Dr. Lawrence Gama ameaga dunia

Nadhani wenye jibu watakujibu!
Kiongozi mwingine mzalendo aliyeugulia na kufia nchini hivi karibuni ni Mhe. Mbunge Sigfrid Ng'itu wa Lindi, huyu naye kaugulia na kufia Muhimbili! Hakuna cha nje ya nchi wala nini!


RIP mzee Gama...
mhuu!!hivi kiongozi kufia nchini ni kipimo cha uzalendo?hapana!!!!!!Mwalimu JK alikuwa mzalendo au hapana!
 
Habari zilipatikana sasa hivi zinaleza kwamba mwanasiasa na mtumishi wa zamani serikalini, Dr. Laurence Gama ameaga dunia katika Hospitali ya Agakhan, Dar es Salaam. Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi Ameen.
alikuwa akisumbuliwa na nini?
nauhakika kule Ruvuma muda huu ni msiba mzito,
aliisaidia sana timu ya Majimaji.
Tuko nao pamoja kwenye msiba huu mzito,
Kazi ya Mungu haina makosa.
Tulikupenda ila Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi.
 
Ooh, no. Mungu aiweke roho ya marehemu Dr. Lawrence Gama mahali pema peponi. Amen.

Nawaombea Mama Gama na familia nzima ya Gama wapate nguvu za kuvumilia msiba huu mkubwa. Wengi tulimpenda ila Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Nuru ya milele imwangazie.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Kuna mengi aliyotolea jasho katika ujenzi wa taifa letu. Mema tuyadumishe na yale maovu, tuyasahau na tumuombe mungu amsamehe.I believe zaidi ya kuwa mkuu wa mkoa alishawahi kuwa master spy pia, kama nimekosea mnisahihishe maana mimi sio wa enzi hizo.
 
RIP mzee Gama...
mhuu!!hivi kiongozi kufia nchini ni kipimo cha uzalendo?hapana!!!!!!Mwalimu JK alikuwa mzalendo au hapana!

Mkubwa,
Kwa mtazamo wangu kutibiwa katika hospitali za ndani ya nchi ni uzalendo, ina maanisha kwamba unaziamini. Pili, pesa ambazo unatumia kutibiwa nje ya nchi zingeweza kubaki nchini na kuboresha hali ya huduma zetu za afya. Unakuta tuna hospitali za upasuaji wa moyo na mifupa hapa hapa nchini, lakini watu wanaenda kutibiwa nje ya nchi. Tatizo sisi hatujawekeza katika huduma zetu za matibabu ndio sababu tunakimbilia nje ambako wenzetu wamewekeza katika huduma zao za afya. Khs Nyerere, sina uhakika km alikwenda kwa ajili ya tiba au la, ila nilisikia kwamba alikwenda kwa shughuli binafsi ndipo akapima na afya kule kule na kukutwa na ugonjwa ule wa kansa.
 
Pole kwa ndugu na familia. Nitamkumbuka Gama kama mchapa kazi mzuri sana. Laiti hata robo ya Watanzania tungekuwa tunajituma kama huyu bwana, huenda nchi ingesogea.

RIP Dr. Gama.
 
Pole kwa ndugu na familia. Nitamkumbuka Gama kama mchapa kazi mzuri sana. Laiti hata robo ya Watanzania tungekuwa tunajituma kama huyu bwana, huenda nchi ingesogea.

RIP Dr. Gama.
mzee umepotea kidogo,
KWEMA?
MCHAKATO VIPI?
 
Rip mtazama...you tried very hard to block the current system to come into power in 1995 until they cried out loud...........
 
RIP mzee Gama...
mhuu!!hivi kiongozi kufia nchini ni kipimo cha uzalendo?hapana!!!!!!Mwalimu JK alikuwa mzalendo au hapana!

Haya mambo ya uzalendo yana mipaka yake, wewe umchulie mtu kama JK akalazwe M'nyamala hata dk kumi tu lazima ataaga dunia na uzalendo wake kwishney.
 
SIkumbuki yeye kuwa kwenye kundi la mafisadi na nina imani kuwa alikuwa kiongozi muadilifu

...Huu ni wakati wa majonzi kwa wafiwa na taifa... tumkumbuke Gama kwa mema aliyofanya na mungu atamlipa kadri ya alivyopanda
 
Haya mambo ya uzalendo yana mipaka yake, wewe umchulie mtu kama JK akalazwe M'nyamala hata dk kumi tu lazima ataaga dunia na uzalendo wake kwishney.
...Burn, mi nashauri siku moja hata yeye JK kweli akiugua apelekwe tu huko huko M'nyamala bila kuonja dhahama ya pale wataamini vipi kama huduma ni mbovu na zinatakiwa kuboreshwa? Kila siku ni story tu mara m'nyamala, mara temeke sijui amana wamama wanazalia nje ya geti za hospitali na vitimbi vya kila aina....lakini wao akisikia baridi kidogo amekamata pipa anarushwa zake kwenye zile hospitali zao za St...St..St....
 
Back
Top Bottom