Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 142,617
- 287,342
Hii ni baada ya kuliambia bunge kwamba hali ni tete hasa baada ya mapato kwenye sekta ya madini kupungua kutokana na baadhi ya makampuni kusitisha uchimbaji , Ukosefu wa Ajira mpya katika nchi na kukosekana kwa mapato kutoka kwa sekta isiyo rasmi ( machinga ) kunakotokana na kukosekana kwa kumbukumbu za mapato kulikosababishwa na machinga kutokutunza kumbukumbu na kutokuwa na sehemu maalum za kufanyia biashara.
Dr Mpango amedai kwamba kushindwa kuongezwa mishahara ya wafanyakazi , na hivyo kupunguza mzunguko wa pesa ni sababu nyingine ya kuanguka kwa uchumi wa nchi .
Mytake , itafika wakati wote tutaongea lugha moja .
Dr Mpango amedai kwamba kushindwa kuongezwa mishahara ya wafanyakazi , na hivyo kupunguza mzunguko wa pesa ni sababu nyingine ya kuanguka kwa uchumi wa nchi .
Mytake , itafika wakati wote tutaongea lugha moja .
Kwa mara nyingine Waziri wa Fedha Daktari Phillip Mpango amepasua mbarika na kuuleza umma kupitia Bunge kuwa uchumi umeporomoka. Mpango ameamua kuendelea kusimama katika UKWELI MCHUNGU bila kujali gharama ya kuwa mkweli.
Waziri Mpango ameweka bayana changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 kuwa ni pamoja na kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi wa migodi na kutoongezeka mishahara kwa wafanyakazi kama ilivyotarajiwa.
“Changamoto kubwa zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 ni pamoja na ugumu wa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, kwa kuwa hawana sehemu rasmi na za kudumu za kufanyia biashara na hawatunzi kumbukumbu.
“Sababu nyingine ni kutofikiwa kwa lengo la kodi zitokanazo na ajira kwa maana ya ‘PAYEE’ kulikosababishwa na kutofikiwa kwa malengo ya ajira mpya na kutoongezeka kwa mishahara kwa wafanyakazi kama ilivyokuwa imetarajiwa.
“Vilevile kodi hizi zimeathirika kutokana na kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi kwenye migodi ya madini kufuatia kupungua kwa shughuli za uchimbaji madini kwa baadhi ya migodi.
“Sababu ya tatu ni kushuka kwa biashara za kimataifa kulikosababisha kutofikia malengo ya uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa imetarajiwa.
“Sababu nyingine ni upungufu wa wafanyakazi na vitendea kazi ndani ya Mamlaka ya Mapato nchini kulikopunguza ufanisi wa utendaji kazi wa mamlaka hiyo na sababu nyingine ni kupungua kwa misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo,” alisema Dk. Mpango.
Aidha Mpango ameliambia Bunge kuwa misaada na mikopo nafuu, inatarajiwa kupungua kutoka Sh trilioni 3.38 kwa mwaka 2019/20, hadi Sh trilioni 3.28 mwaka 2021/22.
“Mikopo kutoka nje na ndani inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 6.93 mwaka 2019/20 na shilingi trilioni 6.76 mwaka 2021/22,” alisema Dk. Mpango.
“Malipo ya riba na mtaji kwa deni la ndani na nje yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 8.62 mwaka 2019/20 na kuongezeka hadi shilingi trilioni 8.62 mwaka 2021/22,” alisema Dk. Mpango.
KAMBI YA UPINZANI
Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima James Mdee alisema Serikali inatakiwa kutoa maelezo juu ya zinapotoka fedha za kugharamia mradi wa reli ya standard gauge.
“Septemba 20, Jarida la Expogroup liliripoti kuwa Tanzania imepata mkopo wa Dola za Marekani bilioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 3 kutoka Benki ya Standard Charterd kwa ajili ya kugharamia kipande cha reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora Dodoma.
“Habari hiyo ni tofauti na maelezo ya rais kuwa tunajenga reli ya kati kwa fedha zetu wenyewe ila kwa kuwa jarida hilo limemnukuu Waziri wa Fedha, ni vema akaeleza Bunge ugharamiaji wa mradi huo ukoje,” alisema Mdee.
Pia Mdee alihoji ni kwanini reli hiyo inaanza kwenda Mwanza hadi Rusumo badala ya kwenda Tabora hadi DRC ambako kuna fursa za kiuchumi.
MAONI YA MBUNGE Zitto Kabwe Zitto Kabwe Ruyagwa: "Nataraji Maneno haya ya Waziri wa Fedha Dkt. Mpango yataifanya Serikali ianze kutumia MAARIFA badala ya mabavu na ukatili katika masuala ya sera za Uchumi. Fedha ya Kodi iliyopotea kwenye PAYE za Wafanyakazi wa Migodi ni kubwa zaidi ya thamani ya Makanikia ‘yaliyopo’ Bandarini.
Kabla ya suala la makanikia Halmashauri ya Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka, Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa? Zaidi kuna Multiplier Effect, Nimeona mji unavyokufa, Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka Kijiji cha Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka".
Maoni yangu: Hii si mara ya kwanza kwa Mpango kuchagua kuusimamia ukweli bila kujali gharama. Hivi karibuni alifanya hivyo katika sakata la ufisadi wa makontena ya Makonda ambayo yaliingizwa nchini kifisadi pasi na kulipiwa kodi. Sijui hadi leo serikali imemchukulia hatua gani Makonda kwa kosa hilo.
Naamini itafika wakati wote tutaongea lugha moja. Hadi leo ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji imekuwa ni ndoto, ajira zimekuwa ni za kusadikika, ongezeko la mishahara na kupandishwa madaraja kwa Watumishi imegeuka kuwa fumbo la imani, bei ya mazao ya Korosho, Mbaazi, Mahindi imeporomoka vibaya mno. Watanzania wengi bila kujali itikadi zetu tunazungumza lugha moja tu, nayo ni "ugumu wa maisha" wa kihistoria.
Sijui wale Maprofesa wetu wa makongamano waliokuwa wanamwaga sifa za kusadikika, Je wamemsikiliza Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Uchumi?
Nini maoni yako?
MDAU MWINGINE NAE ANAELEZEA
Kilichokwamisha Bajeti na Mpango wa Maendeleo 2017/2018, Waziri anasema ni Serikali kukosa fedha kutokana na...
1. Ugumu wa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wasio katika sekta na mfumo rasmi wa kodi. Hawana ofisi za kudumu na hawana kumbukumbu za biashara.
>Serikali ilitegemea Machinga !?
2. Kutofikiwa makusanyo ya Kodi ya Mishahara kutokana na Kutoongezeka mishahara ya wafanyakazi, kutokuwapo ajira mpya na kuounguzwa kazi wafanyakazi wengi hasa wa migodini kutokana na shughuli za uchimbaji madini kupungua.
>Serikali ilisema hali za wafanyakazi ni nzuri, ajira zimeongezeka, viwanda 3600 vipya..hali ni nzuri sana !!
3. Kushuka kwa Biashara za Kimataifa kutokana na kuoungua kwa uingizaji bidhaa kutoka nje.
> Serikali ilisema Bandari inafanya vizuri sana kuliko miaka yote na inapokea bidhaa za kuvunja rekodi.. mambo ni sagi sana
4. Upungufu wa wafanyakazi na videndea kzi vya ukusanyaji mapato.
>Hapa tuliambiwa TRA wana mifumo ya kisasa na hakuna tena upotevu wa mapato maana kila kitu kinaenda kielektroniki sasa.. Wizi umedhibitiwa kiasi kwamba trend ya mapago ilikuwa ni matrilioni na point... Mambo safi !!
_____
Namtafuta mhenga aliyetunga methali "Mficha Uchi Hazai" ninywe nae chai jioni.