Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Kwa mlolongo huu hakuna La kubeza hata moja,NI MUNGU TU MWEZA YOTE ATATENDA!

Hizo vitu unasoma then unarelate na mambo yetu ya Kitanzania, Uneza kujikuta unakufa pasipo sababu!
 
Comreds, let us get ready. it wil start raining soon, am cleaning my Rifle. Wakianza na cc tunaanza!
 
Watanzania hatujafikia mahali kutokuamini ushirikiana, ushirikina upo na Mungu pekee ndiyo anayeweza kutulinda na ushirikiana.

Hapa si ushirikina pekee bali ni vitendo vimepangwa mpaka wameletewa alshabab, halafu wametumia mgongo wa udini, hii ni mbaya mno.

Nikiingalia hiyo list ya walengwa naona kama ifuatavyo Mwandosya - possible candidate 2015 bila shaka Mwakyembe ni mpambe wake, Membe ni possible candidate 2015, Kilango ni mpambe wa candidate yeyote ndani ya CCM lakini asiwe kwenye kundi la kina RA na EL.
Dr. Slaa kipenzi cha watz na potential candidate, Mengi yeye amekuwa na malumbano makubwa na the so called mafisadi papa. kwa haraka haraka tunaona kama kweli mpango huu upo basi malengo ni :

1. kujisafishia njia ya kwenda ikulu kwa kuondoa vikwazo.
2. kwa upande wa Mengi ni kumaliza bifu kati yake na Mapapa.
3. kutokana na kuona kuwa maji yako shingoni na kwamba mapinduzi ya kisiasa yanaaza kutokea Tz, ili kulinda maslahi yao basi mafisadi wamedhamiria kuiingiza nchi kwenye machafuko ili isitawalike.Haitakubalika hata kidogo watu watano maarufu wauawe ghafla halafu nchi ibake tulivu, never.

watuhumiwa:

1. Mtu yeyote anayeutaka urais kwa udi na uvumba mbali ya hao walengwa wa mauaji.
2. Mafisadi ambao ni wafanyabiashara ndani ya chama cha mafisadi (CCM)
 
Kuna watu wanapenda kuchanganya mambo, hapa hakuna cha udini, ila hawa ni tishio kwani ni watu wa haki. Sasa msiwaguse mkatutoa uvumilivu. Tifu lake kamwe hamtaiweza.

Chonde chonde asisubutu.:hand:
 
Uislamu sio insu hapo,hili suala la dini limeingizwa kama propaganda ya kuwashawishi hawa al-shabab wakubali kuja kufanya kazi,lakin ni insu ya kisiasa..
 
Hii habari ilikuwa itoke mwanahalisi leo, na imetoka. Walichokifanya Mtanzania ni kuihujumu habari hiyiyo......kama unataka uone haba hiyo kwa uzuri soma Mwanahalisi la leo.......wametaja hadi gari moja iliyotumika kuwa ni ya Caspian kampuni ya Rostam, wametaja majina ya watu woote woliohusika Kuanzia Shehe Yahaya bila kufichaficha! katajwa hadi mtoto wa Lowassa Fred kuwa alishiriki kuwapelekea chakula wauaji hao.....

Mtanzania waliihujumu hiyo habari baada ya kupata tetesi ya walichopanga kuandika Mwanahalisi.......na ndiyo maana mwisho wamesema eti wasomi wamemponda Mwakyembe! sasa wamemponda saangapi wakati habari ndiyo kwanza imetolewa! walijuaje!....Hicho ni kehoro cha Rostam na Lowassa.....habari yenyewe isomeni kwenye mwanahalisi....
 
nadhani tendo la kuuwawa kwa DR.MWAKYEMBE na SLAA ni kitu ambacho hakitakuwa na tija katika taifa na nafikiri kama kuna kikundi cha watu wanadhani ni tija basi hawajafanya tafiti za kutosha. kwani hakitakuwa na suluhisho lingine zaidi ya kuingiza nchi kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe na wananchi kuanza kuwasaka wahusika wa mauaji hayo pasipo kujali vyeo na wasifa wao.

ila kama watu wanaotaka kufanya hivi kwa lengo la kufanya biashara ya silaha basi watakuwa wamefanikiwa malengo yao

mungu ibariki tanzania ila natambua TANZANIA utateketea muda si mrefu
 
Mimi naamini raisi alikuwa anafahamu mpango mzima, maana hata polisi na usalama wa taifa wamehusishwa!! Ndiyo alijua akakaa kimya akisubiri wabaya wa rafiki zake wafe!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kama alikuwa hajui, nchi hii imeishakufa bado kuzikwa tu...., nakama kesha jua sasa lkn anauchuna basi JK hafai kabisa kuendelea kuiongoza nchi hii....
 
Hadi ifikapo 2015 tutashuhudia mengi...................... Ee mwenyezi mungu naomba ulinzi wako niendelee kuwepo nishuhudie hii sinema live bila malipo
 
Igp mwema tunaomba uchunguzi na majibu ya kina juu ya suala hili tafadhali.

Watanzania tumechoka kutishwa jamani.
 
hizi ni tuhuma nzito, ila kuamini ushirikina hapo namuondolea credits

hayajawatokea ndio maanamnajifanya hamuamini ushirikina.....kuna baadhi ya magonjwa ukienda hospital hayaonekani, ndio maana akina kakobe na mwakasege huwa wanayashughulikia....
Ushirikina upo hata kama humanini, huna haja ya kumuondolea credit kwa kuzungumzia ushirikina...
 
this shows how these fisadis wamelewa na ufisadi wao! Inafikia mahala mtu unaona bora utoe roho za watu kwasababu ya uchu wa madaraka! this is so sad!

Anyway, waache waanze then waone nguvu ya umma itakavyofanya kazi....
 
Aaaaah wapi!. Wataua miili yao bali hawataua roho zao na fikra zao.

Mapambano bado yanaendelea mpaka Mafisadi watakapo tuachia nchi yetu ili tuiongoze wenyewe na si kuitawala kama ambavyo wenzetu wanafanya kwa maslahi ya Watanzania wenyewe!!!!!!!!!!!!!!.
 
Suala la msingi ni jeshi na vyombo vyote husika kufuatilia hizi tuhuma ili kujua undani na ukweli wake na sio suala la wasomi na wahadhiri kuanza kumlaumu na kumshauri mwakyembe upuuzi na ujinga eti msomi mzima kuamini mambo ya uchawi -

Na labda hawajaelewa au hawajasoma na kuelewa vizuri huu waraka ni kwamba mwakyembe amejaribu kuelezea mtiririko mzima au mpango mzima ulivyosukwa kwa kuwa husisha hata waganga wa kienyeji, na kama binadamu wengine ni lazima awe na hofu juu ya maisha yake kama kweli kuna hujuma juu ya maisha yake,........

Nafikiri jeshi la polisi litakua na kazi ndogo sana kwani mwakyembe amejaribu kuwa mkweli na amewataja kwa majina karibu wahusika wote.
I also now understand what He meant...by the way Mungu huyo aliyemsaidia ku expose hayo yote ndo huyo huyo atakayemlinda dhidi ya hao magaidi.

Amechukua hatua stahiki kwani believing does not mean being careless Mungu akikuonyesha adui wewe usipomshughulikia kwa nguvu alizokupa Mungu yeye anakushugulikia kwa nguvu alizopewana devil; uzuri ni kwamba kwetu sisi waamini we are more than conqueres for in all war fares we win before we engage into war...So awe relaxed tu God is in control and please relaxing does not mean neglect...

The power they are using to destroy him will go back to them with seven times more strength to crush/burn them into ashes! They came with one door but because of confusion shall escape using seven ways while some hurting each other...This is true and Amen; I hereby declare this as an oracle of God whom Mwakyemba is my brother in christ Jesus!
 
Habari nzima imenukuliwa toka gazeti MTANZANIA

Jeshi la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua. Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.

Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili “kuwapumbaza Watanzania wote” baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.

Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe


“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.

“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.

“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.

“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).

“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

Maoni ya wanasiasa na wasomi

Baadhi ya wasomi na wanasiasa mbalimbali waliohojiwa na MTANZANIA wameshangazwa na taarifa hii ya Dk. Mwakyembe, hasa kwa msomi kama yeye kuamini masuala ya uchawi.

“Ninachoweza kumshauri kaka yangu (Mwakyembe) ni kuchapa kazi zake alizopewa za ubunge na uwaziri, akiingiza masuala ya kuamini ushirikina atakuwa anapoteza sifa yake ya usomi,” alisema mmoja wa wahadhiri.

Dk. Mwakyembe anatambulika katika Jeshi la Polisi kama mmoja wa viongozi wanaotoa maelezo yenye utata kuhusu usalama wao.

Ameibua suala hili huku kukiwa bado na kumbukumbu za yeye kupata ajali mkoani Iringa na kudai kwamba lori lililohusika lilikuwa limepangwa kumtoa uhai.

Hata hivyo, Polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni uzembe na mwendo kasi wa dereva wa Dk. Mwakyembe.

Watake Radhi Mtanzania au hujui maana ya nukuu? kuna vitu kibao umeweka vya kwako na vinatofautiana na vilivyo ndani ya gazeti la Mtanzania. Hebu kwa kuanzia tuanzie na sub-heading yenye red hapo juu isome vizuri gazetini na uifananishe na ulivyo inukuu, ukilitambua hilo kosa nitakuonyesha kosa la pili. la tatu mpaka la nane
 
Hizi ni tuhuma nzito, ILA KUAMINI USHIRIKINA HAPO NAMUONDOLEA CREDITS
Kama umesoma vizuri hoja kuu ni kuwa kuna watu wenye lengo la kumuua physically, na sio kwa kutumia ushirikina. Wauaji waliotajwa na waliopanga mpango mzima ndio wanaoamini ushirikina kwa kwenda kwa mganga ili kuwapa kinga na mambo mengine.
 
Hii habari ilikuwa itoke mwanahalisi leo, na imetoka. Walichokifanya Mtanzania ni kuihujumu habari hiyiyo......kama unataka uone haba hiyo kwa uzuri soma Mwanahalisi la leo.......wametaja hadi gari moja iliyotumika kuwa ni ya Caspian kampuni ya Rostam, wametaja majina ya watu woote woliohusika Kuanzia Shehe Yahaya bila kufichaficha! katajwa hadi mtoto wa Lowassa Fred kuwa alishiriki kuwapelekea chakula wauaji hao.....
Mtanzania waliihujumu hiyo habari baada ya kupata tetesi ya walichopanga kuandika Mwanahalisi.......na ndiyo maana mwisho wamesema eti wasomi wamemponda Mwakyembe! sasa wamemponda saangapi wakati habari ndiyo kwanza imetolewa! walijuaje!....Hicho ni kehoro cha Rostam na Lowassa.....habari yenyewe isomeni kwenye mwanahalisi....

Uchambuzi mzuri!
 
Mmmh!these are not good signs at all,whether habari hizi ni za kweli ama si za kweli lakini bottom line is it's not a good sign.huu ndio mwanzo wa kuvuruga fikra za watanzania....baada ya uchaguzi yametokea mambo mengi sana yenye utata wa kila aina na hadi leo binafsi sijui hii nchi inakoelekea tena.....I dont know what to believe anymore maana at the end of the day everything is just confusing and threatening!i dont want to think about the worst for my country but i guess at this point it is safe to prepare for the worst.God help us maana political interest ya wachache imetufikisha pabaya.
 
If this is a true story then it is now obvious: It is ISLAM vs CHRISTIANITY. Ni dhahiri sasa UDINI hatimaye umeingia rasmi Tanzania. Tumekwisha! CCM na makuwadi wake wameuza nchi rasmi. Haiwezekani walengwa wote wa kuuwawa ni wa dini fulani tu na watuhumiwa ni watu wa mipango yote ni watu wa karibu na chama tawala.

dudus this is a political war,hakuna dini hapo.that is just a disguise covering the real issue here (political war under the umbrella of religion).kweli aliyesema politics is a dirty game hakukosea!!!!
 
Sasa hapo kwa mwema IGP ndio kikwazo kipo na ndio anaekwamisha mambo kufanyika sasa sitoshangaa report ikisema kuwa huo ni uzushi na uongo lakini interejensia ya maandamano inajua kuwa waandamanaji wataleta fujo......
 
Back
Top Bottom