kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,636
- 2,885
Nakubaliana na wewe kuwa mh rais ni mkali na huchukua hatua kwa baadhi ya watu tu wengine kutokana na unasaba nao anaona haya kuwachukulia hatua, kwa tuhuma alizozitoa mh Dr Mpango kwa Makonda ingetosha kabisa kwa mh Rais wetu mpendwa kuwa ameshamfukuza kazi na hatua zaidi dhidi yake zimekwisha chukuliwa ikiwemo kufunguliwa kesi za kuhujumu uchumi, matumizi mabaya ya ofisi ya umma nk.Mpango nilimuheshimu sana alipojieleza issue ya Makonda kwenye kodi ya makontena.
Mpaka hapo nilikuwa namchukulia kuwa just another Magufuli stooge. Ila pale nilipomsikiliza nikaona kama kuna matumaini ya japo kidogo ya mtu mwenye professional standards na respect for intellectual honesty.
Dr. Mpango ana mengi ya kujibu, na pengine kakosea mengi.
Ila kuna sehemu moja kajionesha kwamba ni mtu wa integrity kuliko siasa za kujipendekeza.
Jinsi alivyo deal na Makonda.
Tatizo likaja kuonekana wazi kwamba hata washauri wa rais wanapofanya maamuzi sahihi, rais anazembea.
Pale Dr. Mpango alikuwa presidential kuliko Magufuli, alimu expose Magufuli kwamba ukali wote wa Magufuli ni kwa watu fulani tu.
Wwatu kama Dr. Mpango wakimpa cards Magufuli acheze sawa, Magufuli analeta siasa za kuwaogopa watu fulani.
Pale nilimkubali sana Dr. Mpango kusema ukweli.
Na nikaweka points kwamba kumbe inawezekana huyu mtu akasimamia ukweli.
Na hizi habari za kusema uchumi unafanya vibaya nimekuwa nikizisema kitambo hapa JF.
Dr. Mpango angeendelea kuimba uchumi unakua, ningemuona mnafiki.
Ila karudi ku i redeem serikali kwamba kuna watu wanaweza kusema ukweli mchungu, hata katika context ya serikali, ambayo, ukweli ni jinai.
Eneo lingine ninalolitazama ni kwa wasaidizi wa mh Rais kutomueleza ukweli kwa sababu ama wanamhujumu Rais au wameshamgundua Rais wetu ni mtu asiyependa kukosolewa hivyo hawana namna zaidi ya kwenda nae vile anavyopenda yeye, nachelea kusema hivyo kwasababu Urais ni taasis, mh rais ana wasaidizi lukuki