uko sahihi mkuu.me sio kwamba napingana na wewe au vipi but huwa sipendi sana hii tabia.mbowe katumia pesa ya umma kwenda kustarehe na mtu wake ughaibuni lijitu linakuja linakujibu mbona mwigulu naye kafanye hivyo!!!!so what?kwamba coz mwigulu kafanya(actually ni kosa) ndio ihalalishe kufanya mbowe?(point of correction:natambua kuwa katibu wa bunge ameweka sawa hii issue so sio kwamba namtuhumu mbowe itz just an example).kwa nini cdm wasiwe tofauti?kwa nini wahalalishe maovu yao coz tu wa ccm nao wamefanya?
kwenye hiyo issue yako ya upinzani kuingia madarakani sahau.......majitu ya nchi hii hayatabiriki anytime yanaweza kubadilika.we subiri hapa uone 2015 ccm wanamweka lowassa(huyu huyu ambaye wengine tulitamani afe tu kwenye skendo ya richmond tukamwita majina ya kila aina and trust me kama angesimamishwa kugombea hata udiwani na mimi ningembwaga kwa mbaaali sana) wanampamba kwa nyimbo na ngonjera mijitu yotee inampigia kura.Raia wa nchi hii mkuu wanakera sana yaani hadi inauma kufiria.kiukweli ccm wameshindwa na watanzania tulio wengi tunahaha kuangalia mbadala wake but kwa upande mwingine huko tunakotarajia kupata mbadala nako mambo hayaendi sawa ni mvurugano tupu.i wish kungekuwa na craiteria za kupata viongozi but kule sifa kuu ni nani unamsapoti na kwa wakati gani basi.
mkuu umeelimika kidogo? manake naona unakuwa mzito kweli kuelewa. achana na chemba la mavi, mamvi, slaa, zito sijui nani, hao ni watu kaka, wanapita...ongelea mfumo. nchi ni mifumo (systems) si watu, kwa maana nyingine nchi ni taasisi si kikwete wala mbowe. mifumo ikiwa imara halafu wewe chicco ukaiba utashughulikiwa na mfumo. likewise na moshdar akiiba mfumo utamwadhibu kwa uzito na kwa haki ile ile kama ulivyofanya kwa Chicco, vinginevyo ukitaka kupindisha hutaweza coz systems zitakataa. sasa ninyi ccm hamtaki kujenga mifumo imara, mnataka mifumo ibaki kisaniikisanii tu ili akibaka kapuya tumpigie makofi, lakini akizini slaa tumuulie mbali.
vinginevyo hapo kwenye red huna lolote zaid ya kutumia lugha ya kutugonganisha sisi wanamapinduzi wa cdm na kutufanya tujione, wrongly, kuwa sisi ni dhaifu na tumeparanganyika. ndicho mnachofanya ma-ccm. bahati mbaya kwenu na nzuri kwetu ni kuwa mbinu mnazotumia ni za ki-analog mnooooo.
enway, kitu ambacho sijakielewa na ambacho bado nakitafiti ni kuwa kwa nini magamba, kimakosa sana, mna-underate uwezo wa cdm na hivi mnakuwa mnatumia vitekiniki dhaifu sana kwenye gemu? hivi kwa kiwango cha kina mbowe kweli, tuwe wa kweli, unaweza kutumia vitekniki vya kinyonge kama hivi vya magamba na masalia na ukawaangusha kweli? kweli magamba ndo mnavoaamini? mmefanya analysis zenu vizuri kwel nyie? embu acheni kucheza makida bhana nyie!
hivi, for instance, hii plan ya dakitari Kitila, from designing to implementation, ilikuwa sahihi kweli kutumiwa na mtu msomi wa kiwango cha Kitila? hivi hata kama aliamini kuwa alichokuwa anafanya ni sahihi, je, hakuona kabisa njia nyingine effective zaidi - hata kama iwe ya siri kama hiyo aliyotumia - kuliko hiyo aliyotumia? kwa nini mnakuwa na plans dhaifu sana ukilinganisha na ubora wa mpinzani wenu? ni kwa bahati mbayaaaaa au ni kwa kutokuelewa?! ni uwezo wa kufikiri na kupima umekuwa mdogo mnooooo au ni ulevi wa kukaa madarakani mda mrefu mno bila upinzani wa uhakika kama huu wa cdm? au ndo kuzeeka kwa ccm?
well, sjajua bado.