Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Naona wapiga Lamri wanaongezeka kwa ari mpya zaidi, kasi mpya zaidi na nguvu mpya zaidi. Viva wapiga LAMRI

Whatever, its just a matter of time.
 
Acha ujjinga wewe,yaani sababu kipenzi chenu kimaenasa mtegoni ndio iwe kawaida!!!!!

Jingazzz saaaaanaaa

Ujinga ni mtizamo na definition ya mtamkaji wa neno ujinga, inawezekana yeye ndo akawa mjinga zaidi na hajitambui kuwa mjinga.
 
Kuwakwenye chama,maana yake ni kunia mamoja,kama utaenda kinyume na chama basi lazima uwe msaliti.Chama mara zote kinakuwa na lengo moja, kama kuna mawazo mengine ya kukijenga chama lazima uwashirikishe na wenzako ili kwa pamoja mueze kufikia lengo mlilojiwekea.Mimi nafikiri kwa kuwasaidia mawazo kina Mkumbo ni kuanzisha chama chenu ambacho kitakubali mawazo nje ya malengo ya chama,labda mnaweza kuwa mbadala wa CCM na CDM.
 
Hivi kwa nini kama ZZK na Kina Kitilaa na Mwigamba wasianzishe Chama chao? Kama ZZT anataka Uenyekiti si aanzishe chama chake? Yeye si maarufu na ana uhakika watu watamfuata? Anaogopa nini? Tena wakianzisha ZZT Mwenyekiti Kaimu Mwenyekiti Kitilaa na Katibu Mwigamba.
 
I can not urge with a fool.
Nani kakwambia ukiwa na kidegree cha SOCIOLOGY ndio unakuwa bweg? Unatakwa kuwaambia wote wenye SOCIOLOGY ni mabwege?

Uzuri ni kuwa ukiwa bweg unaweza usijitambue kuwa wewe ni bweg, na akina Kitila watawadanganya Mabwege kama ninyi. Kwa akili yako Kitila na Zitto ndio unadhani watakuletea hicho chama mbadala. KEEP WAITING, utakuja kudawazwa na ndipo utakapotambua kuwa wewe kweli ni mmoja wa Mabwege.
 
I can not urge with a fool.

Ki-English cha Lumumba bhana. URGE or ARGUE? Nadhani wewe ndio fulish (foolish) kwelikweli. Waambie Lumumba wakupatie fedha ya Tuition.

Na pia tambua kuwa unaweza kuwa fool wakati huo hautambui kuwa wewe ni mpumbav. Usidhani unaweza kunyamazisha hoja kwa kuwaita watu wapumbav kwa kutumia kipimo cha akili ya LUMUMBA.
 
.





Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na
utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti' mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.



Source:
Raia Mwema[/QUOTE]


  • Dr Mkumbo ni ujinga kuanza kutamani madaraka wakati wenzako wako busy kuimarisha chama na hushiriki kukiimarisha
  • Ni ujinga kutangaza nia ya kugombea uongozi wa chama huku ukijua fika chama kina operation mbalimbali za kukimarisha nawe hujashiriki ktk operation hizo
  • Lakini zaidi sana Dr. mkumbo ulikuwa mjinga kumwamini Zito wakati hujui malengo yake. hakuna asiye jua kuwa zito ni mslaliti na kama hujatambua hilo basi na huo ni ujinga na tena upofu uliokithiri. Dr Mkumbo usije ukawa umepofushwa na laki mbili mbili ulizokuwa una tumiwa na ZZk kupitia M-Pesa
 
ivi huyu mkumbo confidence ya kuongea haya kaitoa wapi? alishawai hata kugombea na wananchi wakamchagua? akagombee hata udiwani awaeleze watu sense wamchague ndio at least tunaweza mfikiria kumsikiliza!
 
Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara.

Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba.

Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza,
viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila.


Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.


Source:
Raia Mwema
Zitto kakutuma uje umtetee? too late!! Kosa la USALITI huwa halina msamaha!! Matokeo ya Staa wa Kitila 2010 Ubunge haya hapa, hata 50% ya kura zote hakupata
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
[TR]
[TD="colspan: 4"] KIGOMA KASKAZINI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] Candidate
[/TD]
[TD="width: 20%"] Political Party
[/TD]
[TD="width: 20%"]
Number of Votes
[/TD]
[TD="width: 15%"]
Percentage Votes
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] ZITTO KABWE ZUBERI
[/TD]
[TD="width: 20%"] CHADEMA
[/TD]
[TD="width: 20%"]
23,366
[/TD]
[TD="width: 15%"]
48.57
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] LEMBO ROBINSON FULGENCE
[/TD]
[TD="width: 20%"] CCM
[/TD]
[TD="width: 20%"]
18,352
[/TD]
[TD="width: 15%"]
38.15
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mmmh sidhani na kama he is basi alikuwa obsessed na siasa na kama alikuwa obsessed alipoteza objectivity!!!!!!!

Ndio maana mtu smart and objective kuwa siasani tena hizi????!!!!!

Kimsingi mkuu Olesaidimi kajichanganya sana kwenye hoja zake kama walivyobainisha wachangiaji wengine...kwa mtu kama yeye alitakiwa awe better than this...naona anaona zaidi kibanzi kwenye jicho la mwenzake kuliko boriti ndani ya jicho lake mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Doctor umejidhalilisha kwa kutoa utetezi usio na mashiko, bora urudi CCM ili ukafanye ulichokuwa unakifanya CDM. Hakuna chama kina sera mbaya, katiba za vyama vyote zime hakikishwa na kuthibitishwa na vyombo vya Serikali. Hivyo kama wewe hufuati mtu bali chama, nadhani huna haja ya kusumbua moyo wako. Tanzania kuna vyama zaidi ya 10, nenda kimojawapo unacho ona kitakufaa na usifuate watu. Waache watanzania wafuate viongozi wanao waamini na siyo Chama.

Zitto hana sifa wala hawezi kumfikia Mrema katika utendaji, Zitto anatumika kama tambara la deki, kafanikiwa kuwatumia watu kama wewe sasa mmetupwa mbali hamna pa kushika mnaanza kulalamika. Ndiyo maana ameamua kukimbilia mahakamani ili asipotee kwenye uwanja wa kisiasa, angekuwa na ubavu-angeacha wamwage ili aende na kundi la watu wakaimarishe nguvu huko aendako kisha agombee huo Urais!

Zitto mwenyewe anajitambua nje ya CDM hana wafuasi zaidi ya wale aliokuwa anawatumia kubomoa CDM!
 
Zitto mwenyewe anajitambua nje ya CDM hana wafuasi zaidi ya wale aliokuwa anawatumia kubomoa CDM!

Hivi jimboni kwake ana madiwani wangapi wa CDM?

Mbona wanaom-support wote ni wale wenye shutuma kama za kwake; Chagulani, Matata, + vijana wasiojua kinachoendelea nchini?

Zubeda hana lolote huyo; aungane na wenzake wakaimbe Chigomaaa
 
Tafakuri tunduizi, nakushauri hata wewe uangalie namna ili urudi kundini, nafasi yako bado ipo, ni mtu mhimu.
 
aanzishe chama chao, maana walikuwa na mkakati mzuri sana, nafikiri ndio itakuwa mbadala wa ccm na cdm. kila la kheri Dr uliyedanganyika.
 
sijui dhamira yako moyoni DK,pengine mlikua na nia njema lakini njia mlizotaka kutumia ni njia haramu,za kimafioso.kumchafua mnayetaka kumtoa ni uhuni.Na aina ya usiri wenu vinatia mashaka .isitoshe kama kweli nyie ni waumini wa demokrasia ni demokrasia gani ya watu wanne kati ya watu labda tufanye 1000.kwa hiyo nyie watu watatu mna akili kuliko watu 1000 .mlichokua mnataka kufanya sio demokrasia ila ni kuwachagulia wanachama wenzenu kiongozi wao.nyinyi watu watatu mlitaka kumsimika mtu wenu MM.Hata hivyo sio kila kilichowezekana kufanyika kumpata Obama USA kinafaa au kuweza kufanyika kumpata kiongozi fulani hapa TZ.
 
Anachokifanya Kitila ni kutaka kujisafisha kwa kuichafua Chadema ,akili ya Kitila ktk hili inarudi kinyume nyume katika kifikiri/kuamua ni bora angekaa kimya pengine ingesaidia.Kama kweli wananchi wanataka chama mmbadala asubirie majibu katika operesheni zilizotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
 
aanzishe chama chao, maana walikuwa na mkakati mzuri sana, nafikiri ndio itakuwa mbadala wa ccm na cdm. kila la kheri Dr uliyedanganyika.

vipi huyu dakitari ameendelea na makala yake ktk Raia Mwema la leo au ameingia mitini baada ya kupigwa sana za uso. Maana naona alikuwa anaanapima upepo.
 
Kumbe watu tunatofautiana sana katika kuona na kutafsiri mambo na kwa kuisoma hii makala ya Kitila (japo anasema itaendelea wiki ijayo), basi leo nimepata uhakika kabisa kwamba nchi hii inarudishwa nyuma na wasomi waliojijengea taswira ya kuwa kwa vile ni wasomi walioelimika katika jambo moja wanadhani hiyo inawapa freepass ya kuwa sahihi kwa mambo mengine.

Kitila ni mfano mmojawapo. Makala imeanza vizuri ila ilipofika katikati ikaonyesha mambo fulani wazi. Kumbe makala imelenga kujipoza machungu kwa kufukuzwa uanachama wa Chadema, imelenga kuficha udhaifu wake kuuhamishia kwa wengine, imelenga kufurahisha saikoljia yake kwamba upande wake uko sahihi, upande wa wengine uko hovyo.

Na hii ndo saikolojia ya wakosaji katika asili ya binadamu, hatuwezagi kukaa kimya tukikosea. Sasa tukirudi kwenye article yake kuna vitu vichache vinavyoonyesha wazi kabisa malengo ya Dr. Kitila ni nini. Hebu mcheki hapa:



Kwa haraka haraka tayari umeshajua Kitila anaelekea wapi. Tayari keshataka kuwaamninsha watu kwamba kwa vile yeye kafukuzwa hii ni sawa na mgogoro uliosababisha NCCR ikaffifia, na Chadema haina jipya inaelekea huko huko.

Watu wa dizaini hizi huwa hawawezi kuondoka sehemu halafu wakapatakia mema sehemu waliyotoka. Ni ubinafsi tu wa mwafrika, na pengine binadamu tulio wengi. Leo hii nikifukuzwa kazini kwangu kwa utovu wa nidhamu fulani, deep inside nitapaombea sehemu yangu hiyo ya kazi pafilisike -- kwa style ile ile ya 'adui mwombee njaa'. No, Dr. Kitila, you can do better than this.

Umenena vyema, ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom