Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Yaliyotokea Uganda kwa Museven ya kumkamata Mzee wa WALK TO WORK sasa yamehamia Tanzania kwa Wazee wa LIWALO NA LIWE vs NGUVU YA UMMA.... Ama kweli NYINYIEM imeshikwa kwenye masaburi sasa wanatumia mbinu za KUWA-ULIMBOKA watu..
 
padri slaa ndio ulikuwa wito wake sema tamaa mbaya sana

Na atawanyoosha sana nyie MABWEPANDE, ni aibu jinsi Serikali inavyoendesha nchi hii! Muiteni padri lakini mtanyooka hivyohivyo! huyu padri ndo kiboko ya sheikh masafari a.k.a Vasco Da Gama
 
Kweli, credibility ya polisi imeisha sana. Siyo Dr Slaa tu ambaye hana imani hata raia hawana imani na polisi, na ndo maana matukio ya sheria mkononi yameongezeka sana. Siku hizi wahalifu ndo wananafasi lakini raia wema hawana nafasi pale.
Ukiweka mali yako polisi, ni nadra sana kuikuta ikiwa salama, uende kule kufanya nini? Jambazi anapigiwa saluti na polisi.
 
Wel hapa ndo movie inapoanza kuwa tamu,daktari anawaonyesha jinsi gani nchi haiko salama. ulimboka kafanyiwa umafia lini mpaka leo hakuna habari yoyote! Mnyika alimstahi sana jk kumwita dhaifu na kafulila alikuwa mstaarabu kuita serikali ya magamba kuwa ni legelege.Mi nasema serikalini inaongozwa na WANYELA TU
 
Katibu mkuu wa Chadema na aliyekuwa Mgombea wa urais mwaka 2010 kupitia chama cha CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani na kinacho ongoza kwa umaarufu na kupendwa na watu wote hasa vijana Nchini tanzania na Nchi za jirani Dr.W.Slaa, amesema hatokubali kuhojiwa na polisi juu ya habari za kutishiwa kuuwawa kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa kile alichodai kwamba hana imani na jeshi hilo la polisi.

Ni hayo tu.

KAULI ZA KIJINAI HAZINA KINGA ZA KISIASA
Kifungu cha 214 cha KANUNI YA ADHABU Sura ya 16 inasema:
Mtu yeyote atakayekula njama na mtu mwingine yeyote kumuua mtu yeyote, iwe mtu huyo yuko Tanzania Bara au pengine, mtu huyo ni mwenye hatia atapaswa kifungo cha miaka kumi na nne jela.

Taarifa zilitolewa kwa vyombo vya HABARI kuwa kuna njama ya kuwaua viongozi wa Chama Cha Siasa. Nchi yeyote yenye kuheshimu utawala wa Sheria ni lazima itawahoji waliotoa tuhuma hizi.

NI WAJIBU WA POLISI kupeleleza tuhumu hizi. Nitashangaa endapo POLISI hawatatimiza wajibu wao na kupeleleza kauli hizi. Na katika kutimiza wajibu wao, polisi wanayo mamlaka ya kumuita MTU YEYOTE kwa mahojiano. NA UNAPOITWA NA POLISI HUNA MAMLAKA YA KUSEMA SITAKI !!
HAKUNA MTU YEYOTE ambaye yuko JUU ya SHERIA kiasi cha KUKATAA WITO WA POLISI MPELELEZI. Kukataa wito wa Polisi anayepeleleza tuhuma kuwa kuna nkjama ya mauaji ni kosa la jinai. Kukataa au kukaidi wito au amri ya Mahakama ya MAHAKAMA ni kosa la jinai.

Demokrasia itajengwa kama viongozi WOTE watajenga utamaduni wa kuheshimu SHERIA. Ninashangaa pale kiongozi anayetarajia kuchaguliwa ili asimamie sheria anaposema kuwa hawezi kukubali kuhojiwa na vyombo vya kisheria. Kiongozi bora ni yule anayeheshimu SHERIA ZOTE ZA NCHI YETU.
 
Bado kasahau ile wine ya kule kwa mazengo (dodoma) kuwa nayo hawakurudishaga majibu. Serikali ya mashwaini 2 na si ya raia wema kama sisi.
 
Dr wa thesis vrs dr wa heshima, power of reasoning vrs power of force
Ngoma inogile
 
Kumvimbia tu yani huyo NCHIMBI(mbunge aliyeiba kura) kama anataka kupotea basi akuulize MASHA.
 
polisi vile vinasa sauti alivyowekewa dr chumbuni ddm waliishia wapi? embu jiulize wale waliowapiga wabunge wa chadema mwanza walifanywa nini? Dr ana sbb ya kutokuwa na imani na polisi
 
MziziMkavu Hii ni very strong message kwa Waziri Nchimbi,Jeshi la Polisi,Usalama wa Taifa na Chama Cha Mabwepande-CCM.

Kwamba NYUMBA YAO INAVUJA. Kwa lugha rahisi na ya uwazi ni kwamba THERE IS LEAKAGE OF INFORMATION kutoka ndani ya Serikali,Jeshi la Polisi,UWT na CCM. Serikali lazima ijue kuwa si wote walio ndani ya CCM na Serikali wanafurahia huu UPUUZI unaofanywa na watu wachache waliolewa madaraka. Kuna watu kule wanachukizwa sana tena sana na huu ujinga wa Serikali ya CCM, hawa ndiyo wanao-VUJISHA taarifa za Intelijensia!

Hivyo Polisi wasijisumbue kutaka kuwahoji kina Dr.Slaa kwa tuhuma walizozitoa. Tuhuma hizo ni za kweli kwasababu zimevuja toka ndani ya Polisi haohao na UWT. Kinachotakiwa ni wao kujipanga upya na wamtafute huyo mchawi mwenzao anayefanya kazi ya WIKI-LEAKS kwa kuvujisha siri za mipango yao ya kuwadhuru Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wanaoikosoa CCM na Serikali yake.

Tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dr.Ulimboka nusura ya kufa ni MPANGO MKAKATI wa kujaribu kuwanyamazisha kwa nguvu Watanzania wapenda Haki,Vyama vya Upinzani na Wanaharakati ili CCM waendelee kutawala nchi hii milele kama wanavyodai kwenye kauli zao. Leo ni siku ya siku ya 14 (2 weeks solid) zimeshapita tangu Dr.Ulimboka apatikane na lile balaa na si POLISI wala UWT wamekamata mtuhumiwa yeyote! Hii inadhihirisha kwamba mpango ule ulikuwa umesukwa na haohao Polisi na UWT!!!
 
Last edited by a moderator:
Wazo mbadala: Labda ni vema kwa Dr Slaa kuwapa polisi information aliyo nayo ili wapate pa kuanzia kufanya uchunguzi wa kina. Ni lazima polisi wawe na pint ya kuanzia na yule anayejua pint hiyo ni vema akaiweka wazi polisi wafanye kazi yao. Nashauri hivyo ingawaje hata mimi sina imani na jeshi la polisi ila hatuna namna yoyote ila kuwatumia kwa sababu, pamoja na kuwa wachakachuaji wana wajibu wa kutulinda. Dr Slaa na CDM ni vema mkawa na mnepo (flexible) lakini kwa uangalifu mkubwa.

Mungu ibariki Africa, Tanzania na CHADEMA
 
KAULI ZA KIJINAI HAZINA KINGA ZA KISIASA
Kifungu cha 214 cha KANUNI YA ADHABU Sura ya 16 inasema:
Mtu yeyote atakayekula njama na mtu mwingine yeyote kumuua mtu yeyote, iwe mtu huyo yuko Tanzania Bara au pengine, mtu huyo ni mwenye hatia atapaswa kifungo cha miaka kumi na nne jela.

Taarifa zilitolewa kwa vyombo vya HABARI kuwa kuna njama ya kuwaua viongozi wa Chama Cha Siasa. Nchi yeyote yenye kuheshimu utawala wa Sheria ni lazima itawahoji waliotoa tuhuma hizi.

NI WAJIBU WA POLISI kupeleleza tuhumu hizi. Nitashangaa endapo POLISI hawatatimiza wajibu wao na kupeleleza kauli hizi. Na katika kutimiza wajibu wao, polisi wanayo mamlaka ya kumuita MTU YEYOTE kwa mahojiano. NA UNAPOITWA NA POLISI HUNA MAMLAKA YA KUSEMA SITAKI !!
HAKUNA MTU YEYOTE ambaye yuko JUU ya SHERIA kiasi cha KUKATAA WITO WA POLISI MPELELEZI. Kukataa wito wa Polisi anayepeleleza tuhuma kuwa kuna nkjama ya mauaji ni kosa la jinai. Kukataa au kukaidi wito au amri ya Mahakama ya MAHAKAMA ni kosa la jinai.

Demokrasia itajengwa kama viongozi WOTE watajenga utamaduni wa kuheshimu SHERIA. Ninashangaa pale kiongozi anayetarajia kuchaguliwa ili asimamie sheria anaposema kuwa hawezi kukubali kuhojiwa na vyombo vya kisheria. Kiongozi bora ni yule anayeheshimu SHERIA ZOTE ZA NCHI YETU.
.

Tuweke vizuri, Hoja ya Slaa hakatai kuhojiwa, ila anataka yale mahojiano ya nyuma yaliyofanyika kwa sheria hiyo uliyoitaja yazae matunda. Ametoa masharti hayo. Je, yupo sahihi kiasi gani hapo?
 
Wazo mbadala: Labda ni vema kwa Dr Slaa kuwapa polisi information aliyo nayo ili wapate pa kuanzia kufanya uchunguzi wa kina. Ni lazima polisi wawe na pint ya kuanzia na yule anayejua pint hiyo ni vema akaiweka wazi polisi wafanye kazi yao. Nashauri hivyo ingawaje hata mimi sina imani na jeshi la polisi ila hatuna namna yoyote ila kuwatumia kwa sababu, pamoja na kuwa wachakachuaji wana wajibu wa kutulinda. Dr Slaa na CDM ni vema mkawa na mnepo (flexible) lakini kwa uangalifu mkubwa.

Mungu ibariki Africa, Tanzania na CHADEMA

Sikiliza mheshimiwa,

Swala la Dr.Slaa au viongozi wengine wa CDM au mtu mwingine yeyote kuwapa Polisi sijui point ya kuanzia is IMMATERIAL! Hawa watu(Polisi) ni trained professionally kwenye fani hiyo ya Upolisi na wanajua kazi yao.Kwa hiyo ni wajibu wao kuanza kutafuta na kuchunguza ukweli wa tuhuma zinazopelekwa kwaobila ya kuanza kuwabughuzi walewale wanaotoa tuhuma zile.

Kama Dr.Slaa ameshasema kuwa nyumba ya Polisi inavuja means OFISI YA POLISI INATOA SIRI ZAKE NJE ni taarifa tosha kabisa kwa Polisi kujua pa kuanzia.Kuwa kuna wenzao ndani ya Jeshi la Polisi wanatoa siri za mipango yote inayopangwa kuhusu kuwateka,kuwanyanyasa,kwadhuru na hatimaye kuwaua viongozi na wanachama wa Vyama vya Upinzani simply because wanaikosoa na kuisahihisha serikali ya CCM iliyoko madarakani! Katika nchi yenye Demokrasia ya Vyama vingi hili jambo kamwe halikubaliki!

Polisi waanzie ndani ya nyumba yao kujichunguza na kujisafisha kabla hawajatoka nje kuanza kusumbua raia.Vinginevo watuambie kuwa kazi ya Upolisi imewashinda kwa kundekeza kutetea,kulinda na kudumisha sera za Chama Cha Mabwepande-CCM.
 
Back
Top Bottom