Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Dr. Slaa yupo sahihi kabisa kusema kuwa hana imani na jeshi la police. Sababu zipo nyingi sana ila ipo moja inayomhusu
yeye binafsi. Alipokuwa mbunge aliwekewa vinasa sauti chumbani kwake(na usalama wa Taifa ah,sorry I mean usalama wa viongozi na walala heri wa Tanzania). Baada ya sakata hilo, jeshi la police lilifanya uchunguzi. Cha ajabu ni kuwa mpaka leo jeshi la police halijawahi kutoa matokeo ya uchuguzi waliofanya.

Naturally nadhani hawawezi kujichunguza wao wenyewe na kutoa taarifa inayowahusu wao wenyewe. Kwa maana hiyo Dr. Slaa hata kama angekuwa na uwendawazi nusu sio rahisi kuwa na imani na jeshi la polisi.

I salute this guy Dr. Slaa, the fella is so smart and I am glad I voted for him in 2010-
 
Umeona eeeh, halafu juu huko post #167 nimeweka picha, kamuomba Rais wa hiyo Serikali asiyokuwa na imani nayo akaongoze matembezi ya kumchangishia fedha za kazini kwake. Isitoshe, "sponsor" mkuu wa hayo matembezi ni Rostam Aziz kupitia kampuni yake ya Vodacom.
Hela anazokopa zinaenda wapi? Kutoka deni 0 2005 mpaka trilioni 23 mwaka 2012 kwi! Kwi! Kwi! Eti anagawa hela kupitia ule mtindo wa mabilioni ya jk
 
mie mrombo!
Mrombo gani unasema eti "ndizi zilizooza" na unashangaa utumbo, we utakuwa mswahili wewe.Na ukitaka kuanza mambo ya stereo type, utajikuta na wewe unatoka nishai...
 
Ocampo alikwishaondoka!

wakuu, ocampo ameshasepa ile nafasi. sasa yupo mama fatou bensouda kutoka gambia. juzi juzi nae kaanza makeke yake kwa kwenda libya kucheki muamar qadafi mambo yake ilikuwaje kule?
 
Matusi ni ushahidi wa upunguani
mbona ninyi huwa mkitukana humu nanyi ni punguani? Mimi sioni mantiki ya Slaa kukataa kuhojiwa na kutaka polisi waende mahakani huko ndio akaseme, sasa hao polisi wataendaje mahakamani bila maelezo ya kufungulia mashtaka! Dr Slaa hana cha kuiogopa serikali ya JK na ni kweli serikali hii haina uwezo wa kumlazimisha, basi aende ili kuwasadikisha wafuasi wake kuwa alichosema ni kweli!
 
Akitaka atake asitake atahojiwa tu, hao vibaraka zake wa nchi za nje walio mwambia alete uzabi zabina wa maneno ya uwongo waje wamsaidie, kwani kwa hili hatoki hata chembe.

Chezea kitu kingine wewe sio chadema, wajaribu Waone pale ni full ushahidi.
 
Wamkumbuka mkurugenzi wa makosa ya jinai inchin (Dci) Robert Manumba? Alisema Dk. Mwakyembe hakupewa sumu! Ali muhoji pia Mh.Sita lakini hakuna kitu.Unafikiri kuna jipya kwa dk Slaa!.Tuwe na kumbukumbu jamani!
 
Amesema wapeleke kesi mahakamani ili yeye akatoe ushahidi mbele ya mahakama. Inaonekana anataka kumwaga mchele kwenye kuku wengi. Bila shaka ana ushahidi wa kutosha. Lakini hata hivyo sidhani kama hiyo kauli yake itafanya kazi, maana Nchimbi amesema suala la ulinzi wa mtu si la hiari, serikali inaweza kutumia nguvu kumpa ulinzi au kumlazimisha aisaidie polisi kulichunguza jambo hilo. Nafikiri siasa za bongo zimefika pazuri. Kama serikali ingeamua kujikausha na kujifanya haijasikia, ingeweza kulimaliza jambo hili kirahisi sana, lakini ikishaanzisha malumbano tu, ndo itajiweka kwenye wakati mgumu zaidi.

mkuu, hapa inaonesha dr atakataaa kataaaa! ila lazma ataenda kuojiwa kwa njia yoyote ile! au unaonaje?
 
wana jf makini jiadharini na mamluki.Humu kuna mapandikizi ya Magamba club wanajifanya kukandia kila point inayo wahusu viongozi wajao wa tz kuanzia 2015.kila ukisema dr.silaa wanakaba na kuponda ili kuwakatishaa tamaa wana jf makini.kuweni makini hamko peke yenu
 
wana jf makini jiadharini na mamluki.Humu kuna mapandikizi ya Magamba club wanajifanya kukandia kila point inayo wahusu viongozi wajao wa tz kuanzia 2015.kila ukisema dr.silaa wanakaba na kuponda ili kuwakatishaa tamaa wana jf makini.kuweni makini hamko peke yenu

Kijana hujiamini inaonekana au unataka kuwa yaya wa Juniour
 
Back
Top Bottom