Pohamba,
Mimi nimefanya kazi na Dr. Dau mie nikiwa ofisa mdogo katika idara yake.
Siku moja wakubwa wenzake wakawa wanamsema kuwa kaja kunufaika
bandarini.
Mimi sikuweza kustahamili.
Nikawaambia kuwa kwa ''standard,'' za hapa kwetu Dar es Salaam Dr. Dau
katoka ukoo unaojiweza sana kiasi hata darasa la kwanza kasoma Aga Khan
sio Kinondoni Primary School kama Mohamed Said au Makurumula na Mzimuni.
Nikawaeleza kuwa Dr. Dau anasoma anaendesha gari yake mwenyewe kapewa
na baba yake.
Mohamed Said kapanda sana gari hii.
Nikaendela kuwaeleza kuwa na baba yake ana majumba kadhaa hapa mjini.
Nikawamalizia kwa kuwaambia kuwa wasidhani kuwa suti Dr. Dau kaja kuvaa
hapa Bandarini.
Dr. Dau akivaa suti na tai toka utoto wake.
Ndiyo ile unavyomuona yuko ''dandy.''
Jamaa walibaki kinywa wazi.
Sahihi kabisa! Kuna mtu kaandika eti Dau kajiunga NSSF hata Nyumba yake haina lipu. Hahaha kweli Chuki ni ugonjwa!