Dr. Salim Ahmed Salim kuwa Obama wa Tanzania 2015?

Umetumia kigezo au vigezo gani kumlinganisha na Obama? Maana sioni similarities zozote kati ya hawa watu wawili.
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?
.............haiwezekani,atakuwa mzee sana!
 
Huyo ni Mpemba ingawa inasemwa kuwa aliukana Upemba alipokuwa katika Kinyanganyiro kwa kuwa mama yake ana asili ya Kimanyema au ni mmanyema baba yake ni muarabu pure hata kiswahili hakitamki vizuri ,vipi atakubalika katika jamii ya WaTanzania kuwa Raisi wao ? Pili ni Muislamu wakati japo sijawahi kumuona msikitini wengine wanasema ni mkoministi kama kingunge ,sina uhakika ,si kuna msemo kuwa Mpemba hatawali ,sasa huoni kama kwamba unawasimanga WaPemba ,si unajua kuna msemo unasemwa kuwa Mpemba si ntu ?
Sidhani kama hizi ni sifa za mtu anayetaka kuwania urais wa tanzania
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?

tulikosea tangu 2005 kutomchagua. haitasaidia sasa na wala sidhani kama atakubali
 
jamani someni waraka wa kanisa mjue ni mgombea yupi anafaa sio kutajataja tu ebo
!
unataka huyo salim afie kwenye madaraka kama kingunge?
 
Jamani Uwaziri mmkuu unamtosha sasa nini tena mizigo ya uongozi?. Hata yeye mwenyewe hatokubali kwani kuna mazingaombwe mengi sana mjomba JK kayaingiza ingiza kinamna.

Nawasilisha jama
 
Baija Bolobi

Anao mtandao??

Inawezekana 2005 alikurupuka au alihujumiwa kwa sifa ulizotaja hapo juu alikuwaa juu zaidi ya yeyotee...
 
Last edited by a moderator:
naheshimu sana mawazo ya watu wote wanaompigia debe dk salim ahmed salim lakini ningependa mtu mwenye kujua mambo au mwenye kumbukumbu nzuri ya nini kilichojiri mwaka 1985 wakati wa mchakato wa kumtafuta mtu wa kumrithi baba wa taifa katika kiti cha urais atuambie ni kwa nini sas hakupewa nafasi hiyo.
tukipata ukweli wa nini kilichotokea huku kukiwepo habari kwamba ndiye aliyetakiwa na mwalimu nyerere tutaamua kama bado anastahili au hastahili kwa kazi hiyo.
lovulovu
 
Wana JF katika kampeni zinazoendelea, Mmoja wa wana CCM ambao nilitegema na ambaye ni mwanachama mwenye ushawishi simsikii kabisa! SALIM AHMED SALIM. Jama mbona amekaa kimya sana? Kulikoni?
 
Kichwa cha habari kina walakini kidogo....but anyway, umeeleweka!.......................Hii maneno ililetwa pia na member mwingine akihoji juu ya Salim, lakini pamoja na wengine kama Mwinyi, Mkapa, Msuya, sUMAYE NA wengine, lakini watu walitoa maoni tofauti, kubwa likiwa kwamba wakipanda jukwaani watasema nini, maana wanajua kwa uhakika kuwa JK hauziki kutokana na kuukumbatia uovu kwa kasi ya supersonic!
 
Huyu Mzanzibar huwa ninamwona mtu makini sana! Si mkurupukaji, angependeza sana kama angelikuwa raisi wa Tanzania kipindi cha 2005-10, ni aibu ya wanamtandao kumchafua. Kikwete hawezi kuingia kabisa kwenye mizani ya Dr Salim
 
Huyo mheshimiwa hukumbuki aliyofanyiwa 2005 wakati wa kura za maoni ya urais? Jamaa ana CV nzuri lakini kura za maoni 2005 ni sawa na za mwaka 2010.
Watu walichakachua kila kona, mtandao ulifanya kazi yake, mzee akapigwa benchi. Mojawapo ya skendo ni madai ya kuwa yeye ni raia wa nchi nyingine na siyo tanzania.
 
Ama yamempata yaliyompata Aboud Jumbe? Kuleee Kilimahewa!
Naskia alitaka kuchafua hali ya hewa.
 
Paka Jimmy shauri kichwa cha habari kingekuwaje. Cc tulifundishwa na mwalimu Makaaaaaaaaaamba vicha vyetu butu kidogo
 
Huyo mheshimiwa hukumbuki aliyofanyiwa 2005 wakati wa kura za maoni ya urais? Jamaa ana CV nzuri lakini kura za maoni 2005 ni sawa na za mwaka 2010.
Watu walichakachua kila kona, mtandao ulifanya kazi yake, mzee akapigwa benchi. Mojawapo ya skendo ni madai ya kuwa yeye ni raia wa nchi nyingine na siyo tanzania.
Na Nyingine walidai alimuua Karume lakini baada ya uchanguzi huo kuisha hatukusikia tena tuhuma hizo zikizungumziwa...CCM kwa mbinu chafu hawajambo...
 
Wana JF katika kampeni zinazoendelea, Mmoja wa wana CCM ambao nilitegema na ambaye ni mwanachama mwenye ushawishi simsikii kabisa! SALIM AHMED SALIM. Jama mbona amekaa kimya sana? Kulikoni?

Kaka sawa SAS hasikiki lakini ujue jamaa amekaa sana katika duru za siasa anafahamu kusoma nyakati za siasa. Kijana wa nyerere huyu amekulia ndani ya chama na anajua kitu kinaitwa uadilifu sasa katika mimbari za siasa atanadi sera zipi?
a. Kikwete ni kijana wetu na anafahamu misingi ya chama chetu (ataulizwa mbona alikujeruhi 2005? Ulichukua hatua zipi, na pia misingi ya CCM ni kusema ukweli na rushwa ni adui wa haki, sasa mbona anajiumauma kuhusu sakata la epa na richmond? na mbona hawachukulii hatua wahujumu uchumi oops sorry wala rushwa!!!)

b. Kikwete ni msafi (ataulizwa kweli, yeye si ndie alisign mkataba wa Bulyanhulu?, Richmond si alikuwa waziri? EPA sio ndio zimemuingiza madarakani?).

c. Kikwete anadumisha siasa za ujamaa na kujitegemea (Hili litawavunja mbavu kabisa, Tanzania ya leo kuna ujamaa kweli au kuna ubepari na ukoloni mamboleo? Viongozi ndio wamiliki wakubwa wa biashara zote mjini, wanavijisenti katika mabenki yet they claim to be wajamaa!!)

Sijui atamnadi kwa lipi? Hatari ni kwamba akianza kumnadi na yeye watu wataanza kuhoji ufanisi wake wa kazi na kwa kuwa ni mtu makini sidhani atalifikiria hilo
 
Na Nyingine walidai alimuua Karume lakini baada ya uchanguzi huo kuisha hatukusikia tena tuhuma hizo zikizungumziwa...CCM kwa mbinu chafu hawajambo...

Usisahau na ile ya kwamba ni Hizbu hivyo atahatarisha muungano hehehe Tanzania ione tu kuna vitu vya ajabu sana
 
Unakumbuka kina Butiku na MNF washawahi kuitwa wehu na Makamba nafikiri sasa kwenye kampeni hii watasema nini, to them (CCM) only fresh is gold but old is not gold.
 
Back
Top Bottom