HIvi Lowassa ambaye tunaambiwa na wengine kuwa is the best thing that is waiting to happen to Tanzania alishindwa kujitetea mbele ya watu 300 halafu siku chache baadaye aliweza kusimama kujitetea mbele ya watu milioni 40? Really? Lowassa ambaye alisimama kubishana juu ya hoja ya kupaa kwa ndege yake na kuzungumza kwa umahiri kila hoja za serikali zilipokuja kweli unaamini alishindwa kupangua hoja za Kamati ya Mwakyembe moja baada ya nyingine? Umejaribu kuipitia hotuba ya Lowassa kujiuzulu uone jinsi alivyoanza vizuri lakini akafikia kuachia ngazi?
Lowassa abebe lawama ya kujiuzulu kwake. Siyo Kamati ya Bunge wala Bunge lililomtaka ajiuzulu. Tuwe wa kweli Lowassa kama Waziri Mkuu alikuwa na nafasi ya kujitetea na kwa hiari yake alikataa kuitumia. Alipomuomba Spika nafasi ya kuzungumza asubuhi ile Spika alimpa. Ikumbukwe asubuhi ile ilikuwa ni kwa ajili ya mwendelezo wa michango ya wabunge (kukaangwa kwa kina Lowassa - angalia kwenye youtube yangu bado ninazo zile clips). Lakini Lowassa alitoa taarifa kwa Spika kuwa angependa kuzungumza.
Spika anafuata taratibu za Bunge - Waziri Mkuu ana priority ya kuzungumza Bungeni halafu anayefutia ni msemaji wa Kambi ya Upinzani. Lowassa aliposimama asubuhi ile angeweza:
a. Kuonesha kuwa hoja za wabunge ni kali dhidi yake lakini siyo sahihi kwa sababu hawajui ukweli wote.
b. Angeweza kuonesha kidogo sehemu ya ukweli kwa upande wake - hakuna ambaye angeweza kumkatisha. Ila angeweza kujibiwa.
c. Lowassa hakutaka kusema alichokuwa anakijua (siyo Mwakyembe). Watu wengi hawajui kuwa Lowassa lolote ambalo angelisema pale lingejibiwa na kina Mwakyembe na ndio mtego ambao aliwekewa (sehemu ya siasa hiyo). Lowassa angesimama na kusema kuwa x, y, na z kilichotajwa na Mwakyembe siyo kweli kina Mwakyembe wangetakiwa kujibu na wabunge kuwez akuamua. Lowassa hakutaka kufanya hivyo. Alijiuzulu.
d. Angeweza kutoa hoja ya kuomba Bunge liahirishwe ili akutane na Kamati Teule na kuwapa sehemu ya maelezo yake maana hawakumpa nafasi hiyo.
e. Lowassa alikuwa na haki kama Watanzani awengine kutoa mawazo yao kwa Kamati TEule. Uzuri wa Kamati teule ni kuwa inaweza kukuuita au kama kuna mtu anaweza kutoa ushahidi wowote anayo haki ya kuutoa. Lowassa alitulia kimya na alijua hajaaitwa kwa kadiri muda ulivyokuwa unapita. Angeandika barua kuuliza au hata yeye mwenyewe kuwapelekea maelezo yake - si lazima aitwe. Hakufanya hivyo. Alipeleka maelezo yake kwa Spika siku moja kabla ya ripoti ya Mwakyembe (nje ya muda). Rejea hotuba ya kujiuzulu kwake. Lowassa hakufanya hivyo. Alitarajia kuwa yeye ni Waziri Mkuu basi lazima angefuatwa au kuombwa well.. hakufanyiwa hivyo. Kama maelezo yake kuwa angeweza hata "kutembea kwa miguu" ni ya kweli well alijua vikao vinapofanyika kwanini hakujipeleka?
f. Lowassa angeweza kutoa hoja kwa Spika Bunge liahirishwe ili akutane na wabunge wa chama chake. Kama Waziri Mkuu alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na Spika angemsikiliza (wote chama kimoja); angeweza kutumia hata hoja ya kutaka kuzungumza na Rais wake (mwenyekiti wa CCM). Bunge lingeahirishwa au hata ile hoja ingeahirishwa kwa muda wakati Waziri Mkuu anazungumza na Rais. Hakufanya hivyo. Alijiuzulu. Siyo kosa la Mwakyembe wala Bunge.
Of course, lakini siyo ripoti tu, kama Lowassa angeamua kujitetea yeye na Rais wake wangeondoka. Lowassa ndiye mtu anayejua ukweli wote wa kuhusika kwa Kikwete, kwanini hakufanya hivyo? Leo tunasikia ametumia ujuzi huu kule Dodoma kuweza kuzuia kujivua gamba? Kwanini hakutumia siku ile kujitetea? Kwanini hakusimama na kusema kuwa "Jamani, miye nilimuambia Rais..." Hakufanya hivyo. Alijiuzulu.
Hapana simaanishi Waziri Mkuu ni nguvu kubwa ambayo haiwezi kuhojiwa na Kamati. La hasha, ninaamini - kama Kamati ilivyoamini - suala la Waziri Mkuu ni suala la Bunge zima. Kamati TEule haiwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu bali Bunge. Na Kamati ilileta suala la WAziri Mkuu kwenye Bunge. Kumbuka kuwa Kamati Teule ni sehemu tu ya Bunge ambayo imekasimiwa madaraka ya Bunge. Bunge zima linaweza kukaa kama Kamati Teule! Na wangeweza hata kufunga milango kwanza kama Kamati na kuzungumza! Walichofanya kina Mwakyembe ni kurudisha kwa Bunge ambalo ndilo linamuidhinisha Waziri Mkuu kumhoji. Lowassa alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge ambalo lilimpitisha miaka miwili nyuma. Ndicho chombo sahihi cha kumwajibisha Waziri Mkuu. Lowassa alijua hili. Alijua moto wa Wabunge wa CCM jana yake asingeweza kuuzima kwa kuzungumza. Lowassa hakutaka kupambana na kujitetea. Aliogopa kwa sababu alijua kuwa amewekwa kona isiyowezekana (an improbable angle).
a. Ajiteteee lakini wabunge wakatae wampigie kura ya kutokuwa na imani na hivyo alazimishwe kujiuzulu na kupoteza haki zake kama Waziri Mkuu.
b. Ajitetee na kumtaja Rais wake na Rais amruke na kulivunja Bunge na hivyo kuanzisha mgongano mkali.
c. Ajitetee halafu kina Mwakyembe wayaweke wazi yale mengine ambayo walimuachia kiporo halafu aonekane kuwa ujanja wake wa maneno haukuwa na njia ya kumuokoa.
Lowassa aliamua njia rahisi - the path of least resistance. Ndio maana wengine tunakebehi kabisa wazo ati ni kiongozi mzuri na kwamba wapo watu wanafikiria ati anaweza kuwa Rais anayefaa wa Tanzania.
Mwanadamu huru anaweza kuletwa na mtu mwingine huru hadi kwenye genge la jiwe lenye kina kirefu. Anaambiwa kuwa anatuhumiwa kufanya x,y na z. Wanaomtuhumu wanamwambia ajipime "yeye mwenyewe na kuchukua uamuzi unaostahili". Sasa yule mtu huru baada ya kutafakari anaamua kuruka na kupoteza maisha yake. Haulizi, habishi, wala hajaribu kuwaambia wanaomtuhumu kuwa tuhuma zao si za kweli. Hachambui ushahidi uliotolewa dhidi yake anaamua tu kuruka. Well, mtu yeyote aliyekaa pembeni ambaye anaona kuwa hakuna mtu aliyemshikia Bunduki kumwambia aruke au aliyemsukuma. Wanamuona ametumia kutemba kidogo, kukaa chini kufikiria na kisha anaomba nafasi ya kuzungumza. Nafasi hii ya kuzungumza angeweza kujitetea maana wale wanaomtuhumu wanatarajia kuwa atajitetea. Badala yake anasimama na kusema.
"kweli hamkuniuliza muda wote huo hadi mmenifikisha hapa, ningeweza kuja hata kwa miguu hadi kwenye ofisi zenu lakini hamkufanya hivyo. Ningeweza kujitetea kwani ushahidi mliotoa hauna msingi. Kwa kweli hamkunitendea haki na natural justice haikufuatwa. Najua mnachokitaka, mnataka nyumba yangu, mnataka magari yangu na kwa hakika mnataka cheo chengo".
Halafu anaruka kwenye genge!
Bahati nzuri ananusurika japo amejeruhiwa. Anarudi na kusema "mmenisukuma nijirushe"?
Wanamuuliza
"Kwanini uliruka?"
anasema
"Nisingeruka ningeonekana mbishi!"
"Sasa huoni kwa kuruka watu waliona una hatia?" wanamuuliza.
"Nisingeruka bosi wangu angeonekana vibaya"
"Kwanini sasa uliruka kama ushahidi haukuwa mzito hivyo"?
Hajibu na badala yake anaanza kueneza kampeni kuwa "nilionewa nilionewa". Bahati nzuri kuruka kwake kulitangazwa kwenye televishenina kurekodiwa.