Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Source:
Raia Mwema

  • A%20S-alert1.gif

    mkumbo atueleze mbona mwanzo alikuwa akisifia CDM kuwa ina demokrasia ya kweli, je imekosa demokrasia kwakuwa yy kafukuzwa uanachama. mm naamini hata kufukuzwa mtu uanachama ni sehemu ya demokrasia

    pia kama wao walikuwa na mkakati wa ushindi hivi kulikuwa na mantiki gani kwao kama wasomi kuandika lugha ya dharau na kutowaheshimu viongoozi wao, kwann hawakutaka kushindana kwa nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu?

    mbona hajatueleza kuhusu fedha zinazodaiwa walipewa kwa lengo la kuvuruga cdm, kwann alipokea???

    yy na kundi lake wanahitaji kutafakari, kujipima na kuona endapo wana sifa hata za kupewa wadhifa huo

kitila na kundi lenu mmewasaliti watanzania ,mmeisaliti democrasia ya kweli.mnaanzisha democrasi mpya ya majungu na fitina.kwel mhadhili mwandamizi unadirik kuendesha siasa za ajabajab.utubu
 
Dr. Kitila Mkumbo, he is right, and will always be right on this matter.
 
Kitila anashabikia itikadi, anashabikia mabadiliko, ana ndoto ya kuona mabadiliko ya kweli yanatokea ndani ya nchi hii.sasa kama una imani na mtu fulani kuwa ndiye dereva anayeweza kulifikisha gari unalosafiria salama kule uendako,ni dhambi ama ni ushabiki kusema kuwa fulani ndio awe dereva?

umeanza vizuri lakini mara ghafla...

umerudi mule mule.

kwenye hili si mtu atakayetufikisha mkulu, ni chama, ni taasisi, ni mifumo imara ndani ya cdm. vinginevyo kaolewe na zito kama unampenda sana. tuachie chama chetu, tumekijenga kwa jasho na damu zetu mbichi kabisa hiki chama. si rahisi kiivo kama unavofikiri kaka.
 
Kwa watanzania wote wanaoitakia mema nchi yetu, kwa pamoja hatuwezi kukaa kimya na kukubaliana na upotoshaji, ubabaishaji, uzandiki, ujinga, usaliti na kutufanya sote ni mapunguani uliofanywa na Bw, Mkumbo na kundi lake hadi kutimuliwa na chama chao. Kama hii haitoshi bado anadiriki kuandika makala iliyopungufu na ambayo kwa bahati mbaya inakuwa ni nyepesi ki hoja na inadhidi kuthibitisha yale yote watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao wamekuwa wakiyaona.
Lakini kwa bahati mbaya sana, sisi sote tumejikita katika kumchambua yeye Mkumbo na wenzake ambao kidhahiri ni wasaliti, huku tunaacha kuaangalia nini hasa msingi wa usaliti huu. Kama ambavyo baadhi wa wachangiaji wameonyesha, ni kuwa inawezekana hawa akina Mkumbo na Zitto wake ni waajiriwa wa wanaotaka Chadema isambaratike. Hawa walioko nyuma ya usaliti huu ndiyo ningependa tuwajadili. Kuendelea kumjadili Mkumbo ni kuendelea kufanikisha nia na njama za WALIO NYUMA YA MPANGO HUU MWOVU. Mimi naanza:

1. Ni ukweli usiopingika TISS (Hawa ni waajiriwa wetu. Tunawalipa kwa kodi zetu) Kwa nini wanatumia taasisi kuvuruga upinzani ambayo ni nguzo kuu ya democrasia? Kwa nini. Ni kwa ajili ya maslahi ya nani hasa?

2. Ni ukweli usiopingika kwamba sasa wimbi la mageuzi limeshika kasi kweli, kama ambavyo huwa nasema, ni WIMBI, halimjui Mbowe or Zitto. Leo hii Zitto akiondoka CDM na kwenda CCM, hataondoka na mtu yeyote. Kwa sababu hawampendi Zito kama Zitto. After all ana nini cha kumpendea?? Sasa kama ni WIMBI, hawa TISS na police hawalioni hili? Kwa nini wasifacilitate fairness. Kwa sababu, kama itatokea kasheshe iwe ni kwa wanainchi or nguvu ya umma kuchukua hatua or wanajeshi vichaa kuvurumisha vifaru wao ndo watakuwa na kazi ya ku clean hiyo mess kama hawakuwakuwa historia.

3. Kwa taarifa mikakati ya kusambaratisha upinzani iliwezekana miaka hiyo. Lakini kipindi hiki hawezekani. Na ushahidi upo kwa Chadema kusurvive matukio mengi likiwemo la akina Mkumbo, in a nutshell, Vurugu uchaguzi Bavicha, group ya kina Shonza na wenzake, mawasiliano tata ya Zitto, Mgomo baridi wa Zitto, mauaji na mabomu Arusha, kupata support ya wanaCCM, Kauli za Chadema kufa kabla ya 2013 nk nk

Naomba tuwaseme ili tuikomboe nchi. Upinzani wenye nguvu ni heri kwa nchi, nchi zote tunazozisifia kwa maendeleo, demokrasia imechangia.
 
si wote kaka, ni wale wazee wachache pale juu kwenye hierarchy, ni waoga wa mabadikiko na huwa wanaogopa kuwa mabadilko yakitokea eti watapoteza vyeo vyao( which is false anyway). Vijana wengi TISS ni wana-cdm, hilo wala halina ubishi.
 
umeanza vizuri lakini mara ghafla...

umerudi mule mule.

kwenye hili si mtu atakayetufikisha mkulu, ni chama, ni taasisi, ni mifumo imara ndani ya cdm. vinginevyo kaolewe na zito kama unampenda sana. tuachie chama chetu, tumekijenga kwa jasho na damu zetu mbichi kabisa hiki chama. si rahisi kiivo kama unavofikiri kaka.
taasisi haiwezi kuwa imara kama watu wanaiongoza hiyo taasisi hawasimamii misingi ya kuiendesha hiyo taasisi ili kufikia malengo yake mkuu.
Pia jaribu kuwa na lugha nzuri maana sasa naona unataka kulithibitishia jukwaa hili kuwa wale wanaomuunga mkono fulani wote ni watu wa v...ba,mimi nisingependa kukuchukulia hivyo mkuu
 
misingi ipi hiyo mkulu? ni hiyo ya kuandaa mikakati ya siri ya kuwatusi viongozi wa chama na kisha kuwapindua kisirisiri? hiyo siyo misingi bali ni uhuni mkubwa.
 
umedhihirisha wewe huna tofauti na nyumbu tu kufuata mkumbo!! yaani unakiri kabisa kwamba hujasoma makala yake na bado unadhani una haki ya kuchangia mjadala huu?!
wafuasi wengi wa mbowe (sio chadema!) ni maamuma!!!!!!!!
Mkuu punguza povu,na mwaka huu nawashauri mtafute kazi,umbea una mwisho wa kutoa posho ya kujikimu.
Nitetee hoja yangu kwanini sina muda wa kusoma hoja za wasaliti:
-Mwaka 1995 NCCR mageuzi ilionekana tishio kwa ccm watu wa system wakafanya mambo yao ccm ikaendelea kuchukua nchi,kwa hoja hizi hizi za tunahitaji chama mbadala NCCR haikuwika tena,mbadala ukaonekana ni CUF,wapenda mabadiliko wakaiunga mkono CUF tukiamini itatukombea kwenye mikono ya udhalimu wa ccm
-Mwaka 2000 CUF ikiwa imeonesha nguvu ya kushika dola,akajitokeza mtaalam muhita na sera ya visu,hivyo hivyo wakaibuka wenye hoja dhaifu ya kuhitaji chama mbadala,CUF haikutajwa tena kuwa chama cha pili baada ya ccm
-mwaka 2010 CDM ikasimama na historia(trend) inaonyesha graph ya CDM ilikuwa inapanda polepole haijawahi kushuka
wapendamapinduzi tukaona trend yake,tukaamini kwamba ni chama mbadala na kikawa na nguvu za hoja,tumeshuhudia movements nyingi walizofanya nchi nzima na ccm wameamshwa ofisi hazikaliki na maendeleo tunayaona,anatokea mtu eti Dokta,msomi bila aibu anasema tena TUNAHITAJI CHAMA MBADALA...?najiuliza kila uchaguzi ukikaribia,chama cha upinzani chenye nguvu tunaki-discolify kwa hoja dhaifu,hivi kweli kwa mtindo huu tutafika?
Kuna haja gani kuwa na wasomi kama hawa wachumia tumbo eti wamebobea kwenye siasa,
Sitamani goodluck5 unijibu maana una hasira,na mtu mwenye hasira uwezo wa kufikiri unapungua anaishia kutukana.
Nikushauri wewe na wenzio mtafute kazi,maana watanzania tumeamka hatudanganyiki tena.
Period.
 
Dr. msaliti hata vikija mbadala wa CCM na CDM utasaliti tu, huna maana ktk jamii kwa sasa labda familia yako tu. Once a traitor will always be.
 
Ahsante mkuu nimepata uelewa wakutosha unajua kupambanua mambo mungu Akubariki.
 
Nadhani kwenye hili kipofu wa kwanza atakuwa ni Dr. Kitila Mkumbo mwenyewe kwa kuacha kushabikia chama akaamua kumshabikia Zito. Sisi wengine ni mashabiki wa Chama ndiyo maana tutaendelea kushikamana na uongozi halali kikatiba na vyombo vyote vya chama vilivyopo kwa mujibu wa katiba.

Nadhani Dr. Kitila na wale wanaomshabikia Zito ndiyo vipofu maana wanamshabikia mtu badala ya kushabikia chama.

Inahitaji Weledi wa hali ya juu kumuelewa Nguli Kitila Mkumbo, Pale tutakapoacha kushabikia Viongozi na badala yake kupenda CHAMA, tutaweza kuchambua hoja za msingi na kasoro zilizopo katika uongozi.
 
amesema hajavunja katiba. na ndo maana alikataa kuomba radhi. rudia kusoma hiyo thread. tatizo lenu mnasoma utafikiri mnaiba.

Nafikiri wewe hata masikio hauna , yeye mwenyewe alikiri amevunja katiba. Soma katiba ya CDM inakataza matusi, uongo na kuanzisha vikundi vya fitina na majungu, inakataza makundi, na kampeni kabla ya muda kutangazwa na taratibu kutolewa. Rejea uchaguzi wa umoja wa vijana uliowachomoa akina Mchange , Ben Saanane nk. Je kwenye harakati zao za waraka 2013 kulikuwa na matusi? Makundi?, kampeni kabla ya muda? tuhuma pasipo kuzipeleka kwenye vikao vya chama? Uongo na uzushi? Ndio maana nikaomba mwenye waraka aulete, video ya serena nk ili akili za wanaosahau haraka na wanaofuata watu badala ya kweli iyonekane.
 
Dr Kitila nilikuwa nakuheshimu sana, kumbe wa hovyo tu wewe, msomi mzima umekaa kimajungu majungu tu, utapata sana pressure, ulifikili kuisaliti chadema ni kazi nyepesi, na bado hayo yaliyokukuta ni mwanzo tu, dhambi ya usaliti itakutafuna sana, unajuta kuifahamu chadema, pole sana uliyataka mwenyewe, unadhalilika sana heri ukae kimya tu kuliko unavyofanya.
 
Kitila anashabikia itikadi, anashabikia mabadiliko, ana ndoto ya kuona mabadiliko ya kweli yanatokea ndani ya nchi hii.sasa kama una imani na mtu fulani kuwa ndiye dereva anayeweza kulifikisha gari unalosafiria salama kule uendako,ni dhambi ama ni ushabiki kusema kuwa fulani ndio awe dereva?

----- mtupu
 
  • A%20S-alert1.gif

    mkumbo atueleze mbona mwanzo alikuwa akisifia CDM kuwa ina demokrasia ya kweli, je imekosa demokrasia kwakuwa yy kafukuzwa uanachama. mm naamini hata kufukuzwa mtu uanachama ni sehemu ya demokrasia

    pia kama wao walikuwa na mkakati wa ushindi hivi kulikuwa na mantiki gani kwao kama wasomi kuandika lugha ya dharau na kutowaheshimu viongoozi wao, kwann hawakutaka kushindana kwa nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu?

    mbona hajatueleza kuhusu fedha zinazodaiwa walipewa kwa lengo la kuvuruga cdm, kwann alipokea???

    yy na kundi lake wanahitaji kutafakari, kujipima na kuona endapo wana sifa hata za kupewa wadhifa huo

Mimi nimekuelewa kwa namna alivyoeleza kama cdm wanahitaji demokrasia ya kweli wanahitaji kusameheana ila wewe ni wale ambao ameleza kuwa mnawasikiliza viongozi na sio chama.
Wewe usema eti mbona haelezi pesa alizochukua kwa upande huo hata vingozi wa juu nao walichukua pesa mbona na wao hawasemi kama walichukua.
Hata kama unawapenda namna gani hao viongozi ukweli unabaki pale pale kwa uongozi wa CHADEMA ni wa kiimla kwamba Mpaka Mtei aruhusu vinginevyo huwezi kuwa kiongozi cdm.
 
no compromise with traitors
 
Back
Top Bottom