Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Huwezi kusema swali la msiba halikuulizwa, nukta, kwa mujibu wake. Inasemwa: swali la msiba halikuuliwa, koma, kwa mujibu wake.

Sijui unanielewa?

Ukikoma maana yake unakiri kuwa ulichokisema kabla ya koma huna hakika nacho, hujui, ukitua maana yake umemaliza, ulichokisema umekisema, lakini huwezi kuhitimisha kama mamlaka yako ni "kwa mujibu wake." Hatujui, wewe hujui, kilichoulizwa wala kilichojibiwa.

Kitila ameshutumiwa na Mbeki kwamba katoa taarifa potofu, sasa huwezi kutegemea Kitila huyo huyo aje hapa awe mamlaka hakika ya alichokisema, anaweza akakipaka chokaa alichokisema ili kubakiza smokescreen ya tukio zima. Yeye si mjinga, alikuwa hapa chini muda wote kabla hajachangia, akachekiiiii akaona watu wenyewe wanatapa tapa hakuna aliyekuwepo, waliokuwepo hawajui Kiingereza (amesema hivyo mwenyewe).

Tutakubali nothing short of this balancing evidence or the ultimate incontrovertible proof: Tunataka Mbeki nae aje hapa ajitee au tuna demand video ya tukio!

There is no such this as the ultimate incontrovertible proof. The very act of gathering that ultimate incontrovertible proof interferes with the integrity of that proof.

Hata Thabo Mbeki akija hapa utasema anavutia kwake.Hata ikiletwa video utaweza kuhoji angle iliyochukuliwa, jinsi ilivyokuwa edited, quality ya audio na visuals.

At some point you have to choose what is practical and acceptable.

Ama sivyo unaweza kubisha hata kama Thabo Mbeki ni mtu kweli au hadithi tu.
 
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.
Alishindwa nini basi kulifafanua hivyo alipoulizwa kama ndivyo alivyotaka aeleweke? Kuna udhaifu hapo!
 
At some point you have to choose what is practical and acceptable.
Huwezi kusema swali la msiba halikuulizwa, nukta, kwa mujibu wake. Inasemwa: swali la msiba halikuulizwa, koma, kwa mujibu wake.
 
Ulimi ni kiungo kidogo lakini hatari sana!!
Wala Dr hana kosa kuuliza swali la namna hiyo.
Sema viongozi wetu hawataki kuambiwa au kuulizwa ukweli halisi
 
my self kama kweli ni kauli ya rais aliye staafu inabidi kuuliza hilo swali sioni tatizo kwa dr
 
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.

Spot on mkuu, unajuwa waswahili wengine upenda sana kuigiza mambo wanayo yasikia kutoka media za magharibi - hapa anataka wazungu wamuone naye anawahunga mkono, suala hili kuhusu Mbeki na Ukimwi liliwahi kuzungunzwa sana na kukejeliwa sana na wazungu; nafikili watu hawakumuelewa Mbeki au walifanya maksudi kuonyesha Viongozi wa Africa ni mbumbumbu kuhusu suala la UKIMWI.

Naona mwenzetu kakosa ustaarabu, mila za kiafrica mtu uwezi kuhuliza swali la kumkejeli mwenzako aliye poteza mtoto wake kwa ugonjwa wa ukimwi!!! Sina uhakika kama swali hilo alimuhuliza Mbeki kwa nia nzuri au alikuwa na nia ya kumtega/kumdhalilisha and 4 what reason if I maya ask? - Jibu la Mbeki alinishagazi hata kidogo infact amemstahi sana.
 
Dr. Kitila Mkumbo
Afrika inakabiliwa na matatizo ya demokrasia na tatizo kubwa ni viongozi kutofuata misingi ya demokrasia; yalikuwa ni mategemeo yetu ungeuliza swali lenye kulenga zaidi matatizo ya uongozi yanayosababishwa na mapungufu ya demokrasia, swali ulilouliza hukulifanyia utafiti wa kina na halikuwa mahala pake, changamoto inayozikabili nchi za Afrika ni demokrasia, wewe ni msomi halafu ni mwanasiasa usikatae kukosolewa hiyo ilikuwa ni bahati pekee ya kumuuliza swali Mbeki ili kupata msimamo wake kwenye hali ya kisiasa barani Afrika haya mambo AIDS waachie kina kigwangalah, AIDS sio tishio kama ilivyokuwa wote tunajua nini cha kufanya, je hivi ingekuwa Raisi Zuma ungemuuliza nini? Kwasababu yeye alimbaka mwanamke mwenye HIV huku akiamini akioga hatapata maambukizo; nina uhakika swali angeuliza mwanafunzi wako ungemfelisha mtihani.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Who is MBEKI?Mnadhani kule Bondeni kuna mtu mwenye akili nzuri anayemsikiliza?Kule anatuhumiwa yeye na wa kusoma wenzie kuwauza Waafrika wholesale!Kule hana jina kubwa,ni kama Mchee Nkapa alivyokuwa na uwezo wa kupatanisha Kenya lakini Zanjibara akatumia risasi za moto:NABII HAKUBALIKI KWAO!Hapa kafurahi sana kama mlijaa Nkrumah!Wa Tanzania kwa kujazana tu mahali mmejaliwa!
 
Huwezi kusema swali la msiba halikuulizwa, nukta, kwa mujibu wake. Inasemwa: swali la msiba halikuulizwa, koma, kwa mujibu wake.

Sikusema, nimeandika.

If you really want to split atoms like CERN.
 
Spot on mkuu, unajuwa waswahili wengine upenda sana kuigiza mambo wanayo yasikia kutoka media za magharibi - hapa anataka wazungu wamuone naye anawahunga mkono, suala hili kuhusu Mbeki na Ukimwi liliwahi kuzungunzwa sana na kukejeliwa sana na wazungu; nafikili watu hawakumuelewa Mbeki au walifanya maksudi kuonyesha Viongozi wa Africa ni mbumbumbu kuhusu suala la UKIMWI.

Naona mwenzetu kakosa ustaarabu, mila za kiafrica mtu uwezi kuhuliza swali la kumkejeli mwenzako aliye poteza mtoto wake kwa ugonjwa wa ukimwi!!! Sina uhakika kama swali hilo alimuhuliza Mbeki kwa nia nzuri au alikuwa na nia ya kumtega/kumdhalilisha and 4 what reason if I maya ask? - Jibu la Mbeki alinishagazi hata kidogo infact amemstahi sana.

Hili ni tatizo kubwa kwa baadhi ya watanzania wengi kwenye mikutano, hasa ya kimataifa. Huwa hawaulizi maswali kwa kuogopa kuonekana kiherere. Tuna shida pia ya umakini-ni wapi katika swali langu nilipuuliza habari za mtoto wa Mbeki au ndio unafuata tu upepo mheshimiwa? Soma vizuri mada kabla hujajibu, ni muhimu!
 
Gongolamboto, unaleta siasa. Nipo kwenye field hii kwa muda mrefu sasa. Mbeki thesis yake imekuwa kwamba hakuna uhusuano kati ya hiv na aids na kwa hivyo akadai kwamba arvs ni sumu, ndio maana akaweka kizingiti hizi dawa zisiingie nchini mwake. Haya mambo yapo wazi hata kwa google tu. Soma acha uvivu!

Wape elimu kaka hao wavivu wa kusoma.
 
Mbeki alisema kuwa upungufu wa kinga mwilini hautokani na ukimwi bali umaskini... lishe duni....utapiamlo.... akatolea mfano wa watoto wa sudan, somalia na ethiopia kuwa wanaoneka ni dhaifu wenye kinga hafifu.... lakini hawana ukimwi..

Nakumbuka wanasayansi wakatoka nje ya ukumbi wa mkutano... wakisema mbeki anaongea vitu vizito vya kisayansi wakati hajawahi kanyaga hata siku moja maabara.....

Nakumbuka ilikuwa afrika kusini mwaka 1999 au 2000.

Kuhusu kuuliza swali.... muuliza swali hakutumia busara.... kufiwa na mtoto ni kitu cha kuhuzunisha sana... siyokitu cha kukichukulia kiwepesi...... mimi napenda nimshauri Kitila kuwa apime maswali ya kuuliza.... lile swali halikuwa lenye kufariji hata chembe.... bali lenye kuumiza.....

Namsihi kitila akamuombe msamaha mzee wetu mbeki ........
 
inakuwa inaudhi mtu anataka kuleta upotoshaji tena kwa kurejea kwa msiba wa mtu wako wa karibu huku ukiwa na uhakika kwamba alikuelewa ulichosema.

Hahahaha, mkuki mtamu kwa Nguruwe eeeh
 
Dr. Kitila Mkumbo
Afrika inakabiliwa na matatizo ya demokrasia na tatizo kubwa ni viongozi kutofuata misingi ya demokrasia; yalikuwa ni mategemeo yetu ungeuliza swali lenye kulenga zaidi matatizo ya uongozi yanayosababishwa na mapungufu ya demokrasia, swali ulilouliza hukulifanyia utafiti wa kina na halikuwa mahala pake, changamoto inayozikabili nchi za Afrika ni demokrasia, wewe ni msomi halafu ni mwanasiasa usikatae kukosolewa hiyo ilikuwa ni bahati pekee ya kumuuliza swali Mbeki ili kupata msimamo wake kwenye hali ya kisiasa barani Afrika haya mambo AIDS waachie kina kigwangalah, AIDS sio tishio kama ilivyokuwa wote tunajua nini cha kufanya, je hivi ingekuwa Raisi Zuma ungemuuliza nini? Kwasababu yeye alimbaka mwanamke mwenye HIV huku akiamini akioga hatapata maambukizo; nina uhakika swali angeuliza mwanafunzi wako ungemfelisha mtihani.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

AIDS ni tishio kubwa, tena kubwa sana. Kuna utafiti umefanywa hivi karibuni hapa Tanzania, mpaka Serikali inafikiria mara tatu, kuuweka huo utafiti wazi, ili watu waelewe. Sasa hivi asilimia ya maambukizi ya Ukimwi Tanzania yanakaribia kufikia "two digits number"

Na ukumbuke, juzi juzi tu, wakati muheshimiwa anakwenda kugeresha kupima pale mnazi mmoja, maambukizi yalikuwa ni asilimia tano tu.

Hali ni mbaya..na hilo swali la Kitila, ni mahali pake. Wanasiasa hawawezi kuachiwa jambo hilo peke yao...kwakuwa kwanza sio watafiti, na mara nyingi hujadili mambo kwa kuangalia upepo!

Juzijuzi, askofu wa Anglikana, Dr. Mokiwa alizitaka taasisi za kimataifa..kushughulikia kupatikana kwa dawa ya kutibu ukimwi haraka. Unadhani ni coincidence kwa yeye kutoa matamshi yale? Au aliongelea kwa bahati mbaya? Kwa kifupi hali ni mbaya!!!
 
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.

Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.

Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila

Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla
Wakuu salaam.nafikiri Mbeki alikuwa sahihi kwa matamshi aliyoyatoa kuhusu suala la ukimwi.kwamba ni kwasababu ya umaskini wetu.nadhani kuna tofauti kati ya njia inayoeneza ukimwi na sababu ya kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi.Ofcourse ni wazi kwamba ukimwi unaenezwa kwa njia ya ngono ila ila sababu kubwa zaidi ya kukua kwa uenezaji wa ukimwi ni umaskini.waenezaji wakubwa wa ugonjwa wa ukimwi ni makahaba ambao wanafanya biashara ya kujiuza ili wapate fedha ya kuishi.tunakumbuka jinsi yule bosi wa B.O.T alivyokuwa anahonga magari na pesa za kimarekani ili kupata wanawake.na alikuwa akiwahonga dola miambili kwa masharti ya kulala nao pasipo kutumia condom.kutokana na umaskini wetu wengi waliingia mtegoni kwasababu walihitaji zile pesa.hivyo ni kweli kwamba umaskini ni sababu kubwa ya kukua kwa gonjwa la ukimwi.Ngono ni njia tu ya uenezaji wa ukimwi.na kwenye kutafuta solution ya tatizo hili sio kujadili njia ya uenezaji bali ni kujadili sababu ya uenezaji.mbona nchi zilizoendelea nao wanafanya ngono ila hawafi kama tunavyokufa africa?Mbeki alikuwa na makusudi yake alipotamka hivyo na si kwamba he is not aware kwamba ngono inaeneza ukimwi.aliongelea sababu na sio njia ya kueza ukimwi.be blessed!
 
Hizi habari za msiba hazikuulizwa, soma Dr. Mkumbo kaweka swali zima lilivyoulizwa. Kwa mujibu wake.

Mkuu,sasa kwa kuwa mods wameshindwa kuweka swali sahihi kama lilivyoulizwa na Dr Kitila basi mimi nimejipa kazi ya kuwaelekeza wavivu wa kusoma uzi wote kwa kuandika "Mleta mada ameposha swali la Kitila,hebu tafuta swali sahihi kama lilivyoulizwa na Kitila kwani liko katika uzi huu huu"
 
Wape elimu kaka hao wavivu wa kusoma.
Dr. Kitila
Kuwa kwenye field muda mrefu haimaanishi unajua kila kitu pale kilichokuwa kinaongelewa ni siasa mimi sijawa mvivu wa kusoma naimeisoma sana hiyo na naielewa ni kwanini wanasayansi walipingana kimawazo,kama ulilisoma ulisoma research study moja tu ukaitumia kama reference, Dr. Usiwe muoga wa kukosolewa swali ulilouliza halikupaswa kuwa swali la msingi.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
AIDS ni tishio kubwa, tena kubwa sana. Kuna utafiti umefanywa hivi karibuni hapa Tanzania, mpaka Serikali inafikiria mara tatu, kuuweka huo utafiti wazi, ili watu waelewe. Sasa hivi asilimia ya maambukizi ya Ukimwi Tanzania yanakaribia kufikia "two digits number"

Na ukumbuke, juzi juzi tu, wakati muheshimiwa anakwenda kugeresha kupima pale mnazi mmoja, maambukizi yalikuwa ni asilimia tano tu.

Hali ni mbaya..na hilo swali la Kitila, ni mahali pake. Wanasiasa hawawezi kuachiwa jambo hilo peke yao...kwakuwa kwanza sio watafiti, na mara nyingi hujadili mambo kwa kuangalia upepo!

Juzijuzi, askofu wa Anglikana, Dr. Mokiwa alizitaka taasisi za kimataifa..kushughulikia kupatikana kwa dawa ya kutibu ukimwi haraka. Unadhani ni coincidence kwa yeye kutoa matamshi yale? Au aliongelea kwa bahati mbaya? Kwa kifupi hali ni mbaya!!!

Mkuu unaishi dunia gani? Sababu kubwa ya maambukizo ya HIV ni ngono na matumizi ya kujidunga sindano kwa wanaotumia madawa; rekebisha mienendo na tabia yako utakuwa salama 99.9%; tafiti nyingi zimeonyesha sehemu mbalimbali maambukizi ya VVU yamepungua baada ya watu kuelemika; sasa kama wewe hujaamua kubadilika tabia tishio litaendelea kuwepo. Hivi sasa ukimwi si tishio kama unavyodai elimu nyingi zimetolewa na zinaendelea kutolewa kama hujao tafuta mchumba pima afya zenu oaneni mambo ya kuokota mizoga acha remember that AIDS can be avoided don't put yourself at risk for 5minutes pleasure, it's a self inflicted problem !

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Dr. Kitila
Kuwa kwenye field muda mrefu haimaanishi unajua kila kitu pale kilichokuwa kinaongelewa ni siasa mimi sijawa mvivu wa kusoma naimeisoma sana hiyo na naielewa ni kwanini wanasayansi walipingana kimawazo,kama ulilisoma ulisoma research study moja tu ukaitumia kama reference, Dr. Usiwe muoga wa kukosolewa swali ulilouliza halikupaswa kuwa swali la msingi.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mie nimekulia kwenye debates, napenda sana criticism. Lakini unapokosoa uwe na msingi wa kukosoa na vizuri ukawa mkweli na sio kuzusha. Sasa unaposema halikuwa swali la msingi unamaanisha nini? Je, wewe unajua kulikuwa na mwongozo wa maswali fulani na mengine hapana? Seriously unaweza kuthubutu kusema kwamba ukimwi katika afrika hii sio jambo la msingi? Je, unajua huko kwao Mbeki anajulikana kwamba ndiye adui mkubwa wa mapambano dhidi ya ukimwi, ambalo ndio tatizo namba moja afrika kusini?
 
Debate ni moja ya maeneo yangu uwanja unaweza kuwa mdogo sana hapa tunaongelea nini ulipaswa kuuliza na sio kuuliza for the sake of kuuliza, yalikuwapo maswali ya msingi na muhimu yahusuyo Afrika nitakubaliana na wewe tu kama lengo kuu la swali lilikuwa ni personal attacks dhidi ya Thabo Mbeki au kama lingetumika kama swala la nyongeza, unaongelea kuhusu kuwepo mwongozo wa kuuliza maswali sidhani hilo kama ndilo lilokufanya uulize ulichouliza; adui mkubwa wa mapambano dhidi ya ukimwi ni tabia binafsi mtu hiyo ndiyo kinga namba moja; hebu nieleze uzushi wangu upo wapi ili niurekebishe.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom