Dr. Lawrence Gama ameaga dunia

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Habari zilipatikana sasa hivi zinaleza kwamba mwanasiasa na mtumishi wa zamani serikalini, Dr. Laurence Gama ameaga dunia katika Hospitali ya Agakhan, Dar es Salaam. Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi Ameen.
 
oooh no, this is very bad news, RIP mzee Gama, Dr waaina ya kipekee, ni daktari afananae na Dr salimin Armour, Dr NCHIMBI, Dr Makongoro Mahanga, ila yeye hakuwa kibaraka wa mafisadi kamwe, kwake kazi ilikua kwa maendeleo.
 
RIP Mzee Gama. Namkubuka sana mara zote nilizokutana naye pale ofisini kwake akiwa RC Moro. Mungu awape nguvu wafiwa ili wakabiliana na huu msiba. Bwana ametoa.........Amina.
 
RIP,mkuu wangu wa mkoa Tabora,Tabora tutakukumbuka kwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na timu uliyoianzisha ya Milambo.
 
oooh no, this is very bad news, RIP mzee Gama, Dr waaina ya kipekee, ni daktari afananae na Dr salimin Armour, Dr NCHIMBI, Dr Makongoro Mahanga, ila yeye hakuwa kibaraka wa mafisadi kamwe, kwake kazi ilikua kwa maendeleo.

Hilo tu ndilo la kusema hata wakati huu umauti ulipomfika? Uungwana na vitendo nguvumali.
Alikuwa ni kiongozi shupavu mpenda watu na mwanamichezo wa ukweli, katu sitoweza kusahau mchango wake alipokuwa mkuu wa mkoa wa tabora haswa kusimamia timu ya milambo hadi kuwa tishio miongoni mwa timu za ligi kuu. Innalilah wainna illlah rajoon.
 
RIP Mzee Laurence Mtazama Gama. Tutakukumbuka kwa juhudi zako za kukuza michezo hasa katika mikoa ya Iringa(Timu ya Lipuli) na Tabora (Timu ya Milambo na usimamizi uliofanya kujenga uwanja wa Ali Hassan Mwinyi)

Nikiwa kama chipukizi wa CCM miaka hiyo nakukumbuka sana hasa katika sherehe za CCM kitaifa 1988, Ulipotuandalia chakula na Rais Mwinyi wakati huo pale kwako Bomani.

"Sisi sote ni wa mwenyezi mungu na marejeo kwake ni lazima"
 
RIP Dr. Gama...:(
Hivi huyu bwana alikua anafanya nini siku za karibuni, ni muda mrefu sijamsikia
.
 
RIP Dr. Gama...:(
Hivi huyu bwana alikua anafanya nini siku za karibuni, ni muda mrefu sijamsikia
.

Alikuwa anajiandaa kugombea ubunge katika jimbo lonaloshikiliwa na Dr. Nchimbi!

RIP former Katibu Mkuu wa CCM.
 
Alikuwa anajiandaa kugombea ubunge katika jimbo lonaloshikiliwa na Dr. Nchimbi!

RIP former Katibu Mkuu wa CCM.

Huyu bwana aliwahishutumiwa na muungwana kwenye mbio za 1995 kuwa anampendelea C D Msuya, hivyo muungwana akatangaza kuwa hana imani naye kama msimamizi mkuu wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM wakati huo. R.I.P hivi kulikuwa na maandalizi yoyote ya kumpeleka nje kwa matibabu kabla ya mauti kumfika?.
 
Hilo tu ndilo la kusema hata wakati huu umauti ulipomfika? Uungwana na vitendo nguvumali.
Alikuwa ni kiongozi shupavu mpenda watu na mwanamichezo wa ukweli, katu sitoweza kusahau mchango wake alipokuwa mkuu wa mkoa wa tabora haswa kusimamia timu ya milambo hadi kuwa tishio miongoni mwa timu za ligi kuu. Innalilah wainna illlah rajoon.
Alikua Shupavu kwelikweli, zaidi ya yote nina urafiki na familia yote, wakati wa kufa ni wakati wa kukumbuka mazuri na mabaya, sorry for that.

kwangu nimempoteza moja ya watu waliokasirishwa na tabia ya kuependeleana kazini na na upuuzi wote, alijituma kujenga taifa lake mpaka kifo, doa pekee ni udaktari wake. RIP mzee wangu GAMA.
 
.... hivi kulikuwa na maandalizi yoyote ya kumpeleka nje kwa matibabu kabla ya mauti kumfika?...

Nadhani wenye jibu watakujibu!
Kiongozi mwingine mzalendo aliyeugulia na kufia nchini hivi karibuni ni Mhe. Mbunge Sigfrid Ng'itu wa Lindi, huyu naye kaugulia na kufia Muhimbili! Hakuna cha nje ya nchi wala nini!
 
Idimi,....Hawa walikosa muda wa kwenda kutibiwa huko kutokana na aina za vifo zilizowapata!...Otherwise, poleni jamaaaza marehemu!
 
Habari zilipatikana sasa hivi zinaleza kwamba mwanasiasa na mtumishi wa zamani serikalini, Dr. Laurence Gama ameaga dunia katika Hospitali ya Agakhan, Dar es Salaam. Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi Ameen.
R.I.P. Namkumbuka sana wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma jinsi alivyokuwa anilea majimaji ya songea.....na baada ya hapo kila mkoa aliokwenda, timu za mpira wa miguu za mikoa hiyo zilinyamyuka sana. POLENI WAFIWA
 
R.I.P Dk. L.M. Gama,wanamichezo daima tutakukumbuka kwa juhudi zako za kuendeleza michezo(hasa Soka) katika mikoa ya Tabora,Morogoro na Ruvuma
 
Back
Top Bottom