Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Nadhani umuhimu wa swali hili ulikuwa ni kuhusu umuhimu wa viongozi kuwa makini na matamko yao kwani wakati mwingine yanaleta madhara kwa raia wao kwa kiwango kikubwa sana. Tamko hilo la Mbeki kuhusu ukimwi lilisababisha watu wengi wa Afrika ya kusini kufa kwa ukimwi bila kupata ARV ambazo nchi yao ilikuwa na uweo wa kuzipata.
 
Wakati mwingine chuki na kutokujua hutufanya kushindwa kuhukumu kwa haki;

Mwanzo ilikuwa Kitila ameuliza mtazamo wa Mbeki kuhusu maambukizi na kwamba mtoto wake alikufa kwa sababu ya ugonjwa huo.
Baadhi humu wakashikilia "habari ya mtoto wa Mbeki", kwamba Kitila amekurupuka Mbeki hana mtoto aliyekufa kwa ugonjwa huo.

Ilipoelezwa kwamba Kitila hakumzungumzia mtoto wa Mbeki, mada ikageuzwa ikawa "AIDS sio tishio kwa bara la Afrika na kwamba muulizaji hakupaswa kuuliza swali la aina hiyo!!" kwamba Afrika ina matatizo mengi na msomi huyo hapaswi kuuliza swali la aina hiyo!!

Sasa hivi mwelekeo utakuwa ni wa ukosoaji kwa Kitila kwenye muundo, lugha na ufundi wa kuuliza swali!!

Seriously tumesoma swali la Kitila kwa moyo safi na kulielewa?

The findings of this study have been validated by my scientists, including those in South Africa.
i) Reflecting and looking back to your presidency, and given the pace at which South Africa has reduced the HIV infection rates and HIV related deaths, do you still maintain the same position regarding the cause of HIV?
ii) Do you have any regrets over your position?
 
Authority ni kwenye kasa na kobe sio kwenye Kiswahili cha kuwaelezea kasa na kobe.
Huwezi kuwa mamlaka "isiyokisia" ya kitu ambacho huwezi kukielezea, nyinyi ndio mamlaka za kibongo, mtu anakwambia mimi ni authority ya kasa na kobe lakini sijui jinsi ya kuwaelezea kasa na kobe! Sasa utaalam wako utasaidia vipi jamii kama huwezi kutuelezea unachokijua?

Na alichonacho kobe jee?
Umetuambia kwamba wote wana miguu/mikono/magome na magamba ila tofauti ni katika miundo yao, sasa utatuulizaje sisi tena kama Kobe ana mikono au nini? Hahahaaa.... (Gaijin: "Tofauti nyengine ni kwenye muundo wa magamba (magome?) na miguu (mikono?) yao.") Wewe ndio umetuambia wote wanayo, tena umeogelea nao na kuwapanda kasa na kobe! Ghafla umegeuka eti hujui Kiswahili cha mikono na miguu, khaa! Hujui Kiswahili kwani we wa wapi, Mnyarwanda?

Siku ingine kama hujui kuelezea kitu na unabahatishabahatisha kati ya miguu na magome na mikono na magamba basi usituambie "mimi huwa sikisii"! Tumia maelezo modest yanayoacha nafasi ya makosa ya kibinadamu pamoja na kukisia. Hujui Kiswahili? Ushindwe na ulegee!
 
Ngoja data mpya za Tanzania zitoke hivi karibuni, then nitakukumbusha. Halafu utaniambia, hiyo awareness ya vijarida vya WHO, UNICEF n.k. imekusaidia nini? Please watch this space!!

Mkuu vita dhidi ya ukimwi vinaanzia kwa mtu binafsi elimu ya ukimwi ipo nje nimekwambia acha kuokota mizoga utakuwa salama 99.9% njia kubwa ya maambukizo ya ukimwi ni ngono hilo nalo pia unataka kubisha?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kwa mwendo huu siwezi kushangaa Waafrika miaka 100 baada ya uhuru tukiendelea kulalamikia ukoloni na wazungu.

mbeki mtu rais wa nchi iliyo na resources kama SA kama hakukubaliani na model hiyo mbona haku commandeer the alternative badala ya kulalamika tu HIV pekee haisababishi AIDS?

Au kuwaambia wa SA waende kwa herbalists ndo ilikuwa alternative yenyewe?

Mkuu Kiranga
unakuja na hoja nyepesi sana suala la Mbeki lipo wazi tafiti zipo zilizothibitisha yote dawa za wakati ule zilikuwa ni toxic na upo utafiti ambao hata WHO walikiri idadi ya watu waliokuwa wakitumia dawa walikuwa wanakufa haraka kuliko wasiotumia SA imepiga hatua kwenye tafiti usifikri wao walikuwa wapumbavu; kama wao walikuwa wapumbavu mbona hata hapa USA wamebadili taratibu za matibabu? wanaanza na nutrition kabla hawajaanza kukupa ARVS? Yale yale walioyokuwa wabisha ndiyo wanayoyafanya sasa hivi kwa mantiki hiyo upo ukweli mkubwa; unajidhalilisha sana waafrika si wapumbavu kama unavyotaka kuamini; hata hapa USA waafrika wengi waliadhirika na ukimwi baada ya serikali kwa makusudi kutowaeleimsha kama waliyafanya hapa USA je huko Afrika walifanya managapi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuwa mamlaka "isiyokisia" ya kitu ambacho huwezi kukielezea, nyinyi ndio mamlaka za kibongo, mtu anakwambia mimi ni authority ya kasa na kobe lakini sijui jinsi ya kuwaelezea kasa na kobe!

Una matatizo ya ufahamu au ndio kujitia unjufu bila ya sababu?

Kwanza wapi niliposema sikisii kwenye kuwaelezea kasa na kobe?

Nimesema "Huwa sikisii" nikijibu shutuma kuwa nimekosea kwa kuweka picha ya kobe badala ya kasa. Key words: kuweka picha

Naelewa kuwa Kiswahili ni kigumu ila sikudhani kama mtu anaweza kushindwa kuelewa tofauti ya "sijui kuwaelezea kasa na kobe" na "sijui kipi ni Kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe"



Umetuambia kwamba wote wana miguu/mikono/magome na magamba ila tofauti ni katika miundo yao, sasa utatuulizaje sisi tena kama Kobe ana mikono au nini?

Sijawaambia kitu hicho kamwe na kama nimewaambia zile alama za kuuliza zina kazi gani? Elewa tofauti ya kusema na kuuliza.



Hujui Kiswahili kwani we wa wapi, Mnyarwanda?

Wewe ndo unaonekana hujui Kiswahili sawa sawa mpaka kushindwa kuona mantiki ya mtu kuuliza kama kasa ana miguu, mikono au mapezi.



Siku ingine kama hujui kuelezea kitu na unabahatishabahatisha kati ya miguu na magome na mikono na magamba basi usituambie "mimi huwa sikisii"!

Inasikitisha kuwa mtu mzima na shughuli zake hawezi kusimamia hoja zake mpaka atunge na uongo, ikisha akosoe huo uongo alioutunga ili tu apate cha kukosolea mwengine.....SMH



Tumia maelezo ya staha yanayoacha nafasi ya makosa ya kibinadamu pamoja na kukisia.

Sawa nitajirekebisha
 
Mkuu Companero
Wengi hawakuelewa Thabo Mbeki amesema nini Kitila alikurupuka na kusoma views za mtu mmoja, ukweli dawa zilizoletwa Afrika hazikuwa na ubora WHO ilitaka kulazimisha serikali ya Afrika Kusini inunue dawa ambazo hazijaidhinishwa kwa matumizi na zilikuwa kwenye majaribio Mbeki alichokataa ni kuwafanya raia wake wapewe dawa za majaribio; pia ipo research ilionyesha watumiaji wa ARV`S walikuwa wanakufa haraka kuliko wasiotumia na hiyo ndiyo iliyoleta maswali mengi hata WHO wenyewe walishindwa kuipinga; dawa zilizokuwa zinapelekwa dunia ya tatu hazikuwa kwenye ubora; wengi wanasahau kuwa Afrika ya kusini ipo juu sana kwenye nyanja ya tafiti za kisayansi; Kiranga nimemnakili jibu atakalo kujanolo ni kiingereza kingi cha kutumia dictionary. Jitihada za Mbeki zimesaidia sana hivi angalau tunaletewa dawa zenye ubora kidogo

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama, nina mfano hai wa madawa hayo ambayo hayakuwa na ubora wowote, kuna jamaa yangu wa karibu tulikwenda kumununulia dawa hizo ambazo zilikuwa zinauzwa bei mbaya - laki nane kwa dozi!! Baada ya kuzitumia kwa muda kidogo afya yake ilibadirika ghafla 4 worst, haikuchukuwa muda akafariki dunia!!!

Mwanzo alikuwa anakataa kata kata kutumia dawa hizo, alipendelea kutumia dawa za kienyeji alipo kuwa Mwanza, kuja Dar tukamlazimisha atumie dawa hizo za kizungu, baada ya kushuhudia hali yake ya afya inabadirika kwa kasi ya ajabu tulijilahumu sana.

Mzee Mbeki alikuwa jasiri sana kuwasema wazungu bila simile na hii ilisaidia sana katika kuwarudisha kwenye mstari na kuacha kuwachukulia Wafrica 4 a ride, mambo aliyo kuwa anasisitiza ndio yana tekelezwa moja baada ya jingine - lakini waswahili wenzetu wamekalia kumbeza beza tu!

Tusisahau kwamba katika harakati za Mh.Mbeki za kuwapasha watu wa magharibi alikuwa anashirikiana na waziri wake wa afya mwanamke alikuwa na taaluma ya UDAKTARI yaani Dr.Manto Tshabalala-Msimang (mama huyo alisha fariki) but she was equally vocal kama MBEKI; mama huyo aliwahi kuishi Tanzania wakati wa vita vya ukombozi, alifanya kazi pale Muhimbili kama daktari.

Vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinamzulia mambo chungu nzima mama wa watu, walifika hatua ya kusema eti ni mwizi aliwahi kushikwa akimwibia mgonjwa saa ya mkononi huko Botswana!! Hii inadhilisha kwamba kulikuwa na mipango kabambe ya kuwa-discredit Mzee Mbeki na Waziri wake wa Afya wa zamani.
 
Kwanza wapi niliposema sikisii kwenye kuwaelezea kasa na kobe?

Nimesema "Huwa sikisii"
Well, "huwa sikisii" is universally inclusive, inamaanisha wewe hukisii period! Ndio matatizo ya kutumia lugha za jumla jumla kama hizo. Ni wapi uliposema kutokukisia kwako ni katika kubandika picha tu? (Gaijin: "Huwa sikisii. I have swum with kasa and rode a kobe")... Umesema huwa sikisii, nukta! Kwa hiyo usiruke makosa ya matumizi yako mwenyewe ya maneno. Au mwenzetu huwa hukosei?

Sijawaambia kitu hicho kamwe na kama nimewaambia zile alama za kuuliza zina kazi gani? Elewa tofauti ya kusema na kuuliza.
Alama za kuuliza kazi yake ni kutuonyesha kwamba hujui kama ni mikono au miguu, au magamba au magome lakini wote wanayo, tofauti ni muundo wa hivyo viungo vyao. (Gaijin: "Tofauti nyengine ni kwenye muundo wa magamba (magome?) na miguu (mikono?) yao.") Notice hilo neno "yao." Ina maana unatuambia wote wanavyo viungo hivyo. lakini kama ulikuwa hujui bali unauliza swali tu, kwa nini ulianza na "Tofauti nyengine ni..." Kwa hiyo ulitaka kutufundisha kwamba wanayo tofauti nyingine lakini wewe mwenyewe ndio unatuuliza sisi swali tofauti yao ni nini? Haileti maana! hahahahaaaaa...

Wewe ndo unaonekana hujui Kiswahili sawa sawa mpaka kushindwa kuona mantiki ya mtu kuuliza kama kasa ana miguu, mikono au mapezi.
Si umekiri mwenyewe kwamba hujui kiswahili fasaha cha kuelezea miundo ya kobe na kasa, sasa unanishambulia mimi kwamba sijui Kiswahili tena? Umepoteza mamlaka ya kukosoa kiswahili cha wengine kama umeshakiri hujui Kiswahili cha kuelezea viungo vya kasa na kobe ilhali unasema umeogelea nao na kuwapanda. Halafu hata kama sijui kiswahili mimi sifungwi na matamshi kama ya "huwa sikisii" ambayo hayaachi nafasi ya kukosea kama mtu yeyote. Wewe ndio umejikuza kupita uwezo wako halisi wa kuelezea kasa na kobe!

tofauti ya "sijui kuwaelezea kasa na kobe" na "sijui kipi ni Kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe"
that's trivial semantics, maana ni ile ile! Hujui kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe lakini unaweza kuwaelezea kasa na kobe, kwa hiyo unaweza kuwaelezea kwa lugha gani muafaka, Kilingala? Haya waeleze Kilingala au lugha yeyote ile, au la kama hujui lugha muafaka yeyote ambayo unaweza kuwaelezea basi maana yake hujui kuwaelezea, nukta.

Inasikitisha kuwa mtu mzima na shughuli zake hawezi kusimamia hoja zake mpaka atunge na uongo, ikisha akosoe huo uongo alioutunga ili tu apate cha kukosolea mwengine.....SMH
Hapana, mie sitakuita muongo kamwe, sidhani kama ulikusudia kupotosha, bali ni saratani yetu kama jamii, ya kutokuwa makini na Kiswahili chetu, huwezi kutumia lugha za jumla jumla za "huwa sikisii" halafu sekunde mbili baadae unaanza kubahatishabahatisha na kukisia viungo vya wanyama ambao umejinadi umeogelea nao na umewapanda. Ukishajinadi hukisii na umeogelea nao na umewapanda huwezi kuja tena kutuuliza sisi kama wana miguu ama wana mikono ama wana magome!

Sawa nitajirekebisha
Hahahaaaaa.... such disciplined modesty is more Gaijin-esque than the vainglorious "huwa sikisii"! Reminded me of a most respected general of his generation succumbing to hunky punky indiscipline. In any event, it was penultimate fun picking the brains of one of the most illustrious person of letters on the board.

Alamsik.
 
Who is MBEKI?Mnadhani kule Bondeni kuna mtu mwenye akili nzuri anayemsikiliza?Kule anatuhumiwa yeye na wa kusoma wenzie kuwauza Waafrika wholesale!Kule hana jina kubwa,ni kama Mchee Nkapa alivyokuwa na uwezo wa kupatanisha Kenya lakini Zanjibara akatumia risasi za moto:NABII HAKUBALIKI KWAO!Hapa kafurahi sana kama mlijaa Nkrumah!Wa Tanzania kwa kujazana tu mahali mmejaliwa!

Well said mkuu
 
si jambo zuri kumuuliza mtu mambo binafsi hasa yanayo husu misiba iliyompata kwenye mkutano wa hadhara halafu wa kisomi.

Just for An interpretation that removes obstacles to understanding
 
Mkuu Chama, nina mfano hai wa madawa hayo ambayo hayakuwa na ubora wowote, kuna jamaa yangu wa karibu tulikwenda kumununulia dawa hizo ambazo zilikuwa zinauzwa bei mbaya - laki nane kwa dozi!! Baada ya kuzitumia kwa muda kidogo afya yake ilibadirika ghafla 4 worst, haikuchukuwa muda akafariki dunia!!!

Mwanzo alikuwa anakataa kata kata kutumia dawa hizo, alipendelea kutumia dawa za kienyeji alipo kuwa Mwanza, kuja Dar tukamlazimisha atumie dawa hizo za kizungu, baada ya kushuhudia hali yake ya afya inabadirika kwa kasi ya ajabu tulijilahumu sana.

Mzee Mbeki alikuwa jasiri sana kuwasema wazungu bila simile na hii ilisaidia sana katika kuwarudisha kwenye mstari na kuacha kuwachukulia Wafrica 4 a ride, mambo aliyo kuwa anasisitiza ndio yana tekelezwa moja baada ya jingine - lakini waswahili wenzetu wamekalia kumbeza beza tu!

Tusisahau kwamba katika harakati za Mh.Mbeki za kuwapasha watu wa magharibi alikuwa anashirikiana na waziri wake wa afya mwanamke alikuwa na taaluma ya UDAKTARI yaani Dr.Manto Tshabalala-Msimang (mama huyo alisha fariki) but she was equally vocal kama MBEKI; mama huyo aliwahi kuishi Tanzania wakati wa vita vya ukombozi, alifanya kazi pale Muhimbili kama daktari.

Vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinamzulia mambo chungu nzima mama wa watu, walifika hatua ya kusema eti ni mwizi aliwahi kushikwa akimwibia mgonjwa saa ya mkononi huko Botswana!! Hii inadhilisha kwamba kulikuwa na mipango kabambe ya kuwa-discredit Mzee Mbeki na Waziri wake wa Afya wa zamani.

Bukyanagandi; Tatizo letu tumebweteka sana katika nyanja zote ndio maana kunafanywa wa majaribio. Serikali yetu haina hata vifaa bora vya kuchuguzia bidhaa zinazoingizwa nchini achilia mbali rushwa iliyopo. Hatuwezi kujitegemea kabisa. Dr. Kitila Mkumbo alitakiwa ajue kabisa kwamba SA kama nchi tajiri imeendela kwa sababu ya tafiti zinazojitegemea kama nchi na serikali inazitumia. Rais kama Mbeki ni moja ya maraisi ambao walikuwa wanafanya kazi kwa kupitia tafiti ndo maana alikuwa na ijasiri wa kusema hivyo.
 
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.

Alipopotoka Mbeki, ni kukataa kuwa AIDS inasababishwa na HIV, na kukataa dawa.
Pamoja na kuwa immunodeficiency ina sababu nyingi km lishe duni, dawa i.e steroids, kansa ya damu (Leukemia), ila HIV ndo leading cause, na makali yake yanapunguzwa na ARV, ambazo Mbeki alizikataa!
 
Haya ni moja ya mahojiano mengi ambayo Raisi Mbeki aliyafanya na hii ndiyo kauli yake na alichouliza Dr.Kitila majibu yake tayari yalikuwapo kama asingefanya uvivu wa kusoma angeuliza maswali yenye mwelekeo na maana zaidi kwa demokrasia ya bara letu


DATE: 15 July 2003
EVENT: Interview with Gavin Esler, Newsnight, BBC
SOURCE: BBC Subtitling Transcript
ESLER: Could I turn to a big problem which affects everybody in the continent and affects the conscience of everybody outside Africa, the problem of AIDS. Do you think with some 600 South Africans a day dying because of the AIDS problem, that your government has been too slow to act?
MBEKI: I don't know where you get the figure from, I don't have it. I don't know where that figure comes from. The South African Government has got, I am certain, the most comprehensive programme on the matter of AIDS and the best-funded. I think the response is very good, very comprehensive.
ESLER: Have you changed your personal views about medical research and the relationship between the HIV virus and AIDS?
MBEKI: I never raised that question. I don't know where that comes from.
ESLER: There were many reports that you doubted the two were related?
MBEKI: They were false, I have never said that. The issue we raised was that in terms of responding to AIDS we've got to have a comprehensive response. Look at the entirety of the health conditions of a person. Because for instance, you can't feed a person who has no food. Feed them with medicines and drugs and so on. You have to take care of things like that.
ESLER: Will antiretroviral therapy become available paid for publicly in South Africa?
MBEKI: It is available now.
ESLER: Your government will pay for it?
MBEKI: It is available now.
ESLER: To anybody who wants it?
MBEKI: There is mother to child transmission, those drugs are given. People who have injuries at work and people who get raped and go to the public health hospitals and so on. The matter of the general availability of antiretroviral drugs is a matter that was raised even by President Bush, do you have the health infrastructure to handle such a programme?
ESLER: Those activists who complain you are going too slowly, are they wrong?
MBEKI: They are very wrong. They started off by saying all you needed was to give drugs and we are saying no it is not. They've changed. Now they are saying you must also take care of nutrition.

Chama
Gongo la Mboto DSM

CC: Kitila; Kiranga, Bukyanagandi, Mundu

Thanks 4 the info mkuu, sina shaka kwa taarifa hii wengi wetu tutafunguka macho na kuanza kumuona Mh. Mbeki in his true colour, kwamba hakuwa na nia mbaya. Watu wanacho sahau ni kwamba vyombo vya habari vya nchi za magharibi ni mahili sana katika nyanja za propaganda, watasema chochote kukidhi malengo/matakwa yao - Tusichukue habari RAW kutoka CNN, FOXNEWS, The Sun nk bila ya kuzi-digest vizuri kwanza.

Nataka nikili kwa mara ya kwanza kwamba upenda sana kusoma post zako na jinsi unavyo wajibu wenzako, nikisema you are gifted na a brilliant analytical mind sidhani kama ntakuwa nimekosea - honestly.

Nimalizie kwa kusema wana JF ni watafiti sana na weledi wa mambo mengi sana ya kusaidia katika ujenzi wa TAIFA letu, kama wangekuwa wanasikilizwa na kuchukuliwa seriously katika uchambuzi wao, mbona Taifa letu lingesonga mbele kwa kasi yakutia moyo - lakini hata hili la magazeti kuwa na courtsey ya kukili kwamba habari nyingine wanazi copy kutoka Jamii Forums siyo ya kupuuzia, we count a lot behind the scene I guess.
 
Ukweli ni kwamba Mzee Mbeki alijibu swali lakini alisema angehitaji muda zaidi kufafanua. Aliendelea kusisitiza msimamo wake kwamba 'AIDS is a syndrome caused by many conditions'. Lakini tofauti na nyuma this time around alitaja, kimakosa, kwamba HIV kama moja ya conditions zinazosababisha AIDS. Kuhusu utafiti niliomtajia wa wana sayansi wa Havard alisema kwamba kuna utafiti mwingine unaopingana na huo, na akaahidi kunitumia ripoti yake.

Kwa hiyo sio sahihi kwamba hakujibu kabisa swali. Alijibu, lakini sio kikamilifu kwa sababu aliyosema ni kutokuwa na muda wa kutosha.

Sasa mimi sielewi kwa nini watu hapa JF wameanza kuwa na tabia za kujadili mambo nusunusu na kiupotoshaji, hasa pale inapotokea kwamba lugha iliyotumika ni Kiingereza. Nililiona pia hili juzi kwenye ushiriki wangu kwenye kipindi cha 'This Week in Perspective'. Watu wanatabia ya kudaka neno moja na kuibuka nalo na kufanya ndio mjadala. Sasa najiuliza tatizo ni udhaifu katika ujenzi wa hoja za kimantiki au hii lugha inayoonekana kutushinda sisi wa TZ?

Dr. umeanza kuongea vyema ila ukaishia weka maelezo nunsu nusu kama Mbeki.hapo kwenye red .Unachokisema kimekuwepo kwa miaka kdhaa nchini , kimefanywa sana na waandishi na watangazaji km akina Juma Nkamia, na huyu ,jamaa yetu wa dkk 45.Ila hakun alaiyewahi warekebisha kwa hilo.Pia wewe ukiwa kama mwalimu sijui kama ktk darasa lako umekuwa ukiwakumbusha watu kuhus hilo.

Hata presidaa wetu anapenda sana longolongo kwa kurefusha maelezo na kuanza describe maneno anayotumia kw akiafi ch akupotosha au amplify vitu vidgo sana.Juzi nimesikia J makamba akiongelea security na auditing na watu walioandaa mkutano kama wanaandaa dinner tuu.Wameongea vitu dhaifu sana kuhusu hiyo security ila wame amplify kama vile wanchofanya ni kitu kikubwa sana ktk ukubwa wa tatizo.Kwa watanzania "what matters is not the size of fight on a dog but the size of dog."

Walikuwa wakiongelea security km vile issue ya migambo na police wetu huku mitaani na wanachokiita mitego.Wanaongelea auditing kama ndio security, hawaongelea kuhusu kukaza nuts and bolts, best practices, hawaongelei technologies na mitigation.Ni yale yale ya TBS kuangalia bidhaa iliyo tayari na kusema inafaa au haifai.Ila hawajui kuwa bidhaa iliyozalishwa nchini inahitaji kuangaliwa ubora tangu materials zikiandalia .Km ni za kilimo tangu ardhi inapoandalia hadi kuvunwa mazao kunachangia sana ubora wa bidhaa, na mara nyingine kunaweza ficha madhara yake haki pale inapotumika.

Dr. michezo ya kuigiza ndiyo imetufikisha hapa, na imechezwa sana pale UDSM, na watu hawajaafundishwa kuwa makini ktk mambo yao.Ndio maana watu wapo very shallow ktk mambo mengi.
 
Bukyanagandi; Tatizo letu tumebweteka sana katika nyanja zote ndio maana kunafanywa wa majaribio.

Nakuhunga mkono kwa 100% mkuu, naona neno "kubweteka" is too soft a word!! Maneno ya kutumia ni: ukosefu wa uzalendo na ukatili. Viongozi walio pewa dhamana ya kusimamia sekta muhimu wanajali pesa zaidi kuliko hatma ya Taifa hili na RAIA wake, cha kutia simanzi zaidi ni kwamba baadhi ya Viongozi hao ni wasomi wazuri katika nyanja zao wanajuwa vizuri madhara ya madawa fake na kugeuza Raia wenzao a guinea pig! wengi wao wamesomeshwa bure na Taifa hili lakini hayo yote wanasahau wanashirikiana na wafanya biashara Mafiosa kuangamiza RAIA wasio na hatia.

Serikali yetu haina hata vifaa bora vya kuchuguzia bidhaa zinazoingizwa nchini achilia mbali rushwa iliyopo. Hatuwezi kujitegemea kabisa.

Well said mkuu hawana vifaa bora, swali ni: Nani kaagiza vifaa fake vya kuchunguza bidhaa zinazo ingizwa nchini TBS ndio taasisi ya kuchunguza kwa umakini Measuring instruments/Systems zinazo ingizwa nchini, waliwahi kuwachukulia hatua gani Wakurugenzi wanao ingiza nchini vifaa vya uchunguzi fake; Kwanza TBS yenyewe ndio wakiukwaji wakubwa wa sekta hii, kumbuka sakata la kusema wana garage nchi za nje za kuchunguza magari kabla hajaingizwa nchini, oh yes walisema wana ma agent wao Dubai, Singapore nk wakawa wanalipwa in terms of $ i.e USD kumbe ni uongo tu watu wanao fanya kazi hiyo ni wakazi wa Kigamboni wenye makampuni kwenye briefcase!!! Mkuu unaweza kuanimi kwamba kuna waziri/Wakurugenzi walio kuwa wanamkingia kufua mtu kama huyo???


Dr. Kitila Mkumbo alitakiwa ajue kabisa kwamba SA kama nchi tajiri imeendela kwa sababu ya tafiti zinazojitegemea kama nchi na serikali inazitumia.

Siwezi ku-comment chochote kuhusu Dr. Mkumbo maanake niliona humu anakanusha kwamba vitu tunavyo andika humu hajawahi kuvisema!! Mkuu SA ni first World katika nyanja za utafiti, viwanda na mabo mengine mengi, Mzee Mbeki alikuwa well informed kila kitu kilicho kuwa kinaendelea katika utafiti wa AIDS ndio maana alikuwa na ujasiri wa kuwa-comfront watu wa magharibi, mimi sikutaka kulisema hilo.

Rais kama Mbeki ni moja ya maraisi ambao walikuwa wanafanya kazi kwa kupitia tafiti ndo maana alikuwa na ijasiri wa kusema hivyo

Ni kweli mkuu read my last but one comment kuhusu Mzee mbeki - Nakushukuru SANA kwa uchambuzi wako.
 
Mkuu Nguruvi3
Napingana na kauli yako; hakuna mwenye kumfanyia personal attack Dr. Kitila hapa kinachojadiliwa je ilikuwa sahihi au sio sahihi kwa yeye kuuliza swali lile; nimepingana Dr. Kitila kwasababu ambazo zipo wazi na nazisimamia; mpaka sasa hivi si Dr. Kitila au wale wenye kumuunga hawajaweza kutoa kauli zenye ushawishi kuunga mkono hoja zao. Naamini wewe upo kwenye taaluma ya afya labda nikuulize kabla hujakuja jamvini kumtetea Dr. Kitila na kumtuhumu Raisi Mbeki umefanya kajiutafiti gani; hii habari si kuichulia juujuu. Mkuu Nguruvi3 naamini umepitia mahojiano na ya Mbeki na BBC; wengi mmejaribu kutia maneno ya sumu kwenye kinywa cha Mbeki; naamini nafsi zenu zinawasuta sana; ni aibu kubwa kuona waafrika tunavyokuwa na mawazo duni na wavivu wa kufikiria; Raisi gani angependa kuwaona raia wake wanakufa kama kuku? Mbeki angepata faraja gani hilo? Wanasayansi wa Afrika walichopigania wakati ule ndio kinachofanyika hivi sasa; je kama wao walikuwa si sahihi wakati ule kwanini iwe sahihi hivi sasa? Je ni nani alikuwa mkweli katika hili? Mkuu Nguruvi3 hapa USA kabla hujaanza kupatiwa matibabu VVU wanaangalia mambo mengi; kwanza wanafanya tathmini ya mgonjwa wanafanya blood work kuangalia kama una infections; Labs Liver function test (LT`s); Complete metabolic panel (CMP) hapo ni kuangalia je figo na ini zitakuwa na uwezo wa kuchuja na kutoa toxic ndani ya mwili; proteins, vitamins yote ni katika kuangalia mwili wa mgonjwa; kutegemea na lab results hapo ndipo wanapokupangia ule nini; haya yalionekana si sahihi wakati Mbeki anahoji lakini mkuu haya ndiyo yanayofanyika sasa hivi; mkuu labda umesahau kitu kimoja VVU havina uwezo wa kuua; kwa hapa wakiona kuna tatizo kwenye hizo major organs wanachofanya ni kukuweka kwenye reverse isolation huku waliendelea kutafuta dawa itakayokusaidia; mkuu walichotaka watu wakati ule ni kuuza dawa na haikuwa vinginevyo; walishikiniza Mbeki ananunue AZT hata kabla ya kuidhinishwa matumizi yake; mkuu najaribu kuileza hali halis kwa ufupi ili kila mtu apime mwenyewe; mkuu waafrika ni watu wenye akili na tuna uwezo kuchambua mambo si kila asemalo mzungu ni sahihi; wazungu siku zote ni ambao hawataki kuzidiwa hapa USA wapo waafrika hawajui kama ni mwafrika ndiye aliyechora ramani ya Washington DC; ni mwafrika ndiye aliyegundua namna ya kuweka trafic lights kuongoza magari; nenda kasome historia ya mti anaitwa Vivien Thomas itakuonyesha kumbe waafrika akili tunazo nyingi na wazungu wakiona mtu ni tishio kwao watatafuta kila njia kumpaka matope; swali alilouliza Dr. Kitila ni jepesi sana kwa mtu wa kaliba yake.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Nguruvi3
Napingana na kauli yako; hakuna mwenye kumfanyia personal attack Dr. Kitila hapa kinachojadiliwa je ilikuwa sahihi au sio sahihi kwa yeye kuuliza swali lile; nimepingana Dr. Kitila kwasababu ambazo zipo wazi na nazisimamia; mpaka sasa hivi si Dr. Kitila au wale wenye kumuunga hawajaweza kutoa kauli zenye ushawishi kuunga mkono hoja zao. Naamini wewe upo kwenye taaluma ya afya labda nikuulize kabla hujakuja jamvini kumtetea Dr. Kitila na kumtuhumu Raisi Mbeki umefanya kajiutafiti gani; hii habari si kuichulia juujuu. Mkuu Nguruvi3 naamini umepitia mahojiano na ya Mbeki na BBC; wengi mmejaribu kutia maneno ya sumu kwenye kinywa cha Mbeki; naamini nafsi zenu zinawasuta sana; ni aibu kubwa kuona waafrika tunavyokuwa na mawazo duni na wavivu wa kufikiria; Raisi gani angependa kuwaona raia wake wanakufa kama kuku? Mbeki angepata faraja gani hilo? Wanasayansi wa Afrika walichopigania wakati ule ndio kinachofanyika hivi sasa; je kama wao walikuwa si sahihi wakati ule kwanini iwe sahihi hivi sasa? Je ni nani alikuwa mkweli katika hili? Mkuu Nguruvi3 hapa USA kabla hujaanza kupatiwa matibabu VVU wanaangalia mambo mengi; kwanza wanafanya tathmini ya mgonjwa wanafanya blood work kuangalia kama una infections; Labs Liver function test (LT`s); Complete metabolic panel (CMP) hapo ni kuangalia je figo na ini zitakuwa na uwezo wa kuchuja na kutoa toxic ndani ya mwili; proteins, vitamins yote ni katika kuangalia mwili wa mgonjwa; kutegemea na lab results hapo ndipo wanapokupangia ule nini; haya yalionekana si sahihi wakati Mbeki anahoji lakini mkuu haya ndiyo yanayofanyika sasa hivi; mkuu labda umesahau kitu kimoja VVU havina uwezo wa kuua; kwa hapa wakiona kuna tatizo kwenye hizo major organs wanachofanya ni kukuweka kwenye reverse isolation; mkuu walichotaka watu wakati ule ni kuuza dawa na haikuwa vinginevyo; walishikiniza Mbeki ananunue AZT hata kabla ya kuidhinishwa matumizi yake; mkuu najaribu kuileza hali halis kwa ufupi ili kila mtu apime mwenyewe; mkuu waafrika ni watu wenye akili na tuna uwezo kuchambua mambo si kila asemalo mzungu ni sahihi; wazungu siku zote ni ambao hawataki kuzidiwa hapa USA wapo waafrika hawajui kama ni mwafrika ndiye aliyechora ramani ya Washington DC; ni mwafrika ndiye aliyegundua namna ya kuweka trafic lights kuongoza magari; nenda kasome historia ya mti anaitwa Vivien Thomas; swali alilouliza Dr. Kitila ni jepesi sana kwa mtu wa kaliba yake.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Tatizo sisi tumejaa ushabiki, jambo akilifanya mtu ambaye unayempenda basi watu wanakuwa na upofu hawawezi hata kuhoji. Mkuu endelea kutoa elimu ya uraia na kuwafahamisha tatizo la HIV/IDS.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chama,
Tatizo sisi tumejaa ushabiki, jambo akilifanya mtu ambaye unayempenda basi watu wanakuwa na upofu hawawezi hata kuhoji. Mkuu endelea kutoa elimu ya uraia na kuwafahamisha tatizo la HIV/IDS.

Mkuu Ritz
Ndiyo sababu tupo JF hapa tunaongea kweli hata kama inauuma; watu wanataka kupindisha hoja kwa mapenzi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.

Kuna tofauti kati ya AIDS and HIV. Nadhani hamjaelewa huyu mtu anauliza nini hasa. Kilichopo hapa ni msimamo wa huyu jamaa uliosababisha ARVs kuachwa kupelekwa South Africa. Kwa ufupi tu ebu angalia hizi definitions;

HIV-It is a virus that attacks the human immune system. Someone infected with the virus can live with HIV or be HIV positive for many years without becoming ill or showing symptoms. During this time however, HIV remains in the body damaging the immune system and the person remains infectious; able to spread the virus to others if a few simple precautions are not followed.

Being HIV-positive, or having HIV disease, is not the same as having AIDS. Many people are HIV-positive but don’t get sick for many years. As HIV disease continues, it slowly wears down the immune system. Viruses, parasites, fungi and bacteria that usually don’t cause any problems can make you very sick if your immune system is damaged. These are called “opportunistic infections.” The illness alters the immune system, making people much more vulnerable to infections and diseases. This susceptibility worsens as the disease progresses.
Over time, HIV can damage the immune system to such a degree that infections may begin to occur as a result of a weakened immune system. Eventually, one may acquire various illnesses due to the damage done by the virus. When this happens this is called AIDS or Acquired Immune Deficiency Syndrome. That is, a collection of illnesses.



Mkumbo anajua vizuri sana Area anayoongelea kwani second Degree yake amesoma HIV/AIDS kwa kiwango kikubwa. Anaelewa anachosema na kuuliza. Ila nadhani tusichukue neno mojamoja na kujenga hoja. Ndio maana muulizwa swali alihitaji reference zaidi ili aweze kujibu. Hivyo nasi tusitoe conclusion tu.Soma swali la Mkumbo between and within lines!
 
Back
Top Bottom