Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Mkuu unaishi dunia gani? Sababu kubwa ya maambukizo ya HIV ni ngono na matumizi ya kujidunga sindano kwa wanaotumia madawa; rekebisha mienendo na tabia yako utakuwa salama 99.9%; tafiti nyingi zimeonyesha sehemu mbalimbali maambukizi ya VVU yamepungua baada ya watu kuelemika; sasa kama wewe hujaamua kubadilika tabia tishio litaendelea kuwepo. Hivi sasa ukimwi si tishio kama unavyodai elimu nyingi zimetolewa na zinaendelea kutolewa kama hujao tafuta mchumba pima afya zenu oaneni mambo ya kuokota mizoga acha remember that AIDS can be avoided don't put yourself at risk for 5minutes pleasure, it's a self inflicted problem !

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Naishi dunia gani wakati nimetoa hint kuwa hali si shwari? Hivi hujafahamu kuwa wanaoeneza HIV ni watu ambao wengi wana uelewa kuhusu maambukizi? na huwapatia wale, ambao ama wana ufahamu mdogo, ama hawana maamuzi sahihi kuhusu masuala ya kingono. Nawe una takwimu zipi kuhusu kupungua kwa maambukizi basi? hata nikikuuliza mkoa upi sasa hivi Bongo unangoza kwa maambukizi huwezi kunitajia.
 
Hili ni tatizo kubwa kwa baadhi ya watanzania wengi kwenye mikutano, hasa ya kimataifa. Huwa hawaulizi maswali kwa kuogopa kuonekana kiherere. Tuna shida pia ya umakini-ni wapi katika swali langu nilipuuliza habari za mtoto wa Mbeki au ndio unafuata tu upepo mheshimiwa? Soma vizuri mada kabla hujajibu, ni muhimu!

Mkuu sikutaka kueleza mambo mengi hapa, labda tuwekane sawa -la kwanza: Watanzania hawana woga wowote kuzungumza/kuhuliza maswali kwenye mikutano ya kimataifa, wenzako wanauliza maswali kidiplomasia without offending anyone, la pili - mimi sina uheshimiwa wowote ‘am a four chamber hearted binadamu mwenye akili timamu za kutafakali mambo si ongozwi na trade winds (monsoon), kuwasema wenzako ambao uwajuhi vizuri kwamba wanafuata upepo kuna-reveal mambo mengi kuhusu hulka yako!!!

Usifikili hatuna uwezo wa kutumia unfortunate remarks kama za kwako, actually wana JF karibu wote wanajiheshimu na kuheshimu wenzao. Wewe ni msomi (if I am not mistaken) nilitegemea ungekuwa tofauti kidogo kwa kutumia lugha ya staha, lakini kama huko wired hivyo ndio maana sishangai Mzee Mbeki kuamua kuku-ignore - nadhani tume elewana.

Back to the point - Mzee Mbeki si mtu mbumbumbu katika masuala mengi, AIDS notwithstanding, kasoma Uingereza katika Chuo Kikuu cha Cambridge au one of the respectable Universities in UK kama sikosei - mimi nilimuona kwenye luninga alipo kuwa anatoa kauli kuhusu AIDS; nchi za magharibi walipotosha sana kauli yake maksudi - walijuwa alichokuwa ana maanisha lakini wakamgeuzia kibao - actually alikuwa anazisema nchi za magharibi kwa mafumbo.

Wazungu wanapenda sana kusingizia Wafrica kuhusu AIDS lakini hawasemi virusi hivyo vili rukaje kutoka equatorial Rain Forest ya Congo na kwenda San Francisco kwenye community ya mashoga na kwenye Magereza ya wafungwa ambao wengi wao ni Blacks na ndio wahanga wakubwa wa ugonjwa huu huko Merikani! Kwa nini ugonjwa huu ilikuwa unawa-target raia ambao walionekana kama kero kwa wenzao, je hii ilikuwa bahati mbaya au..., kwa nini ugonjwa huo alikuja Africa Mashariki na kati kwa kufuata barabara ya kutoka Mombasa - Uganda - Rwanda mpaka DRC kumbuka enzi hizo za mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini kulikuwa na kituo cha wanajeshi wa Majini wa Merikani hapo Mombasa, nani aliwahi kufatilia kwa karibu shughuli zao zilihusu mambo gani ya ziada.

Watu tunacho sahau ni kwamba wana sayansi hasa wa jeshi (Merikani, Urusi, Uchina nk) wana jihusisha na mambo ya (bio-weapon research) wana uwezo wa kutengeneza bacteria na virusi mfano: smallpox, anthrax, influenza, sugarcane mosaic nk; kama wana uwezo wa kuchonga magonjwa kama hayo watashindwaje kutengeneza virusi vya ukimwi - we sema katika majaribio yao kuna kitu which went seriously wrong ndio maana tuna angahika mpaka leo. Mzee Mbeki alipo kuwa anazungumza suala zima la AIDS had all these facts at back of his MIND - please revisit hotuba yake, soma kwa makini alicho kuwa anataka ku-put across.

Naishi dunia gani wakati nimetoa hint kuwa hali si shwari? Hivi hujafahamu kuwa wanaoeneza HIV ni watu ambao wengi wana uelewa kuhusu maambukizi? na huwapatia wale, ambao ama wana ufahamu mdogo, ama hawana maamuzi sahihi kuhusu masuala ya kingono. Nawe una takwimu zipi kuhusu kupungua kwa maambukizi basi? hata nikikuuliza mkoa upi sasa hivi Bongo unangoza kwa maambukizi huwezi kunitajia.
Mkuu huitaji rocket science kumuelewesha mtu juu ya maambukizi ya VVU pitia majarida mbalimbali ya UNICEF na WHO yatakuonyesha progress inayofanyika duniani na Tanzania tishio la ukimwi limepungua sana na sababu kubwa ni elimu ya maambukizi na upatikanaji wa dawa bora; dawa kubwa ya ukimwi ni kubadili tabia hakuna kingine zaidi, angalia studies zilizofanywa kwenye wafanyakazi wa migodini South Africa hiyo itakusaidia kuelewa naongea kitu gani.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.

Kwa taarifa yako Dr Kitila Mkumbo ni mtaalam wa psychology, na hapo Mlimani yeye ni mtaalamu wa kutoa ushauri nasaha kwa wote wenye matatizo ya ukimwi pale chuoni. Hivyo yeye kama mtoa ushauri nasaha alikuwa na haki ya kuuliza swali kama lile kwa muhusika mkuu, kwanza ndie aliyesema ukimwi unatokana na umasikini, (kumbuka alisema hayo yeye akiwa ndio Rais wa South Afrika, hivyo sio masikini yeye na familia yake), pia ni muhusika kwa kuwa mtoto wake wa kumzaa aliambukizwa ukimwi na akafariki. Msingi wa swali hapo ni kutaka kujua je bado ni kweli kuwa ukimwi unawapata masikini tu na sio matajili?? Kama hivyo ndivyo kwanini mtoto wa Mbeki aliambukizwa na akafariki???
 
Haya ni moja ya mahojiano mengi ambayo Raisi Mbeki aliyafanya na hii ndiyo kauli yake na alichouliza Dr.Kitila majibu yake tayari yalikuwapo kama asingefanya uvivu wa kusoma angeuliza maswali yenye mwelekeo na maana zaidi kwa demokrasia ya bara letu

DATE: 15 July 2003
EVENT: Interview with Gavin Esler, Newsnight, BBC
SOURCE: BBC Subtitling Transcript
ESLER: Could I turn to a big problem which affects everybody in the continent and affects the conscience of everybody outside Africa, the problem of AIDS. Do you think with some 600 South Africans a day dying because of the AIDS problem, that your government has been too slow to act?
MBEKI: I don't know where you get the figure from, I don't have it. I don't know where that figure comes from. The South African Government has got, I am certain, the most comprehensive programme on the matter of AIDS and the best-funded. I think the response is very good, very comprehensive.
ESLER: Have you changed your personal views about medical research and the relationship between the HIV virus and AIDS?
MBEKI: I never raised that question. I don't know where that comes from.
ESLER: There were many reports that you doubted the two were related?
MBEKI: They were false, I have never said that. The issue we raised was that in terms of responding to AIDS we've got to have a comprehensive response. Look at the entirety of the health conditions of a person. Because for instance, you can't feed a person who has no food. Feed them with medicines and drugs and so on. You have to take care of things like that.
ESLER: Will antiretroviral therapy become available paid for publicly in South Africa?
MBEKI: It is available now.
ESLER: Your government will pay for it?
MBEKI: It is available now.
ESLER: To anybody who wants it?
MBEKI: There is mother to child transmission, those drugs are given. People who have injuries at work and people who get raped and go to the public health hospitals and so on. The matter of the general availability of antiretroviral drugs is a matter that was raised even by President Bush, do you have the health infrastructure to handle such a programme?
ESLER: Those activists who complain you are going too slowly, are they wrong?
MBEKI: They are very wrong. They started off by saying all you needed was to give drugs and we are saying no it is not. They've changed. Now they are saying you must also take care of nutrition.

Chama
Gongo la Mboto DSM

CC: Kitila; Kiranga, Bukyanagandi, Mundu
 
Last edited by a moderator:
Kwa taarifa yako Dr Kitila Mkumbo ni mtaalam wa psychology, na hapo Mlimani yeye ni mtaalamu wa kutoa ushauri nasaha kwa wote wenye matatizo ya ukimwi pale chuoni. Hivyo yeye kama mtoa ushauri nasaha alikuwa na haki ya kuuliza swali kama lile kwa muhusika mkuu, kwanza ndie aliyesema ukimwi unatokana na umasikini, (kumbuka alisema hayo yeye akiwa ndio Rais wa South Afrika, hivyo sio masikini yeye na familia yake), pia ni muhusika kwa kuwa mtoto wake wa kumzaa aliambukizwa ukimwi na akafariki. Msingi wa swali hapo ni kutaka kujua je bado ni kweli kuwa ukimwi unawapata masikini tu na sio matajili?? Kama hivyo ndivyo kwanini mtoto wa Mbeki aliambukizwa na akafariki???

Hapa hakuna mwenye tatizo la kisaikolojia wote tuna akili timamu na kamilifu; binafsi namuheshimu Kitila kama mwanataaluma; hii hoja hapa haina mshiko; mgonjwa wa ukimwi anakutana na watu 3 wa kwanza daktari wake na pili social worker na watatu dietician hao ndio watakaopanga namna ya matibabu na jinsi mgonjwa atapewa support ya huduma mbalimbali za kijamii na mpangilio wa vyakula; hili la kumuona saikolojisti labda kama matatizo ya akili; vinginevyo huitajiki kumuona saikolojisti.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
MBEKI: They are very wrong. They started off by saying all you needed was to give drugs and we are saying no it is not. They've changed. Now they are saying you must also take care of nutrition.

Chama
Gongo la Mboto DSM

CC: Kitila, Mundu; Bukyanagandi

Naomba umnakili na Kiranga!

Niliwahi kufanya utafiti kuhusu ARV katika viijiji na miji kadhaa, watumiaji hoja na dai lao kuu ilikuwa ni hitaji la lishe na jinsi umaskini unavyosababisha madawa yawazidi nguvu sasa jamaa wa watu aliposema hili suala la VVU sio la kuwapa watu makemikali tu wahafidhina wa sayansi na vibaraka wa makampuni makubwa ya madawa wakamjia juu!

Ni vigumu sana kuwa mpinzani!
 
Mkuu Companero
Wengi hawakuelewa Thabo Mbeki amesema nini Kitila alikurupuka na kusoma views za mtu mmoja, ukweli dawa zilizoletwa Afrika hazikuwa na ubora WHO ilitaka kulazimisha serikali ya Afrika Kusini inunue dawa ambazo hazijaidhinishwa kwa matumizi na zilikuwa kwenye majaribio Mbeki alichokataa ni kuwafanya raia wake wapewe dawa za majaribio; pia ipo research ilionyesha watumiaji wa ARV`S walikuwa wanakufa haraka kuliko wasiotumia na hiyo ndiyo iliyoleta maswali mengi hata WHO wenyewe walishindwa kuipinga; dawa zilizokuwa zinapelekwa dunia ya tatu hazikuwa kwenye ubora; wengi wanasahau kuwa Afrika ya kusini ipo juu sana kwenye nyanja ya tafiti za kisayansi; Kiranga nimemnakili jibu atakalo kujanolo ni kiingereza kingi cha kutumia dictionary. Jitihada za Mbeki zimesaidia sana hivi angalau tunaletewa dawa zenye ubora kidogo

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Naomba umnakili na Kiranga!

Niliwahi kufanya utafiti kuhusu ARV katika viijiji na miji kadhaa, watumiaji hoja na dai lao kuu ilikuwa ni hitaji la lishe na jinsi umaskini unavyosababisha madawa yawazidi nguvu sasa jamaa wa watu aliposema hili suala la VVU sio la kuwapa watu makemikali tu wahafidhina wa sayansi na vibaraka wa makampuni makubwa ya madawa wakamjia juu!

Ni vigumu sana kuwa mpinzani!

Kwa mwendo huu siwezi kushangaa Waafrika miaka 100 baada ya uhuru tukiendelea kulalamikia ukoloni na wazungu.

mbeki mtu rais wa nchi iliyo na resources kama SA kama hakukubaliani na model hiyo mbona haku commandeer the alternative badala ya kulalamika tu HIV pekee haisababishi AIDS?

Au kuwaambia wa SA waende kwa herbalists ndo ilikuwa alternative yenyewe?
 
mbeki mtu rais wa nchi iliyo na resources kama SA kama hakukubaliani na model hiyo mbona haku commandeer the alternative badala ya kulalamika tu HIV pekee haisababishi AIDS?

ali-commandeer mkamfanyia coup de tat kama "miafrika ndivyo tulivyo" mingine ilivyowasaliti mashujaa wetu!
 
"mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'i will not respond to that pinching question' alisema mbeki."

mbeki knows the answer. Issue yangu hapa ni kuwa viongozi wengi wamekuwa wakitoa kauli ambazo impact yake ni mbaya sana.

swali aliloliuliza dr. Kitila lilifunga milango ya fursa ya kupata habari nyingi toka kwa bwana mbeki . Sidhani hili swali lilikuwa ndio lenye umuhimu wa kwanza ktk kuuliza. Hata kama ni la kwanza uzito wake ulipaswa kupimwa ili kuyapa nafasi maswali mengine yasiyomkera muulizwaji maswali. Period.
 
Ndio, kasa ama turtle kwa Kiingereza.

images

*Tanabahi
Kwa Kiswahili cha pwani kulishwa kasa maana yake ni kulishwa taarifa zisizokuwa na uhakika wa ukweli wake kama kulishwa kasa ambae kwa mujibu wa sheria za Kiislam uhalali na uharamu wake una utata

uyu ni kobe sio kasa braza..labda kama ulikuwa umelala wakati wenzio wakifundishwa 'classification'.
 
uyu ni kobe sio kasa braza..labda kama ulikuwa umelala wakati wenzio wakifundishwa 'classification'.

Huwa sikisii. I have swum with kasa and rode a kobe

Kasa anaishi ndani ya bahari lakini huja nchi kavu kutaga mayai. Mayai yake meupe malaini anayafukia mchangani karibu na maji.

Kobe anaishi nchi kavu na si kwenye bahari.

Japo wote wanakuwa classified kama Chelonia ila tofauti kubwa kati yao ni mmoja kuishi baharini na mmoja nchi kavu. Tofauti nyengine ni kwenye muundo wa magamba (magome?) na miguu (mikono?) yao; Kobe ana umbo la mviringo zaidi, kiwiliwili pamoja na miguu yake, wakati kasa yupo bapa umbo na miguu yake ili kumsaidia kuweza kuogelea kwa urahisi zaidi.

Rejelea picha hizi

Kobe (tortoise)

ImageUploadedByTapatalk1353818376.416608.jpg

Kasa (turtle)
ImageUploadedByTapatalk1353818444.629587.jpg
 
Dr Kitila,
Ahsante kwa kuweka swali lako kama lilivyokuwa katika mkuatano.

Mleta mada, kwakweli umeupotosha umma vilivyo. Katika swali hakuna mahali Kitila ametaja mtoto wa mbeki.
Nakubaliana na Nsiande kuwa maelezo ya Dr Kitila yawe samba mba na mada ili kuondoa upotoshaji

Wanajamvi
Swali la Dr Kitila lina mantiki sana. Kwanza mada inaongelea uongozi Afrika. Mbeki alikuwa rais wa taifa kubwa Afrika.
Kauli yake kuhusu Ukimwi ilileta sintofhamu kubwa sana si kwa nchi za Magharibi na dunia bali hata nchini mwake.
Ushahidi wa maandiko kuhusu madhara ya kauli zake upo wazi kwa anayetaka kujifunza au kuelewa zaidi.

Viongozi ni lazima wawe tayari kuzungumzia hata mambo yenye maumivu kwao.
Kiongozi ni public figure na maisha yake yana thin line between public and private life.

Nelson Mandela alisimama na kusema mtoto wake alifariki kwa Ukimwi. Mandela huyo huyo aliwahi kuwaambia vijana wa south Africa kuwa kama wanataka wapewe mapanga walipe kisasi kwa wazungu yeye anaach uongozi.
Pamoja na kujua alikuwa anawakumbusha Vijana machungu lakini alisimama kwa kile alichokiona sahihi kama kiongozi.

Mbeki hana sababu ya kutetewa kwa hisia tu. Alitakiwa ajibu swali ambalo ni fair. Ni fair kwasababu yeye alisema liyoyasema na kuleta sintofahamu duniani. Bila kujali ukweli au uongo wa kauli yake hii ilikuwa ni fursa nzuri ya yeye kujieleza tena na tena na kuweka rekodi sawa.
Sioni wapi swali la Dr Kitila lilimbana au kumuonea zaidi ya kuwa fair.

Wanajamvi wanamtuhumu Dr Kitila kwa kuwa unfair na kufanya personal attack kwa Mbeki. Ninashangaa kuona hao hao wanaotaka ''fairness'' itawale wanafanya personal attack kwa Dr Kitila kwa kumwekea kauli ambazo hakuzisema.

Niliwahi kuhudhuria mkutano unaohusu chanjo ya ugonjwa wa Malaria iliyoonyesha mafanikio sana.
Wasomi waliuliza maswali ya Biochemistry, immunology na jinsi gani nuleus, ATP, Ribose n.k zitakavyofanyakazi na chanjo mpya. Kuna wakati ilikuwa ni rocket science inaongelewa tu.

Mwisho wa mjadala Profesa mmoja maarufu akapewa heshima ya kuuliza swali. Yeye aliuliza ''je bei ya hiyo chanjo ni kiasi gani kwa dozi'' Kila mtu alipigwa na butwaa na kumshangilia sana kwasababu in the end bei ya dawa ndiyo inge determine outcome ya chanjo si electrons, ribose n.k.

Nimetoa mfano huo kwasababu tuna hulka ya kutaka kusikia tunachokitaka si kile tunachopaswa kusikia na kibaya zaidi Watanzania hatuna tabia ya kuangalia vitu kutoka different angle.

Lisomeni swali la Kitila, mada husika na anayepaswa kulijibu utaona mantiki.
Ili kuelewa swali sharti moja kubwa ni kuondoa chuki kwanza na kulisoma swali kama lilivyo.
 
Wait a minute now, who knows? You are the surefooted authority on kasa's and kobe's here!

Authority ni kwenye kasa na kobe sio kwenye Kiswahili cha kuwaelezea kasa na kobe.

Alichonacho kasa ni miguu,mikono au ni mapezi?

Na alichonacho kobe jee?
 
Mkuu huitaji rocket science kumuelewesha mtu juu ya maambukizi ya VVU pitia majarida mbalimbali ya UNICEF na WHO yatakuonyesha progress inayofanyika duniani na Tanzania tishio la ukimwi limepungua sana na sababu kubwa ni elimu ya maambukizi na upatikanaji wa dawa bora; dawa kubwa ya ukimwi ni kubadili tabia hakuna kingine zaidi, angalia studies zilizofanywa kwenye wafanyakazi wa migodini South Africa hiyo itakusaidia kuelewa naongea kitu gani.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Ngoja data mpya za Tanzania zitoke hivi karibuni, then nitakukumbusha. Halafu utaniambia, hiyo awareness ya vijarida vya WHO, UNICEF n.k. imekusaidia nini? Please watch this space!!
 
Dk Kitila na Dk Benson Bana wanashabihiana sana kimatamshi...!
 
Maelezo ya Kitila (Phd) nayo yamepinda... SOMA:::: .." you boldly and courageously claimed that AIDS is not caused by HIV ...::: SOMA SWALI:::..."...do you still maintain the same position regarding the cause of HIV?"....!
 
Back
Top Bottom