Dr. Ramadhan Dau aunguruma darajani Kigamboni

Kwani Dr. Dau kua na imani yake ndo amekosea au ndo anaonekana kuwa na udini. Serikali sio ya kidini ila watu wake wana dini
 
Rubawa,
Hizi chuki zimeletwa kwa watu kutoijua historia ya wazee wetu.

Laiti ingesomeshwa historia ya kweli na watu wakajua mapenzi
yalikuwapo enzi zile za kupigania uhuru vipi Nyerere Mkristo kaja
kapokelewa na Waislam na wakamweka madarakani hii ingeleta
kujua tulipotoka.

Tungejua mizizi yetu ilikochimbukia.

Hii khiyana ya kutaka kubadili historia na kufanya kama vile Nyerere
alikuwa peke yake na kuleta uhuru peke yake ndiyo iliyotufikisha
hapa.

Miaka ya 1950 dini ya mtu haikuwa tatizo kwa wazee wetu hata kidogo.
Angalia mfano huu.

Wakati wazee wetu wanataka kubadilisha uongozi wa TAA baada ya Vita
Vya Pili Vya Dunia aliyekuwa mbele kutaka Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes
wachukue uongozi kama rais na katibu alikuwa Schneider Abdillah Plantan.

Huyu Schneider ndiye akaja kuwa katibu wa Daawat Islamiyya (Wito kwa
Waislam) chini ya Sheikh Hassan bin Amir.

Na huyu Sheikh Hassan bin Amir ndiye aliyemjenga Nyerere kwa umma wa
Waislam kama kiongozi wa harakati za kudai uhuru.

Hawa Waislam wote niliowataja hapa wapi historia yao imeandikwa?
Hili ndilo tatizo kubwa.
Siku ujinga ukikutoka na kugunduwa hawa wazee ID yao ni Utanganyika na si uislamu basi utaifurahia dunia na utaona ni mahala pema pa kuishi.

Unaweza kunitajia katika hao wazee kuna aliyepigana vita ya majimaji?

Ukitaka uheshimike na kama una nia njema andika watu walioshiriki harakati za uhuru unaowajuwa wewe na siyo dini zao, utadharaulika na tutakuona ni mpuuzi tu sawa na wapuuzi wengine.

By the way wajurishe waislamu wenzako wa kariakoo kwamba daraja si la Dau bali la Nyerere.
 
Matola,
Unaghadhibika bila sababu.
Unatoa matusi bure.

Nimekwishakueleza kuwa ni jamaa wa Kidaresalaam wanapokutana likija suala
la daraja wao utawasikia wanasema, ''Daraja la Dau.''

Sikusema kuwa hiko ndilo jina la daraja.

Kudharaulika si kweli.

Kwa kusahihisha historia hii ya Tanganyika nimealikwa vyuo vingi kuzungumza
hadi kutiwa kwenye maradi wa Harvard na Oxford University Press, New York
na kazi yangu imechapwa ndani ya Dictionary of African Biography (DAB).

Ingia hapa:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

Mtu anaedharaulika hawezi kupewa heshima ya kualikwa kuzungumza Northwestern
Univeristy, Evanston Chicago ambao ndiyo wanaongoza duniani katika African History.

nathaniel%252520and%252520me.jpg

Matola,
Babu yangu hakupigana Maji Maji kwa kuwa 1905 bado alikuwa ni mtoto.

Lakini babu yangu Salum Abdallah alitoa mchango mkubwa kwa katika
harakati za kudai uhuru.

Ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
 
Ukimuandama mtu kwa dini yake jua atatetewa kwa dini yake!
Ushawahi kusikia Rostam,Karamagi, Said lugumi katetewa kwa dini yake?
Chuki yenu dhidi ya Dr.Dau imeanza tangu kateuliwa January 2001 kabla hajaanza lolote NSSF mlishaanza Chuki na husda zenu.

Kama ni tuhuma za ufisadi wanazo wengi what is so special kwa Dau mpaka mnafikia kumtoa kwny vigazeti vyenu anasulubiwa?
"...Kama mnashindana shindanen kwa yaliyo bora..."

Fanyeni kazi bora kuliko aliyofanya badala ya kuishia kufoji Auditors report na kusambaza na kutumia nguvu kubwa kumuandama wakati alikuwa ni Mkurugenzi tu Mfuko wa hifadhi ya Jamii!
Acha kugushi ushahidi mkuu. Alipoteuliwa 2001, dau alikuwa hata hajulikani. Hakuna aliyemfahamu Dau. Dau amejulikana baada ya habari kusambaa kwamba NSSF ilikuwa na ajira za kidini. Ni bahati mbaya kwamba yeye mwenyewe alijidai mtu wa busara kwa kutolisemea hilo.

Kwa sasa alipoondolewa, likaja kundi la kumtetea kwa nguvu sana na kuonyesha kaonewa. Kaonewa kitu gani? Kwani alipoteuliwa alipendelewa? Kwa nini iwe mpaka kifo? Angalia wachangiaji wamnavyojiuliza, ni nini cha kunufaisha alichokuwa akikitoa mpaka ionekanae eti kaonewa. NSSF siyo kampuni yake! Kama ni wizi, yaweza kuwa ni kweli. Nani unayemfahamu ktk serikali iliyopita ambaye hakugeuka tabia na kuwa mwizi?
 
2016%2B-%2B1

2016%2B-%2B1

‘’Wastara haumbuki,
Wa mbili havai moja…’’

Haya ni baadhi ya maneno kwenye nyimbo niliyokuwa nikiisikia katika gramaphone nyumbani kwetu wakati nikiwa na umri mdogo sana. Mama yangu akipenda kuuimba mwimbo huu kila afanyapo kazi iwe kupika au kufua. Kuna beti za mwisho nazikumbuka na nikizpenda sana. Zilikuwa na maneno haya:

''Kwetu Congo natumaini,
Kwetu Kongo natumaini.''

Beti hizo nilizipenda kwa kuwa akifurahi alikuwa akiniadhimisha kwa kuniambia kuwa mimi nimetoka Congo.

Wakati huo Bi. Hawa biti Maftah mwanamke wa Kimanyema akimuimbia Nyerere mwimbo
maarufu katika mikutano ya TANU Mnazi Mmoja: ''Hongera mwanangu hongera...''

Wakati ule Dar es Salaam ilikuwa ndogo na jamii ya Kimanyema mjini ilikuwa na hadhi ya kipekee.

Kuanzia wanawake wao hadi wanaume.

Kubwa ni yale maumbo makubwa ukimouna mwanamke wa Kimanyema kapanda ana futi
sita na mwanamme halikadhalika.

Basi nilikuwa nizkizisikia beti hizo mama akiziimba nikawa nasisimkwa na mwili.

Nilipopata umri na kila nilipokutana na shida za dunia khasa katika mambo ya hasad na mengine kazini na kwengineko, vikwazo na nini... mama yangu akinambia: ''Wa mbili havai moja.''

Maana yake ni kuwa ikiwa Allah kakuandikia kupata ndivyo itakavyokuwa hivyo hivyo hata zije fitna kiasi gani.

Ndipo hapo inaingia, ''Wastara haumbuki.''
Yaani hutoweza kumfedhehesha aliyenyanyuliwa.

Fuatilia ukurasa huu...

Mzee wetu hongera, humo tupeana ukweli.
 
Acha kugushi ushahidi mkuu. Alipoteuliwa 2001, dau alikuwa hata hajulikani. Hakuna aliyemfahamu Dau. Dau amejulikana baada ya habari kusambaa kwamba NSSF ilikuwa na ajira za kidini. Ni bahati mbaya kwamba yeye mwenyewe alijidai mtu wa busara kwa kutolisemea hilo.

Kwa sasa alipoondolewa, likaja kundi la kumtetea kwa nguvu sana na kuonyesha kaonewa. Kaonewa kitu gani? Kwani alipoteuliwa alipendelewa? Kwa nini iwe mpaka kifo? Angalia wachangiaji wamnavyojiuliza, ni nini cha kunufaisha alichokuwa akikitoa mpaka ionekanae eti kaonewa. NSSF siyo kampuni yake! Kama ni wizi, yaweza kuwa ni kweli. Nani unayemfahamu ktk serikali iliyopita ambaye hakugeuka tabia na kuwa mwizi?

Sema ulikuwa humjui usiseme alikuwa hajulikani.

Anaesema kaonewa ni Rais jana hukumsikia Jana Darajani "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"
Wewe tukikuuliza ututajie Wamiliki wa Newcastle unaamini Dau ni mmiliki kwa kuwa tu "anajifanya na busara kutokanusha?"
Sikufahamu lakini inaonekana umemjua Dau baada ya kujiunga NSSF.
Ishu ya Dau imeshajadiliwa sana na majibu yako mengi kama zilivyo shutuma nyingi ila unachopaswa kujiuliza ni kwa nini Rais aliamua kumwita Dau ni Mnyonge mnaetaka kunyonga lakini anawakumbusha kumpa haki yake?
 
MuchunguZI,
Unafananisha mambo mawili yasiyo na uhusiano hata kidogo.

Lakini si kitu ikhtilafu baiana ya binadamu ndiyo inafanya dunia
izunguke.

Umemtaja Prof. Ali Mazrui.
Mimi nimejuana na Prof. Mazrui kupitia Dr. Dau.

Yeye ndiye alikuwa rafiki yake na nilipotoa kitabu changu cha
kwa ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism
in Tanganyika,'' London 998 alimpa kitabu hiki mkononi Marekani.

Niliandika maneno haya katika kitabu: ''Kwa mwalimu wa wa
masafa marefu Prof. Ali Mazrui.''

Prof. Mazrui aliniletea barua na katika maneno aliyosema alisema
kafurshishwa na kitabu changu kwa kueleza nini Waswahili wamefanya
kupinga ukoloni.

Huu ndiyo ukawa mwanzo wetu wa kujuana.

Lakini usuhuba huu ukanoga zaidi pale Dr. Harith Ghassany
alipomweleza Prof. Mazrui kuwa mimi ni rafiki yake.

DSCN0096.JPG

Kushoto Tamim Faraj ( Muslim University of Morogoro),
Prof. Ali Mazrui na Mwandishi Nile Hilton Kampala

Ukipenda habari zaidi ingia hapa:
Mohamed Said: TAAZIA YA PROF. ALI MAZRUI 1933 - 2014
Ni vizuri kutoa mchango wako kadri unavyofahamu historia ya sehemu fulani. Ktk maelezo yako, umeona tofauti yako na Mazrui? Wakati kitabu chako kinaandika juu ya uislamu, Mazrui ana kusifu kwa kuandika vizuri juu ya waswahili. Unadhani kwa nini hakutumia neno waislamu?

Tunahitaji kuwa sensitive ktk mazungumzo na hata ktk uandikaji ili tusiwatenge wengine kama inavyotokea ktk mjadala huu. Utaninyima utashi wangu wa kupenda mtu kwa utumishi wake, pale unapo amplify dini kama kigezo cha mafanikio ya utendaji wa mtu. Kiuhalisia hakuna mchango wowote wa dini ktk mafanikio ya utendaji wa kazi ya serikali.
 
Sema ulikuwa humjui usiseme alikuwa hajulikani.

Anaesema kaonewa ni Rais jana hukumsikia Jana Darajani "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"
Wewe tukikuuliza ututajie Wamiliki wa Newcastle unaamini Dau ni mmiliki kwa kuwa tu "anajifanya na busara kutokanusha?"
Sikufahamu lakini inaonekana umemjua Dau baada ya kujiunga NSSF.
Ishu ya Dau imeshajadiliwa sana na majibu yako mengi kama zilivyo shutuma nyingi ila unachopaswa kujiuliza ni kwa nini Rais aliamua kumwita Dau ni Mnyonge mnaetaka kunyonga lakini anawakumbusha kumpa haki yake?
Hata kwangu Dau was nothing! Eleza alitoka wapi hadi sisi wa TZ tumfahamu? He was not a public figure for recognition!
 
Sema ulikuwa humjui usiseme alikuwa hajulikani.

Anaesema kaonewa ni Rais jana hukumsikia Jana Darajani "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"
Wewe tukikuuliza ututajie Wamiliki wa Newcastle unaamini Dau ni mmiliki kwa kuwa tu "anajifanya na busara kutokanusha?"
Sikufahamu lakini inaonekana umemjua Dau baada ya kujiunga NSSF.
Ishu ya Dau imeshajadiliwa sana na majibu yako mengi kama zilivyo shutuma nyingi ila unachopaswa kujiuliza ni kwa nini Rais aliamua kumwita Dau ni Mnyonge mnaetaka kunyonga lakini anawakumbusha kumpa haki yake?
Very low thinking! Unaingiza hili na lile ili iweje? Unaandika yasiyonihusu nikusaidie nini? Kama wewe ulimjua Dau ktk mizunguko yenu, ulitegemea nami nimfahamu? Nini cha m,aana alichowahi kufanya hadi nimfahamu. Dau tumemsikia hivi karibuni kwa hayo niliyokutajia sasa wewe unalazimisha eti mimi. Una elimu gani wewe?
 
Siku ujinga ukikutoka na kugunduwa hawa wazee ID yao ni Utanganyika na si uislamu basi utaifurahia dunia na utaona ni mahala pema pa kuishi.

Unaweza kunitajia katika hao wazee kuna aliyepigana vita ya majimaji?

Ukitaka uheshimike na kama una nia njema andika watu walioshiriki harakati za uhuru unaowajuwa wewe na siyo dini zao, utadharaulika na tutakuona ni mpuuzi tu sawa na wapuuzi wengine.

By the way wajurishe waislamu wenzako wa kariakoo kwamba daraja si la Dau bali la Nyerere.
Shekhe mohammed said ameeleza vzur sana lkn hutak au unafanya makusud hutak kuelewa wakat huo waloanzsha taa na bdae tanu asilimia kubwa ni waislam na hata wakat wa mikutano ilianza dua ndo watu wanahutubia inamaanisha ustaarab wa kiislam ulitamalak sana na hata nyerere alikarbishwa na waislam na wakampa heshma rejea hotuba yke alivyofunga bagamoyo jua historia ni mwalim mzur ikipotoshwa tu kizaz chetu nacho kitapotea
 
Very low thinking! Unaingiza hili na lile ili iweje? Unaandika yasiyonihusu nikusaidie nini? Kama wewe ulimjua Dau ktk mizunguko yenu, ulitegemea nami nimfahamu? Nini cha m,aana alichowahi kufanya hadi nimfahamu. Dau tumemsikia hivi karibuni kwa hayo niliyokutajia sasa wewe unalazimisha eti mimi. Una elimu gani wewe?

Umesema Dau alikuwa hajulikani nimekukosoa sema ulikuwa humjui usijipe uwakilishi wa kusema hajulikani. Jisemee wewe au kikundi chako kuwa ulikuwa humjui.
 
Ni vizuri kutoa mchango wako kadri unavyofahamu historia ya sehemu fulani. Ktk maelezo yako, umeona tofauti yako na Mazrui? Wakati kitabu chako kinaandika juu ya uislamu, Mazrui ana kusifu kwa kuandika vizuri juu ya waswahili. Unadhani kwa nini hakutumia neno waislamu?

Tunahitaji kuwa sensitive ktk mazungumzo na hata ktk uandikaji ili tusiwatenge wengine kama inavyotokea ktk mjadala huu. Utaninyima utashi wangu wa kupenda mtu kwa utumishi wake, pale unapo amplify dini kama kigezo cha mafanikio ya utendaji wa mtu. Kiuhalisia hakuna mchango wowote wa dini ktk mafanikio ya utendaji wa kazi ya serikali.
MchunguZI,
Kuna kwingi Prof. Mazrui kawataja Waislam na Uislam.
Pitia vitabu vyake na mihadhara yake.

Nami niulize.

Kwani ilipoandikwa historia ya TANU na harakati za
kudai uhuru na Waislam wakaachwa kutajwa ni kuwa
wale waandishi waligopa kuitenga jamii nyingine?
 
Very low thinking! Unaingiza hili na lile ili iweje? Unaandika yasiyonihusu nikusaidie nini? Kama wewe ulimjua Dau ktk mizunguko yenu, ulitegemea nami nimfahamu? Nini cha m,aana alichowahi kufanya hadi nimfahamu. Dau tumemsikia hivi karibuni kwa hayo niliyokutajia sasa wewe unalazimisha eti mimi. Una elimu gani wewe?

Mkuu huyo jamaa nilimwambia arudi shule akasome nilishindwa kufanya nae majadiliano
 
Huyu dau jamani kavur
Kabisa Shekhe wangu Kwenye ukweli uongo hujitenga wanamsingiza sana Dr Dau lkn wanamsingizia kwa chuki zao tu lkn mola atadhihirisha ufalme wke na uongo utajulikana tu Inshaallah

Inshallah mwisho wake ni ubalozi lupango
 
Jiwe la msingi kaweka Kikwete ... Jina liwe la Nyerere? ... Nchi hii itaendelea kuangamia kwa ubaguzi wa kipuuzi kabisa ... Kudos Dr. Dau .... Pole sana Rished Bade ... Tunajua kinachoendelea ...
 
Pole kitilya,pole mramba,pole dau,pole kilango poleeeni,bade ulikuwa ni misheni ya jk na rizi ili waweze kuoitishia makontena,ona sasa makontena zaidi ya 11 elfu yalipita bila kodi ingekuwa China za hizi kichwa cha bade ningekuwa kimetenganishwa na mwili
 
Pengo et al wamepitisha makontena mangapi so far? Tafakari ... tumia akili ....
 
Back
Top Bottom