Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

mbona ninyi huwa mkitukana humu nanyi ni punguani? Mimi sioni mantiki ya Slaa kukataa kuhojiwa na kutaka polisi waende mahakani huko ndio akaseme, sasa hao polisi wataendaje mahakamani bila maelezo ya kufungulia mashtaka! Dr Slaa hana cha kuiogopa serikali ya JK na ni kweli serikali hii haina uwezo wa kumlazimisha, basi aende ili kuwasadikisha wafuasi wake kuwa alichosema ni kweli!

Endelea kutapatapa
 
Sikiliza mheshimiwa,

Swala la Dr.Slaa au viongozi wengine wa CDM au mtu mwingine yeyote kuwapa Polisi sijui point ya kuanzia is IMMATERIAL! Hawa watu(Polisi) ni trained professionally kwenye fani hiyo ya Upolisi na wanajua kazi yao.Kwa hiyo ni wajibu wao kuanza kutafuta na kuchunguza ukweli wa tuhuma zinazopelekwa kwaobila ya kuanza kuwabughuzi walewale wanaotoa tuhuma zile.

Kama Dr.Slaa ameshasema kuwa nyumba ya Polisi inavuja means OFISI YA POLISI INATOA SIRI ZAKE NJE ni taarifa tosha kabisa kwa Polisi kujua pa kuanzia.Kuwa kuna wenzao ndani ya Jeshi la Polisi wanatoa siri za mipango yote inayopangwa kuhusu kuwateka,kuwanyanyasa,kwadhuru na hatimaye kuwaua viongozi na wanachama wa Vyama vya Upinzani simply because wanaikosoa na kuisahihisha serikali ya CCM iliyoko madarakani! Katika nchi yenye Demokrasia ya Vyama vingi hili jambo kamwe halikubaliki!

Polisi waanzie ndani ya nyumba yao kujichunguza na kujisafisha kabla hawajatoka nje kuanza kusumbua raia.Vinginevo watuambie kuwa kazi ya Upolisi imewashinda kwa kundekeza kutetea,kulinda na kudumisha sera za Chama Cha Mabwepande-CCM.
Tuko pamoja mkuu ila ninachofikiri mimi ni kuwa kuna busara katika kuwa tayari kutoa maelezo kama polisi watahitaji. kwa hiyo CDM and Dr Slaa wawe tayari kwa kuwa polisi wanayo haki ya kisheria ya kumhoji yeyote yule, akiwemo Dr Slaa, Lema, nk; ila ni kweli pia kuwa polisi wanao uwezo wa kupata information kwa kutumia "intelegensia" yao.

Pamoja sana mkuu!
 
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgombea wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alichodai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.
Ni hayo tu.

Sawa Slaa, tunakuunga mkono baba, hii serikali ya kiuaji hatuna imani nayo tena. Wakaojiane wenyewe
 
Tuko pamoja mkuu ila ninachofikiri mimi ni kuwa kuna busara katika kuwa tayari kutoa maelezo kama polisi watahitaji. kwa hiyo CDM and Dr Slaa wawe tayari kwa kuwa polisi wanayo haki ya kisheria ya kumhoji yeyote yule, akiwemo Dr Slaa, Lema, nk; ila ni kweli pia kuwa polisi wanao uwezo wa kupata information kwa kutumia "intelegensia" yao.

Pamoja sana mkuu!

Msengapavi,

Hebu jaribu kuvaa viatu vya Dr.Slaa au Mnyika. Kwamba wewe umetishiwa maisha na Polisi kuwa wana mpango wa kukudhuru au kukuua na aliyekupa info hiyo ni mmoja wa polisi(anaweza kuwa rafiki yako au ndugu yako) amabye alihudhuria kikao kile na hafurahishwi na mipango hiyo ya kutaka kukudhuru.Je,ungelikuwa tayari wakuchukue kwa mahojiano?

Kwa sasa tuna matukio kadhaa yaliyotokea yanayohusishwa na Polisi likiwemo hili la juzi la Dr.Ulimboka. Mpaka leo hii ni week ya 2 Polisi haijakamata hata mtu mmoja wa kutiliwa shaka kuhusiana na tukio hilo!!!!?????!!!Kuna tukio la Wabunge 2 wa CHADEMA kukatwakatwa na mapanga mbele ya Polisi na mpaka leo ni miezi zaidi ya 5 hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo!!!???

What kind of a Police Force do we have in this country???Mtu yeyote makini anajua kabisa kuwa haya matukio YANA RATIBIWA NA JESHI LA POLISI NA USALAMA WA TAIFA!!!Huu ni ukweli ambao Polisi hawawezi kuukataa.

Rais Joyce Banda wa Malawi baada ya kuapishwa kuwa Rais kufuatia kifo cha Rais Bingu wa Mutharika KITU CHA KWANZA ILIKUWA NI KUMFUKUZA IGP(MKUU WA POLISI) na kuli-overhaul Jeshi lote la Polisi nchini Malawi kwa mambo kijinga yaliyokuwa yakifanywa na Jeshi hilo wakti wa Mutharika,ikiwemo kuua raia na wapinzani waliokuwa wakiikosoa serikali ya marehemu Bingu wa Mutharika. Hicho ndicho kitakachotokea siku moja hapa Tanzania pale uongozi DHALIMU WA CCM utakapo ondoka madarakani hivi karibuni.
 
[h=2]
Dk.+Peter+Slaa+(wa+kwanza+kulia)+akizungumza+na+wanahabari+leo+makao+makuu+ya+chama+hicho.JPG
[/h]


Na Ninaeli Masaki



11th July 2012




Asema washughulike na kesi za zamani kwanza
Aeleza kuwa Kamati Kuu imelaani vitisho kwao




Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amesema hatakwenda polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano kwa sababu Jeshi hilo limekuwa na desturi ya kumfanyia mahojiano katika matukio mbalimbali, lakini hawayafanyii kazi.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo kufuatia agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alilotoa kwa Jeshi la Polisi juzi la kuwahoji viongozi wote wa Chadema waliosema wanatishiwa maisha na vyombo vya usalama.

Katibu Mkuu huyo alirejea matukio mbalimbali yaliyotokea kipindi cha nyuma likiwemo lile la Aprili mwaka huu katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kirumba, ambapo wabunge wawili wa chama hicho mkoani Mwanza, Highness Kiwia (Ilemela) na Salvatory Machemli (Ukerewe), walivamiwa na kushambuliwa na mapanga na watu waliosadikika kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema jana asubuhi alipokea simu kutoka makao makuu ya jeshi hilo iliyomtaka kufika polisi ili kufanyiwa mahojiano, lakini alisema hayupo tayari kufanyiwa mahojiano mengine mpaka pale watakapofanyia kazi yale ambayo walishawahoji katika kipindi kilichopita.

"Ofisa mmoja wa makao makuu ya polisi alinipigia simu leo asubuhi (jana) akinitaka niende polisi, lakini nimekataa. Siwezi kwenda kwa sababu yapo mahojiano mengi ambayo walinifanyia baada ya matukio kadhaa yaliyohusisha chama chetu kutokea na hawajayafanyia kazi, wayashughulikie hayo kwanza," alisema Dk. Slaa.

Aidha, Dk. Slaa ameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa taarifa ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutishiwa maisha na vyombo vya usalama badala ya kutafuta kujua aliyetoa taarifa hiyo.

“Kazi ya serikali na vyombo vya usalama ni kulinda amani, walichotakiwa kufanya mara tu baada ya kupata taarifa hizi ni kufanya uchunguzi ili kupata ukweli na siyo kutafuta kumjua aliyetoa taarifa hizo,” alisema Slaa.

Alisema taarifa yao ya awali kuhusu kuwindwa kwa viongozi wa Chadema, walisema kuwa wanawatambua baadhi ya maofisa usalama wanaohusika ambao aliwataja kwa majina ya Zoka na Rama na kwamba mmoja kati yao amekuwa akifuatilia nyendo za Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.

Dk. Slaa aliongeza kuwa kamati kuu ya chama hicho imelaani kitendo cha kutaka kudhuriwa kwa viongozi hao na kwamba mpango huo ni wa kuhatarisha amani ya nchi. “Kamati kuu imelaani kitendo cha kutaka kudhuru viongozi wake na imelaani pia mpango wowote uliopo ambao unalenga kuhatarisha amani ya nchi," alisema.

Jumapili iliyopita uongozi wa juu wa Chadema uliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa chama chao wanawindwa na watu wanadaiwa kuwa ni usalama wa taifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe, alisema viongozi hao ni pamoja na Dk. Slaa, Mnyika na aliyekuwa Mbunge wa arusha Mjini, Godbless Lema.

Alisema mipango hiyo inahusisha kuuawa kwa sumu au kuwapelekea majambazi kwa nia ya kuwaua.

OPERESHENI SANGARA II YAIVA

Wakati huo huo, Dk. Slaa ametangaza kuwa chama hicho kinatarajia kuanza mpango wa nchi nzima wa 'Operesheni Sangara' awamu ya pili, kwa lengo la kuimarisha na kujenga chama itakayohusisha mikoa mitano.

Alisema operesheni hiyo itafanyika kwa siku 44 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Singida na Manyara na kwamba vijiji 4,000, kata 806 na majimbo 44 vitafikiwa.






CHANZO: NIPASHE
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.
Jina lako na akili zak ni sawasawa kaka. Ila 2015 ndio mtakiona jipeni moyo hii miaka 2 iliyobaki.
 
pamoja na hayo.Umeandika taarifa hii kwa ushabiki mno mpaka mtu wa kawaida anaelewa wewe uko katika itikadi gani! Na kupoteza reputation ya kuwa jf!

Hivi kwani kujulikana itikadi ya mtu ni makosa? Hivi WaTz mnataka kujificha hata lini? Tatizo bado wengi hamkubali mfumo wa vyama vingi kwamba ni mtindo wa kawaida wa maisha. Hakuna kitu mbaya kujulikana kuwa wewe ni wa CCM na yule ni wa CHADEMA, CUF, UPDP, UPD, NCCR-Mageuzi, etc. Vyama vinashindana kwa sera na mwenye sera itakayokubalika kwa wananchi atashinda. Tuishi tu kwa amani tukipingana bila kupigana.
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.

Mkuu barubaru, wewe ni mwanazuoni kiasi. Jaribu kuangalia swala hili bila kumhusisha Dr Slaa, jaribu kunagalia historia ya nchi yetu na jaribu kutafuta tafiti zilizofanywa kuhusu imani ya watanzania kwa mahakama na polisi. Kweli unaweza kuamini kwamba kama kuna mkono wa wakubwa Polisi watafanya lolote? Kumbuka first degree murder ya Dito, polisi wote mpaka RPC walikuwa wanaogopa kumkamata, angalia wezi wa EPA wanatesa tu, tell me kama kweli waliompiga Ulimboka watakamtwa au la (siamini kama ni uslama wa taifa), labda mmoja wao au wawili wao walitumiwa. Siwezi kupingana na Slaa hata kidogo, akienda Polisi hakuna litakalofanyika, sana sana ndio atakuwa anawarahisishia kazi wauaji. Kumbuka ya Mwakyembe habari zilianzahivi hivi kwenye mtandao kuwa atawekewa sumu, aliripoti polisi, lakini still sumu aliwekewa. Sasa ukienda kuwaambia maana yake nini? Kilichopo ni kujichukulia hatua za ulinzi binafsi.
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.
Mkuu Avatar yako Vina Uhusiano na Kahawa na Kashata pamoja na pilau za kwenye Hitma. Hapa jirani kwetu kuna turubali linapandishwa usisahau kuja na ndizi mbivu
 
Policcm aende kufanya nini si ndio watampolonium huko huko,,chezea mabwepande?
 
Naona Dr sasa anatafuta umaarufu zaidi baada ya kuona sasa umaarufu wake unazidi kushuka siku hadi siku. Hana jipya la kuwaeleza wananchi wa Tanganyika zaidi ya propaganda na ubishi uso maana.

Hajui kuwa anajiaibisha yeye na taaluma yake aliyobobea ya Canon Law
.

Jina la huyu jamaa linaonyesha ni jinsi gani alivyomvivu kufikiri!! NA hatakaa aelewe hata kwA fimbo!! Labda ahamie baghdad !!
 
tatizo vyombo vya usalama wa raia na mali zao vimekuwa vyombo vya usalama wa viongozi wa ccm na serikali yao.hapo ndio shida.hakuna haki tena kwa raia hasa asiye wa chama cha mapumbavu
 
Riziwani na team yako mnatisha.
Naomba nikuambie mwisho wenu utafika tu,nenda Manyoni kijana ukamalizie usimamizi wa kupaka rangi kituo chako cha mafuta,nimepita juzi hapajakaa vizuri kabisa.

Nasikitika wengine mnajiunga kuwa washabiki kwa ujira mdogo sana huku wazee wenu na ndugu zenu vijijini wanateseka na kuumia.
Mnaowatetea wanazidi kuweka fence kwenye machimbo ya madini na kujilimbikizia mali kila kona.

Mnapiga kelele hapa Jf mwenzenu RZ1 anazidi kujilimbikizia mali,nimepita Geita wananchi wanalalama amejenga sheli juu ya vyanzo vya maji.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa kweli,nawasiwasi wengi wenu mnao pingana na ukweli humu hamnatofauti na misukule,maana msukule ukiupa pumba ama unga hauwezi kuuliza wala kulalamika maana tayari ulimi ulikatwa..
 
Kama wameshindwa kuwahoji wahujumu uchumi na wezi wa rasilimali za taifa kupitia wizi wa KAGODA, EPA, KUTOROSHA WANYAMA KUPITIA KIA, DOWANS, na wengineo, iweje wamuhoji Mtanzania msafi na aliyebarikiwa na kupata uhuru wa fikra za kutoa madukuduku yake juu ya usalama wake na ule wa Watanzania wanyonge? CHAMA CHA MAJAMBAZI (CCM) kitatumaliza jamani.
 
Nafikiri Dr Slaa badala ya kutaka kurudisha umaarufu wake kwa hili naona huku sasa Docta mwenzangu umefilisika kimawazo kama si ki sera.

Kumbuka kuwa ni wewe kabisa ukiwa Mbunge wa Karatu uliapa bungeni kuwa ungelinda Katiba yenu ambapo ndanimwe kuna kipengele cha Usawa mbele ya Sharia zenu.

Nakukumbusha soma Katiba yenu ya JMTz kipengele cha Usawa mbele ya Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 na Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8
​
​
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,​
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
Sheria
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombovinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sharia​
​






5
 
Kila siku mnasema serikali dhaifu halafu hapo hapo mnaigopa hiyo serikali dhaifu.

uoga unakuja pale inapoendelea kuzalisha dhaifu wengi kwa wingi, hivyo mbio za kuwakomboa kwenye udhaifu 2015 bado mbali, udhaifu unaenea kwa kasi kama mafua ya ndege!!
 
Nafikiri Dr Slaa badala ya kutaka kurudisha umaarufu wake kwa hili naona huku sasa Docta mwenzangu umefilisika kimawazo kama si ki sera.

Kumbuka kuwa ni wewe kabisa ukiwa Mbunge wa Karatu uliapa bungeni kuwa ungelinda Katiba yenu ambapo ndanimwe kuna kipengele cha Usawa mbele ya Sharia zenu.

Nakukumbusha soma Katiba yenu ya JMTz kipengele cha Usawa mbele ya Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 na Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,​
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
Sheria
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombovinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa shari
​

Sikubaliani na wewe, Hizo sheria ni Mbwembwe tu, kama ni kulindwa kama unahainisha kwenye sheria hii, mnalinda watu kwa kutumi msitu wa mabwe pande? Acha Utani kwa maisha ya watu wewe, Mwakyembe, Mengi, Mwandosha, Kubenea, Kolimba, Kombe wote wamelindwa?

Sikubaliani na wewe, Hizo sheria ni Mbwembwe tu, kama ni kulindwa kama unahainisha kwenye sheria hii, mnalinda watu kwa kutumi msitu wa mabwe pande? Acha Utani kwa maisha ya watu wewe, Mwakyembe, Mengi, Mwandosha, Kubenea, Kolimba, Kombe wote wamelindwa?
 
Back
Top Bottom