Mzee wangu Mohamed Said napata ukakasi na maneno yako sana....inaonyesha kuna kitu kimekukaa rohoni baada ya huyo bwana kutolewa Nssf..kuna sehemu hapo nyuma ulisema moja ya maajabu yake kutembea nchi nyingi duniani sijajua umeweka kwenye maajabu kwa misingi ipi...hila yote kwa yote punguza mahaba ya ukereketwa maana yakizid sana yanakuwa ugonjwa
Makodinda,
Bahati mbaya sana kuwa kauli zangu zinakutia ''ukakasi.''
Kuwa kuna jambo limenikaa rohoni hilo umesema kweli.
Sipendezwi na hizi chuki dhidi ya
Dr. Dau na ndiyo maana
niko hapa tunajadili lakini sijachukia yeye kutolewa NSSF
na kufanywa balozi.
Kuna aya katika Qur'an Allah anasema unaweza kulichukia
jambo nalo lina kheri na wewe na ukalipenda jambo lina
shari nawe.
Hili la ''globe trotter,'' hakika ni katika maajabu yake na mimi
si mtu wa kushangazwa na hilo kwani Alhamdulilah nimesafiri
kiasi changu.
Nilipata kuzuiwa siku za nyuma Heathrow Airport London kisa
pasi yangu imeingia nchi nyingi sana wakataka kujua vipi na
siku hizo ni kijana katika miaka ya kati.
Miezi mitatu baada ya mkasa ule nikaja tena London.
Mtu wa Uhamiaji kashangaa akaniuliza, ''Wewe si juzi juzi tu
ulikuwa hapa?''
Haukupita mwaka nikaingia tena London lakini nikitokea Paris.
Hawa jamaa wanapenda sana kuweka taarifa.
Akaniuliza nimekuja kufanya nini?
Nikamwambia nenda Cardiff nina shida kidogo na nitaondoka
hata juma simalizi.
Juu ya hilo ilikuwa wakati wa Hija na nilitaka nipite Uingereza ili
niswali Eid Kubwa Regents Park Mosque London.
Niko Paris Central Mosque
Kwa hiyo labda kwa kuwa wewe hujui ukubwa wa hilo ukaona
si kitu kukuambia kuwa
Dr. Dau kaitembea dunia.
Ama kuhusu mahaba na ukereketwa vyote hivyo ni sifa zangu
wala hukukosea.
Katika mafunzo yetu hizi ni sifa njema sana kwani zinampamba
mtu katika jamii.
Sifa hizi ajabu yake hujidhihirisha siku unapokwenda kuzikwa.
Baba yake
Dr. Dau alipokufa alipata maziko hayapata kuonekana
Dar es Salaam.