DR. Mwakyembe na Natural Justice | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR. Mwakyembe na Natural Justice

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kintiku, Dec 23, 2011.

 1. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  ''Silence reigned in the House as the PM read his speech and accused the committee of violating principles of natural justice by condemning him unheard, despite the fact that the allegations leveled against him were serious. ‘I would like to thank Dr. Harrison Mwakyembe for his presentation. Mwakyembe, a university lecturer in the department of law is aware of the law of natural justice, yet he refused to seek my response over the allegations`` Lowassa said.
  (OPEN HEART, OPEN MIND: JK avunja Baraza la Mawaziri)
  [FONT=&amp]
  SITALIPIZA KISASI[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari wa IPP, aliweka mbele nguvu za Mungu, ambapo alisema kama kuna watu walitaka kumuangamiza anawasamehe na hana sababu ya kulipiza kisasi."Sitalipiza kisasi hiyo sio kazi yangu bali Mungu anajua cha kufanya na watu wenye kulipiza visasi maisha yao sio marefu," [/FONT]​
  [FONT=&amp](VIJIMAMBO: Mwakyembe aunguruma)[/FONT]

  What are the rules of natural justice?

  The principles of natural justice concern procedural fairness and ensure a fair decision is reached by objective decision maker. Maintaining procedural fairness protects the rights of individuals and enhances public confidence in the process. A word used to refer to situations where audi alteram partem (the right to be heard) and nemo judex in parte sua (no person may judge their own case) apply.

  Kutokana na matukio ya hivi karibuni mpaka sasa nampa Lowasa ‘the benefit of the doubt'', kwasababu inawezekana kweli kamati ya Mwakyembe haiku exercise natural justice. Kama Mwakyembe yeye mwenyewe ameshindwa kujipa natural justice je ataweza kumpa mtu mwingine?. Watu wameongea kuhusu ugonjwa wake, , watu wamenusurika kuuwawa na kupoteza kazi kwa ajili yake, watu wamefunga na kuomba kwa ajili yake ili tu Mungu ampe uzima na aseme kuhusu sababu ya ugonjwa wake.

  Lakini cha ajabu yeye anarudi anasema sitalipiza kisasi! Kwa maana nyingine tayari kisha jenga visasi na watu. Maana yake nini? Je Mwakyembe anaweza kulipa kisasi? Ana nguvu gani za kumlipa kisasi mtu aliyetaka kumuua?. Je kisasi cha mtu anayetaka kukutoa roho ni nini?. Kwa utaratibu wa natural justice mtu hawezi kuwa hakimu wa kesi yake mwenyewe. Inatkiwa aseme anayoyajua kuhusu ugonjwa wake, kisha sisi wananchi (natural court) ndo tutoe maamuzi. Kwanini hataki kuwa muwazi kama hajalishwa sumu mambo ya visasi yanatoka wapi? Na kama ni sumu kwanini hataki kusema ukweli?. Mtu mwenye PHD ya sheria ni mtu ambaye anatakiwa kuwa sio muoga na kikubwa asimamie ukweli daima. Sasa hizi kauli za ''kiswahili'' kuwa sitalipiza kisasi maana yake nini?

  Amesema ameiachia serikali; hakuna mtu anaweza kujali uhai wa mtu mweingine. JB katueleza humu kuwa LTK's ndo wanaohusika, halafu leo yeye anatuambia ameiachia serikali sisi tumueleweje?. Toka nimezaliwa sijawahi kusikia serikali au bunge likitangaza ripoti ya ugonjwa wa mtumishi wake, kwanini iwe kwa Mwakyembe tu? Ingekuwa bora asingetoa kauli ya kusema hatalipiza visasi, angewashukuru watz basi ingetosha. Kama anaficha mambo ya kuhusu uhai wake mwenyewe, angeshindwa vipi kuficha mambo mengine ya Richmond kama alivyosema mwenyewe bungeni?

  Nashauri Dr . Mwakyembe atoe ultimatum kwa serikali kuwa isipotoa tamko kuhusu ugonjwa wake kufika muda fulani i.e 5[SUP]th[/SUP] January 2011, basi yeye ataitangaza ripoti ya ugonjwa wake. Hebu awasikilize hata wanafamilia na rafiki zake, na ndugu ambao wanataka aweke wazi ripoti ya ugonjwa wake kama alivyofanya kuhusu ajali na ''Alshababy"
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Inaweza kuwa kweli kuwa hatalipiza kisasai, lakini aseme tu ni nani!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  kuwa mwakyembe hakumuhoji Lowassa kwenye ile kamati...yet watu wanaisifia ile kamati ..imetuacha uchi wa mnyama!!
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,028
  Likes Received: 7,422
  Trophy Points: 280
  Ukimnyima mbongo chakula inaweza isiwe issue, lakini ukitaka kumtesa na kumsababishia mahangaiko moyoni basi mnyime maneno....yaani mnyime kile ukijuacho, atahangaika sana.
   
 5. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mwakyembe ni kiongozi wa umma, kiutaratibu, taarifa (report) kuhusu ugonjwa wake inapaswa itolewe na daktari wake/ waziri wa afya/ msemaji wa familia... zaidi ya hapo sioni cha kumlaumu DR.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,975
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii.
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,975
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Alitawaliwa na woga toka mwanzo au alitishwa.
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ndo mana mleta mada kamshauri mwishoni kua aitake serikali hadi tar 5 january itoe tamko otherwise ripot ataitoa mwenyewe ndo matatizo ya kusoma tu heading halafu unadandia kujibu
   
 9. k

  kuzou JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa hana record ya uchapakazi serikalini ni lbd ukosoaji ndo unampa chati.kapewa wizara fanya kazi tukuone basi kama unafaa si kulaumu watu nini mafisadi.si upo serikalini tumia nafasi yako sema.kazi kuwasema watu tusowajua ni kama unatufikiriiisha kitu kisichokuwepo
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.

  Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaomfahamu Dr. Harisson George Mwakyembe, uwezo wake wa kitaaluma na uwezo wa kujenga hoja, hawezi kutishwa na mtu kama Lowassa ambaye ni average mind na ambaye uwezo wake wa mambo ni wa chini sana, kutokana na ufinyu wake wa kujenga hoja (eloquence). Mwakyembe yuko streets ahead katika kila jambo la kitaaluma.
   
 12. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sio kila anayepinga CCM yuko Upinzani (CHADEMA), na siyo kila anayepinga CCM yuko Upinzani wengine wanapinga wakiwa ndani ya hivyo vyama. So kila anayesema mawazo tofauti kuhusu Mwakyembe basi ni mfuasi wa Lowassa, na kinyume chake ni kweli.

  Mimi nina msimamo wa kujitegemea, husema jambo kulingana na ukweli unaoprevail kwa wakati huo, kwa hiyo ni makosa kunisema ni mfuasi wa Lowassa. Ukisoma vizuri nilichoandika unaweza kuona kuwa ni njia ya kistaarabu ya kumprovoke Mwakyembe aseme.....
   
 13. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Mwakyembe ni mnafiki mkubwa!
  Bado ninasubiri kwa hamu atuambie yale aliyo yaficha kwa kulinda heshima ya serikali!
  Sina shaka na uchafu wa LOWASSA,ila nina shaka na ripoti ya kamati teule ya mwakyembe!
  Nahisi walisiliba matope juu ya mwili mchafu wa LOWASSA!
   
 14. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa........................huyu jamaa anatuhangaisha sana.........kweli bora atunyime mchele wa Kyela kuliko habari....maana information is power lakini chakula is energy. Weye wataka power au energy?
   
 15. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Red = Ili iweje - shughulikia akul ya watoto wako na wewe mwenyewe kuliko kupoteza muda kwa kujaribu kupasua mwamba kwa kutumia kichwa
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Regardless ya Lowassa alikuwa mchafu au sio, hili swala la kutopewa nafasi ya kuhojiwa mie nililibonda tangu mwanzo. Limeweka a dark cloud of questions of integrity over the report and its intentions kiasi kwamba hata kama imefanya kazi nzuri kuna technicality ya kuidoubt.

  Ni kama kumkamata mtu kwa kutumia wiretap ambayo haijapata proper warrant, hata kama unamnasa mtu anasema implicating things, anaweza kukushinda kwa technicality kwamba "the evidence is inadmissible because it is illegal"

  Mwakyembe kwa kutomhoji Lowassa prior to writing the report kajiweka katika position hiyo hiyo ya kuwa dismissed on a technicality.

  Ila hili jambo kwangu binafsi haliwezi kuondoa ukweli kwamba Lowassa ni corrupt, na hivyo haliwezi kumsafisha.
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mbopo,

  Tangu Ripoti ya Mwakyembe itoke kuna mambo mengi sana yametokea na yana ashiria kuna uvundo mwingi sana ambao ulifichwa ili usijulikane kwa watu. Hoja ya Waberoya hailengi kumtetea Lowassa au kukubaliana na utetezi wa Lowassa. Hoja kuu hapa ni kwamba kuna mambo yalifichwa kwa malengo fulani.

  Moja, Lowassa anadai hakuhojiwa na Kamati Teule ili na yeye aeleze upande wake na hivyo Kamati Teule iwe na ripoti yenye maelezo ya wahusika wote. Kuna dots nyingi sana ambazo zinahitaji maelezo kwamba ni kwanini Lowassa hakuitwa kuhojiwa. Hoja ya kwamba ni Waziri Mkuu, haikuwa na mashiko.

  Mbili, baada ya JK kurudi Dar, akiwahutubiwa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alisema kwamba Lowassa amepata "ajali ya kisiasa". Hiyo kauli ilikuwa na maana pana sana na mpaka leo hii watu wanajiuliza maswali mengi sana.

  Tatu, Lowassa akiwa anajitetea kwenye kipindi cha TBC, matangazo yake yalikatishwa ghafla bila hata kutoa taarifa. Hilo nalo linaweka alama kubwa ya kuuliza.

  Nne, Dr. Mwakyembe kwa nyakati tofauti amesikika akisema kwamba kuna mambo ambayo hawakuyaweka kwenye ripoti kwa kuwa wangeyaweka wangeivua nguo serikali au kwamba walikuwa wanalinda heshima ya serikali, je ni serikali ipi na yupi hasa waliyekuwa wanamlinda.

  Ukiunganisha hizo dots nne tu unaweza kukuta kwamba Mwakyembe na wenzake walisita kumwita Lowassa kwa lengo la kuilinda Ikulu kwa kuwa kama angeitwa basi lazima na Ikulu nayo ingehusishwa moja kwa moja. Lowassa juzi kasema kwamba alijiuzulu ili kulinda heshima cha chama na serikali. Lakini ukweli ni kwamba alikuwa analinda heshima ya mkuu wa kaya na ndio maana wameshindwa kumvua gamba.

  Swala hapa sio Lowassa, swala ni ukweli ulio ndani ya Ripoti ya Mwakyembe. Ukiichunguza sana na ukaangalia mwenendo wa swala zima unapata mashaka sana.

  Bunge lilipendekeza watu wengi sana wachukuliwe hatua kinidhamu na ikiwezekana kufikishwa mahakamani. Naomba niambie kati ya hao wote waliotakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu, ni nani alichukuliwa hatua ya kinidhamu na ni hatua gani ilichukuliwa? Dr. Mwakapugi alistaafu na kupewa haki zake zote. Mwanyika alistaafu na kupewa haki zake zote. Dr. Hosseah mpaka leo bado anadunda kama DG-PCCB. Bashir Mrindoko mwaka huu amepewa u-Naibu Katibu Mkuu. Kwanini serikali ilipata kigugumizi kuwachukulia hatua hao wote ambao walishiriki kwenye huo mchakato? Hilo pekee linatakiwa kukupa alama kubwa ya kuuliza.

  Hakuna mtu anamtetea Lowassa, bali watu wanataka ukweli. Ripoti ya Mwakyembe ilisema mambo nusu ili kuilinda Ikulu na ndio maana Mwakyembe amebaki kuwa ni mtu wa kusema, nitasema ukweli, mara sijui warudishe hoja Bungeni ili tuseme kila kitu. Kwanini hakusema kila kitu tangu mwanzo?
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwenye tume ile watu walipitia, waliona official document na correspndence nyingi Ndio maana pamoja na kujaribu kuwadaaa wahojiwa jinsi ya kujibu maswali haingesaidiana haikusaidia sana.
  NDio maana wahojiwai wengine walijaribu kupotosha lakini Official document ambazo haziongei lakini ziko kwenye rekodi zilifunua mengi.

  Labda kwa kutokumuhoji Lowasa ilikuwa kwa manufaa yake mwenyewe na U PM asiadhirike . Lowasa hakuhojiwa sio kwa sababu alitaka kukomolewa . No hakuhojiwa ili alindwe au walindwe ( yeye na JK) Na ndio maana hadi sasa anapaza sauti.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hatujali sababu iliyomfanya Lowassa asihojiwe.

  Tunajali kwamba Lowassa hakuhojiwa, na kwa sababu hakuhojiwa anasema hakutendewa haki na ripoti nzima imejaa ukungu wa maswali.
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Si lazima kuangalia au kuhoji mambo kwa upande mmoja wa shilingi.Mimi nietoa possble scenario ambayo inawezekana ilitumika kutoumhoji Lowasa kwa faida yake mwenyewe. Hakutendewa haki kivpi na Yeye ni waziri Muu na ripoti iisomwa bungeni. Kwa nini hakujibu au kujitungia maswali na kuyajibu bungeni ili wanachi wajue ukweli tofauti na uwongo wa tume uliosowa bungeni.

  Badala yake yeye akaamua kuzira. Na ukungu wa maswali hata angehojiwa lowasa ulikupwepo na utakuwepo sababu kuna wengine walipewa rehersal laini tatizo ni offiacial document zipo.

  May be ikifika sehemu Lowasa mwenyewe aombe hizo official document zake zote ziwe public
   
Loading...