Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,989
Points
2,000
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,989 2,000
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.

Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.

Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila

Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla

Post Update - Kitila's question:
Katika swali langu sikuzumzungumzia chochote kufariki kwa mtoto wa Mbeki kwa sababu wala sijui hilo jambo. Swali langu lililenga kupata ufafanuzi juu ya madai ya Thabo Mbeki alipokuwa Rais kwamba UKIMWI hausababishwi na virusi vya UKIMWI bali unasababishwa na kuharibiwa kwa mfumo wa kinga mwili kwa sababu ya umaskini na lishe duni. Msimamo wake ulisababisha Afrika Kusini kukataa kupokea msaada wa ARVs na maelfu ya watu kufa bila sababu.

Kwa Kiingereza swali lilikuwa framed kama ifuatavyo:

In the 1990s, supported by scientists described as minority, dissident and maverick, you boldly and courageously claimed that AIDS is not caused by HIV, but by a collapse of the immune system due to poverty and poor nutrition. As a result of your stance, your Government refused to receive the ARV assistance from international pharmaceutical industries. Your stance also almost caused a moratorium in HIV prevention efforts not just in south africa, but in the whole continent. Recently, Harvard scientists published a study report showing that about 300,000 died in South Africa because of your policy stance. The findings of this study have been validated by my scientists, including those in South Africa.
i) Reflecting and looking back to your presidency, and given the pace at which South Africa has reduced the HIV infection rates and HIV related deaths, do you still maintain the same position regarding the cause of HIV?
ii) Do you have any regrets over your position?
Ukweli ni kwamba Mzee Mbeki alijibu swali lakini alisema angehitaji muda zaidi kufafanua. Aliendelea kusisitiza msimamo wake kwamba 'AIDS is a syndrome caused by many conditions'. Lakini tofauti na nyuma this time around alitaja, kimakosa, kwamba HIV kama moja ya conditions zinazosababisha AIDS. Kuhusu utafiti niliomtajia wa wana sayansi wa Havard alisema kwamba kuna utafiti mwingine unaopingana na huo, na akaahidi kunitumia ripoti yake.

Kwa hiyo sio sahihi kwamba hakujibu kabisa swali. Alijibu, lakini sio kikamilifu kwa sababu aliyosema ni kutokuwa na muda wa kutosha.

Sasa mimi sielewi kwa nini watu hapa JF wameanza kuwa na tabia za kujadili mambo nusunusu na kiupotoshaji, hasa pale inapotokea kwamba lugha iliyotumika ni Kiingereza. Nililiona pia hili juzi kwenye ushiriki wangu kwenye kipindi cha 'This Week in Perspective'. Watu wanatabia ya kudaka neno moja na kuibuka nalo na kufanya ndio mjadala. Sasa najiuliza tatizo ni udhaifu katika ujenzi wa hoja za kimantiki au hii lugha inayoonekana kutushinda sisi wa TZ?
 
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,488
Points
2,000
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,488 2,000
Huyu jamaa ni muoga maswali kama Sultani Kikwete anavyo ogopa midahalo alikuwa radhi kumfukuza mchapakazi kama Tido kuliko kusikia neno mdahalo
 
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,989
Points
2,000
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,989 2,000
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
Kwanini?
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,917
Points
2,000
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,917 2,000
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,991
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,991 2,000
naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.

sure maundumula
 
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
5,380
Points
1,195
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2012
5,380 1,195
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
Lazima utakuwa na matatizo ya uelewa. Msimamo wake ni hatari sana.
 
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
5,380
Points
1,195
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2012
5,380 1,195
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.
Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,844
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,844 0
Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?

*Kama Mkumbo ameuliza kweli suala kwa namna hiyo, ninaelewa kwa nini Mbeki amekataa kulijibu, kwa sababu limekaa kusuta zaidi ya kutaka ufafanuzi........Ila sidhani kuwa Mkumbo ameuliza suala hilo, hivyo lilivyo
 
JOYCE PAUL

JOYCE PAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2010
Messages
1,006
Points
1,195
JOYCE PAUL

JOYCE PAUL

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2010
1,006 1,195
kitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
 
Manyi

Manyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Messages
3,254
Points
1,195
Manyi

Manyi

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2011
3,254 1,195
Kila mtu ana fikra zake juu ya jambo fulani. Sidhani kama Dr. Kitila alikuwa sahihi sana kuuliza hilo swali. Siyo kila kinachosemwa na mwanadamu basi kitakuwa kama anavyodhani au kufikiri. Hata katika sayansi, kuja assumptions nyingi tgu zinatumika!
 
C

chama

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Messages
8,005
Points
0
C

chama

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2010
8,005 0
Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.
Sababu ya kushamiri ulimwi Botswana ni wafanyakazi wa kwenye migodi hawakupewa elimu ya kutosha na mila na desturi zao zilichangia sana

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Messages
10,218
Points
1,250
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2009
10,218 1,250
Kama kiongozi wa nchi ni lazima mtu kama huyo awe na uwezo wa kutoa maelezo yaliyojitosheleza kuondoa sintofahamu kama iliyomkuta Dk Nkumbo
 
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
3,938
Points
1,195
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
3,938 1,195
Naona mnamjibia swali Mbeki wakati alikuwepo mwenyewe
 
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
4,787
Points
1,500
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
4,787 1,500
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.

Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.

Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila

Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla
Kama Mbeki wakati akitoa statement hiyo hakutoa exceptions, Kitila alikuwa sawa! Kama kiongozi mkuu wa nchi anatakiwa awe makini sana na matamshi yake, siyo kama yale ya watoto wa shule wanapata mimba kwa sababu ya kihelehele chao! Si kweli kwamba watoto wote wanaopata mimba ni kihelehele chao, ndo maana mtoto wa Mbeki akafariki sababu ya ukimwi, Mbeki ana dhiki na umasikini?
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,844
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,844 0
Kama Mbeki wakati akitoa statement hiyo hakutoa exceptions, Kitila alikuwa sawa! Kama kiongozi mkuu wa nchi anatakiwa awe makini sana na matamshi yake, siyo kama yale ya watoto wa shule wanapata mimba kwa sababu ya kihelehele chao! Si kweli kwamba watoto wote wanaopata mimba ni kihelehele chao, ndo maana mtoto wa Mbeki akafariki sababu ya ukimwi, Mbeki ana dhiki na umasikini?
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,045
Points
1,225
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,045 1,225
kitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
waambie hawa jamaa wanakuwa wabishi utafikiri nini sijui
 
M

Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Joined
Nov 3, 2012
Messages
139
Points
0
M

Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Joined Nov 3, 2012
139 0
Mbeki alisema dr kitla alikuwa na wrong information hasa kuhusiana na takwimu alizo zitoa kuwa mtizamo wa mbeki kuhusu ukimwi umesababisha watu wengi kupoteza maisha.Kwa ujumla swali la dakt lilionekana kutowaridhisha wengi na zaidi ya hapo lilihuzunisha wengi na ilionekana watu wapo upande wa mbeki kwa kuonyesha waziwazi kwamba hilo swali ni mwiba kwa mbeki.Licha ya kukataa kulijibu lakn alitoa ufafanuzi nini alikusudia alipotoa kauli hiyo
 
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
4,787
Points
1,500
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
4,787 1,500
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?

"Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki."

Mbeki knows the answer. Issue yangu hapa ni kuwa viongozi wengi wamekuwa wakitoa kauli ambazo impact yake ni mbaya sana.
 
Forum statistics

Threads 1,295,183
Members 498,180
Posts 31,202,427
Top