Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,806
- 31,823
‘’Wastara haumbuki,
Wa mbili havai moja…’’
Haya ni baadhi ya maneno kwenye nyimbo niliyokuwa nikiisikia katika gramaphone nyumbani kwetu wakati nikiwa na umri mdogo sana. Mama yangu akipenda kuuimba mwimbo huu kila afanyapo kazi iwe kupika au kufua. Kuna beti za mwisho nazikumbuka na nikizpenda sana. Zilikuwa na maneno haya:
''Kwetu Congo natumaini,
Kwetu Kongo natumaini.''
Beti hizo nilizipenda kwa kuwa akifurahi alikuwa akiniadhimisha kwa kuniambia kuwa mimi nimetoka Congo.
Wakati huo Bi. Hawa biti Maftah mwanamke wa Kimanyema akimuimbia Nyerere mwimbo
maarufu katika mikutano ya TANU Mnazi Mmoja: ''Hongera mwanangu hongera...''
Wakati ule Dar es Salaam ilikuwa ndogo na jamii ya Kimanyema mjini ilikuwa na hadhi ya kipekee.
Kuanzia wanawake wao hadi wanaume.
Kubwa ni yale maumbo makubwa ukimouna mwanamke wa Kimanyema kapanda ana futi
sita na mwanamme halikadhalika.
Basi nilikuwa nizkizisikia beti hizo mama akiziimba nikawa nasisimkwa na mwili.
Nilipopata umri na kila nilipokutana na shida za dunia khasa katika mambo ya hasad na mengine kazini na kwengineko, vikwazo na nini... mama yangu akinambia: ''Wa mbili havai moja.''
Maana yake ni kuwa ikiwa Allah kakuandikia kupata ndivyo itakavyokuwa hivyo hivyo hata zije fitna kiasi gani.
Ndipo hapo inaingia, ''Wastara haumbuki.''
Yaani hutoweza kumfedhehesha aliyenyanyuliwa.
Fuatilia ukurasa huu...