Dr. Salim Ahmed Salim kuwa Obama wa Tanzania 2015?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Wadau mnamuonaje Dr. Salim, kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?

By 2015 nazani atakuwa anakaribia miaka 80 na kama sio basi atakapomaliza mihula miwili atakuwa keshafikia umri huo!!! Hatuna haja na wa2 kama hao kwavile bado kuna vijana au wazee kidogo wengi tu wenye uwezo wa kuongoza!!!
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?
Ndo umeanza kumfanyia kampeni? Haya anafaa kama atapambanishwa na wanyonge watakaojitokeza wakati huo
 
NasDas hujui Uzee ni Dawa?

Uzee unakuwa dawa pale anapokuwa nje ya madaraka!! lakini anapokuwa ndani ya madaraka uzee unakuwa sumu!! Huoni hata kingunge siku hizi anaongea hoja za maana kuliko alipokuwa waziri!!
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?

Kimsingi Mh. Salim Ahmed Salim anafaa kuongoza taifa letu right from next year. Kusubiri mwaka 2015 atazeeka sana na huu is unyanyapaa kwake. Matetemeko yote yanayoendelea nchini kwa sasa yatakoma akiingia kwenye usukani kwa sababu:
-Uzoefu wake katika kuongoza hautiliwi shaka hata na maadui wake
-Hajawahi kuonyesha dalili za kulewa itikadi
-Hana udini wala ukabila
-Chokochoko za Muungano zitajibika (Msiniulize kivipi, ni imani tu)
-Mpasuko wa zanzibar utayeyuka
-Uadilifu wake hauhojiwi na yeyote hata Salva Rweyemamu wala Muhingo
-Anaheshimu dini za watu wote
-Yuko tayari kusikia asiyoyapenda
-Ana marafiki si maswaiba
-Anaheshimu vyama vya upinzani
-Sifa zake kimataifa zimetosha

Wengine ongezea, lakini nasisitiza 2010 siyo 2015.
 
Between now and 2015, there might be so many things that will happen, which for sure may shape differently the political landscape of Tanzania. It is too earlier to start speculating.
 
Wanamtandao walimchafua sana mara muarabu,mara alihusika na mauaji ya kiongozi siku za nyuma na mambo mengine mengi.Sidhani kama atathubutu tena kugombea.
 
mma..... Tatizo si uzee
hatufai kwani hajainvest tz na wala hakai tz
hajui twala nini twaishi vp

Duuuuu! We vipi?
Rais wako wa sasa anajua unakula nini? unaishi vipi?
Hivi kigezo ni ku-invest Tz? Basi Rais awe Rostam kwani ame-invest nchini kwenye Richmond/Dowans, Kagoda Agriculture, New Habari Corp, Vodacom, TRL...
Hapo atakuwa ni Rais rasmi siyo tena by proxy.

Seriously I think Dr. Salim is no longer interested (and by the way, his domicile is in Tz, so stop mis-information).
Start thinking about other alternatives: How about Mwandosya? Magufuli? Shein? Dk Slaa? Shibuda? Mwanakijiji?
 
Kama anahitaji na anaona anaweza kuleta tofauti kwa Tanzania, kwanini asubiri 2015? Ajitose 2010, akimaliza muongo mmoja anastaafu kama alivyofanya Mandela. If yoy see him as a right candidate, why not now? We real need someone to avert Tanzania now than five year to come probably!
 
Wadau mnamuonaje Dr.Salim,kwa uadilifu wake na taswira na haiba yake Kitaifa na Kimataifa haimtoshi kuongoza Nchi yetu ya Tanzania kwenye ngazi ya Urais?
Mkku mmaroroi heshima mbele,

Unazungumzia 2015 wakati tuna uchaguzi mwaka kesho 2010 una maana gani?
 
haya ndo siyataki mimi
hivi mnataka mtu mpaka aitwe fataki wa uongozi wa siasa
huyu jamaa yupo toka ana umri wa miaka 19 kwa nini tusitafute mwingine huyu atusaidie kwa ushauri
 
UNAWEZA KU PROVE VIPI SALIM KUWA NI MPEMBA KWA BABA YAKE KUFANYA KAZI PEMBA TU NDIO SALIM AWE MPEMBA?
Acheni kuandika vitu visivyokua na uhakika ndiio Salim Kagombea Ubunge Pemba na kushinda ila ni kwa sababu Wapemba si wabaguzi ndio the same kwa Ali Hassan Mwinyi sio Mzanzibari yeye mwenyewe amekiri hilo ila aligombea URAIS na kupewa kura japo sio mzanzibari .
 
Back
Top Bottom