Kiranga, unachosema ni kujaribu kumuweka Lowassa kuwa ni object ya investigation wakati hakuwa. Uchunguzi ulihusu Richmond na ndio maana ukisoma mahitimisho kuhusu Richmond were swift and precise. Sasa watu waliokuwa implicated kimsingi walihitaji hatua zaidi dhidi yao kuchukuliwa na kuchunguzwa zaidi na vyombo husika.
Lowassa alikuwa implicated and that is it. He was not accused or even condemned of any wrong doing. Ukisoma maelezo niliyoyaweka ya Kamati ni kuwa hatua zozote zaidi dhidi ya Waziri Mkuu zilikuwa zichukuliwe na Bunge na yeye mwenyewe. Kamati isingeweza kwenda zaidi ya mandate iliyopewa kwani hata kumuita Waziri Mkuu kumhoji ingekuwa ni kujipa ajenda wasiokuwa nayo. Wao waliangalia nyaraka wakaona zina muimplicate WM kwa kiasi kikubwa. Sasa kwenda the next level - ya kuanzisha uchunguzi dhidi ya Waziri Mkuu - Bunge lilitakiwa kukubali kwani ndicho chombo cha nidhamu ya juu ya Waziri Mkuu ukiondoa Rais.
Lakini pia implication ya Waziri Mkuu ilikuwa na jambo jingine ambalo watu tayari wameliona - ilikuwa ina muimplicate Rais vile vile. Fikiria hivi - kama aliyoyasema Lowassa kuhusika Kikwete na Richmond yaliripotiwa kwa usahihi na kuwa ndivyo ilivyokuwa ina maana kuwa ushahidi ambao kina Mwakyembe waliuona kumhusu Waziri Mkuu ulimhusu Rais vile vile. Sasa je, kamati ingeenda na kumuita RAis? Watu wanachosahau ni kuwa hata Kikwete hakuhojiwa na Kamati! Kikwete ndiye aliyesimama na kutuambia kuwa Richmond haitolipwa n.k na alikuwa anajua kilichokuwa kinaendelea lakini hakuitwa na Kamati.
Hapa ndipo unaona ni kwanini kutomhoji Lowassa na kuachilia Bunge ilikuwa ni kamba yenye vifungo viwili - kwa upande wa Rais na upande wa Waziri Mkuu. Kina Mwakyembe walijua - kwa usahihi na kwa uhakika wa kisheria - wasingeweza kumhoji Waziri Mkuu bila kumuita RAis vile vile.
Fikiria - Lowassa anaitwa na kusema "Nilimuambia Rais..", "Rais alinielekeza"... "Niliandika barua kwa Rais" n.k n.k Je kwa kumtaja Rais si kunalazimisha Rais naaye kuhojiwa maana asipohojiwa naye yeye angesema "Miye Rais lakini hamkuniita". Hivyo, walimpa Lowassa kitanzi cha kumnyoshea kidole Rais. Lowassa leo anaweza kumnyoshea Rais kidole kwenye vikao vya vyama lakini alishindwa kufanya hivyo mbele ya wabunge? Leo anaweza kunyosha kidole hadharani lakini alishindwa kufanya hivyo Bungeni? Hakuna fact iliyobadilika kuhusu Richmond. Lolote analolijua Lowassa leo, alikuwa analijua 2008.
Kina Mwakyembe walimuambia "yeye mwenyewe ajipime". Well, alitumia masaa akajipima, akafikiria na kushauriana na Regina na alipomaliza aliona hana njia isipokuwa kuruka. Alitambua asingeweza kuilaumu ripoti ya Mwakyembe bila kujibiwa. Alijaribu kudai kuwa ripoti iliokoteza toka magazetini na Selelii alisimama akamjibu Bungeni aoneshe ni wapi kwenye hiyo ripoti vilitoka magazetini au afute kauli yake - akafuta! Lowassa, alipewa nafasi ya kupinga yote yaliyosemwa na Kamati Teule na hata kuweka ushahidi kuwa yeye ndiye alijitahidi kuvunja mkataba wa Richmond hakufanya hivyo. Hakufanya hivyo Bungeni isipokuwa aliamua kufanya hivyo siku chache kwenye TVT na ever since amejaribu sana.
Lazima watu waseme ukweli kuwa Lowassa alijiuzulu kwa makosa yake mwenyewe. Alijiuzulu bila kuombwa kujiuzulu na Bunge wala Rais hakumuambia ajiuzulu. Kamati ya Mwakyembe haikumuambia ajiuzulu. Yeye mwenyewe alijipima. Alijigundua hafai kuwa Waziri Mkuu, aligundua hakuwa na hoja ambayo isingeweza kujibiwa Bungeni. Ndio maana yeye mwenyewe aliamua kujiuzulu. Lowassa hakuonewa, Lowassa hakunyimwa haki ya asili, Lowassa aliogopa kujitetea na aliogopa kusimama kuonesha upande wake. Hili ni kosa la Lowassa peke yake na wale waliomshauri kujiuzulu. Siyo kosa la Kikwete wala Mwakyembe wala wabunge waliozungumza kwa ukali Bungeni. Hili ni kosa la Lowassa na tuanze kuliita hivyo.
kuongezea yeye kapewa nafasi aongee mi nilitegemea aongee huo ukweli anaousema kwenye vikao vya ccm na tv yeye analalama utafikiri hafikiri oh nimeonewa sana, nimesikitishwa sana, sikusikilizwa, tatizo uwaziri mkuu lol!!
kamati haikumsikiliza yeye sio wa level yake, kamati ni ndogo sana kwa waziri mkuu jamani, yeye ni level ya bunge!! hivyo siku aliyopewa nafasi alitakiwa ajitetee sio kujiuzuru na ndipo angepimana na bunge zima na ndipo amtaje na jk na serikali kifo kiwe pale! na kujipima huko na bunge alijua angeshindwa maana wangempigia kura ya kutokuwa na imani nae!
kumchukia mwakyembe ni kumuonea, makosa ni yako mwenyewe na huyo rafiki ako mnajua fika mlichokuwa na mnachokifanya.