njia za kupata daraja ni pamoja na michango ya mtu, kuanzia ya mabandiko yake na ya kuiwezesha JF.

Dr. Slaa na wengine watapanda chati taratibu kwa kufuata njie ile ile waliyoifuata wengine. Hilo hata hivyo halina maana ya kumshusha hadhi au kumfanya duni bali ni kuonesha kuwa katika JF wanachama wote ni sawa.

Dr. Slaa amekuwa mwanachama hapa kwa muda mrefu na amekuwa akifuatilia kwa kina yanayosemwa hapa na sasa umefika wakati wa kujiunga tena rasmi. Note the word "tena". Alishajiunga hapa lakini alipoteza password yake na leo aliamua tu kujisajili upya.

b. Swali kwamba ni yeye hilo lisiwatie shaka na kuna watu wanaangalie nenno kama "nondo" jamani lugha hii wazee nayo wanayo. Nimewahi kumpigia simu Waziri Mmoja tuliposalimiana akaniambia mambo vipi nikasema "pouwa za huko" akaniambia "Pouwa tu". Sasa enzi zile ningeona anatumia neno la ajabu! Then akaja Bush.. guess aliwasiliamiaje watu "mambo!". Kwa hiyo, ameamua kuingia kwa jina lake ili kusiwe na utata wowote ule. Mojawapo ya vitu ambavyo tumekuwa tukivifanya ni kuona kuwa anapoingia mtu mwenye cheo fulani serikalini kwa jina lake tunacheki moja kwa moja na mtu huyo au wasaidizi wake wa karibu.

Miezi ka miwili iliyopita kuna mtu aliingia hapa na kujiandikisha kwa jina la Kikwete na kutoa speech moja ndefu sana. Mara moja tukazungumza na Ikulu (within minutes) na kukuta Rais alikuwa anauchapa usingizi na msaidizi wake akatuhakikishia kabisa aliyeandika siyo Rais na hakuna mtu aliyeidhinishwa kufanya hivyo. Well tukafuta na jamaa aliyeingia akafungiwa. So, kina invisible wanachukulia haya ya kutumia majina halisi very serious.

c. Kujiunga kwa Dr. Slaa rasmi ni mfano mwingine wa kuthubutu kwa viongozi wetu. JF siyo adui yao lakini ni mahali ambapo yote yanazungumzika. Dr. Slaa anajua kwa kutumia jina lake amejiweka kama swala kwenye mbuga iliyozungukwa na simba! Atapata personal attacks na vurugu mechi za kila aina. Hilo bila ya shaka litakuwa ni wimbi la kwanza na akisurvive basi sidhani kama kuna magumu mengine. Uamuzi wake uwe mfano kwa wabunge wengine kuungana nasi, wakijua wazi kuwa ni bora zaidi kuingia kwa majina ya kupachika kuliko majina halisi (ni distraction kubwa sana) kwani akimfokea mtu barabarani na mwana JF akikuona watakuandika humu! Ukionekana umeshikana mkono na mtu basi jina lako litatangaa. Ndio maana kutumia majina halisi kunapoteza sana hoja muhimu. Hata hivyo mtu akishapima pro and cons kwa upande wake binafsi basi afanye kila anachotaka. Hivyo tunawakaribisha wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu waidara n.k kuungana nasi kwani hapa ndiyo Jamii Forums.. where we dare talk openly!!! Hapendwi mtu, haogopwi mtu, na hapendelewi mtu.
 
Mh Daktari

Nakupa changamoto...ukiwa kule seminari lazima ulipitia msemo huu wa kilatini: Vita vivenda non vitanda est! Haya ndio maisha aliyokuchagulia Mungu kuishi kwa wakati huu..watumikie wananchi wote bila woga, tuko pamoja, ukiwa na jambo unataka tukufanyie research tutakupa the whole of our dedication mpaka kieleweke! Its in our hands!

Karibu sana!

Comments ni nyingi zenye sura mbalimbali ila hii imenigusa zaidi.
Asante mkuu - mfano wako ni wa kuigwa.

.
 
Haya amwage mambo...Kwani lugha zao sasa tunazijua sana tu.
Tunamkaribisha aweke mambo hapa tuendelee kukata issue bila woga!
 
Naomba niingili hapa mara moja.

a. Hakuna mwanachama ambaye atavushwa hapa kwa kuangalia jina lake au mchango wake mahali kwingine. Akija Kikwete, Salim, hata mmojawapo wa wa mitume watapanda daraja taratibu kama wengine walivyofanya. Hivyo hilo wazo la kurusha watu madaraja sidhani kama lina nafasi katika JF. Njia za kupata daraja ni pamoja na michango ya mtu, kuanzia ya mabandiko yake na ya kuiwezesha JF.

Dr. Slaa na wengine watapanda chati taratibu kwa kufuata njie ile ile waliyoifuata wengine. Hilo hata hivyo halina maana ya kumshusha hadhi au kumfanya duni bali ni kuonesha kuwa katika JF wanachama wote ni sawa.

Dr. Slaa amekuwa mwanachama hapa kwa muda mrefu na amekuwa akifuatilia kwa kina yanayosemwa hapa na sasa umefika wakati wa kujiunga tena rasmi. Note the word "tena". Alishajiunga hapa lakini alipoteza password yake na leo aliamua tu kujisajili upya.

b. Swali kwamba ni yeye hilo lisiwatie shaka na kuna watu wanaangalie nenno kama "nondo" jamani lugha hii wazee nayo wanayo. Nimewahi kumpigia simu Waziri Mmoja tuliposalimiana akaniambia mambo vipi nikasema "pouwa za huko" akaniambia "Pouwa tu". Sasa enzi zile ningeona anatumia neno la ajabu! Then akaja Bush.. guess aliwasiliamiaje watu "mambo!". Kwa hiyo, ameamua kuingia kwa jina lake ili kusiwe na utata wowote ule. Mojawapo ya vitu ambavyo tumekuwa tukivifanya ni kuona kuwa anapoingia mtu mwenye cheo fulani serikalini kwa jina lake tunacheki moja kwa moja na mtu huyo au wasaidizi wake wa karibu.

Miezi ka miwili iliyopita kuna mtu aliingia hapa na kujiandikisha kwa jina la Kikwete na kutoa speech moja ndefu sana. Mara moja tukazungumza na Ikulu (within minutes) na kukuta Rais alikuwa anauchapa usingizi na msaidizi wake akatuhakikishia kabisa aliyeandika siyo Rais na hakuna mtu aliyeidhinishwa kufanya hivyo. Well tukafuta na jamaa aliyeingia akafungiwa. So, kina invisible wanachukulia haya ya kutumia majina halisi very serious.

c. Kujiunga kwa Dr. Slaa rasmi ni mfano mwingine wa kuthubutu kwa viongozi wetu. JF siyo adui yao lakini ni mahali ambapo yote yanazungumzika. Dr. Slaa anajua kwa kutumia jina lake amejiweka kama swala kwenye mbuga iliyozungukwa na simba! Atapata personal attacks na vurugu mechi za kila aina. Hilo bila ya shaka litakuwa ni wimbi la kwanza na akisurvive basi sidhani kama kuna magumu mengine. Uamuzi wake uwe mfano kwa wabunge wengine kuungana nasi, wakijua wazi kuwa ni bora zaidi kuingia kwa majina ya kupachika kuliko majina halisi (ni distraction kubwa sana) kwani akimfokea mtu barabarani na mwana JF akikuona watakuandika humu! Ukionekana umeshikana mkono na mtu basi jina lako litatangaa. Ndio maana kutumia majina halisi kunapoteza sana hoja muhimu. Hata hivyo mtu akishapima pro and cons kwa upande wake binafsi basi afanye kila anachotaka. Hivyo tunawakaribisha wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu waidara n.k kuungana nasi kwani hapa ndiyo Jamii Forums.. where we dare talk openly!!! Hapendwi mtu, haogopwi mtu, na hapendelewi mtu.

kabisa hasa ikizingatiwa jf hatushabikii chama chochote cha Siasa ila tunajalii tu maslahi ya taifa ambayo yapo mikononi mwa wachache
 
Ni yeye na nimempigia simu na akaniambia kuwa ni yeye hivyo shaka ondoeni na kasema akitoka bungeni jioni basi atakuwa anatoa nondo hapa .

Naomba namba yake nithibitishe, nitumie kwenye pm kama hapa haipendezi,lakini amekuwa akitumia JF kwa muda mrefu kutafuta hoja au alikuwa akiprintiwa tu?
 
a. Hakuna mwanachama ambaye atavushwa hapa kwa kuangalia jina lake au mchango wake mahali kwingine. Akija Kikwete, Salim, hata mmojawapo wa wa mitume watapanda daraja taratibu kama wengine walivyofanya. Hivyo hilo wazo la kurusha watu madaraja sidhani kama lina nafasi katika JF. Njia za kupata daraja ni pamoja na michango ya mtu, kuanzia ya mabandiko yake na ya kuiwezesha JF.
Mhh nilijua tu....Mwkjj kiongozi humu....

Mojawapo ya vitu ambavyo tumekuwa tukivifanya ni kuona kuwa anapoingia mtu mwenye cheo fulani serikalini kwa jina lake tunacheki moja kwa moja na mtu huyo au wasaidizi wake wa karibu.
haya sasa.....

Miezi ka miwili iliyopita kuna mtu aliingia hapa na kujiandikisha kwa jina la Kikwete na kutoa speech moja ndefu sana. Mara moja tukazungumza na Ikulu (within minutes) na kukuta Rais alikuwa anauchapa usingizi na msaidizi wake akatuhakikishia kabisa aliyeandika siyo Rais na hakuna mtu aliyeidhinishwa kufanya hivyo. Well tukafuta na jamaa aliyeingia akafungiwa. So, kina invisible wanachukulia haya ya kutumia majina halisi very serious.
ndio mzee......
 
Mhh nilijua tu....Mwkjj kiongozi humu....

haya sasa.....

ndio mzee......

ungesema Mwkjj ni mwanachama humu.... niliye mstari wa mbele kuhakikisha JF inaendelea kusimama kama chombo huru cha kuwakilisha mawazo na maslahi ya Watanzania wote. Sorry to disappoint you, siyo kiongozi mimi. Mwanachama niliye na kimbelembele ya kulinda hii tunu iitwayo JF.
 
Naomba niingili hapa mara moja.

a. Hakuna mwanachama ambaye atavushwa hapa kwa kuangalia jina lake au mchango wake mahali kwingine. Akija Kikwete, Salim, hata mmojawapo wa wa mitume watapanda daraja taratibu kama wengine walivyofanya. Hivyo hilo wazo la kurusha watu madaraja sidhani kama lina nafasi katika JF. Njia za kupata daraja ni pamoja na michango ya mtu, kuanzia ya mabandiko yake na ya kuiwezesha JF.

Sikuona cha ajabu kushawishi ID ya Dr. W.Slaa kupewa rangi tofauti kwa mfano, kama heshima maana hiki sio cheo. Kama huo hapo juu ni msimamo au utaratibu wa JamiiForums ambao ushatolewa maamuzi kabla ni sawasawa pia.

b. Swali kwamba ni yeye hilo lisiwatie shaka na kuna watu wanaangalie nenno kama "nondo" jamani lugha hii wazee nayo wanayo. Nimewahi kumpigia simu Waziri Mmoja tuliposalimiana akaniambia mambo vipi nikasema "pouwa za huko" akaniambia "Pouwa tu". Sasa enzi zile ningeona anatumia neno la ajabu!

Nimefurahishwa na wale waliohoji. It is good to question even the minute details katika article yeyote itakayolewa humu JF.

.
 
i HONOUR AND SALUTE YOU DR. IN A COMRADELY SENSE OF THE RESPECT I HAVE FOR YOU, BUT MOST IMPORTANTLY, YOUR STYLE IN DELIVERING POSITIVE END RESULTS
 
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!

Ha! ha! haaa! Siku ukimuona Makamba, fahamu pembeni yake kuna mtu anamsaidia kugusa keyboard. Hawa ni watu ambao hata siku moja utawasikia wakifanya reference kwa mtandao.

Wao kila wakati utawasikia wakisema, magazeti magazeti magazeti. Ndo maana hawawezi kuelimika maana wanasubiri sisi tuwaambie tuliyoona juzi maana ya leo bado ni ya kwetu.
 
Kuna mtu yeyote ana BIO ya DR Slaa,nataka kumjua huyu mpiganaji maana namsikia tuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom