Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kesho anaanza ziara rasmi ya nyanda za juu kusini itakayomfikisha katika mikoa ya Mbeya,Rukwa na Katavi.
Taarifa iliyothibitishwa na msemaji mkuu wa CHADEMA Tumaini Makene inasema kiongozi huyo maarufu nchini atafanya mambo makubwa matatu katika ziara hiyo ambapo ni kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR,kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na chama na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Kiongozi huyo atahutubia mikutano ya hadhara katika miji ya Vwawa,Tunduma,Sumbawanga na Mpanda.
Tayari matayarisho yote muhimu ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.