Kiranga je Lowassa alinyimwa au alikosa nafasi ya kutumia haki ya kujitetea na kujieleza mbele ya Bunge ambalo ndiyo lilimpitisha kuwa Waziri Mkuu? I'm granting you kwamba nafasi hiyo hakupewa kwenye Kamati Teule.
Issue sio kwamba kapewa nafasi bungeni, hilo tushali establish. Katika kutafuta justice, objective sio tu vitu vifanyike, bali pia vifanyike timely. Ndio maana wanasema justice delayed is justice denied, kwa sababu, umeme ukikatika, TANESCO wakichelewa kurudisha umeme unaweza kukuta barafu kwenye friji imeharibika na nyama ishaoza. Kwa hiyo kurudisha umeme ni muhimu, lakini kurudisha umeme timely ni muhimu zaidi.
Hizi processes nyingine ni irreversible, kama kutoa the proverbial genie out of the bottle. Ukishazifanya hurudi nyuma, kwa hiyo nilitegemea Mwakyembe ajue hili na kuhakikisha anakuwa thorough kuhakikisha hakuna mess itakayosababisha integrity ya ripoti yake itiliwe shaka. Hakufanya hivyo.
Sasa wewe mtu kakatiwa umeme, hakurudishiwa timely, by the time karudishiwa nyama ishaharibika. Analalmika "Sikurudishiwa umeme timely, nimeshindwa ku preserve nyama yangu". Wewe unamwambia "Ulirudishiwa umeme, huwezi kulalamika". Tatizo ni timeline.
Kwa wale wanaojua principle ya uongozi ya
"Caesar's wife cannot afford even suspicion of infidelity, let alone actual infidelity", kwamba kiongozi bora hatakiwi hata kuwa implicated na madoa ya scandal, wataelewa kwamba suala zima la Lowassa kuwa implicated katika Ripoti ya Mwakyembe lilimtia mawaa tayari. Yaani hata kama angeweza kusimama bungeni, na kujitetea vizuri, kuna wengine tungebaki na shaka, tungesema Lowassa katumia ukubwa wake tu ku force utetezi.
Kwa hiyo utaona katika situation kama hii, kwa nchi ambayo ina revere viongozi wake kama Tanzania, Waziri Mkuu kuwa implicated tu ni mawaa tosha. Na kwa sababu Waziri Mkuu kuwa implicated tu, hata kama atajitetea vizuri au vibaya, ni mawaa, basi ilitakiwa sana kwa kamati ya Mwakyembe kuhakikisha kwamba haimtii mawaa Waziri Mkuu bila kutafuta habari zote kwa ukamilifu.
Na kutafuta habari zote kwa ukamilifu hakukuwezekana bila kumhoji Waziri Mkuu mwenyewe.
Mwakyembe alichofanya, kaona Caesar's wife yuko implicated katika infidelity, Caesar wife anatembea na bodyguard saa mbaya bustanini, Mwakyembe kaenda moja kwa moja kwenye Senate kapeleka ripoti inayo mu implicate Caesar's wife bila kumuuliza Caesar's wife kwamba alikuwa anafanya nini na bodyguard bustanini. Hatujui pengine Caesar's wife anapanga mipango ya kuficha ugonjwa wa Caesar, na Caesar anajua.
Sasa Caesar's wife kaitwa kwenye Senate ajitetee kwamba hakufanya infidelity, anaona kitendo cha kujitetea kitafichua ugonjwa wa Caesar. Anaamua kukubali kujitoa katika kasri ya Caesar.
Kunyimwa au kupata haki ya kujitetea katika bunge sio material hapa. Kitu material ni kwamba due process haikufuatwa, justice ilikuwa delayed na kwa hiyo justice ilikuwa denied.
Isitoshe Mwakyembe haku act professionally kwa kutomshurutisha Lowassa atupe side yake ya story. Zaidi ya hapo, Mwakyembe kwa kusema "kuna mengine nimeyaacha" ame undermine credibility ya report yake. Wengine tunaona inawezekana Mwakyembe anaujua ugonjwa wa Caesar na ndio alioacha kuuandika ripotini.