Dr Mpango akiri uchumi wa nchi kuporomoka

Dr Mpango akiri uchumi wa nchi kuporomoka

Sasa tuambiane ukwel nn hasa kinasababisha kuwa na uchumi wa namna hii na serikal ifany nn ili kuondokana na ukata huu
Utaiambia nini serikali isiyotaka kuambiwa, watu wamesema sana lakini mwisho wakapata kesi za uchochezi
 
Bora aseme yeye aliye hukohuko jikoni, tukisema sie tunaitwa Ukawa,Ufipa,Nyumbu,wapiga dili,vibaraka wa wazungu,wazee wa kupinga kila kitu.
 
Kwa mara nyingine Waziri wa Fedha Daktari Phillip Mpango amepasua mbarika na kuuleza umma kupitia Bunge kuwa uchumi umeporomoka. Mpango ameamua kuendelea kusimama katika UKWELI MCHUNGU bila kujali gharama ya kuwa mkweli.

Waziri Mpango ameweka bayana changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 kuwa ni pamoja na kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi wa migodi na kutoongezeka mishahara kwa wafanyakazi kama ilivyotarajiwa.

“Changamoto kubwa zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 ni pamoja na ugumu wa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, kwa kuwa hawana sehemu rasmi na za kudumu za kufanyia biashara na hawatunzi kumbukumbu.

“Sababu nyingine ni kutofikiwa kwa lengo la kodi zitokanazo na ajira kwa maana ya ‘PAYEE’ kulikosababishwa na kutofikiwa kwa malengo ya ajira mpya na kutoongezeka kwa mishahara kwa wafanyakazi kama ilivyokuwa imetarajiwa.

“Vilevile kodi hizi zimeathirika kutokana na kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi kwenye migodi ya madini kufuatia kupungua kwa shughuli za uchimbaji madini kwa baadhi ya migodi.

“Sababu ya tatu ni kushuka kwa biashara za kimataifa kulikosababisha kutofikia malengo ya uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa imetarajiwa.

“Sababu nyingine ni upungufu wa wafanyakazi na vitendea kazi ndani ya Mamlaka ya Mapato nchini kulikopunguza ufanisi wa utendaji kazi wa mamlaka hiyo na sababu nyingine ni kupungua kwa misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo,” alisema Dk. Mpango.

Aidha Mpango ameliambia Bunge kuwa misaada na mikopo nafuu, inatarajiwa kupungua kutoka Sh trilioni 3.38 kwa mwaka 2019/20, hadi Sh trilioni 3.28 mwaka 2021/22.

“Mikopo kutoka nje na ndani inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 6.93 mwaka 2019/20 na shilingi trilioni 6.76 mwaka 2021/22,” alisema Dk. Mpango.

“Malipo ya riba na mtaji kwa deni la ndani na nje yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 8.62 mwaka 2019/20 na kuongezeka hadi shilingi trilioni 8.62 mwaka 2021/22,” alisema Dk. Mpango.

KAMBI YA UPINZANI

Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima James Mdee alisema Serikali inatakiwa kutoa maelezo juu ya zinapotoka fedha za kugharamia mradi wa reli ya standard gauge.

“Septemba 20, Jarida la Expogroup liliripoti kuwa Tanzania imepata mkopo wa Dola za Marekani bilioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 3 kutoka Benki ya Standard Charterd kwa ajili ya kugharamia kipande cha reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora Dodoma.

“Habari hiyo ni tofauti na maelezo ya rais kuwa tunajenga reli ya kati kwa fedha zetu wenyewe ila kwa kuwa jarida hilo limemnukuu Waziri wa Fedha, ni vema akaeleza Bunge ugharamiaji wa mradi huo ukoje,” alisema Mdee.

Pia Mdee alihoji ni kwanini reli hiyo inaanza kwenda Mwanza hadi Rusumo badala ya kwenda Tabora hadi DRC ambako kuna fursa za kiuchumi.

MAONI YA MBUNGE Zitto Kabwe Zitto Kabwe Ruyagwa: "Nataraji Maneno haya ya Waziri wa Fedha Dkt. Mpango yataifanya Serikali ianze kutumia MAARIFA badala ya mabavu na ukatili katika masuala ya sera za Uchumi. Fedha ya Kodi iliyopotea kwenye PAYE za Wafanyakazi wa Migodi ni kubwa zaidi ya thamani ya Makanikia ‘yaliyopo’ Bandarini.

Kabla ya suala la makanikia Halmashauri ya Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka, Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa? Zaidi kuna Multiplier Effect, Nimeona mji unavyokufa, Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka Kijiji cha Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka".

Maoni yangu: Hii si mara ya kwanza kwa Mpango kuchagua kuusimamia ukweli bila kujali gharama. Hivi karibuni alifanya hivyo katika sakata la ufisadi wa makontena ya Makonda ambayo yaliingizwa nchini kifisadi pasi na kulipiwa kodi. Sijui hadi leo serikali imemchukulia hatua gani Makonda kwa kosa hilo.

Naamini itafika wakati wote tutaongea lugha moja. Hadi leo ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji imekuwa ni ndoto, ajira zimekuwa ni za kusadikika, ongezeko la mishahara na kupandishwa madaraja kwa Watumishi imegeuka kuwa fumbo la imani, bei ya mazao ya Korosho, Mbaazi, Mahindi imeporomoka vibaya mno. Watanzania wengi bila kujali itikadi zetu tunazungumza lugha moja tu, nayo ni "ugumu wa maisha" wa kihistoria.

Sijui wale Maprofesa wetu wa makongamano waliokuwa wanamwaga sifa za kusadikika, Je wamemsikiliza Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Uchumi?

Nini maoni yako?

MDAU MWINGINE NAE ANAELEZEA

Kilichokwamisha Bajeti na Mpango wa Maendeleo 2017/2018, Waziri anasema ni Serikali kukosa fedha kutokana na...

1. Ugumu wa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wasio katika sekta na mfumo rasmi wa kodi. Hawana ofisi za kudumu na hawana kumbukumbu za biashara.

>Serikali ilitegemea Machinga !?

2. Kutofikiwa makusanyo ya Kodi ya Mishahara kutokana na Kutoongezeka mishahara ya wafanyakazi, kutokuwapo ajira mpya na kuounguzwa kazi wafanyakazi wengi hasa wa migodini kutokana na shughuli za uchimbaji madini kupungua.

>Serikali ilisema hali za wafanyakazi ni nzuri, ajira zimeongezeka, viwanda 3600 vipya..hali ni nzuri sana !!

3. Kushuka kwa Biashara za Kimataifa kutokana na kuoungua kwa uingizaji bidhaa kutoka nje.

> Serikali ilisema Bandari inafanya vizuri sana kuliko miaka yote na inapokea bidhaa za kuvunja rekodi.. mambo ni sagi sana

4. Upungufu wa wafanyakazi na videndea kzi vya ukusanyaji mapato.

>Hapa tuliambiwa TRA wana mifumo ya kisasa na hakuna tena upotevu wa mapato maana kila kitu kinaenda kielektroniki sasa.. Wizi umedhibitiwa kiasi kwamba trend ya mapago ilikuwa ni matrilioni na point... Mambo safi !!
_____
Namtafuta mhenga aliyetunga methali "Mficha Uchi Hazai" ninywe nae chai jioni.
 
Ushauri wangu kwa serikali mapato yatokanayo na faida yasipewe kipaumbele kikubwa kama chanzo cha pato kuu la serikali; hii itafanya watu wengi wawekeze kwenye biashara na serikali itapata mapato kwenye kodi ya ongezeko la thamani VAT na kodi za wafanyakazi.

Ilivyo sasa TRA inakimbizana sana na wafanyabiashara kukataa baadhi ya matumizi ili mradi tuu kampuni ionekane ina faida wakusanye kodi bila kujua wanaiua na lazima wafanyakazi wapunguzwe.

Nchi zilizoendelea kodi itokanayo na faida si chanzo kikuu cha mapato kwa serikali, PAYE ni chanzo kikuu
 
Uchumi wetu umeporomoka?!!!
220px-Tundu_A._M._Lissu.jpg

Ulikuwa unasema ukweli all along...pona haraka halafu tia timu, wao ndio waisome it's time to change.
 
Huu mfano wako uliotoa hapa ni moja ya mambo ambayo yangempa Magufuli hadhi kubwa kama yangetekelezwa vizuri na kama angeachana na siasa za chuki kwa maoni yangu.

Wengine wanaweza kukwambia kuwa kama wewe unalalamika juu ya kuminywa na kufaidika huko, wewe ungewekwa kwenye kundi la wapigaji; nami ningekubaliana nao.
Mimi siwezi kukubaliana na hili la kutowa na kudai risiti kwa sababu seikali yenyewe haijajipanga kwa hili. Nakupa mfano chini.

1.Unajuwa wateja wakubwa wengi ni kutoka nchi jirani. Na unajuwa kuwa ikiwa umenunuwa bidhaa kwa ku export unatakiwa aidha usilipie VAT au ukilipia urejeshewe kwenye mpaka kwa kuthibitisha manunuzi. Jee unafikiri serikali iko tayari kuwatejeshea hawa wateja wa nje VAT yao waliyolipia kwenye bidhaa au huduma?

2. Wewe kusafiri kwako kote katika nchi zilizoendelea ushawahi kubuhhddiwa na mamlaka husika ikiwa ni police ama watu wa kodi kuhusu kuonesha receipt? Na kama ungekuwa unabughudhiwa katika hiyo nchi ungerudi.tena?

3. Kuna nchi yoyote duniani ambayo mfumo wa mauzo wa duka una link na revenue authority kama kwetu? Na.kama ni hivyo jee designer na service provider wa hiyo system ni wenyewe au anatoka nje ya nchi na kuwafaidsha wao kwa malipo nono?

4. Ikiwa system ya TRA inayopata hits kama 5000 tu kwa siku inagoma kila wiki, jee hii system yao ya ku monitor.mauzo na manunuzi ya wenye maduka ambayo kama iko fully implemeted nationwide inatakiwa iwe na hits kama 1,000,000, jee itaweza vishindo?

Receipt mteja ni haki yako kwa kuthibitisha umelipia na thus legal ownership lakini haitumiki kama ni determining factor ya ulipaji kodi. Watendaji wasio waaminifu katika baadhi ya vyombo husika wanatumia excuse hii ya receipt kujipatia maslahi yao na kusbabisha usumbufu kupindukia. Mh Raisi juu ya nia yake njema juu ya hili kakini kuna wajanja wanaitumia hii to their own advantages
 
Ukiachana na hii sentesi " tunaisoma namba" iliyotamkwa sana hapo kabla nadhani sasa "maisha magumu" imeshika kasi na huenda ikatuunganisha na tukawa wamoja au kutugawa tukapoteana muda si mrefu
 
kampuni za michezo ya kubashiri zichunguzwe zinadhulumu pesa nyingi toka kwa watanzania mbumbu wanaoamini wanaweza kushinda milioni 200 kwa 500, ukichunguza pesa inayokusanya kwa siku kampuni 1 ya michezo ya kubashiri, inazidi pesa ambayo shirika letu la umeme inaingiza kwa wiki.
Tatizo ni sheria zetu mbovuu mkuuu
 
Hiyo siku ikifika utakuwa unatafuta nchi ya kukimbilia badala ya kusubiri Jiwe kutoka madarakani. Refer to Venezuela na Zim. Na Wabongo wengi mlivyokuwa na elimu ya kuungaunga hata sijui mtakimbilia nchi gani.
Kijana mdogo ulikuwepo 1980 hadi 1985..unafikiria Nyerere kwa nini aling'atuka ???watu walikuwa wanatembea uchi hakuna nguo..njaaa ya hatari..sukari na sabuni kulikuwa hakuna ..watu walifua nguo kwa mabunda ya mpapai...Ndio maana yule mzee aliachia nchi hata huyu mnaweza kumtengenezea chaos ambayo atajuta kuwa raisi...Akaja baba Mwinyi kwa kuwa ni mtu wa watu akatuondolea madhira..Kwangu Mwinyi ndio best President hapa Tanzania ingawa wengi hawataki kusema...Binadamu anapambana na mazingira yake watakimbia waogo..majority tutakuwepo..
 
Back
Top Bottom