Dr. Slaa aanza ziara nzito Nyanda za juu Kusini

Dr. Slaa aanza ziara nzito Nyanda za juu Kusini

@ Simba wa Yuda leo anaunguruma Arusha,habari za Dr.Slaa zimepitwa na wakati,habari ya mujini sasa hivi ni Lowasa
 
@ Simba wa Yuda leo anaunguruma Arusha,habari za Dr.Slaa zimepitwa na wakati,habari ya mujini sasa hivi ni Lowasa

Waandishi wa habari wanaowaambia watanzania kwamba shule za kata alianzisha Lowasa huo ni uwongo ambao unapaswa kulaaniwa na watu wanaosimamia ukweli katika maisha . Shule za kata zimeanza wakati wa utawala wa rais Mkapa miaka ya 2002. Mpango huo wa MMEM na MMES ulioasisiwa na rais mkapa na kusimamiwa na waziri mkuu Sumaye na waziri wa elimu wa wakati huo bila shaka atakuwa Mungai kama sikosei ndio waliosimamia utakelezaji wa mipango ya MMEM na MMES . Tukumbuke mipango hiyo ilianza na crush program iliyolenga kuongeza idadi ya walimu nchini ikazoa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kuwapeleka vyuoni kwa mwaka mmoja na wale wa sekondari wapo waliopata mafunzo ya miezi mitatu ili kuziba pengo la walimu
Lowasa anaingia madarakani tayari shule za kata zilishaanza kujengwa . Lazima tukubaliane Lowasa kaingia madarakani novemba 30, 2005 na kuondoka madarakani kama waziri mkuu february 7 , 2008. Kwa maana hiyo yeye Lowasa kaweza kusimamia bajeti mbili tu katika utawala wake, bajeti ya julai 2006- juni 2007. bajeti ya julai 2007 hadi juni 2008. sasa kwa bajeti hizo mbili tu unaweza kujenga shule za kata nchi nzima. Huo ni uwongo wa dhahiri. tena bajeti yenyewe ya 2007-2008 hakuimalizia kutokana na kuondoka miezi minne kabla ya muda wa bajeti mpya

Waandishi wa habari makanjanja msimpe mtu sifa zisizo zake . shule za kata alizikuta zilizoanzishwa na Sumaye na kuziacha zikaendelezwa kujengwa na waziri mkuu wa sasa Pinda. Tena pinda ndiyo aliyofanya kazi kubwa ya kuhakikisha anaongeza idadi ya walimu nchini kwa kupango mipango mbalimbali kama vile kuajiri walimu wengi wa sekondari na kupeleka vyuoni walimu wengi wa sayansi, kuimarisha mafunzo na semina shirikishi kwa walimu. Leo hii walimu nchi nzima wapo udom dodoma wakipata semina. Sumaye alikazia kujenga madarasa na nyumba za walimu , Lowasa akaendeleza tu jitihada alizozianzisha Sumaye kwa miaka miwili na yeye akakazia kujenga nyumba za walimu na si madarasa kwani miaka ya 2006 ilipigwa marafuku kwa madiwani kwamba shule za sekondari zilizojengwa zinatosha kwa kazi aliyoifanya ni kuboresha madarasa na kujenga nyumba za walimu na kuongeza madawati .

Sifa anazopewa Lowasa kana kwamba yeye ndiye aliyeanzisha huo mpango na wengine waliomtangulia na kumpokea majukumu ya uwaziri mkuu hawajafanya kitu. tunawakatisha tamaa viongozi wetu. Leo hii kila shule ina maabara waziri mkuu atakaye kuja atakuwa na kazi ya kupeleka vifaa tu hii haina maana kwamba sasa tumbeze aliyefanya kazi ya kuzijenga maabara hizo.

Kila mtu apewe sifa zake stahiki na si kumpa mtu sifa kwa sababu ya njaa yako inayokusumbua.
 
Safari njema kiongozi wetu mpendwa.

Dalili zote zinaonyesha kwamba Slaa ndiye chaguo la Watanzania. Lakini kwa sasa nchi iko mikononi mwa watu wenye uzoefu mkubwa wa kuiba kura na kukwapua kiasi kikubwa cha fedha za uma kwa ajili ya shughuli za kununua kura.

CHADEMA naomba muiwekee sana macho serikali ya CCM ili isichapishe fedha za uchaguzi. Maana kama watu wao wa huko Hazina hawana za kutosha basi wataweza KUCHAPISHA nyingine. Hawajali kuharibu uchumi, wanachojali ni kupata fedha za kununua kura na wapiga kura.


 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kesho anaanza ziara rasmi ya nyanda za juu kusini itakayomfikisha katika mikoa ya Mbeya,Rukwa na Katavi.

Taarifa iliyothibitishwa na msemaji mkuu wa CHADEMA Tumaini Makene inasema kiongozi huyo maarufu nchini atafanya mambo makubwa matatu katika ziara hiyo ambapo ni kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR,kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na chama na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Kiongozi huyo atahutubia mikutano ya hadhara katika miji ya Vwawa,Tunduma,Sumbawanga na Mpanda.

Tayari matayarisho yote muhimu ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.

mungu akutangulie rais wetu ukitoka huko upumzike usubiri kuapishwa
 
Last edited by a moderator:
updates zinatakiwa , watanzania wanataka kujua , huyu mtu kiboko ya wezi na mafisadi anaongea nini leo?
 
@ Simba wa Yuda leo anaunguruma Arusha,habari za Dr.Slaa zimepitwa na wakati,habari ya mujini sasa hivi ni Lowasa

Sema team mafisadi leo wapo ARUSHA
na mkimpa nchi miezi sita mingi watagawana nchi kama wakoloni walivyofanya kwa AFRICA
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kesho anaanza ziara rasmi ya nyanda za juu kusini itakayomfikisha katika mikoa ya Mbeya,Rukwa na Katavi.

Taarifa iliyothibitishwa na msemaji mkuu wa CHADEMA Tumaini Makene inasema kiongozi huyo maarufu nchini atafanya mambo makubwa matatu katika ziara hiyo ambapo ni kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR,kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na chama na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Kiongozi huyo atahutubia mikutano ya hadhara katika miji ya Vwawa,Tunduma,Sumbawanga na Mpanda.

Tayari matayarisho yote muhimu ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.

hakuna atakayezuia anguko la ccm mwaka huu, ngoja tuendelee kuongeza wapigakura wetu kuelekea magogoni
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom