Dr. Salim Ahmed Salim kuwa Obama wa Tanzania 2015?


Lakini kama ni HIVYO kumuacha SULTANI - Zanzibar pia ingekuwa MEMBER wa COMMONWEALTH? Kwahiyo Ina Maana kama Sultani asinge kuwepo MAPINDUZI yasingefanyika??

Kuhusu SAS; Una Maana alikuwa achukue nafasi Rais Mstaafu MWINYI aliyoichukua?? Kwasababu Then; nilikuwa na Family Member close to MWINYI DINESTY -- Ile Miaka ya Mwanzo Miwili hadi Mitatu; kila Mara alikuwa anatishia kujiuzulu sababu ya NYERERE kumuingilia... Uzuri ni kuwa then Mzee THABIT KOMBO alikuwa bado HAI Na Nyerere alikuwa anamsikiliza Thabit Kombo even zaidi ya Mzee Karume... So Mwinyi alikuwa anachukua NDEGE usiku hadi Zanzibar anaenda kwa Mzee Thabit Kombo anasema nimemuachia nchi... So Mzee Kombo anampigia Nyerere wanaongea - Nyerere anasema ngoja niende kuongea nae IKULU...

Mzee Kombo ansema niko nae hapa kwangu - Kwahiyo MWINYI anatoa Masharti yake through Thabit Kombo na Nyerere anasema OK...

Bila Mzee Thabit Kombo sijui kama Mwinyi angeweza kuwa na Makucha ya kutawala... na kumfurahisha amaletea Nyerere POPE...

Ningependa kweli kama Mwinyi ataandika his AUTOBIOGRAPHY!!!
Nianze na mstari wa chini kabisa, hilo la Autobiography! Hakika wazee wetu katika hili wanatuangusha sana na ndio maana unakuta mambo yaliyotokea kiasi cha miaka 50 tu iliyopita, bado yanakinzana kutoka kwa msimulizi mmoja hadi mwingine!

Tukirudi kwenye suala la ZNZ kubakizwa kwenye utawala wa Sultani na uwezekano wake wa kuwemo kwenye Commonwealth, binafsi nazani dhima kuu ya Mwingireza awali ilikuwa tu kutaka kumwacha Mwarabu aendelee kuwapo pale! Labda inawezekana kv walimuona tayari ameshakaa muda mrefu na ameshaji-establish kama kwake au labda walikuwa na agenda yao! Tusisahau kwamba, hata baada ya Sultan kutimuliwa ZNZ, familia yao walianza kukimbilia Uingereza badala ya Oman walikotkea!

Suala la SAS kwamba ndo alikuwa achukue nafasi ya Mwinyi; sina hakika nalo sana ingawaje ninavyohisi ni kwamba wengi walimtarajia sana SAS kuliko Mwinyi! Na hoja uliyoileta kuhusu Mwinyi kuingiliwa sana na Nyerere nazani ina-prove kwamba Mwinyi hakuwa first choice ya Baba wa Taifa! Wengine wanasema Baba wa Taifa alitamani sana amwachie mtu wake Kawawa lakini bila shaka aliona si busara....akaona ni bora kama uongozi ungeenda ZNZ! Lakini vyovyote iwavyo, hata kama Baba wa Taifa angependa Kawawa ndo awe mrithi wake, bado wananchi wengi walimpenda SAS! Na am very certain kwamba hata Baba wa Taifa mwenyewe nae hakuwa na tatizo na SAS! Kwamba, kama ingekuwa ni kwa matakwa yake, basi SAS kwake angekuwa ni best candidate kuliko Mwinyi! Hata hivyo, alifahamu hali tete ambayo ilikuwapo ZNZ....alifahamu kwamba wanazi wa Mapinduzi hawamtaki SAS!

Suala la Mwalimu kumuingilia Mwinyi siwezi kushangaa hata kidogo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, nazani Mwalimu alishitushwa na kasi ya mabadiliko iliyokuwa inafanywa na Mwinyi. Hii ni sawa na mtu anakuja nyumbani kwako kwa mara ya kwanza na kuanza kupangua pangua mpangilio mzima wa nyumba! Lakini pili, vile vile alikuwa ni mtu ambae hakuwaamini sana wenzake kama wangeweza kuendesha mambo vizuri! Na ndio maana hata kwenye mchakato wa uchaguzi wa CCM 1995, Mwalimu alipigana kufa na kupona kuhakikisha yule aliyemtaka si tu anapata nafasi ya kugombea kupitia CCM, bali pia alihakikisha anaingia Ikulu! Bado taswira ya katuni kwenye gazeti la Majira haijafutika kichwani mwangu ikimuonesha Mwalimu amembeba (kwa mbeleko) Mkapa huku Mkapa nae akiuchapa usingizi mgongoni!! Very funny cartoon!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom