DR. Jakaya Kikwete: Mnyonge Mnyongeni!

- Huku bongo yaani Ground Zero, pamoja na mapungufu ya Awamu ya nne, kuna mambo mawili muhimu mazuri sana nimeyaona kama legacy ya Rais, Dr. J. Kikwete, nayo:

1. MVUMILIVU WA DEMOKRASIA na 2. CREATION OF MIDDLE CLASS.:

- kwa haya mawaili ni matumaini yangu kwamba historia itamuhukumu kwa haki.

FMEs: ni WAZEE WA SAUTI YA UMEME & DATAZ!

Maisha bora kwa kila Mtanzania au bora maisha kwa kila mtanzania???!!!!
Kuna Gap kubwa sana kati ya matajiri na masikini.....Middle class ya Tanzania ndio ipi?
 
- Mushi ni kweli middle class haikuwepo sasa ipo, na pia namba za kisayansi sijazipata lakini kwa kuona tu najua kwamba sasa tuna middle class na haikuwepo siku za nyuma!, na infact most of my friends wanatokea humo ndio imekwua rahisi sana kwangu kuelewa hili!

Es!
Kwa nchi za wengine middle class ni waalimu, white collar workers, polisi, na upper middle class ni lawyers na madaktari. etc. Kwetu waalimu bado wanalipwa minimum wage, polisi ndiyo usiseme kabisa. Madaktari wanalipwa chini ya mishahara wanayolipwa wabunge, sasa sijui Bongo middle class ni akina nani?
 
Kwa nchi za wengine middle class ni waalimu, white collar workers, polisi, na upper middle class ni lawyers na madaktari. etc. Kwetu waalimu bado wanalipwa minimum wage, polisi ndiyo usiseme kabisa. Madaktari wanalipwa chini ya mishahara wanayolipwa wabunge, sasa sijui Bongo middle class ni akina nani?

Mishahara ya madaktari wetu inasikitisha!

Yaani hata wabeba maboksi wanawazidi. It's a shame.
 
- Mushi ni kweli middle class haikuwepo sasa ipo, na pia namba za kisayansi sijazipata lakini kwa kuona tu najua kwamba sasa tuna middle class na haikuwepo siku za nyuma!, na infact most of my friends wanatokea humo ndio imekwua rahisi sana kwangu kuelewa hili!

Es!
labda ungedefine middle class mkuu inaonekana hujui unachoongea
 
To me Kikwete is hopeless and spineless head of the state! Hajui kwanini taifa lake ni maskini . Uswahili na uislam umemjaaa

nakupongeza kwa ujasiri mkubwa wa kunena kitu ambacho hata viongoz wako wa kiimani hawana ubavu wa kukitamka hadharani 'uswahili na Uislam wa JK' ndio chanzo cha chuki zenu kwake,wafundishe wenzako wawe majasiri wa kutaja chanzo cha chuki zao kama ulivyoonesha ujasiri hapa,hongera sana!
 
labda ungedefine middle class mkuu inaonekana hujui unachoongea

- Tatizo ni kwamba kama wewe sio haina maana hawapo, ha! ha! ha! ha! maana kwa maneno yako unaonyesha tu kwamba una hasira ya kutokuwa1 ha! ha! ha! I mean vijana wadogo sana kiumri wapo mjini hapa wanatanua tena kwa makazi makubwa sana kwenye mashirika ya umma na binafsi, wapo sana kama huwaoni hapa mjini basi labda upo huko swekeni! ha! na sio kosa langu! ha! ha! naona mjomba umedata sana kila kukicha wewe mahasira utapasuka hapa watu tunaendelea tu kutoa hoja zetu bila kuogopa maneno wala vitisho, pole pole usije pata kohoro! ha! ha! ha! ha!

- Leo Jumamosi kwenye viwanja sasa!

Es!
 
Kwani hao kina middle class ndio kina nani? Wanaishi hapa hapa tz?
Utawatambua middle class kwa matakwa na matamuzi,na hilo si shida,lazima tukubali ukweli wa mabadiliko katika jamii yetu.
Matabaka yamekuwa yakijitokeza nchini kwa Muda sasa.
Watu wanaona mabaya tu ya middle class lakini hawaoni jinsi wanavyojituma kwa udi na uvumba kutafuta pesa.
Hawa watu hawasubiri kuletewa neema na serikali,neema hiyo wanajitafutia.
Ma-Vogue,ma-landcruiser LC200, na hata mahekalu vitongojini, hii yote ni middle class .
Mtu ukilia huna pesa sana sana wanakuhurumia kwani nchi hii ni tajiri sana .
 
JK haja "create" middle class.
Labda museme kuwa jamii yetu ina acknowledge uwepo wa middle class chini ya utawala huu.
Sababu kubwa ni kwasababu chini ya utawala wa ujamaa na kujitegemea, tuli assume a "classless society" Lakini haikuwa na maana kuwa there weren't no classes.
 
Shida yako umekaa marekani sana na ujui yanayoendelea hapa pamoja na kuja kutalii kwako! Sawa endelea kuamini hivyo wewe peke yako! Maana hilo unalojaribu kusema ni middle class imekuwepo katika hawamu zote!! sitaki kusema mengi lakini nadhani umethiliwa sana na kukaa nje ya Tanzania kaka
 
- Huku bongo yaani Ground Zero, pamoja na mapungufu ya Awamu ya nne, kuna mambo mawili muhimu mazuri sana nimeyaona kama legacy ya Rais, Dr. J. Kikwete, nayo:

1. MVUMILIVU WA DEMOKRASIA na 2. CREATION OF MIDDLE CLASS.:

- kwa haya mawaili ni matumaini yangu kwamba historia itamuhukumu kwa haki.

FMEs: ni WAZEE WA SAUTI YA UMEME & DATAZ!

kwenye RED-si kwamba hawezi zuia-maana akizuia mambo yatamgeukia yeye-coz wengine ni folks wake na wanamjua a-z-so inabid aache tu
nilipo bold-hio middle class si kwamba inarise kwa sababu ya pesa watu wanazoibia serikali-ambao wengi hawafanywi kitu
 
Kwa nchi za wengine middle class ni waalimu, white collar workers, polisi, na upper middle class ni lawyers na madaktari. etc. Kwetu waalimu bado wanalipwa minimum wage, polisi ndiyo usiseme kabisa. Madaktari wanalipwa chini ya mishahara wanayolipwa wabunge, sasa sijui Bongo middle class ni akina nani?
Middle class wetu sisi pengine ni wabunge, mawaziri, viongozi wa chama, taasisi za serikali na za binafsi etc.
Na maybe wenye vyeo kwenye makampuni makubwa ya binafsi etc.

Labda creation inayozungumziwa hapa ya hao middle class ni hao wabunge na mishahara yao?
 
Mzazi mwambie hupo dogo amewahi kumsikia mtu anayeitwa Paulo Kagame au Julias Nyeyere,au kama anamkumbuka wanaume Moringe Sokoine hao ndo viongozi sio hili baba Mwanahasha ambaye hajui anacho kifanya kukenua na kuzurura nchi za watu

Hizi ndizo gharama Dr. Jakaya Kikwete anazolipia kwa kuwa MVUMILIVU WA DEMOKRASIA! Watu ambao wana skewed MINDS can call him names under the SUN! Watu wanasahau kwamba katiba ya nchi hii inamruhusu kuwa Dikteita kuliko Stalin-ana uwezo wa kufanya lolote atakalo na hasihulizwe na mtu yeyote au kushitakiwa. Sasa jamani uhuru usizidi mipaka mpaka tukafikia hatua ya kutaka kumdhalilisha, kumkosea adabu - yeye ni Raisi wa nchi hii utake husitake, lugha mnazo tumia humu zinapashwa kuwa na staha, ukisoma kwa umakini sentensi yenye wino mwekundu utagunduwa kwamba aliye andika ni bwana mdogo si mtu mzima, hapa hata malezi yanachangia.

Maraisi unaowasifia jaribu kuwahuliza watu walio wahi kuonja shubiri zao (wengi wao kwa kuonewa tu na majungu) ndiyo utagunduwa kwamba Jakaya ana ubinadamu sana, hukurupukii mambo kwa shinikizo la watu, anapima kwa umakini sana kabla ya kutoa uhamuzi. Kuna siku niliwahi kumuona akisikitika sana kwamba aliwahi kumtimua afisa kazi bila kutambuwa kwamba mambo waliokuwa wanamsema afisa huyo yalikuwa majungu tu na alisema hatarudia kufanya kosa hilo TENA, JK angekuwa kama ma Raisi mnao wasifia wasigekuwa na muda wa kufikilia kitu kama hicho, lakini si Jakaya bwana!

Mwisho nisema kwamba maneno uliyo yasema hapo juu kuhusu JK, kama zigekuwa enzi za Kambarage na Sokoine ungeozea jela, kwa hiyo jamani we don't need to try JK's uvumilivu tukidhani kwamba labda yuko WEAK hiyo si kweli, tumpe ushauri pale inapobidi na kusema kwa lugha ya staha pale tunapo ona kakosea-yeye ni binadamu siyo Malaika Gabriel.
 
Bw, Malecela, niliwahi kuamini kwamba wewe ni mtu muwazi na makini. Kumbe hakuna kitu, hapa umetumia alias na huwezi hata kujificha katika kivuli cha uwongo wako kwani topic hii pia umeiposti kule fb kwenye wall yako. Pia, I think you write too much na hii si nzuri sana kwa aspirations zako katika siasa. Ni mtazamo tuu!!
 
punguza chuki,hata kama humpendi jaribu kuwa na adabu kwa wakubwa zako.Utake usitake huyu ndio rais bora kuwahi kutokea TZ.Propaganda zote mlizopendesha kwenye majumba yenu ya ibada zimefeli watz wamestuka
Dogo middle class hujengi bila umeme,barabara na elimu inayoeleweka ; nenda katembelee shule alizosoma baba Mwanahasha Kibaha na Tanga School hata kupita tu nakusabahi hajawahi zote zimeoza, kijiji chake alichokuwa mbunge miaka kumi na tano watu wanaishi kama walivyo ishi babau zao miaka mia mbili iliyopita .......kuzaa na kuwanga...........nafikiri akifa itabidi ubongo wake uchukuliwe na wataalamu kwani inawzekana wakagundua jambo haiwezekani utawale nchi masikini na wananchi wako wanalia shida wewe unakenua meno masaa ishiri na nne .....................there must be something wrong with baba Ridhiwani brain and never system
 
FMES, Mkuu wangu hao unaowaona ni working class tu, na wanatamba mjini kwa sababu rushwa limehalalishwa. Ukienda benki lazima uwe na mtu wako umpe kidogo urushwe msitari, Ukienda bandarini unatoa kidogo upunguziwe ushuru, Ukienda dukani au Bar unarushwa bei inategemea na wanavyokuona.. Ndio maisha ya Bongo lakini hakuna middle class kama unavyotaka kuisema kwa sababu hatuna daraja la working class na upper class isipokuwa Upper na Walalahoi anayetoboa hapo ni working class tu. Lini umeona wewe Daktari anapokea mshahara mdogo kuliko mbeba box wa huku, halafu unamwita middle class kwa sababu anawatoza wagonjwa cha juu na kubangaiza huku na huko... Kila mtu Tanzania anachukua kazi kwa sababu anajua ndani ya kazi hiyo he will make 10x ya mshahara huo?.. uliona wapi kitu hii..Ndio maana sisi wengine tunapingana na mfumo mzima na sio kilichopo machoni.
 
Labda museme ... Sababu kubwa ni kwasababu
duuuh!

chini ya utawala wa ujamaa na kujitegemea, tuli assume a "classless society" Lakini haikuwa na maana kuwa there weren't no classes.
tuli assume a "classless society" lakini haikuwa na maana "there weren't no classes" ! Tunaongea viswahili, tunasomeshwa viingereza na tunafikiri vichwani kwa lugha zetu za asili za vichagga, basi huo mkorogo ukitoka hapo... sumu tupu!

Kama tuli assume a "classless society" ina maana unasema hakukuwa na classes!
 
Daktari anapokea mshahara mdogo kuliko mbeba box wa huku, halafu unamwita middle class.
Huwezi kulinganisha hali ya maisha ya watu wanaoishi kwenye mifumo tofauti ya kiuchumi kwa kutumia mshahara.

Maisha ya mbeba box wa $10/saa ana maisha ya masaibu na adha za ajabu kuliko daktari wa Tanzania anaelipwa mshahara mdogo zaidi. Mbeba box huyo wa $20,000 kwa mwaka kwa nchi kama US ni fukara wa kutupwa, anaishi hundi kwa hundi, hawezi kumfikia daktari, hawezi kumiliki au kujenga nyumba kama daktari wa Tanzania, mbeba box hawezi kuajiri shamba boy, mbeba box hawezi kuleta ndugu kijijini kuwatunza bure, mbeba box hawezi kusomesha wanae kwa mshahara wa $20,000/yr, ye mwenyewe kujisomesha kakwama, hawezi hata kumudu pango inabidi waishi watatu watatu, wawili wawili, ushasikia Tanzania daktari wawili wanaishi pamoja kwa saab hawana hela ya kutosha pango?

Semeni Tanzania ni masikini lakini msiende huko kabisa kwenye kumlinganisha mbeba maboxi na daktari wa Tanzania...
 
Back
Top Bottom