BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,337
Nikiwa napitapita humu jamvini nimemuona Dr.Slaa akiwa anaendelea kusoma najua atakuwa mchangiaji muhimu sana kwetu .
Karibu Dr Slaa.
Karibu sana Dk Slaa shujaa wa Watanzania katika kupambana na ufisadi ndani ya nchi yetu. Tunathamini sana juhudi zako na mchango wako katika kupambana na mafisadi wanoiangamiza Tanzania. Watanzania wengi tuko bega kwa bega nawe katika vita hii. Na wengi tunaamini kwamba tutashinda maana haki iko upande wetu na dhuluma iko upande wa mafisadi.
Uwe muangalifu mno katika nyendo zako za kila siku, sehemu unazokula n.k. maana mafisadi wanaweza kukudhuru kwa lolote na Mwenyezi Mungu atakulinda.
Mungu ibariki Tanzania