DR. Mwakyembe na Natural Justice

said:
By Consigliere

Ukimnyima mbongo chakula inaweza isiwe issue, lakini ukitaka kumtesa na kumsababishia mahangaiko moyoni basi mnyime maneno....yaani mnyime kile ukijuacho, atahangaika sana..

TUNAITA CHOYO... NA NDIO HUUA MATAJIRI NA PESA KWENYE VYUNGU

pamoja na hayo your mfano doesnt hold water....

Sikumbuki kutoa mfano mahali popote katika statement yangu hapo juu.....
 
Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari, usifundinshe watu namna ya kuishi utakavyo.... akiamua kusema alikua anaumwa nini ni yeye... ni serikali pumbavu tu inayoweza kutoa tamko la ugonjwa wa mwananchi wake unless kuna kibali cha daktari au ni kwa ajili ya takwimu tu, ndio unaambiwa kuna wagonjwa milioni mbili wa tegu, huwezi kupewa orodha ya wagonjwa kama udhanivyo

Sanasana serikali ndio inatakiwa itoe ultimatum kwa Mwakyembe kutimiza ahadi alizotoa

it is very difficult when it comes to human body, ndio maana Litvinyenko pamoja na data zote waingereza walizokua nazo waliishia kulalama tu kama pinda na suala la jairo
Mkuu hapo kwenye bold naomba kutofautiana na wewe. Rais wetu amewahi kuanguka hadharani mara mbili, na mpaka sasa hatujui anasumbuliwa na nini. Siamini kuwa kama hali hiyo ingemtokea Obama wamarekani wangeambiwa ni siri ya Obama na daktari wake. Inapokuja kwa viongozi, wananchi tunayo haki ya kujua hali ya afya zao, vinginevyo kuna siku tutaongozwa na kichaa kwa mwanvuli huohuo wa usiri wa ugonjwa.
 
Nadhani Dr. HGM angewapa serikali muda maaalum wa kutoa ripoti yake haraka iwezekanvyo. na ni kweli HGM kacheemka kusema hatolipiza kisasi. HGM'S desires for revenge deserve to be recognized as a legitimate factor when deciding what the level of punishment should be, so long as the ultimate sentencing authority remains with the State.
 
HIvi Lowassa ambaye tunaambiwa na wengine kuwa is the best thing that is waiting to happen to Tanzania alishindwa kujitetea mbele ya watu 300 halafu siku chache baadaye aliweza kusimama kujitetea mbele ya watu milioni 40? Really? Lowassa ambaye alisimama kubishana juu ya hoja ya kupaa kwa ndege yake na kuzungumza kwa umahiri kila hoja za serikali zilipokuja kweli unaamini alishindwa kupangua hoja za Kamati ya Mwakyembe moja baada ya nyingine? Umejaribu kuipitia hotuba ya Lowassa kujiuzulu uone jinsi alivyoanza vizuri lakini akafikia kuachia ngazi?

Lowassa abebe lawama ya kujiuzulu kwake. Siyo Kamati ya Bunge wala Bunge lililomtaka ajiuzulu. Tuwe wa kweli Lowassa kama Waziri Mkuu alikuwa na nafasi ya kujitetea na kwa hiari yake alikataa kuitumia. Alipomuomba Spika nafasi ya kuzungumza asubuhi ile Spika alimpa. Ikumbukwe asubuhi ile ilikuwa ni kwa ajili ya mwendelezo wa michango ya wabunge (kukaangwa kwa kina Lowassa - angalia kwenye youtube yangu bado ninazo zile clips). Lakini Lowassa alitoa taarifa kwa Spika kuwa angependa kuzungumza.

Spika anafuata taratibu za Bunge - Waziri Mkuu ana priority ya kuzungumza Bungeni halafu anayefutia ni msemaji wa Kambi ya Upinzani. Lowassa aliposimama asubuhi ile angeweza:

a. Kuonesha kuwa hoja za wabunge ni kali dhidi yake lakini siyo sahihi kwa sababu hawajui ukweli wote.
b. Angeweza kuonesha kidogo sehemu ya ukweli kwa upande wake - hakuna ambaye angeweza kumkatisha. Ila angeweza kujibiwa.
c. Lowassa hakutaka kusema alichokuwa anakijua (siyo Mwakyembe). Watu wengi hawajui kuwa Lowassa lolote ambalo angelisema pale lingejibiwa na kina Mwakyembe na ndio mtego ambao aliwekewa (sehemu ya siasa hiyo). Lowassa angesimama na kusema kuwa x, y, na z kilichotajwa na Mwakyembe siyo kweli kina Mwakyembe wangetakiwa kujibu na wabunge kuwez akuamua. Lowassa hakutaka kufanya hivyo. Alijiuzulu.
d. Angeweza kutoa hoja ya kuomba Bunge liahirishwe ili akutane na Kamati Teule na kuwapa sehemu ya maelezo yake maana hawakumpa nafasi hiyo.
e. Lowassa alikuwa na haki kama Watanzani awengine kutoa mawazo yao kwa Kamati TEule. Uzuri wa Kamati teule ni kuwa inaweza kukuuita au kama kuna mtu anaweza kutoa ushahidi wowote anayo haki ya kuutoa. Lowassa alitulia kimya na alijua hajaaitwa kwa kadiri muda ulivyokuwa unapita. Angeandika barua kuuliza au hata yeye mwenyewe kuwapelekea maelezo yake - si lazima aitwe. Hakufanya hivyo. Alipeleka maelezo yake kwa Spika siku moja kabla ya ripoti ya Mwakyembe (nje ya muda). Rejea hotuba ya kujiuzulu kwake. Lowassa hakufanya hivyo. Alitarajia kuwa yeye ni Waziri Mkuu basi lazima angefuatwa au kuombwa well.. hakufanyiwa hivyo. Kama maelezo yake kuwa angeweza hata "kutembea kwa miguu" ni ya kweli well alijua vikao vinapofanyika kwanini hakujipeleka?
f. Lowassa angeweza kutoa hoja kwa Spika Bunge liahirishwe ili akutane na wabunge wa chama chake. Kama Waziri Mkuu alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na Spika angemsikiliza (wote chama kimoja); angeweza kutumia hata hoja ya kutaka kuzungumza na Rais wake (mwenyekiti wa CCM). Bunge lingeahirishwa au hata ile hoja ingeahirishwa kwa muda wakati Waziri Mkuu anazungumza na Rais. Hakufanya hivyo. Alijiuzulu. Siyo kosa la Mwakyembe wala Bunge.

Of course, lakini siyo ripoti tu, kama Lowassa angeamua kujitetea yeye na Rais wake wangeondoka. Lowassa ndiye mtu anayejua ukweli wote wa kuhusika kwa Kikwete, kwanini hakufanya hivyo? Leo tunasikia ametumia ujuzi huu kule Dodoma kuweza kuzuia kujivua gamba? Kwanini hakutumia siku ile kujitetea? Kwanini hakusimama na kusema kuwa "Jamani, miye nilimuambia Rais..." Hakufanya hivyo. Alijiuzulu.

Hapana simaanishi Waziri Mkuu ni nguvu kubwa ambayo haiwezi kuhojiwa na Kamati. La hasha, ninaamini - kama Kamati ilivyoamini - suala la Waziri Mkuu ni suala la Bunge zima. Kamati TEule haiwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu bali Bunge. Na Kamati ilileta suala la WAziri Mkuu kwenye Bunge. Kumbuka kuwa Kamati Teule ni sehemu tu ya Bunge ambayo imekasimiwa madaraka ya Bunge. Bunge zima linaweza kukaa kama Kamati Teule! Na wangeweza hata kufunga milango kwanza kama Kamati na kuzungumza! Walichofanya kina Mwakyembe ni kurudisha kwa Bunge ambalo ndilo linamuidhinisha Waziri Mkuu kumhoji. Lowassa alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge ambalo lilimpitisha miaka miwili nyuma. Ndicho chombo sahihi cha kumwajibisha Waziri Mkuu. Lowassa alijua hili. Alijua moto wa Wabunge wa CCM jana yake asingeweza kuuzima kwa kuzungumza. Lowassa hakutaka kupambana na kujitetea. Aliogopa kwa sababu alijua kuwa amewekwa kona isiyowezekana (an improbable angle).

a. Ajiteteee lakini wabunge wakatae wampigie kura ya kutokuwa na imani na hivyo alazimishwe kujiuzulu na kupoteza haki zake kama Waziri Mkuu.
b. Ajitetee na kumtaja Rais wake na Rais amruke na kulivunja Bunge na hivyo kuanzisha mgongano mkali.
c. Ajitetee halafu kina Mwakyembe wayaweke wazi yale mengine ambayo walimuachia kiporo halafu aonekane kuwa ujanja wake wa maneno haukuwa na njia ya kumuokoa.

Lowassa aliamua njia rahisi - the path of least resistance. Ndio maana wengine tunakebehi kabisa wazo ati ni kiongozi mzuri na kwamba wapo watu wanafikiria ati anaweza kuwa Rais anayefaa wa Tanzania.

Mwanadamu huru anaweza kuletwa na mtu mwingine huru hadi kwenye genge la jiwe lenye kina kirefu. Anaambiwa kuwa anatuhumiwa kufanya x,y na z. Wanaomtuhumu wanamwambia ajipime "yeye mwenyewe na kuchukua uamuzi unaostahili". Sasa yule mtu huru baada ya kutafakari anaamua kuruka na kupoteza maisha yake. Haulizi, habishi, wala hajaribu kuwaambia wanaomtuhumu kuwa tuhuma zao si za kweli. Hachambui ushahidi uliotolewa dhidi yake anaamua tu kuruka. Well, mtu yeyote aliyekaa pembeni ambaye anaona kuwa hakuna mtu aliyemshikia Bunduki kumwambia aruke au aliyemsukuma. Wanamuona ametumia kutemba kidogo, kukaa chini kufikiria na kisha anaomba nafasi ya kuzungumza. Nafasi hii ya kuzungumza angeweza kujitetea maana wale wanaomtuhumu wanatarajia kuwa atajitetea. Badala yake anasimama na kusema.

"kweli hamkuniuliza muda wote huo hadi mmenifikisha hapa, ningeweza kuja hata kwa miguu hadi kwenye ofisi zenu lakini hamkufanya hivyo. Ningeweza kujitetea kwani ushahidi mliotoa hauna msingi. Kwa kweli hamkunitendea haki na natural justice haikufuatwa. Najua mnachokitaka, mnataka nyumba yangu, mnataka magari yangu na kwa hakika mnataka cheo chengo".

Halafu anaruka kwenye genge!

Bahati nzuri ananusurika japo amejeruhiwa. Anarudi na kusema "mmenisukuma nijirushe"?

Wanamuuliza

"Kwanini uliruka?"

anasema
"Nisingeruka ningeonekana mbishi!"

"Sasa huoni kwa kuruka watu waliona una hatia?" wanamuuliza.

"Nisingeruka bosi wangu angeonekana vibaya"

"Kwanini sasa uliruka kama ushahidi haukuwa mzito hivyo"?

Hajibu na badala yake anaanza kueneza kampeni kuwa "nilionewa nilionewa". Bahati nzuri kuruka kwake kulitangazwa kwenye televishenina kurekodiwa.

I mean conclusion ya haya yote ni kuwa Mwakyembe alikuwa sahihi kutomuhoji Lowassa.
 
Hivi mlikua mnataka huyu mtu mnayemkiri kwa maandishi yenu kuwa ni corrupt atoke kwenye 18 zetu? yaani mnamtengenezea mazingira ya technicalities? jitahidini kuwa serious angalau kwa hili. kama mnabishania njia aliyotumia mwakyembe kumtuhumu lowasa hazikuwa nzuri sana basi furahini nyote ya kuwa mla rushwa kabanwa! hapa nawashauri kutumia common sense. ndio maana ikitokea jambazi lihofishalo jamii kwa ujambazi wake, ikitokea likapigwa risasi na kufa, kama kweli linatambulika kwa ujambazi wake jamii hufurahia kifo hicho! hakuna ooh! mlipaswa kulikamata na kulifikisha jambazi mahakamani, tumsifu mwakyembe kwa kutunasia lowasa, pia tumlaumu mwakyembe kwa kumkosakosa jk!!!!! tusitafute kumtorosha gerezani mla rushwa lowasa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Great question. Lakini nianze kwa kulijibu kutoka mbali kidogo. Anayehojiwa katika uchunguzi wa uhalifu ni mtuhumiwa au mshukiwa. Uchunguzi wa kujaribu kujenga kesi wakati mwingine hata mtuhumiwa hata hajui uchunguzi unafanyika (FBI na polisi wanafanya hivi sana). Wakishakuwa na sababu ya kutosha kuleta mashtaka basi wana mshtaki (indictment) na mtu anakamatwa na kutoka hapo ndio wanampeleka kuanza kumhoji. Maelezo yake hayatoshi hivi hivi kwani baadaye atafikishwa mahakamani ambapo licha ya kushtakiwa atapewa nafasi ya kuwahoji watuhumu wake (cross examination).

Hapa ndio msingi wa hiki tunachozungumzia "natural justice". Kwamba, mtu anayechunguzwa ana haki ya kuhojiwa lakini vile vile anahaki ya kujibu mashtaka yanayotolewa dhidi yake. Kwa maneno mengine, uchunguzi huwa una mtu au chombo kinachochunguzwa.. sasa along the way yawezekana katika uchunguzi huo ikaonekana kuna watu wengine au vyombo vingine vinahusika kwa namna moja au nyingine. Sasa hivi vinaweza kutajwa na vinaweza hata kuletwa mahakamani kuelezea upande wao chini ya kiapo na wengine wanaweza kujikuta matatani kama wanagundulika kuwa wakati uchunguzi unafanyika walijaribu kuficha au kuharibu ushahidi au taarifa - hivyo wanaweza kupata obstruction of justice charges.

Sasa swali lako linauliza "kwanini hawakumuuliza Mwakyembe". Ili tuweze kuona angalau the reasoning turudi kwenye Kamati Teule ilipewa majukumu ya kuchunguza kitu gani na ni nani alikuwa ni "object of the investigation".

Hii hapa sehemu ya taarifa ile katika utangulizi wake (msisitizo wa rangi kali nyeusi wangu) :

sasa swali tunaweza kuuliza: Je, Kamati Teule iliundwa ili kuchunguza nini - jibu tukiangalia hadidu rejea ni "RICHMOND". Tunaweza hata kubadilisha kidogo swali na kuuliza kama iliundwa kumchunguza nani? - jibu bado tunaona katika hadidu zote sita kuwa ni "Richmond". Kwamba, Waziri Mkuu wala afisa yeyote wa serikali hakuwa the OBJECT OF INVESTIGATION. Uchunguzi wa Kamati Teule ulihusiana na Kampuni ya Richmond. Tena Spika aliwakataza kabisa kuwa wasichunguze hata suala la Dowans (rejea maelekezo ya Spika siku ile).

Hii ina maana ya kwamba - vitu na watu wengine wote ambao walijikuta kwenye uchunguzi ule (akiwemo Waziri Mkuu) walikuwa ni incidental to the investigation. Ni katika uchunguzi wake wa Richmond ndio Kamati Teule ikajikuta inakutana na majina mbalimbali ya watu na ofisi zao. Ukisoma vizuri hiyo ripoti utaona kuwa mwisho wa siku jina lililokuwa linatajwa tajwa sana ni la Waziri Mkuu kuwa ndiye aliyefanikisha. Remember - he was not the object of investigation.

Hii ndio sababu walipofika mwisho wa ripoti yao walitoa mapendekezo tu mbalimbali ambayo yaliendana na kile walichokikuta. Kwamba kina Karamagi walifanya hivi n.k wawajibike na hata ilipofika kwa Waziri Mkuu walisema kuwa jina lake lilitajwa sana na wao walitaka yeye mwenyewe ajipime kutokana na uzito wa kuhusika kwake na cheo chake.

Sasa, ndio Mwakyembe akasema maneno haya yafuatayo ambayo yanaendana kabisa na hoja kuwa Lowassa hakuwa anachunguzwa na Kamati Teule (msisitizo wa mistari wangu) :

Sasa, hicho ndicho Mwakyembe alisema kuhusu yote yaliyosemwa kwenye uchunguzi. Mwakyembe hakusema ajiuzulu, Mwakyembe hakusema anapaswa kujiuzulu; alisema "mwenyewe ajipime". Sasa akajipima akaruka! Iweje Mwakyembe abebeshwe lawama?

Hizi siasa mkuu! kuwa kamati inatoa maelezo kuwa jina la waziri mkuu lilijitokeza mara nyingi..yet kamati haina muda wala haina haja ya kwenda kumuuliza waizir mkuu?? you must be kidding...hizi kanuni na vikanuni ambavyo huwa mnazunguka ndivyo vimetufikisha hapa tulipo!!

Mwanakiji in this case please receive my BIG NO...NO..NO..NO!! kamati ya mwakyembe haikuwa sahihi kutomuhoji Lowassa....kisaokolojia ni kuwa they hade their conclusions, before conduncting this investigation and they wanted points to justify their words.

In other words kulikuwa na uadui na ndio maana kamati haikuwa comfortable kumuhoji! kuhoji kuna kula fedha ngapi??

Mwanakijiji andika uandikavyo...hapa hamna sababu...ni uwezo wetu wa kufikiri na kutenda umefika hapo na tunaona sawa...mengine yote tunaona sawa hivi hivi....halafu tunalalamika hivi hivi...na wengine wanatetea hivi hivi.....na maisha yanaendelea hivi hivi tu!

sitaona aibu kusema niliifurahia ile report, EL alijiuzulu, ila sitaogopa kusema kikanuni report ile haikutakiwa kupokelewa..ni nullified
 
Hivi mlikua mnataka huyu mtu mnayemkiri kwa maandishi yenu kuwa ni corrupt atoke kwenye 18 zetu? yaani mnamtengenezea mazingira ya technicalities? jitahidini kuwa serious angalau kwa hili. kama mnabishania njia aliyotumia mwakyembe kumtuhumu lowasa hazikuwa nzuri sana basi furahini nyote ya kuwa mla rushwa kabanwa! hapa nawashauri kutumia common sense. ndio maana ikitokea jambazi lihofishalo jamii kwa ujambazi wake, ikitokea likapigwa risasi na kufa, kama kweli linatambulika kwa ujambazi wake jamii hufurahia kifo hicho! hakuna ooh! mlipaswa kulikamata na kulifikisha jambazi mahakamani, tumsifu mwakyembe kwa kutunasia lowasa, pia tumlaumu mwakyembe kwa kumkosakosa jk!!!!! tusitafute kumtorosha gerezani mla rushwa lowasa.

umezungumza kwa upeo wako na mawazo yako na mtazamo wako juu ya Lowassa, hujazungumza kama unaishi kwenye civilised society!! hujazungumza kama tunaishi kwenye jamii tuliyojiwekea taratibu na tuna sheria na jinsi ya kuwafikisha wanasheria ...you mean Jogi ukijulikana na kuhisiwa mwizi basi daktari ana wajibu wa kukuchoma sindano ya sumu...ili kupunguza kero zingine!! unajua jamani kwenye ukwei tusimamie!

watu wanaomuhukumu Lowassa na wengine ndio hao hao wanaosimama na kusema si vyema kuwapiga na kuwa choma moto vibaka au wanaoitiwa mwizi!!! unarudi nyuma na kunaglia ubongo wetu..unaona tatizo kubwa sana pengine la asili au kilema tu! ninapokuja na kujigundua kuwa tuna tatizo naona shida maana hatuna kanuni za msingi..na hatuna tunachokiamini..ila tumetawaliwa na emotion, matukio na akipendacho mtu

Mwakyembe huyu ameishatoa sentensi nyingi na mara nyingi kuwa hajasema yote ya richmond...still some people wanamwona hero!! wakati ametutukana...guys wake up....hatutakiwi kuwa sample za maabara pindi vitukuu vyetu vitakaposema let find our the IQ of our forefathers!
 
Waberoya naheshimu msimamo wako. Ila ni msimamo ambao umekataa ukweli. By refusing to recognize the facts of the matter as they stand to be observed independently you have reached a wrong conclusion. Sasa hili hitimisho lenye makosa linaendana na imani siyo facts. Sasa imani ni imani siwezi kukubishia. Lakini imani siyo facts. Facts ni kuwa a. Lowassa hakuwa anachunguzwa na bunge b. Kamati teule haikuwa inamchunguza kiongozi yeyote wa umma c. Viongozi wote waliohojiwa ilikuwa ni discretion ya kamati kwa kadiri walivyoweza kusaidia d. Vielelezo vingine vilitosha kuelezea nini kilitokea e. Lowaasa alipewa nafasi na kamati kupinga hata kuhoji kazi ya kamati hakufanya hivyo f. Lowasa hakuta kuelezea upande wake kwenye chombo sahihi yaani bunge.

Waberoya those my friend are facts. Siyo maoni yangu wala siyo imani yangu they are facts. Sasa nioneshe factual background contradicting those.

Waberoya pick any of those facts and show why they are wrong.
 
Hivi huyu mwakembe kwenye ile kamati alikua peke yake? Mbona wengine wako kimya tu! Au kuisoma ripoti ndio kaifanya ya kwake?
Asitumie ugonjwa wake kujinufaisha kisiasa. Kama ni kuumwa wako wengi tu wamebabuka ngozi muhimbili, amana, na kwingineko.
Tume ile ama kwa makusudi au kwa kutokuwa makini walichemka kutomhoji EL. Japo hilo halimwondolei doa EL
 
Sasa yamekuwa Natural Justice na majuzi tuliambiwa sio yeye kuna aliyekuwa anamkingia kifua, yaani mnajaribu kila angle kuona hoja gani inaweza kusimama lakini kote mnapwaya.

- Mwalimu alipomnyima nafasi Lowassa alilia kuonewa akaambiwa amfuate Mwalimu Msasani, alipoenda akaambiwa ni mwizi na kuonyeshwa documents za ununuzi wa magari ya Wabunge na forgery zake, akaondoka kimya kimya.

- Kamati ya Mwakyembe imemuita Rostam akaikwepa, wengi wa walioitwa walikataa kutoa ushirikiano kisa kumlinda Lowassa. Kamati ya Bunge haikumuhoji Lowassa a powerfull PM na the best friend wa the sitting President, now kabla ya ripoti kuletwa Bungeni Lowassa ametumia kila njia kuizuia ripoti mpaka kuibadili isomwe yake, watu wamewatishia na kuwa offer mapesa ya ajabu kina Mwakyembe on behalf of innocent man Lowassa. Woooow!

- Sasa leo yamekuwa haya Natural Justice ambayo Lowassa amewanyima wananchi kwa kuwauzia Umeme ambao haupo. Umenyimwa Natural Justice na kutuhumiwa wizi wa ajabu kwa taifa unapewa nafasi ya kujitetea mbele ya bunge unajiuzulu na kuanza kuhonga wajumbe wa NEC sasa unataka kujitetea kwenye NEC kwamba ulionewa, Msomi kama Lowassa huamini kusafishwa na Mahakama I mean at least usafishwe na bunge basi, unalilia NEC tu! Ha! Ha! Only in Tanzania.

- Tumewaiga Wachina mambo mengi sana lakini tuliacha moja muhimu sana alisema Shujaa wangu Mzee Ndesamburo ile siku ya siku, watu kama huyu Lowassa kule China huwa wanapanga mstari na kuwatwanga shaba na kulazimisha familia zao kulipia ile risasi, lakini in Tanzania Lowassa aliyewafanya wananchi waishi bila umeme mpaka leo anapigana kutafuta kuwa Rais wao na masikini wananchi wale wale wanaoishi bila umeme wanahangaika kila kona ya taifa lao lililo gizani kumsafisha Baba wa giza lao tena very fancy words za Natural Justice!

- ONLY IN TANZANIA! - Le Baharia!
 
Red = Ili iweje - shughulikia akul ya watoto wako na wewe mwenyewe kuliko kupoteza muda kwa kujaribu kupasua mwamba kwa kutumia kichwa

Alijitokeza kwenye vyombo vya habari kutangaza kuwa hata lipiza kisasi ili iweje? Si angekaa nyumbani kwake afikirie mambo ya chakula na watoto wake? Kama anajua kuna watu ambao angewalipiza visasi na amewasamehe na kumwachia Mungu sasa haya yote ya nini kutangaza kwenye vyombo vya habari? Mwakyembe ni mbabaishaji tu hana lolote. Tena ni mdau mkubwa aliyelipelekea taifa kulizwa mabilion 94 kwa kuficha ukweli na kuleta taarifa nusu nusu. Isingekuwa ni yeye aliyemficha huyu hili jinamisi linaloitwa JK tungeshaondokana nalo siku nyingi. Lowassa na Mwakyembe wote ni wahalifu hawafai. Wanatanguliza maslahi na interest zao mbele kwa mambo yanayohusu taifa nzima. Hata kama Mwakyembe atakuja kusema ukweli wote kuhusu RICHMOND na pia kuhusu UNGONJWA hakuna mtu atakae mwamini. Ameonya dhahiri kuwa afanyi kazi kuwahudumia wanainchi bali anafanya kazi ya kumfurahisha boss wake JK. Mwakyembe ni hovyo sana!!!
 
Mwakyembe is my hero, Mbunge wa kwanza Tanzania kuongoza kamati iliyofanya kazi kwa haki na kutupa wananchi na Taifa ukweli wa nani Mwizi na kumkimbiza a powerfull sitting PM in our history. Mwakyembe ni binadam mpungufu kama sisi wote lakini the end of the report justifies the means.
 
Nadhani Dr. HGM angewapa serikali muda maaalum wa kutoa ripoti yake haraka iwezekanvyo. na ni kweli HGM kacheemka kusema hatolipiza kisasi. HGM'S desires for revenge deserve to be recognized as a legitimate factor when deciding what the level of punishment should be, so long as the ultimate sentencing authority remains with the State.

Mwakyembe knows where he got his help from, kama ni kwa nguvu ya principle za ulimwengu mnaoishi ninyi ama ni ule ambao wengi mnaudharau huku kila siku mkiishi katika tabu na mateso. With the experience of 'near to death' my friend ustaarabu wote wa kiulimwengu unawekwa pembeni. DOnt think he is stupid if is concerning education he has a no class ahead certificate then why do you think he resorted into such a decision? And its so fascinating to see now you people coming publicy kum-provoke wakati at that difficult moment all of you were like ....'he can not escape from the episode'...who would have told you the facts you want to hear about his health if he were dead? He has had divine contact and has been transformed into another kingdom where we operate in very different principles. Poleni sana na subiri muone God of vengence huwa anateteaje wale wote wanaoamua kwa hiari to humble before His throne of Grace! Msimsumbue na kumwondoa katika namna ya maisha aliyoamua kuyaishi kwani hafanani nanyi katika mtizamo; incase mko na guity conscious the only way you can be safe is to repent basi! Other wise nyamazeni msubiri hukumu ya Mungu naye ataamua kwa muda na wakati wake na jinsi atakavyoiotoa.
 
Waberoya naheshimu msimamo wako. Ila ni msimamo ambao umekataa ukweli. By refusing to recognize the facts of the matter as they stand to be observed independently you have reached a wrong conclusion. Sasa hili hitimisho lenye makosa linaendana na imani siyo facts. Sasa imani ni imani siwezi kukubishia. Lakini imani siyo facts. Facts ni kuwa a. Lowassa hakuwa anachunguzwa na bunge b. Kamati teule haikuwa inamchunguza kiongozi yeyote wa umma c. Viongozi wote waliohojiwa ilikuwa ni discretion ya kamati kwa kadiri walivyoweza kusaidia d. Vielelezo vingine vilitosha kuelezea nini kilitokea e. Lowaasa alipewa nafasi na kamati kupinga hata kuhoji kazi ya kamati hakufanya hivyo f. Lowasa hakuta kuelezea upande wake kwenye chombo sahihi yaani bunge.

Waberoya those my friend are facts. Siyo maoni yangu wala siyo imani yangu they are facts. Sasa nioneshe factual background contradicting those.

Waberoya pick any of those facts and show why they are wrong.

"mwenyewe ajipime"-Mwakyembe

where the hell this statement is coming from kama swala halikuwa kumchunguza Lowassa? why comments like this was accepted were they in TOR? kuwa kamati ile itoe ushauri wa nini cha kufanya hawa waliohusika kwenye ile chain?
 
Mwakyembe is my hero, Mbunge wa kwanza Tanzania kuongoza kamati iliyofanya kazi kwa haki na kutupa wananchi na Taifa ukweli wa nani Mwizi na kumkimbiza a powerfull sitting PM in our history. Mwakyembe ni binadam mpungufu kama sisi wote lakini the end of the report justifies the means.

Really? how? more than Malecela au Sokoine? unajua ukishabikia sana unaweza ukashangaa unapiga jiwe ukifikiri mpira!! kuweni wa wazi Kikwete mwizi na Lowassa unayemuona mjinga angesimama kidete kama alivyo malecela Kikwete angechomoka! kibaya zaidi unayesema hero ndiye aliyesema ana mengi zaidi ya kusema!!!
 
Sasa yamekuwa Natural Justice na majuzi tuliambiwa sio yeye kuna aliyekuwa anamkingia kifua, yaani mnajaribu kila angle kuona hoja gani inaweza kusimama lakini kote mnapwaya.

- Mwalimu alipomnyima nafasi Lowassa alilia kuonewa akaambiwa amfuate Mwalimu Msasani, alipoenda akaambiwa ni mwizi na kuonyeshwa documents za ununuzi wa magari ya Wabunge na forgery zake, akaondoka kimya kimya.

- Kamati ya Mwakyembe imemuita Rostam akaikwepa, wengi wa walioitwa walikataa kutoa ushirikiano kisa kumlinda Lowassa. Kamati ya Bunge haikumuhoji Lowassa a powerfull PM na the best friend wa the sitting President, now kabla ya ripoti kuletwa Bungeni Lowassa ametumia kila njia kuizuia ripoti mpaka kuibadili isomwe yake, watu wamewatishia na kuwa offer mapesa ya ajabu kina Mwakyembe on behalf of innocent man Lowassa. Woooow!

- Sasa leo yamekuwa haya Natural Justice ambayo Lowassa amewanyima wananchi kwa kuwauzia Umeme ambao haupo. Umenyimwa Natural Justice na kutuhumiwa wizi wa ajabu kwa taifa unapewa nafasi ya kujitetea mbele ya bunge unajiuzulu na kuanza kuhonga wajumbe wa NEC sasa unataka kujitetea kwenye NEC kwamba ulionewa, Msomi kama Lowassa huamini kusafishwa na Mahakama I mean at least usafishwe na bunge basi, unalilia NEC tu! Ha! Ha! Only in Tanzania.

- Tumewaiga Wachina mambo mengi sana lakini tuliacha moja muhimu sana alisema Shujaa wangu Mzee Ndesamburo ile siku ya siku, watu kama huyu Lowassa kule China huwa wanapanga mstari na kuwatwanga shaba na kulazimisha familia zao kulipia ile risasi, lakini in Tanzania Lowassa aliyewafanya wananchi waishi bila umeme mpaka leo anapigana kutafuta kuwa Rais wao na masikini wananchi wale wale wanaoishi bila umeme wanahangaika kila kona ya taifa lao lililo gizani kumsafisha Baba wa giza lao tena very fancy words za Natural Justice!

- ONLY IN TANZANIA! - Le Baharia!
Malecela, leo umenifurahisha kupindukia. Kumbe wewe pia unayafahamu yote hayo! Ama kweli siku hizi dunia kijiji. Mimi huwa sijuwi kuongea kama mwanasheria, lakini yote uliyoandika hapo juu nayafahamu fika kama wewe... ukweli Lowasa anatumia nguvu nyingi kujitakasa lakini siyo msafi na ni Mungu pekee anaweza kumsafisha ila siyo pesa zake na watu wake anaowatumia. Shukrani sana bwana mdogo wangu.
 
Really? how? more than Malecela au Sokoine? unajua ukishabikia sana unaweza ukashangaa unapiga jiwe ukifikiri mpira!! kuweni wa wazi Kikwete mwizi na Lowassa unayemuona mjinga angesimama kidete kama alivyo malecela Kikwete angechomoka! kibaya zaidi unayesema hero ndiye aliyesema ana mengi zaidi ya kusema!!!

Na wewe king'ang'anizi mno, wenziyo wamejenga hoja zenye mashiko lkn wewe unatupotezea muda na hoja zako zisizoeleweka. Sasa unataka kutuhamishia kulinganisha powers za ma-PM waliopita! Acha kuzungusha mada kijana.

Mwanakijiji, Kiranga na sasa Malecela wameku-preempt hoja zako zote.. kwanini usikubali yaishe ? Tuna mengi ya kujadili pia.
 
Really? how? more than Malecela au Sokoine? unajua ukishabikia sana unaweza ukashangaa unapiga jiwe ukifikiri mpira!! kuweni wa wazi Kikwete mwizi na Lowassa unayemuona mjinga angesimama kidete kama alivyo malecela Kikwete angechomoka! kibaya zaidi unayesema hero ndiye aliyesema ana mengi zaidi ya kusema!!!

Wabe sitaki kuingilia ugomvi usionihusu lakini kwa ukweli kama unampenda huyo ndugu mwambie aache kuwa too ambitious na hata kutaka kupata utukufu wa Mungu ambao ni dhambi ya kupitiliza. I myself has experience with his characters ambapo once he wanted to plant his person kwa lazima hata pale wananchi wa mahala pale walipomkataa kwa nguvu zote. Hakujua kwamba si kila jamii inaweza hongeka kirahisi ndipo walipomshangaza kwa huyo mtu wake kupata kura za aibu hadi kutoa machozi hadharani. Ninampenda sana lakini matendo yake si mazuri nami nikinyamaza bila kumwambia ukweli dhamira yangu itanisuta milele.

You being a born again usije ingia kwenye dhambi ukaangamia kwakukosa maarifa. Kama kweli ameamua kumrudia Mungu atulie na kumwamini maana ni kwakurudi na kutulia ndipo tunapopata ushindi na siyo kuhangaika kama anavyofanya sasa. Mfikishie huu ujumbe hata nikipata nafasi ya kukutana naye will tell him before his face. The word of God says in prov 16:18 Pride goeth before destruction, and an haughty spirit before a fall. Labda utasema how proud is he, kwakutopenda kusikia kuwa he has to moderate his ambitions and desires kama amepangiwa kuwa Rais atakuwa tu wakati ukifika hata bila kuwa desparate kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom