DR. Mwakyembe na Natural Justice

DR. Mwakyembe na Natural Justice

Uchunguzi huwa unafanyika pale mtuhumiwa anapokua hana cheo chochote.

1.lowasa alikuwa pm.so ili uchunguzi uweze kuwa ni wa huru pia wa haki ni lazima angejiuzulu kupisha uchunguzi(iwapo yeye ndiyo aliyekuwa anatuhumiwa mean e.l)

2.kilichoundiwa tume ni kampuni ya richmond na si lowasa ambaye alikuwa ni pm wakati ule.
Kwaiyo kumlaumu mwakyembe haina sana mashiko.ni kukosa hoja.

Mwakyembe tumlaumu kwa kuficha baadhi ya ushaidi na tumlaumu sita kw kuuzima bungeni.
 
Wandugu, mimi naona kuwa: Ripoti ya Mwakyembe ilikuwa katika mazingira ya ki-sheria na ki-siasa kwa wakati mmoja
(1) Ki-sheria: Mwakyembe alitakiwa 1. ku-exhaust taratibu zote za uchunguzi ili ku-pre-empt possibility ya mtu kulalamikia uchunguzi juu ya mkataba wa Dowans 2. kutowa haki ya natural justice kwa EL ...pengine na na mh kikwete (Kiranga) 3. ku-act profesionally
(2) Ki-siasa kwa maana kwamba 1. alitakiwa kulinda chama chake na serikali yake 2. kuwa na heshima kwa waziri mkuu na rais 3. ku-act profesionally and politically at the same time

Lakini kuna school of thought inayodai kuwa Ripoti ya Mwakyembe ilikuwa profesionally conducted (M/Kijiji), ilifuata hadidu za rejea zilizotolewa na Bunge, na EL hakuwamo katika hadidu za rejea lakini, hata hivyo bado alipewa fursa ya ku-excercise natural justice ndani ya bunge, na badala yake:
(1) EL hakuitumia hiyo fursa, aliamuwa mwenyewe kwa hiari yake kujiuzuru
(2) Alikuwa na kila fursa aliyohitaji ndani ya Bunge kupinga, kuzuwia, kujitetea, lakini yeye alichagua kulalamika tu na kisha akaamuwa kujipima na kujiuzuru huku akiacha fursa zilizopo zikimshangaa kwa nini hataki kuzitumia...!!!!
(3) Aliacha kusema ndani ya Bunge mambo aliyoyasema kwenye NEC na kwenye vyombo vya habari kama namna pekee iliyosalama kisheria ya kujisafisha na kujinusuru na kashfa zao

Katika scenario hizo mbili, mimi naona kuwa:
  • Mwakyembe anahitaji kupewa fursa ya natural justice ndani ya Bunge aweze kujibu shutuma zinazoelekezwa kwake (pengine na watu wanaotaka kumsafisha EL).
  • Mwakyembe hajapewa fursa hiyo kwa sababu kundi la wanufaikaji wa Dowans wanafahamu kuwa si salama kwao kama atapewa fursa hiyo
  • Hivyo basi fursa pekee anayoweza kupewa ni dozi ya polonium ili kile alichowacha kusema kwenye ripoti yake kisisemwe tena mahali popote na wakati wowote ....
  • Hiyo ni moja ya sababu zilizopelekea Mh Makinda kuwa Madam Speaker
  • Hiyo pia ndiyo sababu Mh Sita alipimwa na kupewa anachostahili...
  • Selileli kwa sababu ya wepesi wake alipelekwa kwao Serengeti kulima mihogo na kukamua maziwa ya ng'ombe na onyo juu ya midomo yao...
 
100% nakubaliana nawe

Labda nijaribu kueleza za wanao mtetea EL

  • Nadhani wana mkubali zaidi EL kuwa ni kiongozi ambaye yupo tayari kufanya maazi magumu kwa manufaa ya walio wengi Maana hii nchi inahitaji kiongozi jasiri
  • Hawaamini kuwa EL pekee yake anasitahiri kubebeshwa lawama za Ufisadi ikiwa ile ilikuwa ni system ilikuwa na watu wengi kama alivyo sema huko NEC kuwa kila hatua Mkuu alijua kinachoendelea
  • Wanasema ndani CCM mtu anayeweza kuingoza hii nchi awe mchapa kazi hivyo EL ni mchapa kazi sijui kigezo wanachutumia (Haya ni badhi tu ya maoni ya watu humuhumu )

Kama mambo ndio hayo basi watetezi wake wamepotoka na yeye mwenyewe amepotoka.

Kama ni kweli EL ndiye pekee mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na ndiye pekee ndani ya ccm mwenye uwezo wa kuiongoza nchi;

Ilikuwaje akashindwa kufanya maamuzi magumu ya kukataa kujiuzulu na kujitetea bungeni kama alivyofanya kwenye vikao vya NEC ya ccm, ili hao wote wachafu waliojazana ndani ya ccm na serikali yake wawajibike?? Kwa kufanya hivyo angekuwa amefanya maamuzi magumu kwa manufaa ya watu wengi, kuliko alivyoamua kujiuzulu kwa manufaa ya mshikaji wake.

Kinachoonekana hapa ni juhudi za makusudi za EL na wapambe wake kutafuta kila mbinu ya kumnasua na scandal ya richmond ili faili lake liwe safi kuelekea kwenye mchuano wa uraisi 2015. Mwakyembe hapa anatumika tu kama bangusilo!!
 
Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.

Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.

Duh! kuwania madaraka kubaya!. Yaani kweli kabisa law ya natural justice huielewi mheshimiwa? kweli kabisa? kutoka moyoni au kutoka TUMBONI?

Haya bana.
 
Ilikuwaje akashindwa kufanya maamuzi magumu ya kukataa kujiuzulu na kujitetea bungeni kama alivyofanya kwenye vikao vya NEC ya ccm, ili hao wote wachafu waliojazana ndani ya ccm na serikali yake wawajibike?? Kwa kufanya hivyo angekuwa amefanya maamuzi magumu kwa manufaa ya watu wengi, kuliko alivyoamua kujiuzulu kwa manufaa ya mshikaji wake.

Naomba nikujibu kifupi tu. Sifahamu uwezo wako wa kufikiri au ufahamu ila jibu ni FUPI.

NEC ya CCM ni CLOSED meeting, taarifa zake hazirushwi na vyombo vya habari.

Bunge ni OPEN meeting.

KIongozi hawezi kuanika mambo ya ndani hadharani kama unavyofikiri.
 
Lakini kuna school of thought inayodai kuwa Ripoti ya Mwakyembe ilikuwa profesionally conducted (M/Kijiji), ilifuata hadidu za rejea zilizotolewa na Bunge, na EL hakuwamo katika hadidu za rejea lakini, hata hivyo bado alipewa fursa ya ku-excercise natural justice ndani ya bunge, na badala yake:
(1) EL hakuitumia hiyo fursa, aliamuwa mwenyewe kwa hiari yake kujiuzuru
(2) Alikuwa na kila fursa aliyohitaji ndani ya Bunge kupinga, kuzuwia, kujitetea, lakini yeye alichagua kulalamika tu na kisha akaamuwa kujipima na kujiuzuru huku akiacha fursa zilizopo zikimshangaa kwa nini hataki kuzitumia...!!!!

Naomba niulize, Ripoti ya Mwakyembe ilikua na HITIMISHO au ilimuachia Lowassa bungeni aongee ndipo itoe PENDEKEZO au HITIMISHO?

Pia refer hapo juu nilipomjibu Mwita Maranya

Ukishajibu hilo tunaendelea.
 
Wataalamu wa Sheria:
  • Je natural justice ina mipaka- kwamba lazima mtuhumiwa aipate katika mazingira fulani au ndani ya muda fulani?.
  • Je kama Mwakyembe alikanyaga haki hiyo ya EL, je kisheria anaendelea kuikanyaga hadi leo?
  • Je Lowasa ana nafasi ya kuyasema leo yale ambayo angeyasema kama Mwakyembe angempa hiyo ''NJ''
  • Je kwanini EL hataki kusema hata alipopata forum tofauti i.e NEC-
  • Kama EL atayasema leo je yataleta mgeuko ''twist'' mpya kwenye sakata hili?
  • Je kwanini pia Mwakyembe hataki kusema yale ''mengine'' waliyoyaacha?
  • Je kama Mwakyembe atayasema leo je bado yanaweza kuclear wingu liliopo kuwa EL alionewa? au yatamtia hatiani zaidi EL ?
 
Mimi si mtaalamu wa sheria, lakini haya maswali ni muhimu sana kiasi kwamba hayawezi kuachwa kwa sababu tu mtaalamu hajajitokeza. Kama weledi wangu wa sheria una mapungufu wataalam watanisahihisha. Ndiyo maana ya forum.

Wataalamu wa Sheria:
  • Je natural justice ina mipaka- kwamba lazima mtuhumiwa aipate katika mazingira fulani au ndani ya muda fulani?.
  • Natural justice inatumika sehemu yoyote panapohitajika fairness, panapohitajika kusikilizwa pande mbili za mashauri.
  • Je kama Mwakyembe alikanyaga haki hiyo ya EL, je kisheria anaendelea kuikanyaga hadi leo?
  • Mtu akikosa kukulipa mshahara wa January 2011, hajakulipa mpaka leo December 2011, anakuwa bado hajakulipa. Kibaya zaidi
  • Je Lowasa ana nafasi ya kuyasema leo yale ambayo angeyasema kama Mwakyembe angempa hiyo ''NJ''
    Anaweza, lakini kwenye sheria kuna msemo "justice delayed is justice denied" Hata kitendo cha kumnyima Lowassa haki ya kujitetea kabla ya tume kuandika ripoti kilikuwa ni kuchelewesha haki ya Lowassa na hivyo kumnyima haki.
  • Je kwanini EL hataki kusema hata alipopata forum tofauti i.e NEC-
    Hili ni swali ambalo EL tu anaweza kulijibu. Logically thinking, ukichukua matamshi yake alipojiuzulu, ameepuka damage kwa chama na serikali yake. Kwangu mimi hili linaweza kabisa kuwa kumlinda Kikwete na serikali yake.
  • Kama EL atayasema leo je yataleta mgeuko ''twist'' mpya kwenye sakata hili?
    Hatuwezi kujua kabla hayajasemwa, lakini kuna mambo fulani ambayo yamefanyika ambayo hayawezi kutofanyika tena.Mathalani tumemuona George Bush kampongeza Kikwete kwa kusema, in effect "You fired that thief, god job". Lowasa kashakuwa tainted, kashajiuzulu etc
  • Je kwanini pia Mwakyembe hataki kusema yale ''mengine'' waliyoyaacha?
    Kwa sababu si muwazi na kuna vitu/watu analinda
  • Je kama Mwakyembe atayasema leo je bado yanaweza kuclear wingu liliopo kuwa EL alionewa? au yatamtia hatiani zaidi EL ?
    Hatujui mpaka yasemwe, lakini kuna mambo hayawezi kufutika kama nilivyosema hapo juu.
 
Mwakyembe alishasema kwamba natural justice inakuwa ktk two principles!
1)ya kwanza ni kumhoji mtuhumiwa

2)ya pili ni kama umeridhika na ushahidi uliotolewa,haina haja ya kumhoji mtuhumiwa!
Je,mwakyembe ali2mia ipi kati ya izo principle mbili?
 
Naomba nikujibu kifupi tu. Sifahamu uwezo wako wa kufikiri au ufahamu ila jibu ni FUPI. NEC ya CCM ni CLOSED meeting, taarifa zake hazirushwi na vyombo vya habari. Bunge ni OPEN meeting. KIongozi hawezi kuanika mambo ya ndani hadharani kama unavyofikiri.
FairPlayer, naomba tuwe fair katika jambo hili...

Kama Bunge ni open meeting, je
  1. ni mambo gani ambayo ni siri na hayapaswi kujadiliwa pale kwenye open forum?
  2. agenda ya dowans ni siri ? Je haikupaswa kujadiliwa ndani ya Bunge?
  3. Kwanini sasa kamati ya Mwakyembe iliundwa na chombo ambacho kinajadili mambo yake openly kuchunguza jambo ambalo ni siri?
Mimi nadhani mambo ambayo hayapaswi kuanikwa kama unavyotaka ni mambo ya ufisadi unaofanywa na viongozi wetu. Ndiyo maana NEC ya CCM ambayo ni closed meeting kimeshindwa kuyagusa mambo ya ufisadi hadi leo pamoja na kuwepo kelele zinazosikika katika nchi nzima. Lakini Bunge ni chombo maalum chenye sauti ya wenye nchi, hakiwezi kuzuiwa kujadili baadhi ya mambo kama unavyopendekeza...wananchi wakitaka hata rais atachunguzwa tu...

Wazo lako lingefaa kutolewa na dada RACHEL na siyo wewe mkuu. Dada RACHEL anajitahidi kuzuwia kuanikwa kwa habari zote za ufisadi kwa njia zote, ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya watu, nafasi za kazi za watu na matumizi makubwa ya pesa. Sijuwi kama kweli kuna mafanikio katika mikakati hiyo...
 
Our country has the best and qualified workforce and only those with proven experience head the department. Problem is most ministers representing those ministries have no idea what their role is except to grab for themselves in the name of their constituencies. Most of them have no idea of what govt budget is, except what they want, just like many people who dont want to work for money but they want to spend.

They use the civil servants to achieve their goals. Politicians come and go after messing the system. I would be very happy if in future the Tanzanians pass a law that require the future presidents to have been a civil servant just like they do in Japan.
 
Wazazi wetu walitupeleka shule ili tusiwe akina "Yohana Mjinga"
 
Mwakyembe (na usomi wake wote) mpumbavu -sio mjinga-. As in idiot, and not ignorant. Kashasoma sana kupewa benefit of doubt ya ignorance, kawa muhadhiri wa kutumainiwa ati.

Hili linanifanya nijiulize sana kuhusu quality ya elimun yetu. Kama hata mhadhiri maarufu wa sheria anaweza kuchemsha hivi, tutegemee nini kutoka kwa sio tu wahadhiri wetu wapya, bali hata wahitimu wetu wapya.

Yoyote ambayo hujayasema katika ripoti, halafu ukasema "kuna mengine sijayasema katika ripoti" unakuwa ushayasema kwa namna moja ama nyingine. Unakuwa kama yule mkimbizi wa vita aliyelala chini ya nyasi, akasikia adui kauliza "kuna aliyebaki hai tumpe maji?". Akaamini na kujibu "Mimi nipo hai". Akamalizwa hapo hapo.

Kama kuna mambo hayaelezeki katika ripoti, huyazungumzii kabisa. Husemi hata kwamba hayaelezeki, kwa sababu ukisema tu hayaelezeki ushaanza kuyaelezea. Mwanasheria aliyebobea anatakiwa kuelewa hili a la "You have the right to remain silent, anything you say can and will be used against you".

Na kutoka hapo ( statement ya "kuna mengine sijayasema katika hii ripoti") unapata the worst of both words.

Wale waliotaka usiseme watakuona mbaya kwa sababu umesema kuna mengine hujayasema, ume spill beans kwamba kuna zaidi ya uliyoyasema.

Wale waliotaka useme watakuona mbaya kwa sababu umesema kuna mengine hujayasema ambayo wangetaka uyaseme.

mijitu mingine, hovyooo.....pambafu mwenyewe!
 
Hatujali sababu iliyomfanya Lowassa asihojiwe.

Tunajali kwamba Lowassa hakuhojiwa, na kwa sababu hakuhojiwa anasema hakutendewa haki na ripoti nzima imejaa ukungu wa maswali.

Na mwisho wa hii ripoti ya Mwakyembe ni serikali kuvunja mkataba kinafiki na kuwakumbatia wote waliohusika na kulitwisha taifa mzigo wa kuilipa Dowans. shame on us!!!!
 
Kwa hivi vikumbo vya kisiasa, Is just the question of time before the coming election things gona be clear
 
Powered by Translate [h=3]MKE WA LOWASSA AZINDUA KITABU[/h] Mada: LOWASSA , RICHMOND SCAM , ROLE OF RELIGION IN FIGHT AGAINST CRRUPTION IN TANZANIA , UFISADI

Mke wa Lowassa azindua kitabu

Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.

Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.

Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho "Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land" kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. "Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo," alisema.

Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.

Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.

Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.

LET'S BE HONEST.LOWASSA ALIJIUZULU KUTOKANA NA UFISADI WA RICHMOND.HILO HALINA MJADALA.SINA TATIZO NA HIYO ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA ISRAEL.KAMA KWELI ALIENDA KUTUBU AU LA,ANAJUA YEYE NA MUNGU WAKE .LAKINI NASHINDWA KUWAELEWA HAO MAASKOFU WALIOJITOKEZA KATIKA SHUGHULI HIYO.NAELEWA KUWA DINI INAHUBIRI UPENDO NA KUSAMEHE WAKOSAJI LAKINI SIDHANI KAMA HIYO INAMAANISHA VIONGOZI WA DINI KUWA KARIBU NA WATUHUMIWA WA UFISADI.

NA MHASHAMU PENGO ANAPOTOA MFANO WA YESU KUSULUBIWA ANATAKA KUTUELEZA NINI?KWAMBA LOWASSA NAE ALISULUBIWA KAMA YESU?HIVI SIO RICHMOND NA BINAMU YAKE DOWANS ILIYOWASULUBU WALALAHOI WA TANZANIA KWA MAMILIONI YA SHILINGI!YESU ALISULUBIWA MSALABANI ILI KUWANUSUBURU WANYONGE,MASIKINI,WAJANE,YATIMA,NK KUTOKA KWA MINYORORO WANAYOFUNGWA NA MAFISADI.

JAPO NINA HESHIMA KUBWA KWA VIONGOZI HAO WA DINI LAKINI YAYUMKINIKA KUELEZA KWAMBA UHUDHURIAJI WAO HUO KATIKA HAFLA YA MTUHUMIWA WA UFISADI UNAWEZA KUTAFSIRIWA NA WAUMINI WAO KUWA NAO WANASAPOTI UFISADI.

IN A WIDER CONTEXT,UFISADI NI MATOKEO YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI YA KIROHO.KITACHOTUPA IMANI KUWA WATUHUMIWA WA UFISADI WAMEAMUA KUMREJEA MUNGU SIO PUBLICITY STUNTS BALI FIRM COMMITMENT KATIKA KUHURUMIA NAFSI NA ROHO ZINAZOANGAMIA KUTOKANA NA MATENDO YA MAFISADI HAO.

Source:MKE WA LOWASSA AZINDUA KITABU ~ Kulikoni Ughaibuni
 
Je Lowassazi aliwaambia nini viongozi hawa wa dini hadi wakaamua kwenda nyumbani kwake?. Navyofahamu kiongozi kama Kardinali sio rahisi sana kwenda nyumbani kwa mtu kwa ajili ya tukio kama hilo labda iwe msiba. Kumbuka tukio hilli lilitokea muda mfupi baada ya EL kujiuzulu na kipindi hicho hata mtoto mdogo alijiua EL kajiuzulu sababu ya kushiriki katika Richmond- kiufupi kila mtua lijua Lowassa ni ''fisadi''.

Cha kushangaza aliwashawishi vipi, alijenga hoja gani mpaka hawa maaskofu na Mwakasege (mtu makini sana) wakamwelewa na hata sasa wameendelea kumuelewa.? Nikifika hapa huwa nachoka kabisa, nikikumbuka kauli ya Mwakyembe kuwa kuna mengine wameyaacha kulinda serikali, najiuliza serikali ipi? nani zaidi ni serikali kama PM kajiuzulu? Haya juzi juzi tena kule NEC EL kasema hadharani '' Rais unajua vizuri hili suala la Richmond nilikushirikisha kila hatua''- hapo ndo nachanganyikiwa kabisa.

Kuhusu Mwakyembe, kuna maneno mengi sana yamesemwa kuwa ugonjwa wake unatokana na kupewa sumu, baadhi ya watu wamehusisha suala hilo na Richmond saga. Je kama Mwakyembe atasema ugonjwa wake ni sumu, nadhani sasa makachero wa JF na wengine wataanza kufanya upelelezi kama kupewa kwake sumu kunahusiana na Richmond saga, na specifically kubaini nani kampa sumu kwasababu ndani ya Richmond kuna kambi nyingi .

Je ni kwasababu ya kusoma ile ripoti au ni kuyaacha mambo mengine?
 
Naomba nikujibu kifupi tu. Sifahamu uwezo wako wa kufikiri au ufahamu ila jibu ni FUPI.

NEC ya CCM ni CLOSED meeting, taarifa zake hazirushwi na vyombo vya habari.

Bunge ni OPEN meeting.

KIongozi hawezi kuanika mambo ya ndani hadharani kama unavyofikiri.

FP,

Huna sababu ya kuhoji uwezo wangu wa kufikiri, unatakiwa kujibu hoja. Kama kila mtu ataanza kuhoji uwezo wa mwenzake, tutaishia kufanya mipasho badala ya mjadala.

Kama kamati ya mwakyembe ilisoma ripoti yake kwenye open forum, Lowasa akapewa nafasi ya kuzungumza kwenye open forum kwa mujibu wa taratibu za bunge, lakini akaishia kulalamika badala ya kutoa utetezi wake, halafu wewe unataka kutushawishi kwamba bungeni hapakuwa mahali sahihi pa lowasa kuusema ukweli, basi nami nalazimika kuhoji uwezo wako wa kufikiri na ufahamu wa mambo.

Sakata la richmond lilitokea bungeni na ndipo lowasa alitakiwa kujieleza lakini hakufanya hivyo. Kwenda kulizungumzia sakata hilo kwenye kikao cha nec, miaka mitatu baada ya kubwaga manyanga ni dalili8 tosha kwamba anafanya hivyo kutafuta huruma ya chama chake ili kimsafishe na aweze kufikia ndoto yake ya kuwania na hatimaye kuwa raisi wa nchi hii. Kama angekuwa kiongozi makini, na kama angekuwa hakuhusika na richmond, angejitetea pale pale bungeni. Lakini kwakuwa alihusika, hakuwa na njia nyengine zaidi ya kubwaga manyanga, na huo ndio ukweli mnaojaribu kuupotosha, wakati kila mtu anayetumia vizuri bongo yake anafahamu.

Kwa mtu anayelitazama sakata hili la lowasa kushindwa kuzungumza madudu ya richmond bungeni na kukimbilia kwenye chama, halafu wanaibuka watu kutaka kumsafisha kwamba hahusiki, hashindwi kuona ni kwa namna gani watu mnavyochezeshwa muziki msioufahamu.
 
Mkuu,

Pamoja na ukweli wote uliouleza hao jamaa hawawezi kukuelewa kwa sababu wana kazi moja tu, kumsafisha mfadhili. Kwanza huo usiri wa NEC uko wapi wakati siku hiyo akiongea aliacha simu zake wazi akiwa ameziunganisha na mhariri mpambe wake!!!

Pili huko NEC wanakojengea hoja kwamba alipasua jipu, ni jipu gani hilo mbona hasemi alivyotuingiza kwenye mkataba amekazana na kuvunja mkataba. Watu wanasimamia utetezi wa kumpigia simu JK kuhusu kuvunja mkataba, tangu lini serikali ikaendeshwa kwa simu!

Inasikitisha kuona watu wamekazana kulazimisha uongo uwe ukweli utadhani Tanzania bila EL haiwezekani.

Lowasa alipima, akijiona ni mhalifu akajiuzulu, hakuna aliyemlazimisha, na hicho ndio kitanzi chake atakachokufa nacho, na kila anapohangaika kukitanzua ndivyo anavyokikaza zaidi!!!
 
Nyongeza ni kuwa Lowassa amekuwa mbunge kwa muda mrefu na alikuwa ni Waziri Mkuu; kama angetaka Bunge likae kama kamati maalum tena katika "closed session" angeweza kutoa hoja na kueleza sababu. Lowassa hakutaka kujitetea Bungeni kwa sababu alijua ni mahali pekee ambapo wenzake nao wanaweza kutumia haki hizo hizo. Watu wengi wanajifanya wamesahau alipotoa hoja ya "magazeti ya mitaani" alipojibiwa na Lucas Selelii mle mle Bungeni!

Lowassa hakuonewa na issue ya natural justice haipo. Alijiuzulu pasipo kuhukumiwa baada ya kujipima yeye mwenyewe na kuamua kuwa ni bora kujiuzulu kuliko kujitetea mbele ya Bunge ambako alituhumiwa na ambacho ndiyo chombo pekee ambacho kingeweza kumcondemn!
 
Back
Top Bottom