Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Kumbe watu tunatofautiana sana katika kuona na kutafsiri mambo na kwa kuisoma hii makala ya Kitila (japo anasema itaendelea wiki ijayo), basi leo nimepata uhakika kabisa kwamba nchi hii inarudishwa nyuma na wasomi waliojijengea taswira ya kuwa kwa vile ni wasomi walioelimika katika jambo moja wanadhani hiyo inawapa freepass ya kuwa sahihi kwa mambo mengine.

Kitila ni mfano mmojawapo. Makala imeanza vizuri ila ilipofika katikati ikaonyesha mambo fulani wazi. Kumbe makala imelenga kujipoza machungu kwa kufukuzwa uanachama wa Chadema, imelenga kuficha udhaifu wake kuuhamishia kwa wengine, imelenga kufurahisha saikoljia yake kwamba upande wake uko sahihi, upande wa wengine uko hovyo.

Na hii ndo saikolojia ya wakosaji katika asili ya binadamu, hatuwezagi kukaa kimya tukikosea. Sasa tukirudi kwenye article yake kuna vitu vichache vinavyoonyesha wazi kabisa malengo ya Dr. Kitila ni nini. Hebu mcheki hapa:

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Kwa haraka haraka tayari umeshajua Kitila anaelekea wapi. Tayari keshataka kuwaamninsha watu kwamba kwa vile yeye kafukuzwa hii ni sawa na mgogoro uliosababisha NCCR ikaffifia, na Chadema haina jipya inaelekea huko huko.

Watu wa dizaini hizi huwa hawawezi kuondoka sehemu halafu wakapatakia mema sehemu waliyotoka. Ni ubinafsi tu wa mwafrika, na pengine binadamu tulio wengi. Leo hii nikifukuzwa kazini kwangu kwa utovu wa nidhamu fulani, deep inside nitapaombea sehemu yangu hiyo ya kazi pafilisike -- kwa style ile ile ya 'adui mwombee njaa'. No, Dr. Kitila, you can do better than this.
 
Dr. Kitila

Sikubahatika sana Kusoma mabandiko yako yoyote Kwa undani Na Kwa mantiki hiyo sijawahi kuccoment negative wala positive Kwenye maelezo yoyote yanayo kuhusu. Nina principle ya kutomwongelea Mtu kabla ya Kujua uwezo wa fikra zake. Sisi tunaoamini NENO la Mungu linasema

Luka 5:45--Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Sasa Kama Bandiko Hili ndio Picha ya Yale yaujazayo Moyo Wa Dr. Kitila Basi SINA shaka wala dukuduku tena Kwamba ilipaswa Kweli aondolewe.

Labda Dr Kitila Uelewe Dhima ya Chama Cha Kisiasa, Na KUSUDIO la Chama CHOCHOTE kuongoza DOLA, sio mambo ya ujingajinga, ubinafsi Na SHAUKU au Tamanio binafsi la Mtu au kikundi flan Cha watu. Na pia wanayekuita Dr Uelewe pia Dhima ya Kiongozi au Mwanachama wa Chama Chochote Cha Kisiasa Chenye mtazamo Na Kusudio la kishika Dola sio KUSINDIKIZA, huelekeza kutumia Akili zake, nia Yake, Elimu Yake Na hata Muda wake kuchochea vuguvugu Hilo la mageuzi Kwa bidii Na sio kila anapogeuza pillow kitandani mwake anawazia Uongozi huu ni Ugonjwa wenye kutu mbaya sana. What is chairmanship?!??! ..

Wakati Mwingine sikatai unaweza kuchochea vuguvugu hili la Mageuzi, lakini ukahisi hawakuelewi au hawakuamini au wanakupuuza, lazima ujifanyie introspect .. Kwanini hawanielewi.. Ni aina ya uzembe wa kufikiri kuamini your are always 100% parfect and these fellows ate fools..

Lakini pia Kama unaamini my fellow are bunch of fools thats why they anderstand not my smart plan, kwanini ung'ang'anie Kuwa Na unaoamini ni wajinga!!? . Kwanini usijiondoe weye mstaarabu ukaanzisha kile chako unachoamini kiko sahihi .. Utauza sera zako yamkini watu wakaziamini Na kukuunga mkono.. Unless uwe Na Tatizo ..unapoanza kuwapinga, kuwakosoa wale unaoamini hawako sawa unadhani nani Hayuko Sawa.
Mwalimu wangu wa Hesabu nayemweshimu sana Marehemu Prop.Shayo alianzisha Chama Chake, Demokrasia Makini Sitaki kuongelea alifaulu au alifeli lakini alianzisha Chama chake kivyake, Sheria Za Kuanzisha Chama Cha Kisiasa Tanzania ziko wazi ANZA CHAKO FANYA YAKO FUJO YA NINI, Makelele ya NINI??!????!

MBAYA zaidi unatumia Vibaya Kurasa Za Magazeti Kufanya political pollution ..! Ungedadavua kwanini mliamua kuandaa waraka kinyume Na Taratibu Za Chama Chenu?!Na kwanini mlikwenda kinyume Na tararibu zenu mwenyewe, Je demokrasia ya VYAMA vingi ni Kufanya kila ukitakacho Ndani ya Chama Kwa jina la Vyama vingi?!?

Ungeeleza Nani Na wapi Alinyimwa nafasi ya Kugombea uongozi mahali Fulani Na Kwa nini!? Na yamkini Sababu hiyo iliwapelekea kuandaa waraka ule!?!?? Lakini Cha zaidi ungeeleza Kama kuna kifungu Ndani ya KATIBA ye Chama Chenu kilichotoa mwanya wa ninyi kufanya kile mlichokifanya? Lakini zaidi sana jiulize mwenyewe Je Kama wewe utakuwa Mwenyekiti wa Chama flani Je utapendelea team yako ya Kazi nayo ikawa inatengeneza side-mastermind Na Fukuto mbalimbali..!?

Lakini Mwisho umetumia 96% ya Waraka wako Kumtetea mwanachama mwenzako wala sio wewe huu ni udhaifu mkubwa unaotoa upenyo mtu ku-smell something fishy around.. Jitambue .. Nyuma kuna Jamii Kubwa ya Watanzania wanaotaka Mageuzi.. Utaingizwa wewe Na ukoo wako wote Na jamaa Za nyumba yako Kwenye record Za wasaliti wa mageuzi..
 
Haya ndo ma-Lecturer yetu! Pambaf.. kabisa!!

Yaani huyu jamaa anataka tuendelee kulea ujinga kwa kuogopa mtu kwamba atayumbisha chama? Hebu aache hizo mambo bwana. Hivi hawa jamaa walipoanzisha mkakati wa chini kwa chini walikuwa wanafanya vizuri kweli hivyo? Kama hawa jamaa wanataka madaraka makubwa waende wakaanzishe chama chao ndo tutawaelewa.

Big up CHADEMA kwa mkakati huo wa kusafisha mapandikizi.
Mkuu, wameona ng'ombe kanenepa wanataka wamle na watanunua mchanga na kumkuza tena. Mwenye hekima na aelewe.
 
Cha kufurahisha hata mahakamani alizomewa na mahakama ziluzofuata uvccm na cuf wakapeleka wapambe tena wakaanzisha fujo ili ionekane cdm ni fujo na mteule msajili kapata nafasi ya kutoa press release. Zzk huna wafuasi bali wasaluti wenzio na masalia baadhi walishahama. Utaondoka mwenyewe.
 
Kitila anaburuzwa na ZItto tu, namjua vizuri ni kilaza flani hivi. Kana uroho wa madaraka ile mbaya. Kana maneno mengi ndo maana kanaonekana kanajua kitu...kalisoma PCB pale Pugu kakapata ufaulu hafifu kakapita njia za panya kwenda chuo kusoma ungwini...ati nako kana PhD!
Zitto ni kama mlima kwa haka kajamaa..ndo maana anakadrg kwenye matope na ki PhD chake!
However, ni ka home boy kangu na nilikuwa mbele yake pale Pugu A-level.
 
So Kitila Mkumbo you need mbadala wa CDM na CCM, kwa hiyo mlitaka muangamize CDM ili muelekee kwa huyo mbala. Acheni uhuni bhana.

Wakati wa uchaguzi 2010 kampeni zinaendelea. Zitto alikuwa busy kutangaza atagombea Urais 2015. Was it right timing? Acheni uhuni na kuaminisha wananchi ujinga.

Ndio Zitto alitaka kugombea Uenyekiti wa CDM, Kitila nakwambia kwamba, huyo Zitto wako angepata Uenyekiti leo CDM isingekuwepo.

Endelea kutuletea porojo zako unadhani wote ni mabwege.......

Sikutegemea Dr Mkumbo angeweza kuandika ugoro kiasi hiki hapa Jf. Yaani Mm ambae ni Zitto akae na Kina Wasira Igondhu, NCHIMBI, na kina Chemba wakipanga mikakati ya kuia Cdm nyie mnasema mmeonewa? Hivi ni wanafunzi gani unasomesha wewe Mkumbo? Mbona unazungumzia waraka tu huzungumzii usaliti wa kupokea pesa toka Ccm?? Mbona husemi 200,000 ulizokuwa --------- na Zitto kila mwrzi ni za nini? Ulikuwa unamtumikua Zitto au Chadema?? Ingekuwa kuna ruhusa ya kuua bila mahakama nyie mnastahili kufungwa jiwe shingoni mtupwe bahari muwe chakula cha samaki. Acheni ujinga bwana!!!
 
Inakatisha Tamaa sana vyama vyetu vyooooote vimejaa wahuni si ccm, chadema, nccr ...... you name it. Tufanye nini. Binafsi nakata tamaa. Sasa sishangai kwnn Hata wasomi wengi tumeamua kuishi kimkatokato tu. we r a country in a verge of total collapse... morally. Respect kwa watu wachache kama Kolimba, wangwe n Mkumbo. Wote hupotezwa lkn kweli haipotei, you will be remembered.
Kwenye andiko hili la Mh Dr. Kitila nimeona kuna sehemu mbili au tatu kama kajichanganya

1.Anaposema uteuzi ni kwa wateule tu




na sio kama utaratibu ulivyo wa kujaza fomu na kurudisha

Swali katika waraka huo ambao waliuandaa je walipiga kura wenyewe wa nne kwa maana dr kitila,zitto,mwigamba na huyo mm2 na zito akashinda?au waliamua tu kumteua au alijiteua zito mwenyewe?


2.Chama hakijengi mfumo wa kushabikiwa ila viongozi wametengenexa mfumo wa kushabikiwa wao,viongozi

Je hapo haoni kama zitto nae amehusika kutengeneza mfumo huo mbona na yeye alikuwa na watu wanaomuunga mkono yeye kama yeye?

3.Hivi dr katiba yetu ya leo na hii rasimu ikipita umri wa MGOMEA URAIS UTAKUA NA NIKUANZIA MIAKA MINGAPI

JE zitto mungu akitujalia uhai atakua amefikisha umri halisi wa kupigiwa kura kama rais????

4.Hivi NCCR MAGEUZI NA CHADEMA mwaka 2010 waliopeperusha bendera ya kugombea urais walikuwa wenyeviti wa VYAMA VYAO????????


SHUKRANI MLETA UZI NA DR KITILA.
 
Kitila unahitaji kutulia kwa sasa.Hata washabiki wako tunapojilazimisha kukupa haki kwa hili kakweli akili inakataa.Tulia dr.Njia uliyotumia ni ya watu waoga wasuojiamuni.
 
Wenye Akili nyingi tulishaliona hilo kitambo. Na ndio maana huwezi kuona nimesupport upuuzi unaofanywa na akina mbowe hata kidogo. Kazi kwao ma mburula.

Wewe kama nani? na unadhani una akili gani? We bado kipofu wa kawaida kama vipofu wengine tu. Huna uwezo hata wa kuchambua pumba na mchele!
 
Dr. Kitila popote ulipo naomba jitokeze unijibu hapa,

"Hoja zako zimejikita kwenye neno 'demokrasia', je, kwa kuandaa "mkakati wa mabadiriko" ndani ya chama kwa siri, ni moja ya "demokrasia"?

Pia naomba ututolee ufafanuzi juu ya katiba ya chama, inasemaje juu ya "mkakati" wenu wa siri? Katiba inaruhusu? Kama hairuhusu, nini adhabu yake?

Naomba twende taratibu ili tuchambue pumba na mchele.
 
Hakika Kitila Mkumbo umenena.

Hiki chama ulichokuwa kamwe hakina uwezo hata chembe ya kuiondoa ccm maana wao wanafanya kwa kuwa ccm kafanya na ukiwauliza wanasema mbona ccm wanafanya?


Hakika wassira alinena na chadema imekufa rasmi 2014 na hawana uwezo wa kupata kura hata nusu walizo zipata 2010.


Ni kweli chadema ni chama cha kiimla kabisa na ndio maana ina julikana kiti cha uenyekiti kina hodhiwa na mbowe.

Chadema wanapenda kuitamka demokrasia mdomoni lakini wao wanaiogopa sana na ndio maana suluhu yao ni kuita watu wa haini.


kitila una busara sana hakika nime amini wewe ndio uliye kuwa una muandikia Dr.W.Slaa hotuba 2010.


Hakika dr kitila umedhihisha una busara na sasa nimeamini wewe ndiye uliye tatua mgogoro wa kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambapo ulipendekeza nakuainisha njia nzuri za kuwapa japo kuna wengine walishapita kwa njia zisizo.


Dr kitila wewe ni mwamba.
 
Last edited by a moderator:
Naweza nisiwe na tatizo sana na waraka ila content za huo waraka.

Waraka una udini, matusi, majivuno na kila aina ya uchafu.

Huwezi kutafuta cheo kwa kuwakashifu na kuwatukana wenzio, this is unacceptable!

Uliaminika nje na ndani ya chama lakini umejiaibisha... go to hell doctor!
 
dr. Kitila popote ulipo naomba jitokeze unijibu hapa,

"hoja zako zimejikita kwenye neno 'demokrasia', je, kwa kuandaa "mkakati wa mabadiriko" ndani ya chama kwa siri, ni moja ya "demokrasia"?

Pia naomba ututolee ufafanuzi juu ya katiba ya chama, inasemaje juu ya "mkakati" wenu wa siri? Katiba inaruhusu? Kama hairuhusu, nini adhabu yake?

Naomba twende taratibu ili tuchambue pumba na mchele.

yani unge usome hule waraka usinge uliza haya maswali.
 
Mbadala wa CDM? Kwa hiyo mabadiliko 2013 ilikuwa ni kuleta mbadala wa CDM? Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri nia ni kuleta chama kingine cha siasa ili kiwe mbadala ! Kama ni hivyo viongozi na wanachama wote wa CDM wanahaki zote kuwaita wasali, wahaini kwani nia yenu ilikuwa kuuwa CDM na kuanzisha mbadala. Je huoni mlikuwa hamuwatendei haki wale waliokubaliana na CDM, sera, taratibu , katiba, nk. Ni vyema mkaanzisha mbadala mkaendesha kwa vile mnavyoona inafaa ndio maana ZZK anatakiwa atoke mwenyewe kama anafikiri kama unavyofikiri asisubiri tsunami kwani lazima imbebe.

Nadhani Dr. ameanza maandalizi ya chama mbadala na mabandiko kama haya yanaonesha harakati zake. Unaendelea kusaliti mabadiliko ya watanzania, shame on you Dr!
 
inakatisha tamaa sana vyama vyetu vyooooote vimejaa wahuni si ccm, chadema, nccr ...... You name it. Tufanye nini. Binafsi nakata tamaa. Sasa sishangai kwnn hata wasomi wengi tumeamua kuishi kimkatokato tu. We r a country in a verge of total collapse... Morally. Respect kwa watu wachache kama kolimba, wangwe n mkumbo. Wote hupotezwa lkn kweli haipotei, you will be remembered.

bora hata hawa wahuni wa ccm ambao hawajifichi kuliko hawa wa chadema wanao jificha na kujiita wana demokrasia huku wanaogopa demokrasia.
 
Chadema wapo kwenye wakati mgumu sana. Soon watasambaratika
 
Back
Top Bottom