Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Yan ccm B zito awe mwenyekiti!!! ww kitila una utani.AKIUE CHAMA! Acha tufe chini ya hawa tunaowaamini na si wanaouziana na kukodishiana magari.Chama kikikodishwa kwa maccm kwa ahadi za magari.Atafukuzwa na vuguvugu lililoanzishwa na CDM litakuwa hai daima hata kama chama kitakuwa kimekufa.Kwani mtanzania wa jana c wa leo.Kwanini utengeneze mazingira ya mapinduzi ndani ya chama? believe "YOU ARE THE STUPID INTELLECTUAL AT THE HILL"
 
Le Mutuz,
Busara ni kitu kidogo sana, umeanza vizuri lakini katikati ukaingiza matusi (Chama chenye Wah. WABUNGE) unawaita " Wahuni" Chama kina wafuasi wa kila aina, usishange ukakuta hata Mhe. Malecela ni mwanachama.

Dr. Kitila anajua alichokuwa anafanya na wamefanikwa kwa kiasi Fulani maana issue imegundulika karibu na uchaguzi, yeye yupo kwenye system ndiyo maana ulisikia viongozi wengi wa Kitaifa wakitabiria CDM kifo kila kukicha. Jeulize akina Shonza, Machange, Msacky, Yona.......wote hawa wametokea DUCE na Kitila ni mfanyakazi wa Duce.......kwa nini hakufukuzwa Kama Prof. Baregu Baada ya kugundulika ni mwanachama wa CDM?

Ni kweli wameshaanzisha Chama kingine, Muda sio mrefu utasikia viongozi wake, endelea kuchimbua na sio kutoa matusi kaka, hoja hujibiwa kwa hoja.

- Kaka huwezi kuwaita Viongozi wanapokea rushwa kuwa ni wastaarabu zaidi ya genge la wahuni, nasema tena waliomfukuza Kitila ni genge la wahuni wenzake kama yeye, walipokuwa wanafukuzwa wenzake yeye mbona hakusema haya, haya ameyajua lini toka majuzi tu walipomfukuza? siku zote hakujua haya? Please Kitila amefukuzwa na genge la wahuni wapokea rushwa, wajaza mimba wabunge wa viti maalum ambao anafanana nao sana, Zitto hafananai nao wewe hao kama sio wahuni kwa nini wanakwenda kujisafisha kwenye magazeti ya udaku?

- Wewe nitajie mwanasiasa unayemjua mkubwa duniani uluyewahi kumsikia anaedna kujiosafisha kwenye magazeti ya udaku kama alivyofanya Lissu, aibuu ndio maana ya genge la wahuni kaka!!

Le Mutuz
 
.
Sasa kati ya wanachama na kitilya mkumbo ni nani aliyekuwa anashabikia kiongozi badala ya kukishabikia chama? Mimi naona kitilya ni mmoja wa washabiki wa kiongozi. Swali la msingi kwa Mkumbo ni za nini fedha 200000 alizokuwa anapokea kutoka kwa Zitto kila mwezi nje ya pesa yake halali aliyokuwa akilipwa na chama? Ni nini kazi ya pesa waliyokuwa wakiilipa kwa Zitto watabiri wa ccm kwamba Chadema igakufa kabla ya 2014?.
Pia kwa msomi kama Mkumbo kukifananisha chadema na nccr ni kkosa la kuifanyia vurugu taaluma yake. Sijanua ni kwa nini.
Mwisho napenda kumshauri Dr tuliemwamini sana na kumpa heshima zote ndani ya chadema aondoke tu kwa amani kumfuata Zitto tuliempa heshima kubwa pia lakini akatgumia fursa hiyo kuhujumu ukombozi watu kutoka mikononi mwa wakoloni weusi sisiem. Maana ni hakika na yakini kwamba hakimhitaji yena Zitto Kabwe.
.

Nadhan kwa haya maandishi yako tukiyalinganisha na haya hapa chini kweli Mkumbo ni real Dr.

Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA


Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!



Source:
Raia Mwema
 
Ni lini Kitila alijuwa kuwa 'tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA'? Ni baada ya kutimuliwa CHADEMA?

Nisema tu, 'hatuhitaji' mbadala wa CCM au CHADEMA, au TLP au ADC. Tunachohitaji ni wanasiasa wasio cheza na akili za watu (msisitizo). Kama mwanasiasa yuko CCM na abakie huko, kama yuko CHADEMA hivyo hivyo abakie huko CHADEMA, na kama yuko TLP na abakie huko. Tabia ya wanasiasa kujidai ni wana-CCM mchana lakini usiku ni CHADEMA (and vice versa) ndio tatizo tulilonalo.

Na kama unaona hukubaliani na jambo lolote ndani ya chama chako basi uwe na ujasiri wa kuongea na uwazi na sio kuendesha vita kwa siri ndani ya chama chako.

Calculating and manupulating politicians hawatakiwi kabisa.
 
Kitila soma hii , hasa pekundu

"You can see that, there is no easy walk to freedom anywhere and many of us will have to pass through the valley of the shadow of death again and again before we reach the mountain tops of our desires. Dangers and difficulties have not deterred us in the past, they will not frighten us now. But we must be prepared for them, like men who mean business and who do not waste energy in vain talk and idle action. The way of preparation for action lies in our rooting out all impurity and indiscipline from our organization and making it the bright and shining instrument that will cleave its way to Africa's freedom."-By Nelson Mandela
 
Sikubaliani na wale wanaosema Dr. Kitila aache siasa. Dr. Kitila amesema wazi vyama vyote vilivyopo vinaendeshwa kwa "... zidume fikra za mwenyekiti wa chama... au za mwalishi wa chama"...So, Kitila move forward tutoke hapo maCCM na maCHADEMA ni hayo hayo! Namani kuundwa chama chenye demokrasia ambacho kitakuwa game changer... hakuna kudanganya raia... facts only hata kama kitapewa nchi after 20years!!!!
 
2013; huyu Mzamivu alifanya tathmini ya matokeo ya chaguzi ndogo za madiwani country wide...kuna maoni dhidi ya CCM na yale dhidi ya CDM kama kuna watu walisoma ile tathmini na sasa waangalie matendo yake na maneno yake. Huenda ni kweli TIS member kwa kuurejea uansharakati wake akiwa UDSM especially Daruso, hawezi akakaa meza moja na watu ambao 2010 todate wanaamini kampuni ya nyasi ilikwiba ushindi wao!! CDM iliwahi kiri huyu Mzamivu kuwa ndie chekecheo la Viti maalum 2010,akapongezwa na kupongezeka leo anakuja sound mpya!!! Kama kweli ni Kachelo basi Huyu tayari yuko compromised, anaendelea kuwa contradictory na kwakweli amefikia at per ya siasa. Huu ni ushindi mkubwa kwa Mwigulu na wale wana Iramba,Kiomboi,Kisisiri ambao kujivika uafisa wa Tiss ni kawaida na hasa wakipiga picha na wakuu hata kama wakuu waliwahitaji kwa tiba basi tayari u Yahaya mwingi street sasa hii tuhuma kuwa ni Tiss na kwa vile ni walewale basi nasononeka sana.

Binafsi maoni ya Mzamivu Lweitama ni mtambuka kwa hawa bijana wenzetu huko CDM na pia kwa Nape and team huku CCM. Vijana tujitambue ili tuheshimike sasa na kuipa fursa jamii itupiganie ktk kulijenga taifa hili. Majungu na fitina ujanani ; uzeeni tutatembea na bunduki na uchawi ili kulinda hulka ovu za ujanani.
 
Halafu katika walaka wake huo kuna kitu nimekigundua,kwanza huyu jamaa anaonekana kutaka kumtetea zito kiaina anaposema yangemalizwa kimya kimya,pili inaonyesha kabisa hawa mabwana walikuwa wanatumika either na ccm au walikuwa na lengo ambalo si zuri kwa chama kwani wangekuwa na nia nzuri na chama wangekuwa wavumilivu na sio kufanya mambo kwa mfumo ambao wanajua kabisa kwa kufanya hyo ni kuonekana wasaliti wakubwa.hata kama hayo mawazo waliyatoa kwa wazungu lkn kwa nchi zetu ni mambo ambayo ni mageni sna kuvumilika.
 
We'mwapamba unatumika vibaya unabwatabwata tu ujuichochote umebaki kumshambulia Mhe Mbowe ongea kwaoja si'kumshambulia mtu Acha upoyoyo.
 
Kitila kashakufa kisiasa sijui atamwambia nani amwelewe huu utunzi wake.
 
- Kaka huwezi kuwaita Viongozi wanapokea rushwa kuwa ni wastaarabu zaidi ya genge la wahuni, nasema tena waliomfukuza Kitila ni genge la wahuni wenzake kama yeye, walipokuwa wanafukuzwa wenzake yeye mbona hakusema haya, haya ameyajua lini toka majuzi tu walipomfukuza? siku zote hakujua haya? Please Kitila amefukuzwa na genge la wahuni wapokea rushwa, wajaza mimba wabunge wa viti maalum ambao anafanana nao sana, Zitto hafananai nao wewe hao kama sio wahuni kwa nini wanakwenda kujisafisha kwenye magazeti ya udaku?

- Wewe nitajie mwanasiasa unayemjua mkubwa duniani uluyewahi kumsikia anaedna kujiosafisha kwenye magazeti ya udaku kama alivyofanya Lissu, aibuu ndio maana ya genge la wahuni kaka!!

Le Mutuz

Tunapoita viongozi wahuni na wazinzi tufunge macho turudi kwa wazazi wetu waliokuwa viongozi tukawafanyie tathmini.!!!!! Ngoja nianze na mzee wangu!!!
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.


Source:
Raia Mwema

Ulichosahau kueleza kwa kujua au kutojua ni kwamba, huyo mtu mliyetaka kumpa uongozi kwa kufanya mapinduzi, yeye mwenyewe hawapendi watanzania. Katumia kodi zao akitudanganya kwamba anafatilia mabillion Uswiz baadae anasema hawezi kutaja majina. Huwa haji kwenye mikutano ya watanzania.

Sasa ndugu yangu Mkumbo, hata kama viongozi wa Chadema wana matatizo kiasi gani (kitu unachotaka tuamini), huyu mlietaka nyie awe kiongozi ndo basi. Hivi hujui hilo? Hii inamaliza kabisa nia yako ya kutubu. Hakuna jinsi unavyoweza kumfanya mtu aelewe kwamba Zitto ana mapenzi na taifa la Tanzania. Hiki ni kisiki kikubwa kaka yangu.

After all, umri wako unaenda sasa. Hivi na kisomo chote unatumia muda wako kuandika haya yote? Jiheshimu kaka yangu. Hii njia haikuwezekana kwa siri na haitawezekana hadharani. Tafuta kitu cha kufanya na hachana na siasa. Zishawashinda.
 
- Kaka huwezi kuwaita Viongozi wanapokea rushwa kuwa ni wastaarabu zaidi ya genge la wahuni, nasema tena waliomfukuza Kitila ni genge la wahuni wenzake kama yeye, walipokuwa wanafukuzwa wenzake yeye mbona hakusema haya, haya ameyajua lini toka majuzi tu walipomfukuza? siku zote hakujua haya? Please Kitila amefukuzwa na genge la wahuni wapokea rushwa, wajaza mimba wabunge wa viti maalum ambao anafanana nao sana, Zitto hafananai nao wewe hao kama sio wahuni kwa nini wanakwenda kujisafisha kwenye magazeti ya udaku?

- Wewe nitajie mwanasiasa unayemjua mkubwa duniani uluyewahi kumsikia anaedna kujiosafisha kwenye magazeti ya udaku kama alivyofanya Lissu, aibuu ndio maana ya genge la wahuni kaka!!

Le Mutuz

Ukimkimbiza kichaa aliyekuchukulia nguo zako wakati unaoga mtoni nawe utaonekana Kichaa zaidi, siwezi kubishana na wewe kwa matusi. Kama ni hoja karibu, vinginevyo kwa heri.
 
mashabiki wa zitto wataipenda vp cdm wakati wao ni magamba? mpaka sasa ameshafukuzwa mbona siwaoni hao mashabiki wake wanacdm zaidi ya wale masallia na misukule ya lumumba buk 7?

Aliwakodisha siku ya mahakama ya pili na ya tatu baada ya kuzomewa. Shabiki wa cdm ampate wapi saliti hili zinzi la wake wa viongozi. Mbona lilizalisha dada wa watu hajamwoa kazi kutembeza mkuki kila K.
 
- Kaka soma historia ya wanasiasa wakareeez unapoanza kuandika maneno kama haya baada ya kufukuzwa maana yake ni kwamba umeshindwa it is over, mwanasiasa Zitto tizama kinavyoeleweka tatizo wote huko Chadema ni bure wote hawafai wote wanapokea rushwa so hawafai, Kitila hawa wahuni waliomfukuza ni wenzake sana alikuwa nao siku zote wanapowafukuza wengine mbona hakuwa kulalamika, sasa leo analia nini?

- tumemwambia mara ngapi hapa Ktila kwamba hicho chama sio chako wewe mtu wa Singida kina wenyewe, sasa anashangaa nini hasa? Please Zitto ni a serious politician kwa sababu siku zote alikuwa anajua kwamba hiki chama hakimuhusu ndio maana mapema sana alikuwa hajihusishi na maamuzi mengi ya kijinga na kihuni ya Chademaa na ndi maana bado amesimama mpaka leo, huyu Kitila ni mmoja tu na kina Lema, sasa wamemtema asilie aachane tu na siasa hana jinsi!!

Le Mutuz

Hebu ngoja tusubiri tuone ila Politics ni dynamic sana! sometime history can be used to predict the future and vise versa is true!

Alaf kwenye siasa hakuna permanent group (kambi)! nadhan Kenya inaweza kuwa case study nzuri hapa na unaweza kuongezea mfano kutoka CCM! ile kambi ya wana mtandao wa 2005 sasa hivi ikoje?!
 
Naweza nisiwe na tatizo sana na waraka ila content za huo waraka.

Waraka una udini, matusi, majivuno na kila aina ya uchafu.

Huwezi kutafuta cheo kwa kuwakashifu na kuwatukana wenzio, this is unacceptable!

Uliaminika nje na ndani ya chama lakini umejiaibisha... go to hell doctor!

Umeongea vema kabisa ni mjinga tu atakaye unga mkono mkakati ule Mungu saidia ulishitukiwa mapema lakini athari yake ni kubwa sana hapo baadaye kwani ukikiacha chama kikiwa na makundi na kisingetawalika.
 
Back
Top Bottom